Treni ya abiria ya TAZARA ikiwa imesimama katika kituo mjini Mbeya

Historia ya Usafiri wa Reli Tanzania Bara

Orodha ya Yaliyomo

Tanganyika

Kipindi cha ukoloni wa Wajerumani

Njia za reli za kwanza Tanganyika, ikijulikana kipindi hicho kama Ujerumani Afrika Mashariki, zilijengwa mara  tu baada ya reli ya kwanza huko Zanzibar.

Mwaka 1891 Eisenbahngesellschaft für Deutsch-Ostafrika (Kampuni ya Reli ya Ujerumani Afrika Mashariki) ilianzishwa, ikiwa na lengo la kujenga njia ya reli kutoka Tanga, Tanganyika kuelekea Bara. Kwa ajili hiyo, na baadaye, njia kuu katika koloni la Ujerumani, geji

Afrika Mashariki ya Ujerumani, Tanganyika - Wafanyikazi wa reli za asili wakati wa ujenzi wa Reli ya Tanganyika, inayosimamiwa na wazungu - pengine katika miaka ya 1910
Afrika Mashariki ya Ujerumani, Tanganyika – Wafanyikazi wa reli za asili wakati wa ujenzi wa Reli ya Tanganyika, inayosimamiwa na wazungu – pengine katika miaka ya 1910

iliyochaguliwa ilikuwa  mm 1,000 (futi 3 kwa inchi 3 3/8) mita geji.  Kwa kuongeza, reli nyepesi zilijengwa Tanganyika mahususi kwa ajili ya mashamba ya mkonge zenye geji nyembamba, kwa kawaida geji 600 mm (futi 1 kwa inchi 11 5/8)

Ujenzi wa Reli ya Usambara kutoka Tanga kuelekea Bara, ulianza mwaka 1893. Hata hivyo, kumpuni iliyokuwa inajenga reli hiyo ilifilisika baada ya miaka miwili. Kwa kipindi hicho, km 40 (maili 25) ya reli ndizo zilizokuwa zimekamilika, hadi kufikia Korogwe. Hazina ya mkoloni ilichukuwa mradi mwaka 1899. Miaka minne baadaye, mwaka 1903, ilitoa maelekezo kwa ajili ya kuendeleza ujenzi. Baadaye, kulikuwa na majaribio mengine kuendesha reli katika hali imara kiuchumi na kisheria.

Mwaka 1904, reli ndogo ziliboreshwa. Wakati huo huo, nchini Ujerumani Kampuni ya Reli ya Sigi (Sigi-Eisenbahngesellschaft) ilianzishwa, ikiwa na lengo la kujenga reli nyembamba  kutoka Reli ya Usambara, yaani Sigi-Bahn katika geji ya mm 750 (futi 2 kwa inchi 5 1/2).  Mwaka huo huo, 1904 kampuni ya Reli ya Afrika Mashariki (Ostafrikanische Eisenbahngesellschaft (OAEG)) ilianzishwa  kusaidia reli kutoka Dar es Salaam kuelekea Ziwa Tanganyika, yaani Reli/Njia ya Kati (Zentralbahn). Kigoma ilifikiwa februari 2, 1914, mwanzoni mwa vita vya kwanza vya Dunia. Baadaye  mwaka 1914, kazi ilianzia Ruandabahn, njia kutoka Tabora katika ngome iliyokuja kuwa Rwanda. Mradi huu ulikwamishwa na kuzuka kwa Vita vya Kwanza vya Dunia.

Kampeni Afrika Mashariki

Wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia, Vikosi vya Ujerumani na washirika wao vilihusika katika kampeni ya Afrika Mashariki, mfululizo wa mapigano na vita vya msituni ambavyo vilianza katika Ujerumani Afrika Mashariki. Hadi kufikia 1915, washirika  waliamua kujenga reli kutoka Voi, Kenya, Kituo kwenye Reli ya Uganda kuelekea Maktau, kama njia kamili na vamizi ya usambazaji wa koloni la Ujerumani, ukijumuisha njia ngumu chini ya Reli ya Usambara kuelekea Tanga. Baadaye, njia iliongezwa hadi Kahe, kituo cha reli ya Usambara karibu na Moshi, Tanganyika. Kwa kuwa, reli ya Uganda na Usambara zilikuwa katika geji ya mita, hivyo usafirishaji wa magari kutoka mojawapo wa njia hizi kuelekea njia zingine uliwezekana kwa urahisi.

Hadi kufikia Septemba 1916, Reli ya Usambara na Reli ya kati kutoka pwani ya Dar es Salaam hadi Ujiji zilikuwa chini ya udhibiti wa Washirika.

Mamlaka ya Uingereza

Baada ya makubaliano mwaka 1918, Uingereza ikachuwa Tanganyika  iliyopewa Utawala wa Kiraia wa Uingereza kwa  mamlaka ya Shirikisho la Mataifa.  Mnamo tarehe 1 April 1919, utawala mpya wa kikoloni ulianzisha Reli ya Tanganyika na Huduma za Bandari kama mwendeshaji wa reli katika eneo inayotawala.

Mwaka 1928, reli ya Tabora-Mwanza ilikamilika kwa msaada wa maandalizi ya awali ya kivita ya Ujerumani kwa ajili ya Ruandabahn. Mwaka 1930, Reli ya usambara ilipanuliwa hadi Arusha. Mwaka 1948, tawi kutoka Reli ya kati lilifunguliwa kati ya Msagali na Hororo, na mwaka 1949/1950 njia ya Kaliua-Mpanda ilifunguliwa.  Mapema mwaka 1951 njia ya Hororo ilifungwa.

