Masharti ya Matumizi

VIGEZO HIVI NA MASHARTI HAYA YALITENGENEZWA MNAMO TAREHE 8 MEI, 2014 NA KUANZA KUTUMIKA MARA MOJA KWA WOTE WANAOSOMA, KUNUNUA KWA, KUFANYA MANUNUZI KUTOKA, KUSAJILI AKAUNTI NA/AU KUWA NA MUINGILIANO WA NAMNA YOYOTE NA IFAHAMU TANZANIA.

Ifahamutanzania. (https://www.ifahamutanzania.com/), AMBAO, KWA PAMOJA, NI IFAHAMU TANZANIA. NA KUANZIA SASA ITAJULIKANA KAMA “IFAHAMU TANZANIA.” au “Tovuti”) INAHITAJI KUFIKIRIA NA KAMA KIGEZO CHA KUKURUHUSU KUTEMBELEA.

KUSOMA NA KUKUBALIANA NA MASHARTI YA MATUMIZI NA KUSOMA NA KUKUBALIANA NA SERA YA FARAGHA ILIYOTOLEWA YA IFAHAMU TANZANIA. KUNAHITAJIKA NA IFAHAMU TANZANIA. KUKUPA WEWE HAKI ZA KUTEMBELEA, KUSOMA AU KUINGILIANA NAYO KWA NAMNA YOYOTE.

WATU WOTE WOTE HAWATARUHUSIWA KATIKA IFAHAMU TANZANIA. MPAKA PALE WATAKAPOKUWA WAMESOMA NA KUKUBALIANA NA MASHARTI YA MATUMIZI NA SERA YA FARAGHA.

KWA KUTAZAMA, KUTEMBELEA, KUTUMIA, AU KUWA NA MUINGILIANO NA IFAHAMU TANZANIA. AU NA BANGO, HABARI ZA KUJITOKEZA, MATANGAZO YOYOTE AMBAYO YATATOKEA JUU YAKE, AU PROGRAMU ZA SIMU ZITAKAZOUNGANISHA KWAKE NA/AU KUREJEA VIGEZO HIVI BASI UNAKUBALIANA NA MIPANGO YOTE YA SERA HII YA MASHARTI YA MATUMIZI NA SERA YA FARAGHA YA IFAHAMU TANZANIA. NA KUKAMILISHA MKATABA WA MAKUBALIANO YA KISHERIA NA IFAHAMU TANZANIA.

WATU WOTE WENYE UMRI WA CHINI YA MIAKA 18 HAWATAPATA RUHUSA YA KUINGIA IFAHAMU TANZANIA. KAMA UNA UMRI CHINI YA MIAKA 18, NI KINYUME NA SHERIA KUTEMBELEA, KUSOMA AU KUWA NA MUINGILIANO NA IFAHAMU TANZANIA. AU MAUDHUI YAKE KWA NAMNA YOYOTE. IFAHAMU TANZANIA. HUSUSA INAKATAA KUTOA RUHUSA KUINGIA KWA MTU YEYOTE AMBAYE ANALINDWA NA SHERIA YA WATOTO YA ULINZI WA FARAGHA MTANDAONI (COPPA) YA MWAKA 1998.

IFAHAMU TANZANIA. INAHIFADHI HAKI YA KUKATAA KURUHUSU MTU YEYOTE AU MTAZAMAJI KUINGIA KWA SABABU YOYOTE. CHINI YA VIGEZO VYA SERA YA FARAGHA, AMBAYO UNAKUBALIANA NAYO KAMA SHARTI LA KUTAZAMA, [Domain] INARUHUSIWA KUKUSANYA NA KUHIFADHI DATA NA TAARIFA KWA MADHUMUNI HASA YA KUDHIBITI NA KWA MATUMIZI MENGINE.

  1. UFAFANUZI

    Orodha ya Yaliyomo

    Wahusika

    “Wewe” and “yako” inamaanisha wewe, kama mtumiaji wa Tovuti. “Mtumiaji” ni mtu anayefungua, kuvinjari, kutambaa, kukwangua, kutembelea, kutazama, kujisajili, aliye mwanachama, wakala au mteja wa pamoja na/au kwa namna yoyote anatumia Tovuti.

“Tovuti” au IFAHAMU TANZANIA. inamaanisha https://www.ifahamutanzania.com/ na http://www.soko. ifahamutanzania.com/ (kwa pamoja, Ifahamu Tanzania.)

Maudhui

“Maudhui” inamaanisha maneno, picha, sauti, video, data za eneo, na aina zote zingine za data au mawasiliano. “Maudhui Yako” inamaanisha Maudhui ambayo umeyawasilisha au kutuma kwa, kupitia, au yenye uhusiano na Tovuti, kama vile viwango, maoni, sifa, mialiko, kuingia-ndani, jumbe za maneno, na taarifa uliyoionyesha kwa umma katika wasifu wa akaunti yako. “Maudhui ya Mtumiaji” inamaanisha Maudhui ambayo mtumiaji anawasilisha au kutuma kwa, kupitia, au yenye uhusiano na Tovuti.

