Tanzania - Mabanda duni ya Mjini yasiyokuwa na usafi na kutia wasiwasi

Shida za Ukuaji wa Idadi ya Watu na Mabadiliko ya Hali ya Hewa Dar-es-Salaam

Orodha ya Yaliyomo

  • Ukuwaji wa idadi ya watu na miji kwa kasi ya haraka vinaweka watu na mali zao kwenye hatari zaidi zinazoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa
  • Tanzania ni nchi iliyoathiriwa na mafuriko kwa kiasi kikubwa, na kibaya zaidi nchi ina mji mkuu katika Afrika mashariki unaokua kwa kasi zaidi
  • Asilimia 95 ya ukuaji wa miji ulimwenguni inatokea katika nchi zinazoendelea kwa miaka 90 ijayo

“Hakuna kitu kama janga la asili lisilosababishwa na vitu vingine visivyo vya asili” hiki ni kilio kikubwa cha wahusika wa maendeleo nyuma ya Programu ya Uthabiti wa Miji Tanzania, mpango wa wadau mbalimbali ulioundwa kuongeza uthabiti wa Tanzania dhidi ya hatari zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Maafa ya asili, programu hii inaelezea, yanatokea mara nyingi kutokana na mipango mibovu isiyofanikiwa sawa na kutokana na athari halisi za mabadiliko ya hali ya hewa yenyewe.

Chanzo kikuu cha hatari? Kukuwa kwa miji haraka. Zaidi ya nusu ya idadi ya watu ulimwenguni sasa wanaishi mijini na 95% ya ukuaji wa miji ulimwenguni inatokea katika nchi zinazoendelea kwa miaka 90 ijayo. Wakati ukuaji huu unapaswa kuleta na fursa kubwa ya kiuchumi, lakini pia huongeza sana mkusanyiko wa watu na rasilimali ambazo ziko hatarini na athari za hali ya hewa.

Katika Afrika Masharikia, Tanzania ni nchi iliyoathiriwa zaidi na mafuriko katika eneo hili. Mji mkuu wake wa Dar-es-Salaam, haswa, ndio jiji kubwa na linalokua kwa kasi zaidi katika eneo la mashariki mwa Afrika, ukiweka miundombinu ya jiji na mali zake, zenye thamani ya dola bilioni 5.3, athari za mafuriko zinakuwa kubwa zaidi kwa mji huu. Dar-es-Salaam ni jiji tambarare, lenye watu wengi na idadi ya watu yake iko karibu milioni tano.

Mafuriko Dar-es-salaam Aprili 2018
Mafuriko Dar-es-salaam Aprili 2018

Msimu wa mvua wa 2017 ni mfano hai: kwa mara nyingine tena msimu wa mvua umegeuza hatari inayoweza kuepukika kuwa janga, kichwa cha habari cha gazeti la The Guardian la Tanzania kilisomeka hivi: “Mvua zilizosubiriwa kwa muda mrefu na kusababisha uharibifu usiowezekana kuelezwa nchi nzima.” Uharibifu huu ulikuwa wa aina nyingi, kuhamisha watu, kufungwa kwa shule, na kubomoka kwa miundombinu muhimu.

Kwa bahati nzuri, Serikali ya Tanzania inatambua kwamba hatua za kuzuia ni muhimu ili kuepuka vichwa vya habari zaidi kama hivi. Benki ya Dunia imejitolea kusaidia serikali katika hili kupitia ushirikiano wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza. Ushirikiano huu, Mpango wa Uthabiti wa Miji, unatumia njia ya kipekee kushughulikia hatari za mbadiliko ya hali ya hewa kama ifuatavyo:

Kutambua Hatari

Kabla ya kupunguza hatari, ni muhimu kwamba uhusiano kati ya ukuaji wa miji na mazingira ueleweke. Nchini Tanzania, kuna data kidogo kuwezesha upatikanaji wa tathmini sahihi wa hatari iliyopo, unyeti, na uwezo wa kukabiliana uliopo kwa idadi ya watu na mali zake dhidi ya hatari za hali ya hewa za sasa na za baadaye. Mpango huu unaoshirikisha Uingereza unakusudia kuimarisha uelewa huu wa hatari ya hali za hewa na maafa katika muktadha wa Kitanzania.

