Historia ya Maasai

Historia ya Wamasai

Orodha ya Yaliyomo

Kufika Afrika Mashariki

Leo hii wamasai wana makazi yao sehemu za Kusini mwa Kenya  na Kaskazini kati mwa Tanzania. Historia ya wamasai inaonyesha kwamba wao ni jamii ya wafugaji na wanaishi kwa kuhamahama na ndio namna ya Maisha yao. Urithi wao ni watu na ng’ombe. Walihamia kutoka kusini mwa mto Naili kaskazini mwa Afrika kutoka karne ya kumi na tano kabla ya kuanzisha makazi yako Mashariki mwa Afrika katikati mwa karne ya kumi na saba ambayo sasa ni mazingira ya Kenya na Tanzania. Kwenye msafara  wa kuelekea Kusini, Wamasai , wamekuwa

Wapiganaji wanne wa kimasai wakiwa wamevaa mavazi kamili ya vita
Wapiganaji wanne wa kimasai wakiwa wamevaa mavazi kamili ya vita

wanatoka huko wakiogopa kuporwa utu na hekima yao kinguvu na kupoteza jamii yao wamejikuta wakihamia kusini mwa Afrika. Kama vile taifa lililopotea la Israel, Mlinzi wa kimasai anafanana na mlinzi wa Rumi. Kama vile Warumi, Wamasai wamekuwa wakisifiwa kwa ulinzi wao ulio imara.Waliweza kuwapora na kuwaweka kwenye himaya yao makundi ya wachaga, Wasirikwa, Wagalla, Waliatua, Wandorobo na Wakikuyu walipokuwa wakielekea Kusini. Zaidi, Wafanyabiashara za watumwa wa Kiarabu walipovamia bara wakitokea pwani hawakuweza kuwagusa wamasai; wakati  huo wakulima na wapelelezi wa Ulaya wa mwanzoni waliogopa kuwavamia wamasai kwani walikuwa na ulinzi ulio imara.

Customize your samsung galaxy s23 ultra hülle now for ultimate style and protection. Elevate your device with our premium accessories today!

Uvamizi Kutoka Ulaya

Kutanuka kwa kabila la Kimasai kusini mwa Afrika kulisitishwa na idadi kubwa ya wakoloni kutoka ulaya waliofika Mashariki mwa Afrika mwishoni  mwa karne ya kumi na tisa. Watu wa Ulaya kutoka hasa Magharibi mwa Ulaya walianza kufika Afrika kwa kile kinachoitwa “kupigania Afrika”. Watu wa Ulaya walichochewa na sababu za kiuchumi na siasa walipokuwa wakihitaji kuongeza utawala wao. Tangu mwanzo wa historia ya wamasai walikuwa  wengi sana maeneo ya nyanda za juu mwa Kenya, hivyo Waingereza wakapendelea maeneo hayo.Vita vikaibuka kati ya Wamasai na Waingereza, wakoloni wa Wakiingereza walipoanza kuwa na nia kwenye jamii na mipaka ya wamasai kwa kuwazunguka kupitia viongozi wa dini. Pamoja na magojwa na njaa watu walikuwa dhaifu.Waingereza waliwatoa wamasai kutoka kwenye maeneo yao na kuwapeleka milimani ambako kuishi kwao kukawa kugumu. Leo hii, japokuwa idadi yao inakuwa taratibu kila mwaka, kwa Afrika wamasai wamekuwa hawana nguvu tena kama ilivyo kuwa hapo mwanzo.

Wamasai na Dini

Wamasai na Dini
Wamasai na Dini

Imani katika historia ya wamasai, inaonyesha kwamba wamasai wanaamini kuwa mwanzo wa anga na dunia ni moja, na awali wamasai hawakuwa na ng’ombe yeyote. Wamasai ambao ni miongoni ya wachache wa makabila ya Monastiki  Afrika, wanamuita Mungu kama Enkai na wanaamini kuwa alishusha ng’ombe kutoka juu akiwa na kamba itokanayo na magome (au kamba ya ngozi  au katika kijiti cha moto), na wamasai ndio walipokea ng’ombe wote ambao wapo mpaka sasa  hapa duniani. Wadorobo (Ildorobo) , ni kundi la wawindaji na wakusanyaji  ambao hawakupokea ng’ombe yeyote , hivyo waliendelea kukata Kamba ,kutengeneza utenganifu kati ya mbingu na dunia, na kusababisha kuacha kuendelea kushuka ng’ombe kutoka Mbinguni. Kutokana na imani hio , inaonesha kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya Mungu na ng’ombe, na kwamba ng’ombe wote duniani wanamilikiwa na wamasai.

Hadithi ya Senteu na Olanana

Kiongozi wa kidini wa kimasai anaitwa Laiboni na ana maamuzi juu ya vitu vyote vinavyohusu dini, sherehe na madawa. Inaaminiwa kuwa anauwezo wa kuharibu, kutibu na kutabiri. Kukubalika na kuheshimiwa kwake kunategemea  uwezo alionao. licha ya kuwa hana nguvu ya kisiasa, kwa mamlaka yake anaweza kuanzisha vita.