“Maudhui ya IFAHAMU TANZANIA.” inamaanisha Maudhui tuliyoyatengeneza na kuyaweka wazi kupatikana yenye uhusiano na Tovuti.

“Maudhui ya Mwanachama wa Tatu” inamaanisha Maudhui yanayotoka kwa wanachama tofauti na IFAHAMU TANZANIA. au watumiaji wake, ambayo yamewekwa wazi kupatikana yenye uhusiano na Tovuti. “Maudhui ya Tovuti” inamaanisha Maudhui yote yaliyowekwa wazi kupatikana yenye uhusiano na Tovuti, Ikiwemo Maudhui Yako, Maudhui ya Mtumiaji, Maudhui ya Mwanachama wa Tatu, na Maudhui ya IFAHAMU TANZANIA.

  1. MABADILIKO KATIKA MASHARTI VYA HUDUMA

Baada ya kipindi fulani, IFAHAMU TANZANIA. inaweza kubadilisha Masharti. Toleo la sasa la Masharti haya litapatikana hapa. Unaelewa na kukubali kwamba kufungua au kutumia kwako kwa Tovuti kunasimamiwa na Masharti mara moja wakati unapofungua au kutumia Tovuti. Kama tukifanya mabadiliko katika Masharti haya, hautapewa taarifa ya awali. Tutaonyesha juu kabisa ya ukurasa tarehe ambayo marekebisho ya mwisho yalifanyika na marekebisho yote yanapatikana hapa. Unatakiwa kupitia tena Masharti haya mara kwa mara kwa kuwa marekebisho yatakuwa yanakufunga. Mabadiliko yoyote yale yataanza kufanya kazi mara moja baada tu ya kutuma Masharti yetu mapya. Unaelewana kukubali kwamba kufungua au kutumia kwako kwa Tovuti baada ya tarehe ya mabadiliko ya Masharti kunaashiria kukubali kwako kwa marekebisho hayo.

  1. KUTUMIA TOVUTI

Ruhusa ya Kutumia Tovuti

Tunakupa wewe ruhusa ya kutumia Tovuti kwa kulingana na udhibiti ndani ya Masharti haya.

Utumiaji wako wa Tovuti ni kwa hatari yako mwenyewe, ikiwemo hatari ya kwamba unaweza kuonyeshwa Maudhui ya kuudhi, yasiyo ya heshima, yasiyo sahihi, ya kutiliwa shaka, au kwa namna moja yasiyofaa.

Unakubaliana na hatari zote za kutazama, kusoma, kutumia, au kutegemea taarifa hizi. Isipokuwa kama vinginevyo una mkataba wa haraka na tovuti, hauna haki ya kutegemea taarifa yoyote iliyopo humu ndani kuwa ni sahihi. Tovuti haitoi uhakikisho huo.

Ilani kwa MAUDHUI, MADAKTARI WANAOTANGAZWA NA BIDHAA za Tovuti

IFAHAMU TANZANIA. inatoa ilani juu ya usahihi wa maudhui ya tovuti hii na UNATAMBUA NA KUELEWA KWAMBA MAUDHUI YOTE, MAELEZO YA BIDHAA, HUDUMA ZILIZOTANGAZWA NA MAONI YANALENGA KUBURUDISHA TU NA HAKIKA YASITUMIKE KAMA MAPENDEKEZO YA KITABIBU, KISHERIA, AU KIFEDHA AU KAMA USHAURI WOWOTE WA KITAALAMU. NI WAJIBU WAKO BINAFSI KUCHUNGUZA TAARIFA YOYOTE, MAONI, USHAURI AU MAUDHUI YOYOTE MENGINE YANAYOPATIKANA KATIKA TOVUTI.

IFAHAMU TANZANIA. haitoi uhakikisho kwamba maelezo ya bidhaa au maudhui mengine ya Tovuti ni sahihi, kamili, ya kutegemewa, ya wakati huu, yasiyo na makosa.

Upatikanaji wa Mtandao

Tovuti inaweza kubadilishwa, kusahihishwa, kukatizwa, kusimamishwa au kufungwa muda wowote bila kutoa taarifa au kuwajibika.

Akaunti za Mtumiaji

Ni lazima utengeneze akaunti na kutoa baadhi ya taarifa zako binafsi ili uweze kutumia baadhi ya vitu vinavyotolewa kupitia Tovuti. Ni wajibu wako kuhakikisha neno lako la siri linabaki kuwa siri. Pia unawajibika na shughuli zote zinazofanyika zinazohusiana na akaunti yako. Unakubali kutujulisha mara moja kama kuna matumizi yasiyoruhusiwa ya akaunti yako. Tunahifadhi haki ya kufunga akaunti yako muda wowote kwa sababu au bila kuwa na sababu yoyote.

