Kima

Kima, Papa na Punda wa Dobi

Hapo zamani za kale Kee′ma(kima) na Pa’pa (Papa) walikuwa marafiki wakubwa.

Kima aliishi katika mti mkubwa wa mkuyu uliokua kando ya bahari, nusu ya matawi yake yakiwa baharini na nusu ardhini.

Kila asubuhi, wakati kima alipokuwa akila  matunda ya mkuyu, papa alionekana chini ya mti na kumwambia, “Nirushie chakula, rafiki yangu;” .Ambapo kima alikubali kwa moyo mmoja.

Hii iliendelea kwa miezi kadhaa, mpaka siku moja Papa akasema, “Kima, umenitendea wema mwingi: Ningependa twende wote nyumbani kwangu, ili nikulipe.”

“Nitawezaje kwenda na wewe?” aliuliza kima; “Sisi wanyama wa nchi kavu hatuwezi kuingia majini.”

“Usiwe na shaka kuhusu hilo,” alijibu papa; “Nitakubeba. Hakuna hata tone la maji litakalokupata. ”

“Ah, sawa, basi,” Bwana Kima alisema; “Twende.”

Walipokwenda karibu nusu ya safari Papa alisimama, akasema: “Wewe ni rafiki yangu. Nitakwambia ukweli. ”

“Kwani, unanini la kusema?” aliuliza kima, kwa mshangao.

“Naam, ukweli ni kwamba sultani wetu ni mgonjwa sana, na tumeambiwa kwamba dawa pekee itakayo mfaa ni moyo wa kima.”

“Sawa,” akasema Kima, “mlikuwa wajinga sana kwa kuto kuniambia hayo kabla hatujaanza!”

“Kivipi?” aliuliza Papa.

Lakini kima alikuwa akifikiria namna ya kujiokoa, na hakujibu.

“Vizuri?” Alisema papa, kwa wasiwasi; “Kwanini hauongei?”

“Ah, sina la kusema sasa. Umechelewa sana. Lakini ungeniambia kabla ya kuanza kwenda, ningekuja na moyo wangu . ”

“Nini? hauna moyo wako hapa? ”

“Lo!”alishangaa Kima; “Hujui kuhusu sisi? Tunapotoka hua tunaacha mioyo yetu kwenye miti, na kwenda na miili yetu tu. Lakini naona hauniamini. Unafikiri naogopa. Twende nyumbani kwenu, ambapo unaweza kuniua na kuutafuta moyo wangu pasipo mafanikio. ”

Papa alimwamini, ingawa, alishangaa na kusema, “Lo, hapana; turudi tukauchukue moyo wako. ”

“Hapana kabisa,” Kima alipinga; “Twende nyumbani kwenu.”

Lakini papa alisisitiza kuwa wanapaswa kurudi kuchukua moyo, na kuanza upya.

Hatimaye, kwa kusita kima alikubali huku akinung’unika kwa hasira kutokana na shida isiyo ya lazima aliyokuwa amewekwa.

Waliporudi kwenye mti, alipanda kwa haraka sana, akisema, “Subiri hapo, Papa, rafiki yangu, niupate moyo wangu, na tutaanza vizuri wakati mwingine.”

Alipofika kwenye matawi, akaketi na kukaa kimya kabisa.

Baada ya kusubiri kwa muda aliofikiri kima atakuwa ameupata moyo wake, Papa aliita, “Njoo, Kima!” Lakini Kima alinyamaza tu na hakusema chochote.

Muda kidogo aliita tena: “Ah, Kima! twende. ”

Wakati huo kima alitoa kichwa chake kutoka kwenye matawi ya juu na akauliza, kwa mshangao mkubwa, “Kwenda? Wapi? ”

“Nyumbani kwetu”

“Unawazimu?” aliuliza Kima.

“Wazimu? Kwa nini, unamaanisha nini? ” alilia Papa.

“Una shida gani?” alisema kima. “Umenifanya punda wa dobi?”

“Kuna nini cha maana juu ya punda wa dobi?”

“Ni kiumbe ambaye hana moyo wala masikio.”

Papa, udadisi wake ukaishinda haraka aliokua nayo, hapo aliomba kusimuliwa hadithi ya punda wa dobi, ambapo kima aliisimulia kama ifuatavyo:

“Dobi alikuwa na punda, ambaye alikuwa akimpenda sana. Hata hivyo siku moja, alikimbia,akaanza kuishi msituni, ambapo ilipelekea kuwa mvivu, na kwa sababu hiyo alinenepa sana.

“Hatimaye sungura kwa bahati akapita njia ambayo punda anaishi, akamwona punda.

“Sungura ndiye mnyama mjanja zaidi kuliko wote – ukimwangalia mdomo wake utaona kuwa huwa anajiongelesha kila kitu peke yake.