Ramani Huria, kwa mfano, ilitengenezwa kama mwongozo wa ramani ya jamii mjini Dar-es-Salaam, inafundisha wanafunzi na wanajamii kuunda ramani sahihi zenye zana mbalimbali za GIS ambazo zinaweza kutumika kuchambua kiasi cha hatari. Ramani hii iliuliza swali: Je tunaweza kupata njia ya kutumia maarifa ya jamii juu ya maswala yanayohusiana na mafuriko katika maeneo yasiyopangwa na yasiyo rasmi, na tunaweza kutumia maarifa hayo yabadilike kwenye vitendo? Jibu lilikuwa ‘ndiyo’, “alisema Edward Anderson, Mtaalam Mwandamizi wa Usimamizi wa Hatari za Maafa na Mtaalam wa ICT nchini Tanzania.

Kupunguza Hatari

Miji mikubwa ya Tanzania inapanuka kwa kasi, na Dar-es-Salaam pekee inatarajiwa kukua kwa 85% itakapofika mwaka 2025. Mfumo wa mipango ya matumizi ya miji na ardhi kama ilivyo sasa hauwezi kusimamia ukuaji wa kasi kama hii na kuweza kuhifadhi (kutunza)

Bomba la maji machafu linalomwaga maji katika Bahari ya Hindi Dar es Salaam
Bomba la maji machafu linalomwaga maji katika Bahari ya Hindi Dar es Salaam

mazingira ya jiji kwa wakati mmoja. . Programu ya Uthabiti wa Miji Tanzania (Tanzania Urban Resilience Programme) inakusudia kuimarisha mifumo ya jiji ya kupanga na kupunguza athari za hatari za hali ya hewa.

Mbali na kusimamia mifereji ya maji, uwekezaji unafanywa katika kizazi kijacho cha wapangaji wa miji wenye ubunifu, na uundaji wa ‘Chuo cha Uthabiti’ (Resilience Academy) – mtaala uliotengenezwa na wasomi na sekta binafsi kushirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu. Ushahidi wa faida za uwekezaji kama huo upo kwa Mpango wa Ramani ya Zanzibar, ambapo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Jimbo la Zanzibar wamefundishwa ustadi wa kijiografia na kupatiwa DroneLAB iliyo na vifaa kamili.

Kusimamia Maafa

Hakuna eneo la miji ambalo haliko katika hatari ya maafa, haswa lile ambalo katikati ya jiji liko kwenye uwanda wa mafuriko kama Dar-es-Salaam. Hii ndio sababu sehemu ya tatu ya Programu ya Uthabiti wa Miji inakusudia kuimarisha utayari wa majanga na usimamizi wa dharura, sio tu Dar-es-Salaam lakini kote nchini. Kwa kutumia matukio ya hatari yanayotambuliwa tayari nchini, mipango ya kukabiliana na dharura inaanzishwa. Zuia Mafuriko, Kiswahili cha ‘Stop Flooding’, imetumika kama mradi wa majaribio mjini Dar-es-Salaam katika kufundisha na kutengeneza timu za kukabiliana na mafuriko ya dharura zitakazojumuika na mitandao iliyopo yenye wajibu huu.

Kwa msaada wa Kituo cha Ulimwengu cha Kupunguza na Kurekebisha Maafa (Global Facility for Disater Reduction and Recovery – GFDRR) na Jumuiya ya Kuelewa Hatari (Understanding Risk Community), uzinduzi wa kiufundi wa programu hizi unaendelea kuleta maafisa wa serikali na wengine pamoja kujadili fursa ambazo zinaweza kupatikana chini ya mpango wa Zuia Mafuriko. Hafla hiyo ni pamoja na kongamano juu ya Miji ya Afrika ya Kijani (Greening Africa’s Cities) itakayowezesha mazungumzo mapana juu ya athari za ukuaji wa miji kwenye mazingira barani Afrika, na hatua ambazo zinaweza kufanywa kukuza uhusiano wa usawa zaidi kati ya mazingira yaliyojengwa na ya asili.

Kwa nakala zaidi zinazohusu hali ya hewa bofya hapa!