Akaunti yako ni kwa matumizi yako binafsi na ya kibiashara. Katika kuitengeneza, IFAHAMU TANZANIA. inakuomba utoe taarifa zako zilizo kamili na sahihi ili kuimarisha uaminifu wako kama biashara, mmiliki/meneja wa biashara na mchangiaji wa Tovuti. Hautakiwi kumuigiza mtu mwingine (mf kujifanya mtu maarufu au mnyama wa kufugwa – hata kama mnyama huyo ni wako), kutengeneza au kutumia akaunti kwa mtu mwingine ambaye sio wewe, kutoa barua pepe ambayo sio ya kwako, au kutengeneza akaunti zaidi ya moja. Kama ukitumia jina la bandia, kumbuka kwamba wengine bado wanaweza kukutambua kama, kwa mfano, ukiweka taarifa ndani ya maoni yako, ukitumia taarifa sawa katika akaunti yako na kwenye tovuti zingine, kuruhusu tovuti zingine kushirikisha taarifa zako na KAMPUNI. Tafadhari soma Sera ya Faragha kwa taarifa zaidi.

  1. MAWASILIANO KUTOKA KWA IFAHAMU TANZANIA. NA WATUMIAJI WENGINE

IFAHAMU TANZANIA.ni tovuti ya kuorodhesha biashara, ya biashara za mtandaoni na wa rasilimali pamoja na jumuiya ya kijamii, hivyo basi taarifa zako zote za mawasiliano ya kikazi na ya mitandao ya kijamii inapatikana hapa. Kwa kutengeneza akaunti, unakubali kupokea baadhi ya mawasiliano yanayohusiana na Tovuti. Kwa mfano, unaweza kupokea ombi la taarifa zaidi kutoka kwa wateja wako au maombi ya urafiki kutoka kwa Watumiaji wengine. Pia utapokea barua pepe zetu kila wiki za kijarida chetu.

  1. MAUDHUI

Wajibu wa Maudhui Yako

Wewe pekee ndiye unayewajibika kwa Maudhui Yako (ikiwa ni pamoja na lakini sio tu makala au vingine vilivyotumwa, maoni katika makala, matangazo ya siri au ya kujihudumia binafsi ambayo hayatokani na IFAHAMU TANZANIA.), na baada ya kuchapishwa, sio mara zote yanaweza kuondolewa. Fikiria kukubali hatari zote zinazohusiana na Maudhui Yako, ikiwa ni pamoja kutegemea kwa yeyote juu ya ubora wake, usahihi, au uthabiti, au ufafanuzi wako wowote wa taarifa ndani ya Maudhui Yako ambao unakufanya uweze kutambulika binafsi. Unawakilisha kile unachomiliki, au una ruhusa husika kutumia na kuruhusu matumizi ya Maudhui Yako kama ilivyofafanuliwa hapa ndani. IFAHAMU TANZANIA. haibebi wajibu wa hasara yoyote au uaribifu wa aina yoyote utakaotokea kama matokeo ya Maudhui ya Mtumiaji yoyote ndani ya Tovuti.

Hautaweza kudokeza kwamba Maudhui Yako yamefadhiliwa au kuungwa mkono na IFAHAMU TANZANIA.. Unaweza kujiweka mwenyewe katika nafasi ya kuwajibika kama, kwa mfano, Maudhui Yako yana vitu ndani yake ambavyo ni vya uongo, kupotosha makusudi, au kukashifu; kukiuka haki yoyote ya mshiriki wa tatu, ikiwemo hakimiliki yoyote, chapa, leseni ya ubunifu, siri za kibiashara, haki za kimaadili, haki za faragha, haki ya umaarufu, au taarifa yoyote ya kitaaluma au haki ya ubunifu wa siri; kuwa na mambo ambayo ni ya kinyume cha sheria, ikiwemo hotuba za kinyume na sheria za chuki au picha za ngono; njia za unyonyaji au vinginevyo kuathiri watoto; au kwenda kinyume au kutangaza uvunjwaji wa sheria au kanuni.