“Sungura alipomwona Punda alijisemea, ‘Jamani, huyu punda amenenepa!’ Kisha akaenda kumwambia simba.

Dada Punda, Nimetumwa kama mshenga kukuomba uoelewe
Dada Punda, Nimetumwa kama mshenga kukuomba uoelewe

“Simba ndio alikuwa anaendelea kupona baada ya kuumwa sana, bado alikuwa na afya dhaifu kiasi kwamba hakuweza kwenda kuwinda. Kwahiyo alikuwa na njaa sana.

“Bwana Sungura alisema, ‘Kesho nitaleta nyama ya kutosha kwa ajili yetu ili tufanye sherehe kubwa, lakini itabidi uue.’

“‘Sawa, rafiki yangu mzuri,’ alisema Simba, kwa furaha; ‘wewe ni mwema sana.’

“Sungura akaenda msituni, akamkuta punda, akamwambia, kwa heshima, ‘Bibi Punda, nimetumwa kuja kukuposa.’

“‘Na nani?’ alirahisisha punda.

“‘Na simba.’

“Punda alifurahi sana kwa hili, na akasema: ‘Twende mara moja. Hii ni nafasi ya kipekee. ‘

“Walipofika nyumbani kwa simba, walikaribishwa kwa ukarimu, na kuketi. Sungura alimkonyeza Simba kwamba hio ndio nyama aliyoahidiwa, na kwamba atasubiri nje. Kisha akamwambia Punda: ‘Nnakwenda uwani kwanza. Wewe kaa hapa uzungumze na mumeo mtarajiwa. ‘

“Mara tu Sungura alipofika nje, simba alimrukia Punda, na wakapigana sana. Simba alipigwa teke kali, na akampiga kwa makucha kama ambavyo afya yake dhaifu ingemruhusu. Hatimaye punda akamtupa simba chini, na kukimbilia nyumbani kwake msituni.

“Muda mfupi baadaye, sungura alirudi, na kuita,” Haya! Simba! umempata? ‘

“‘Sijampata,’ simba akaunguruma; ‘alinipiga mateke na kukimbia; lakini ninakuhakikishia nilimwachia majeraha mengi, ingawa sina nguvu.

“‘Ah, sawa,’ alisema Sungura; usijilaumu sana juu ya suala hilo.’

“Ndipo Sungura alisubiri siku kwa nyingi, mpaka pale simba na punda walipokuwa wazima na walipopata nguvu, alisema: ‘Unafikiria nini sasa, Simba? Nikuletee nyama yako? ‘

“‘Ay,’ simba aliunguruma kwa ukali; ‘Niletee. Nitairarua vipande viwili! ‘

“Sungura alienda msituni, ambapo punda alimkaribisha na kuulizia taarifa.

“‘Unakaribishwa tena kumwona mpenzi wako,’ alisema Sungura.

“‘Ah, mpenzi!’ Punda alilia; ‘siku hiyo uliponipeleka kwake aliniumiza vibaya. Naogopa kumkaribia sasa. ‘

“‘Ah, pshaw!’ alisema Sungura; ‘hiyo sio shida. Hiyo ni njia tu ya Simba ya kubembeleza. ‘

“‘Ah, sawa,” punda akasema, “twende.”

“Walianza tena; lakini mara tu simba alipomwona Punda alimrukia na kumrarua vipande viwili.

“Sungura alipoinuka, Simba akamwambia:” Chukua hii nyama na uichome.Ninachotaka mimi ni moyo na masikio.

“‘Asante,’ alisema Sungura. Kisha akaenda zake kuichoma nyama mahali ambapo simba hakuweza kumwona, akachukua moyo na masikio akayaficha. Kisha akala nyama yote aliyoitaka, na kuweka mbali iliyobaki.

“Simba alimjia na kusema, ‘Niletee moyo na masikio.’

“‘Viko wapi?’ Alisema sungura.

“‘Hii inamaanisha nini?’ Simba aliunguruma.

“‘Kwani, hukujua kuwa huyu alikuwa punda wa dobi?’

“Hii inahusiana nini na kutokuwa na moyo au masikio?’

“‘Simba’ wewe si mkubwa kiasi cha kujua kwamba mnyama huyu angekuwa na moyo na masikio asingerudi mara ya pili?’

“Ilibidi simba akubali kwamba kile alichosema Sungura ni kweli.

“Na sasa,” Kima alimwambia papa, “unataka kunifanya punda wa dobi. Ondoka hapo, nenda nyumbani mwenyewe. Hautanipata tena, na urafiki wetu umeisha. Kwaheri, Papa. ”

Kwa nakala zaidi zinazohusu hadithi bofya hapa!