Mwaka 1948, Reli ya Tanganyika na Huduma za Bandari ziliunganishwa na reli za Uganda na Kenya na kuunda Reli ya Afrika Mashariki na

Mpango wa Karanga - Groundnut Scheme - Tanganyika
Mpango wa Karanga – Groundnut Scheme – Tanganyika

Usimamizi wa Bandari (Kutoka 1969: Shirika la Reli Afrika Mashariki)

Kutoka 1950, Shirika la chakula la ngambo (Overseas Food Corporation) lilianzisha Reli ya Mkoa wa Kusini (Southern Province Railway) yenye mm 610 (futi 2) kusini mwa Tanganyika. Iliunganisha bandari ya Mikindani na bara katika mikoa iliyokuwa katika mpango wa uzalishaji wa karanga Tanganyika. Hatimaye, mtandao ulifikia urefu zaidi ya kilomita 250 (maili 155). Mwaka 1952, usimamizi ulihamishiwa kwenda Reli ya Afrika Mashariki na Usimamizi wa Bandari.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Katika mfululizo wa hatua kati ya mwaka 1961 na 1964, Tanganyika ilipata uhuru na kuungana na Zanzibar katika shirikisho. Wakati huo huo, historia ya usafiri wa reli unaonyesha kwamba mtandao wa reli uliokuwepo pia ulipanuka. Mwaka 1963, Reli ya Pwani ilijengwa kuunganisha reli ya Kati na Usambara, na mwaka 1965 tawi lilifunguliwa kusini, kutoka Kilosa, katika reli ya Kati kwenda Kidatu. Mwaka 1963, mtandao wa geji nyembamba kusini mwa Tanganyika ulifungwa.

Kutoka 1964, majadiliano yalifanyika kuhusu mapendekezo ya njia ya reli kati ya Tanzania na Zambia. Kwa kuwa Uingereza haikuonyesha nia yoyote katika pendekezo hilo, Jamhuri ya Watu wa China (JWC) ilijiunga. Serikali ya JWC ilifadhili ujenzi wa reli mahususi kuondoa utegemezi wa uchumi wa Zambia kutegemea Rhodesia na Afrika Kusini. Mikataba ilifungwa mwaka 1967, na mwaka mmoja baadaye, Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA) ilianzishwa, kama reli ya muunganiko inayomilikiwa na Tazania na Zambia

TAZARA ilijengwa kwa futi 3 kwa inchi 6 (mm 1,067) kitu ambacho kilikuwa ni kipya kwa Tanzania, lakini ni kawaida kwa Kusini mwa Afrika. Njia hiyo ilikabidhiwa kwa kampuni kwani ilikamilishwa kwa sehemu mwaka 1973 na 1974. Mwaka 1976, tawi lilifunguliwa kwenda Kitadu, ambapo tawi la geji ya mita kutoka Reli ya Kati linaishia.

Treni ya Shirika la Reli Tanzania (TRC)
Treni ya Shirika la Reli Tanzania (TRC)

Mwaka 1977, kwa kuzingatia utofauti wa sera na kupanuka kwa viwango vya maendeleo ya kiuchumi kwa nchi washirika, Umoja wa Afrika Mashariki ulivunjika, na miundo yake yote ya pamoja pia ilivunjika. Reli za Tanzania isipokuwa TAZARA zilirekebishwa kuwa Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Kiuchumi, mtandao uliporomoka kila wakati, kwa sababu ya kuongezeka kwa barabara, rushwa na kupuuzwa kisiasa. Viungo kadhaa vya reli, kama vile kati ya Arusha na Moshi vilifungwa, na huduma za abiria kuachwa, ukijumuisha reli ya Usambara.

TAZARA imekuwa njia kuu ya kiuchumi katika ukanda huo. Lakini, haikuwahi kuwa na faida na hivi karibuni imeathiriwa na ushindani kutoka usafiri wa barabara (kama vile Trans-Caprivi Highway na Walvis Bay Corridor kwenda Namibia) na kuelekezwa upya kwa uhusiano wa kiuchumi wa Zambia kuelekea Afrika Kusini baada ya kumalizika kwa ubaguzi wa rangi. Hadi kufikia Oktoba 2008, gazeti moja la Tanzania lilielezea hali ya TAZARA kama “iko karibu kuanguka kwa sababu ya shida ya kifedha”, huku mwendeshaji akichelewa kwa miezi mitatu kulipa wafanyakazi na sehemu kubwa ya injini zake 12 zikiwa hazifanyi kazi. Mwanzoni mwa mwaka 2010, serikali ya China iliipa TAZARA mkopo wa dola milioni 39 bila riba ili kufufua shughuli zake.

Wakati huo huo, mwaka 2007 RITES Ltd. ya India ilishinda kandarasi kutoka Tume ya Kurekebisha Sekta ya Mashirika ya Umma, Tanzania, kuendesha huduma za abiria na mizigo ya TRC kwa makubaliano ya miaka 25. Mkataba wa makubaliano ulisainiwa tarehe 3 Septemba 2007, na ulianza tarehe 1 Oktoba 2007. Huduma zilizokuwa zinaendeshwa hapo awali na TRC ziliendeshwa kama Kampuni ya Reli Tanzania Ltd, na serikali ikimiliki asilimia 49 ya hisa. Lakini, mwaka 2010 serikali ilisitisha mkataba na kuendelea na uendeshaji.

Kwa nakala zaidi zinazohusu usafiri bofya hapa!