Haki za Tovuti kutumia Maudhui Yako

IFAHAMU TANZANIA. inaweza kutumia Maudhui Yako katika njia kadhaa tofauti, ikiwemo kuyaonyesha wazi, kupangilia upya, kuyaweka katika matangazo na kazi zingine, kutengeneza kazi za kutohoa kutokana nayo, kuyatangaza, kuyasambaza na kuruhusu wengine kufanya hivyo kwa kuhusisha na tovuti zao wenyewe na majukwaa mengine(“Other Media”). Na hivyo, wewe hivi sasa unatoa haki yako duniani kote kwetu isiyoweza kutenguliwa, isiyokwisha muda, isiyo ya kipekee, ya bure, inayoweza kukabidhiwa, inayoweza kutolewa leseni ndogo, inayoweza kuhamishwa kutumia Maudhui Yako kwa lengo lolote na bila wajibu wa kukupa taarifa, mrejesho au kukulipa. Tafadhali kumbuka kwamba pia unatoa haki yako isiyoweza kutenguliwa kwa watumiaji wa Tovuti na Majukwaa Mengine kufungua Maudhui Yako kwa uhusiano wao na matumizi ya Tovuti na Majukwaa Mengine. Mwisho kabisa, unavua  haki ya kushtaki kisheria isiyoweza kutenguliwa, na sababu ya kuvua haki ya kushtaki kisheria, dhidi ya IFAHAMU TANZANIA. na watumiaji wake dhidi ya madai yoyote na usimamii wa haki za kimaadili au kukurejea katika Maudhui Yako. Kwa “kutumia” tunamaanisha kutumia, kunakili, kucheza na kuonyesha mbele ya umma, kuzalisha nakala, kusambaza, kurekebisha, kutafsiri, kuondoa, kuchunguza, kufanyia biashara, na kuandaa kazi zilizo toholewa za Maudhui Yako.

Umiliki

Basi kati yako wewe na IFAHAMU TANZANIA., unamiliki Maudhui Yako. Sisi tunamiliki maudhui ya IFAHAMU TANZANIA., ikiwemo lakini sio tu, vileosura vya kuonekana(visual interfaces), vitu vya kuingiliana(interactive features), picha, ubunifu, mkusanyiko, ikiwemo, lakini sio tu, mkusanyiko wetu na Maudhui ya Tovuti yingine, msimbo wa Kompyuta, bidhaa, programu, mkusanyiko wa viwango vya maoni ya watumiaji, na vitu vingine vyote katika Tovuti ikiwemo Maudhui Yako, Maudhui ya Watumiaji na Maudhui ya Wanachama wa Tatu. Pia tunamiliki hakimiliki, chapa, hakimiliki za huduma, hakimiliki za jina, na hakimiliki zingine za ubunifu duniani (“IP Rights) zinazohusiana na IFAHAMU TANZANIA. Maudhui na Tovuti, ambayo yanalindwa na hakimiliki, ‘trade dress’, leseni, sheria za hakimiliki na sheria zingine zote za hakimiliki. Kwa hiyo, hautakiwi kubadilisha, kuzalisha nakala, kusambaza, kutengeneza kazi iliyotoholewa au kutokana na, Maudhui ya IFAHAMU TANZANIA. yaliyoonyeshwa wazi kwa umma wala kunyonya kwa namna yoyote kwa uzima au sehemu ndogo kasoro kama itakuwa imeruhusiwa na sisi. Isipoelezewa na kufikishwa bila mkanganyiko wowote hapa sasa, hatutoi kwako haki yoyote ya kuelezea(express) au ya msingi (implied), na haki zote za Maudhui ya Tovuti na IFAHAMU TANZANIA. zinahifadhiwa na sisi.

Matangazo

IFAHAMU TANZANIA. na waliopewa leseni wake wanaweza kuonyesha matangazo kwa umma na taarifa zingine kwa pamoja au yakiwa ndani ya Maudhui Yako. Hudai malipo yoyote kwa matangazo hayo. Jinsi, nama na mipaka ya matangazo hayo yanaweza kubadilika bila kuwa na jukumu la kukujulisha wewe.

Malisho ya Maudhui

Baadhi ya Maudhui ya Tovuti (“Feed Content”) tunayafanya kuwa wazi kupatikana kwa kupitia ‘Real Simple Syndication’ na ‘Atom feeds’ (“Feeds”). Unaweza kufungua na kutumia Malisho ili kuonyesha Maudhui ya Malisho katika kompyuta yako binafsi, tovuti au blogu (“Tovuti Yako”), ikiwa tu (i) matumizi yako ya Malisho ni yako binafsi, sio kwa manufaa ya kifedha tu, (ii) Maudhui ya Malisho yako unayoyaonyesha yanaunganisha kwenye kurasa husika ndani ya tovuti ya IFAHAMU TANZANIA., na kutaja IFAHAMU TANZANIA. kama chanzo cha Maudhui ya Malisho, (iii) matumizi yako au maonyesho yako ya Maudhui ya Malisho hayapendekezi kwamba IFAHAMU TANZANIA. inawezesha au inaunga mkono jambo, mawazo, tovuti, bidhaa au huduma, ikiwemo “Tovuti Yako”, (iv) hausambazi Maudhui ya Malisho tena, na (v) matumizi yako ya Malisho hayawi mzigo mkubwa kuzidi uwezo wa mifumo ya IFAHAMU TANZANIA.. IFAHAMU TANZANIA. inahifadhi haki zote ndani ya Maudhui ya Malisho na inaweza kufunga Malisho muda wowote. Tafadhali jisikie huru kuwasiliana nasi kuhusiana na matumizi yoyote ya Malisho.

