Mwalimu Goso

Mwalimu Goso

Orodha ya Yaliyomo

Hapo kale kulikuwa na mtu aliyeitwa Go’so, ambaye aliwafundisha watoto kusoma, sio kwenye nyumba ya shule, bali chini ya mbuyu. Jioni moja, wakati Goso akiwa ameketi chini ya mti akisoma kwa undani masomo ya siku inayofuata, Paa, alipanda juu ya mti kwa ukimya sana kuiba matunda, na kwa kufanya hivyo alitikisa kibuyu, ambacho, wakati wa kuanguka, kikampiga mwalimu huyo kichwani na kumuua.

Kifo cha mwalimu Goso

Wanafunzi wake walipofika asubuhi na kumkuta mwalimu wao akiwa amekufa, walijawa na huzuni; kwa hiyo, baada ya kumzika kwa heshima, wakakubaliana kati yao kumtafuta yule aliyemuua Goso, na kumuua.

Baada ya kulizungumza jambo hilo walifikia hitimisho kuwa upepo wa kusini ndiye mkosaji.

Mlolongo wa watuhumiwa wa mauaji

Upepo wa kusini

Hivyo waliushika upepo wa kusini na kuupiga.

Lakini upepo wa kusini ulilia: “Hapa! Mimi ni Koo’see, upepo wa kusini. Kwanini mnanipiga? Nimefanya nini?”

Nao wakasema: “Ndio, tunajua wewe ni Koosee; ni wewe uliyetupa chini kile kibuyu kilichompiga mwalimu wetu Goso. Hukupaswa kufanya hivyo. ”

Lakini Koosee alisema, “Ikiwa ningekuwa na nguvu sana ningezuiwa na ukuta wa matope?”

Ukuta wa matope

Kwa hivyo walienda kwenye ukuta wa matope na kuupiga.

Lakini ukuta wa matope ulilia: “Hapa! Mimi ni Keeyambaa’za, ukuta wa matope. Kwanini mnanipiga? Nimefanya nini?”

Nao wakasema: “Ndio, tunajua wewe ni Keeyambaaza; ni wewe uliyemzuia Koosee, upepo wa kusini; na Koosee, upepo wa kusini, uliishia kutupa chini kibuyu kilichompiga mwalimu wetu Goso. Hukupaswa kufanya hivyo. ”

Lakini Keeyambaaza alisema, “Ikiwa ningekuwa na nguvu sana ningechoshwa na panya?”

Panya

Kwa hivyo walienda na kumkamata panya na kumpiga.

Panya akielezea kwamba kama angekuwa na nguvu asingeliwa na paka
Panya akielezea kwamba kama angekuwa na nguvu asingeliwa na paka

Lakini panya huyo alilia: “Hapa! Mimi ni panya. Kwanini mnanipiga? Nimefanya nini?

Nao wakasema: “Ndio, tunajua wewe ni Panya; ni wewe uliyemchosha Keeyambaaza, ukuta wa matope; ambao ulimzuia Koosee, upepo wa kusini; na Koosee, upepo wa kusini, uliishia kutupa chini kibuyu kilichompiga mwalimu wetu Goso. Hukupaswa kufanya hivyo. ”

Lakini Panya alisema, “Ikiwa ningekuwa na nguvu sana ningeliwa na paka?”

Paka

Kwa hivyo walimwinda paka, wakamkamata, na kumpiga.

Lakini paka alilia: “Hapa! Mimi ni paka. Kwanini mnanipiga? Nimefanya nini?

Nao wakasema:“Ndio, tunajua wewe ni Paka; ni wewe unayekula, Panya; aliyemchosha Keeyambaaza, ukuta wa matope; ambao ulimzuia Koosee, upepo wa kusini; na Koosee, upepo wa kusini, uliishia kutupa chini kibuyu kilichompiga mwalimu wetu Goso. Hukupaswa kufanya hivyo. ”

Lakini Paka alisema, “Ikiwa ningekuwa na nguvu sana ningefungwa kwa kamba?”

Kamba

Basi wakachukua ile kamba na kuipiga.

Lakini kamba ililia: “Hapa! Mimi ni Kamba. Kwanini mnanipiga? Nimefanya nini?

Nao wakasema:“Ndio, tunajua wewe ni Kaamba; Ni wewe unayefunga Paka; anayekula panya; aliyemchosha Keeyambaaza, ukuta wa matope; ambao ulimzuia Koosee, upepo wa kusini; na Koosee, upepo wa kusini, uliishia kutupa chini kibuyu kilichompiga mwalimu wetu Goso. Hukupaswa kufanya hivyo.”

Lakini Kaamba alisema, “Ikiwa ningekuwa na nguvu sana ningekatwa na kisu?”

Kisu

Basi wakakichukua kisu na kukipiga.

Lakini kisu kililia: “Hapa! Mimi ni Kee’soo, kisu. Kwanini mnanipiga? Nimefanya nini?