Msemo maarufu wa kimasai unasema,”Ushauri unaotolewa kwa mtoto wa kiume wa mke mkubwa na unaweza kusikilizwa na kutekelezwa na mtoto wa kiume wa mke mdogo kabisa” hii inaonesha namna kaka wawili waliokuwa wakiwania nafasi ya kurithi kutoka kwa baba yao kama Laiboni wa kimasai. Kwenye hadithi zilizopo kwenye historia ya wamasai zinazofanana na za kwenye bibilia, hadithi ya Isaka,Esau na Yakobo, Mbatiany, mzee kiongozi wa kimasai alikuwa na watoto wawili,Senteu na Olonana. Senteu akiwa kama ndio mkubwa alikubalika kuwa ndio atakaye mrithi baba yao mzee Mbatiany kama Laiboni anayefuata. Siku moja  akiwa peke yake kwenye chumba cha ndani, Mbatiany alimwita Santeu akisema “ Mwanangu, nipo karibu kufariki na ningependa nikuachie madaraka. Kwahio hakikisha unaamka mapema asubuhi kabla ya yeyote kuamka na uje pembeni  mwa kitanda changu kupokea baraka kama kiongozi wa watu wangu. Utakuwa na nguvu kubwa ya kuongoza watu wangu wote na hakuna yeyote atakaye kukataa”. Bila kujua, Mbatiany na Senteu , kumbe Olonana alikuwa amejificha kwenye jamvi ndani ya chumba cha baba yake na alisikia kila kitu kilichoongelewa na baba yake ikiwa ni pamoja na kila kitu Senteu alitakiwa  kumwendea baba yake asubuhi inayofuata ili kupokea baraka.

Haikupita muda Olonana alisikia baba yake akimwambia maneno Senteu na akaenda kwa mama yake akamwambia yote yaliyojili. Olonana pamoja na mama yake wakakubaliana, Olonana amsaliti Santeu asubuhi iliyofuata ili aweze kutotimiza ahadi yake kwa Mbatiany na kushindwa kumpa baraka na kumfanya awe Laiboni anayefuata. Hivyo asubuhi iliyofuata, Olonana  aliamka na akaenda pembeni mwa kitanda cha baba yake, Mbatiany aliuliza wewe ni nani?, Olonana harakaharaka akajibu,” Baba, mimi ni Kijana wako mkubwa, Santeu” Mbatiany akaendelea kumbariki Olonana na kumkabidhi vifaa vya kiroho na vya kiuongozi. Kukamilisha kumbariki Laiboni ajaye, Mbatiany alisema kwa Olonana “Mwanangu  njoo karibu ili niweze kukukumbatia karibu kwenye kifua changu” Baada ya kumkumbatia Mbatiany alisema “Sasa waweza busu ulimi wangu” ambao ulimaliza sherehe na Olonana akaondoka muda huo ili asiwepo mtu yeyote wa kumuona. Alipokea nguvu zote kutoka kwa  baba yake. Alipokuwa akitoka nje, Olonana alionana na Santeu mlangoni akiingia kwa baba yake kupokea baraka.Wote wawili hawakusalimiana na Santeu alijua nini kimetokea. Mbatiany  alisikia Santeu akiingia na akauliza nani huyo? Santeu akamjibu baba yake iliyomfanya atambue sauti yake na akauliza nani alikuepo awali pale. Santeu alimweleza baba yake kuwa alionana na Olonana akiwa anatoka nje huku yeye akiwa anaingia ndani. Bahati mbaya kwa Santeu kile kimefanyika hakikuwezekana kufutwa  ikiwa Santeu na Olonana wote walikuwa Watoto wa Mzee Mbatiany. Japokuwa Mbatiany alimpa Santeu boksi la Maajabu ambalo lingemwezesha kuua na kufukuza watu. Hivyo Santeu akawa mdogo kwa kaka yake Olonana ingawa yeye alikuwa ndiye mkubwa kwa kuzaliwa. Kutoka hapo Santeu akawa msaidizi wa Mdogo ake,Olonana, ambaye ndiye Laiboni aliyefuata.

Katikati mwa Karne ya  kumi na tisa katika kumbumbuku za historia ya wamasai, ugomvi kati ya jamaa wawili, Olonana, kiongozi wa kidini

Mganga mkuu wa maasai Lenana akiwa na wakoloni wa kijerumani
Mganga mkuu wa maasai Lenana akiwa na wakoloni wa kijerumani

na Santeu, kiongozi anayekubaliwa na jamii, ulisababisha mgongano kati ya watu. Huu ndio ugomvi mkubwa uliowai kujitokeza kati ya jamii ya kimasai na kusababisha mgongano kati yao na kupunguza umoja wao wa kuweza kusimama dhidi ya makundi ya nje. Ili kupunguza nguvu ya Santeu na msaada anaopata kutoka kwa jamii, Olonana aliamua kutumia wakoloni wa kizungu  kama washirika wake kumpinga kaka yake ili kujenga utawala wake juu ya watu na kupunguza nguvu ya Santeu iliyotokana na umaarufu.

Hatahivyo, wakoloni walikuwa na nia zaidi kenye ardhi nzuri ya wamasai kuliko kujihusisha zaidi na ugomvi kati ya jamaa hao wawili na walimtumia Olonana kama chambo ya kupunguza nguvu zaidi ya wamasai ili kupata ardhi zaidi. Wakoloni kwa pamoja na Olonana waliingia Mkataba wa Mwaka 1904 na 1911 uliowahitaji wamasai kuendelea kuhama zaidi kuelekea kusini mwa Afrika na kuondoka kwenye ardhi nzuri ya nyanda za juu. Wamasai walitolewa kutoka kwenye ardhi nzuri ya kufugia katika nyanda za juu na kuwapeleka kwenye ardhi isiyokuwa na rutuba katika uwanda wa Savana kusini mwa afrika. Ardhi yao ilihalalishwa kama ardhi ya malkia na kuchukuliwa na wakulima wa kizungu. Wamasai hawakulipwa chochote zaidi ya kumlinda Olonana kutoka kwa Santeu.

Kwa nakala zaidi zinazohusu kabila la kimaasai bofya hapa!