Mengine

Maudhui ya Mtumiaji (ikiwemo yoyote ambayo yanaweza kuwa yametengenezwa na watumiaji walioajiliwa au kupewa mikataba ya muda na IFAHAMU TANZANIA.) sio lazima kuonyesha maoni ya IFAHAMU TANZANIA.. Tunahifadhi haki ya kuondoa, kuchuja, kurekebisha, au kuweka upya Maudhui ya Mtumiaji na kwa namna tunavyoona kwa sababu, au bila sababu yoyote, na bila wajibu wa kukujulisha wewe. Kwa mfano, tunaweza kuondoa maoni kama tunaamini yanaenda kinyume na Taratibu zetu za Maudhui. Hatuna wajibu wa kutunza au kukupa wewe nakala ya Maudhui Yako, wala hatutoi uhakikisho wa usiri wowote katika Maudhui Yako.

  1. MAKATAZO

Hatuna wajibu wowote kusimamia Masharti kwa niaba yako dhidi ya mtumiaji mwingine. Japokuwa tunakushauri utujulishe kama unaamini mtumiaji mwingine amevunja Masharti, tunahifadhi haki za kuchunguza na kuchukua hatua husika kwa wakati wetu.

Unakubali kutofanya, na hautatoa msaada, kuchochea, au kuwezesha wengine kutumia Tovuti ili kufanya haya:

  • Kukiuka Miongozo yetu ya Maudhui, kwa mfano, kwa kuandika maoni feki au ya kizushi, kununua maoni na biashara zingine, au kumlipa mtu mwingine au kulipwa kuandika au kuondoa maoni;
  • Kukiuka haki za mwanachama wa tatu yoyote, ikiwemo kuvunja uaminifu, hakimiliki, chapa, leseni, siri za biashara, haki za kimaadili, haki za faragha, haki za utangazaji, au haki zozote za kivumbuzi au kibunifu;
  • Kutishia, kufuatilia, kudhuru, au kusumbua wengine au kusambaza ubaguzi;
  • Kusambaza biashara au shughuli nyingine au tamasha, au kutumia Tovuti kwa malengo ya kifedha, kasoro kama kuna muungano na Akaunti ya Kibiashara na kwa ruhusa ya IFAHAMU TANZANIA..
  • Kutuma barua pepe za mkupuo, tafiti, au jumbe zingine za mkupuo kwa watu wengi, bila kujali zina asili ya kibiashara au hazina; kujikita katika kutumia neno kuu kwa ujumbe usiotakwa(‘spamming’), au njia nyingine kujaribu kuhadaa matokeo ya utafutaji wa Tovuti au Tovuti nyingine ya mwanachama wa tatu;
  • Kuomba taarifa binafsi za watoto, au kuwasilisha au kutuma video za ngono; au
  • Kuvunja sheria yoyote inayofaa.

 

Pia unakubali kutokufanya, na hautasaidia, kuchochea, au kuwezesha wengine kufanya:

  • Uvunjaji wa Masharti;
  • Kubadilisha, kutohoa, kuchukua, kuzalisha upya, kusambaza, kutafsiri, kutengeneza kazi nyingine au iliyotoholewa, kuonyesha wazi, kuuza, kufanya biashara, au kwa namna yoyote kunyonya Tovuti au Maudhui ya Tovuti (tofauti na Maudhui Yako), kasoro kama una idhini ya IFAHAMU TANZANIA.;
  • Kutumia roboti yoyote, buibui, programu ya kutafuta/kufuata, au kifaa kingine chochote cha moja kwa moja, kufanya mchakato au kufungua, kufuata, kukwangua, au kufahirisi sehemu yoyote ya Tovuti au Maudhui yoyote ya Tovuti ;
  • Kuunda kwa kurudi nyuma sehemu yoyote ya Tovuti;
  • Kuondoa au kurekebisha hakimiliki, chapa yoyote au haki zingine za kibunifu zinaoonekana katika sehemu yoyote ya Tovuti au kitu chochote kilichochapishwa au kunakiliwa kutoka katika Tovuti;
  • Kurekodi, kufanyia kazi, au kuchimba taarifa kuhusu watumiaji;
  • Kufungua, kuchukua, kufahirisi sehemu yoyote ya Tovuti kwa malengo ya kutengeneza au kujaza hifadhidata inayoweza kutafutwa ya maoni ya biashara;
  • Kufuta upya au kufremu sehemu yoyote ya Tovuti;
  • Kuchukua hatua yoyote ambayo inaweka, au inaweza kuweka, kwa hiari yetu, mzigo usio na mantiki au mzigo mkubwa kupita kiasi juu ya njia za teknolojia ya IFAHAMU TANZANIA. au vinginevyo kutengeneza msongamano mkubwa katika Tovuti;
  • Kujaribu kupata ruhusa ya kuingia bila ruhusa katika Tovuti, akaunti ya mtumiaji, mifumo ya kompyuta au mitandao iliyounganishwa na Tovuti kwa njia za kudukua, kuchimba nywila au namna nyingine yoyote;
  • Kutumia Tovuti au Maudhui ya Tovuti mengine kuhamisha kirusi chochote cha kompyuta, minyoo, kasoro, Farasi wa Trojani au vya kudhuru (kwa pamoja “Vorisi)
  • Kutumia kifaa chochote, programu au njia inayojirudia ili kuingilia na ufanyaji kazi mzuri wa Tovuri, au kwa namna nyingine kujaribu kuingilia na ufanyaji kazi wa Tovuti;
  • Kutumia tovuti kuvunja ulinzi wa mtandao wowote wa kompyuta, kuvinja neno la siri au misimbo ya ufungaji wa ulinzi; kuvuruga au kuingilia kati na usalama, au kwa namna nyingine kusababisha maumivu kwa, Tovuti au Maudhui ya Tovuti; au
  • Kuondoa, kuzunguka, kusitisha, kuharibu au kwa namna nyingine kuingilia na njia yoyote ya ulinzi wa Tovuti, vitu ambavyo vinaepusha au kuzuia utumiaji wa kunakili Maudhui ya Tovuti au vitu vinavyosimika vizuizi katika utumiaji wa Tovuti.