Nao wakasema:“Ndio, tunajua wewe ni Keesoo; unayekata Kamba; inayofunga paka; anayekula panya; aliyemchosha Keeyambaaza, ukuta wa matope; ambao ulimzuia Koosee, upepo wa kusini; na Koosee, upepo wa kusini, uliishia kutupa chini kibuyu kilichompiga mwalimu wetu Goso. Hukupaswa kufanya hivyo. ”

Lakini Keesoo alisema, “Kama ningekuwa na nguvu sana ningechomwa na moto?”

Moto

Wakaenda wakaupiga ule moto.

Lakini moto ulilia: “Hapa! Mimi ni Mo’to, moto. Kwanini mnanipiga? Nimefanya nini?

Nao wakasema: “Ndio, tunajua wewe ni Moto; unaomchoma Keesoo, kisu; ambaye hukata kamba; inayomfunga Paka; anayekula Panya; ambaye humchosha Keeyambaaza, ukuta wa matope; ambao ulimzuia Koosee, upepo wa kusini; na Koosee, upepo wa kusini, uliishia kutupa chini kibuyu kilichompiga mwalimu wetu Goso. Hukupaswa kufanya hivyo. ”

Lakini Moto ulisema, “Kama ningekuwa na nguvu sana ningezimwa na maji?”

Maji

Nao wakaenda kwenye maji na kuyapiga.

Lakini maji yalilia: “Hapa! Mimi ni Maji. Kwanini mnanipiga? Nimefanya nini?

Nao wakasema:“Ndio, tunajua wewe ni Maji; unayeuzima moto; unaomuunguza Keesoo, kisu; anayekata Kamba; inayofunga Paka; anayekula Panya; anayemchosha Keeyambaaza, ukuta wa matope; ambao ulimzuia Koosee, upepo wa kusini; na Koosee, upepo wa kusini, uliishia kutupa chini kibuyu kilichompiga mwalimu wetu Goso. Hukupaswa kufanya hivyo.”

Lakini Maji alisema, “Ikiwa ningekuwa na nguvu sana ningenywewa na ng’ombe?”

N’gombe

Nao walikwenda kwa ng’ombe na kumpiga.

Lakini ng’ombe huyo alilia: “Hapa! Mimi ni ng’ombe. Kwanini mnanipiga? Nimefanya nini?

Nao wakasema:“Ndio, tunajua wewe ni Ng’ombe; unayekunywa Maji, maji; yanayozima Moto, moto; unaomuunguza Keesoo, kisu; anayekata Kamba; inayofunga Paka; anayekula Panya; anayemchosha Keeyambaaza, ukuta wa matope; ambao ulimzuia Koosee, upepo wa kusini; na Koosee, upepo wa kusini, uliishia kutupa chini kibuyu kilichompiga mwalimu wetu Goso. Hukupaswa kufanya hivyo. ”

Lakini Ng’ombe alisema, “Ikiwa ningekuwa na nguvu sana ningeteswa na nzi?”

Nzi

Na walimkamata nzi na kumpiga.

Lakini nzi huyo alilia: “Hapa! Mimi ni nzi. Kwanini mnanipiga? Nimefanya nini? ”

Nao wakasema:“Ndio, tunajua wewe ni Nzi; unayemtesa Ng’ombe, ng’ombe; anayekunywa Maji, maji; yanayozima Moto, moto; unaomuunguza Keesoo, kisu; anayekata Kamba; inayofunga Paka; anayekula Panya; anayemchosha Keeyambaaza, ukuta wa matope; ambao ulimzuia Koosee, upepo wa kusini; na Koosee, upepo wa kusini, uliishia kutupa chini kibuyu kilichompiga mwalimu wetu Goso. Hukupaswa kufanya hivyo. ”

Lakini Nzi alisema, “Ikiwa ningekuwa na nguvu sana je! Ningeliwa na paa?”

Kukamatwa kwa muuaji

Walipompata paa, walimpiga sana
Walipompata paa, walimpiga sana

Nao walimtafuta paa, na walipompata walimpiga.

Lakini yule paa alisema: “Hapa! Mimi ni Paa, paa. Kwanini mnanipiga? Nimefanya nini?

Nao wakasema: “Ndio, tunajua wewe ni Paa; unayekula Nzi, nzi; ambaye humtesa Ng’ombe, ng’ombe; ambaye hunywa Maji, maji;yanayouzima Moto, moto; unaomuunguza Keesoo, kusini anayekata Kamba; inayomfunga Paka; anayekula Panya; ambaye humchosha Keeyambaaza, ukuta wa matope; ambao ulimzuia Koosee, upepo wa kusini; na Koosee, upepo wa kusi, alitupa chini kibuyu kilichompiga mwalimu wetu Goso. Hukupaswa kufanya hivyo. ”

Paa, kwa kushangaa kwa kupatikana na kuogopa matokeo ya mauaji yake ya mwalimu huyo bila kukusudia, wakati alipokuwa akiiba, akawa bubu.

Ndipo wasomi wakasema: “Ah! hana neno la kujisema mwenyewe. Huyu ndiye yule jamaa aliyetupa chini kile kibuyu kilichompiga mwalimu wetu Goso. Tutamuua. ”

Kwa hivyo walimuua Paa, na kulipiza kisasi kifo cha mwalimu wao.

Mwalimu Goso
Mwalimu Goso

Kwa nakala zaidi zinazohusu hadithi bofya hapa!