Makatazo haya juu yanafaa kwa kiwango kadri kinavyoruhusiwa na sheria husika. Hata hivyo, unakubali kutokufanya kinyume chake (hata kama inaruhusiwa na sheria) bila kutoa taarifa ya kuandikwa siku 30 kabla, kwa pamoja na taarifa yoyote ambayo tunaweza kuihitaji kwa sababu maalumu ili kutupa fursa ya kutoa suluhisho lingine au kwa namna nyingine kukukidhi kwa wakati wetu.

  1. MIONGOZO NA SERA

Miongozo ya Maudhui

Unakiri kuwa umesoma na kuelewa Miongozo yetu ya Maudhui.

Ilani Kuhusu Usahihi wa Maudhui

Baadhi ya Maudhui katika Tovuti, ikiwemo lakini sio tu, Maudhui ya Mtumiaji, yamewekwa na au kupatikana kutoka kwa wanachama wengine tofauti na IFAHAMU TANZANIA., Kwa mfano, maudhui yaliyotumwa kwenye https://www.ifahamutanzania.com na http://www.soko.ifahamutanzania.com/ yameandikwa moja kwa moja na Wamiliki wa Biashara au mawakala wao (ambao ni wanachama wa tatu huru, sio wafanyakazi wa IFAHAMU TANZANIA., na hawako chini ya usimamizi au maelekezo ya IFAHAMU TANZANIA.) na yametumwa katika Tovuti na Wamiliki/Mawakala bila kukaguliwa na IFAHAMU TANZANIA.. IFAHAMU TANZANIA. haiwakilishi kwa namna yoyote wala kutoa hakikisho juu ya usahihi au uthabiti wa Maudhui yoyote katika Tovuti yaliyotengenezwa na kutolewa na wanachama wa tatu (ikiwemo na lakini sio tu Wamiliki/Mawakala wao, Wateja). IFAHAMU TANZANIA. haitoi uwakilishi au uhakikisho wowote juu ya usahihi au uthabiti wa Maudhui yoyote katika Tovuti uliyotengenezwa au kutolewa na wanachama wa tatu (ikiwemo lakini sio tu Wamiliki wa Biashara/mawakala wao, Wateja.) IFAHAMU TANZANIA. haitoi uhakikisho wowote au uwakilishi wa namna yoyote kwa bidhaa au huduma yoyote ikiwa tu inatolewa na muuzaji yoyote ndani ya Tovuti (ikiwemo lakini sio tu watangazaji katika Tovuti na watu binafsi au taasisi wanaoweka matangazo binafsi au taasisi zinazoweka matangazo katika Tovuti hii) na unakubaliana na hilo kwamba utegemezi wa uwakilishi na uhakikisho unaotolewa na mwanachama yoyote tofauti na IFAHAMU TANZANIA. utakuwa ni kwa hatari yako mwenyewe. Unakubali kabisa kutoiwajibisha IFAHAMU TANZANIA. kwa madai yoyote ya uharibifu yanayotokana na taarifa yoyote, ushauri, bidhaa au huduma inayotolewa au kusukumwa na mwanachama yoyote wa tatu, ikiwemo lakini sio tu kikwazo kwa Wamiliki wa Biashara./Mawakala wao na Wateja

Faragha

Unawakilisha kwamba umesoma na umeelewa Sera yetu ya Faragha. Kumbuka tunaweza kufichua taarifa zinazokuhusu kwa wanachama wa tatu kama tuna imani kwamba kufanya hivyo ni sahihi ili (i) kuchukua hatua inapohisiwa kufanyika shughuli za kuvunja sheria; (ii) kutimiza au kutekeleza Masharti na Sera Zetu za Faragha; (iii) kufuata taratibu za kisheria, au mahitaji mengine ya serikali, kama vile kibali cha upekuzi, hati ya wito wa mahakama, agizo la kisheria, kesi ya mahakamani, au taratibu zingine za kisheria zitakazotuhitaji; au (iv) kulinda haki, sifa, na mali zetu, au watumiaji wetu, wasambazaji wa bidhaa zetu, au umma. Kama ukitumia Tovuti nje ya Marekani, unakubali taarifa zako binafsi kuhamishwa na kufanyiwa kazi ndani ya Marekani.

Mizozo ya Hakimiliki ya Chapa

Tafadhali tazama Sera yetu ya Kuingilia kwa taarifa zaidi juu ya Mizozo ya Hakimiliki na ya Chapa.

Matukio

Tafadhali tazama Vigezo na Masharti yetu ya Matukio kwa taarifa zaidi kuhusu matukuo yaliyoorodheshwa au kuhusishwa katika Tovuti. Unawakilisha kuwa umesoma na kuvielewa.

  1. MAPENDEKEZO NA MABORESHO

Kwa kututumia mawazo yoyote, mapendekezo, nyaraka za mapendekezo (“Maoni”), unakubali ya kwamba (i) Maoni yako hayana taarifa za siri au zenye hakimiliki ya mwanachama wa tatu, (ii) hatuna wajibu wowote wa kutunza siri, kuonyesha Maoni, (iii) tunaweza kuwa na kitu kinachofanana na Maoni tayari tukifikiria kukifanya au katika maboresho, na (iv) unatupa leseni isiyoweza kuvunjwa, isiyo ya kipekee, ya bure, ya kutumika duniani kote, kurekebisha, na kuandaa kazi iliyotoholewa kutoka kwenye yako, kuchapisha, kusambaza na kutoa leseni ndogo Maoni, na unaachana kimoja na kuchukua hatua za kisheria, na sababu ya kuachana na kuchukua hatua, dhidi ya IFAHAMU TANZANIA. na watumiaji wake mashtaka yoyote na madai ya haki zozote za kimaadili zilizopo ndani ya Maoni.

WANACHAMA WA TATU

Tovuti ina viunga (links) ndani yake vya kuelekea katika tovuti au programu zingine (kila moja, ni “Tovuti za Mwanachama wa Tatu”). Hatusimamii au kuunga mkono Tovuti za Mwanachama wa Tatu yoyote. Unakubali ya kwamba hatuna wajibu juu ya upatikanaji au maudhui wa Tovuti za Wanachama wa Tatu kama hizo. Unatumiaji wako wa Tovuti za Wanachama wa Tatu ni kwa hatari yako mwenyewe.

Baadhi ya huduma zilizofanywa kupatikana kupitia Tovuti zinaweza kuwa na leseni za masharti ya mwanachama wa tatu au huria (open source) na kuhitajika kutaja wahusika(disclosures), ikiwemo baadhi zilizotumwa hapa na zilizohusishwa humu ndani na kwa kurejeshwa.

  1. FIDIA

Unakubali kufidia, kuteteam na kubeba IFAHAMU TANZANIA., kampuni lake mama, matawi yake, wasambazaji wake wa bidhaa, na kampuni lolote husika, wasambazaji, watoa leseni na washirika, na maofisa, wakurugenzi, wafanyakazi, mawakala na wawakilishi wa kila mmoja wao (kwa pamoja “Vitengo vya IFAHAMU TANZANIA.”) bila kudhurika, ikiwemo gharama, uwajibishwaji kisheria na gharama za kesi, kutokana na kesi au madai yaliyotolewa na mwanachama wa tatu yoyote yatokanayo na (i) ufunguaji wako au utumiaji wako wa Tovuti, (ii) uvunjaji wako wa Masharti, (iii) bidhaa au huduma yoyote uliyonunua au kuipata kwa uhusiano na Tovuti, au (iv) ukiukwaji wako, au mwanachama wa tatu yoyote akitumia akaunti yako, wa hakimiliki yoyote au haki ya mtu yoyote au kipengele. IFAHAMU TANZANIA. inahifadhi haki, kwa gharama yako, kuchukua hatua ya kujitetea pekee na kudhibiti jambo lolote ambalo unahitajika kutufidia sisi na unakubali kushirikiana na timu yetu ya utetezi dhidi ya madai haya. Unakubali kutokufikia makubaliano yoyote juu ya madai haya bila kuwa na ruhusa ya maandishi kutoka IFAHAMU TANZANIA.. IFAHAMU TANZANIA. itatumia jitihada husika kukujulisha juu ya madai haya, hatua au maendeleo baada ya kufahamishwa.

11. ILANI NA KIWANGO CHA UWAJIBIKAJI

  • TAFADHALI SOMA KIPENGELE HIKI KWA UMAKINI KWA SABABU KINADHIBITI UWAJIBIKAJI WA VITENGO VYA IFAHAMU TANZANIA. KWAKO. KILA KIPENGELE KIDOGO CHINI KINATUMIKA KWA KADRI MWISHO WA SHERIA UNAVYORUHUSU CHINI YA SHERIA HUSIA. HAKUNA KITU HUMU NDANI KINALENGA KUDHIBITI HAKI YOYOTE UNAYOWEZA KUWA NAYO AMBAYO HAIWEZI KUDHIBITIWA KISHERIA. KAMA HAUJUI KUHUSU HILI AU SEHEMU YOYOTE ILE YA MASHARTI HAYA, TAFADHALI WASILIANA NA MTAALAMU WA MASWALA YA SHERIA KABLA YA KUTEMBELEA AU KUTUMIA Tovuti. KWA KUTEMBELEA AU KUTUMIA Tovuti, UNAWASILISHA KWAMBA UMESOMA, KUELEWA, NA KUKUBALIANA NA MASHARTI HAYA, IKIWEMO KIPENGELE HICHI. UNAKUBALI KUVUA HAKI ZA KISHERIA KWA KUKUBALIANA NA MASHARTI HAYA.
  • Tovuti IMEFANYWA KUPATIKANA KWAKO “KAMA ILIVYO”,”PAMOJA NA KASORO ZOTE” NA KWA MTINDO “INAVYOPATIKANA”, KWA UELEWA KWAMBA VITENGO IFAHAMU TANZANIA. VINAWEZA VISISIMAMIE, KUDHIBITI, AU KUCHAMBUA MAUDHUI YA WATUMIAJI. KAMA HIVYO, MATUMIZI YAKO KATIKA Tovuti NI KWA HIARI NA HATARI YAKO MWENYEWE. VITENGO VYA IFAHAMU TANZANIA. HAVITOI TAMKO AU AHADI JUU YA UBORA, USAHIHI, AU UTHABITI WA Tovuti, USALAMA AU ULINZI WAKE, AU MAUDHUI YA Tovuti. HIVYO HIVYO, VITENGO VYA IFAHAMU TANZANIA. HAVIBEBI WAJIBU KWAKO KWA HASARA YOYOTE AU MADHARA AMBAYO YANAWEZA KUTOKEA, KWA MFANO, KUTOKANA NA Tovuti KUTOKUFANYA KAZI, KUTOKUPATIKANA AU KASORO ZA KIUSALAMA AU KUTOKANA NA UTEGEMEAJI WAKO WA UBORA, USAHIHI, AU UTHABITI WA BIASHARA ZILIZOORODHESHWA, VIWANGO, MAONI, NAMBARI AU CHUJIO LA MAONI LINALOONEKANA, KUTUMIKA, AU KUPATIKANA KWA KUPITIA Tovuti.
  • VITENGO VYA IFAHAMU TANZANIA. HAVITOI MADAI WALA AHADI JUU YA MWANACHAMA WA TATU YOYOTE, KAMA VILE BIASHARA AU WATANGAZAJI WALIOORODHESHWA KATIKA Tovuti AU WATUMIAJI WA Tovuti. HIVYO HIVYO, VITENGO VYA IFAHAMU TANZANIA. HAVINA WAJIBU KWAKO KWA HASARA AU MADHARA YOYOTE AMBAYO YANAWEZA KUJITOKEZA KUTOKANA NA MATENDO YAO AU KUTOKUTENDA, IKIWEMO KWA MFANO, KAMA MTUMIAJI MWINGINE AU BIASHARA NYINGINE IKITUMIA VIBAYA MAUDHUI YAKO, UTAMBULISHO WAKO AU TAARIFA ZAKO BINAFSI, AU KAMA UKIWA NA UZOEFU HASI NA MOJA YA BIASHARA AU WATANGAZAJI WALIOORODHESHWA AU KUSHIRIKISHWA KATIKA Tovuti. MANUNUZI YAKO NA MATUMIZI YA BIDHAA AU HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA WANACHAMA WA TATU KUPITIA Tovuti NI KWA HIARI NA HATARI YAKO MWENYEWE.
  • ILANI – HAKUNA USHAURI WA KITAALAMU

TAARIFA KUTOKA KWA IFAHAMU TANZANIA. AU WAUZAJI WA WANACHAMA WA TATU HAILENGWI KUTUMIKA BADALA YA USHAURI WOWOTE WA KITAALAMU, IKIWEMO LAKINI SIO TU (A) USHAURI WA KITABIBU, VIPIMO, AU MATIBABU AU (B) USHAURI WA KITAALAMU WA KIFEDHA AU WA UWEKEZAJI AU MUONGOZO, AU (C) USHAURI WA KITAALAMU WA KISHERIA. KAMWE USIACHE AU KUCHELEWA KUFUATA USHAURI WA KITAALAMU WA KITABIBU AU WA TAALUMA NYINGINE KWA SABABU YA KITU ULICHOKISOMA KATIKA TOVUTI AU TAARIFA ULIYOPOKEA KUPITIA HUDUMA ZETU. IFAHAMU TANZANIA. HAIJAJIKITA KATIKA TAALUMA YA MADAWA AU SHERIA HIVYO HAIPENDEKEZI AU KUUNGA MKONO BIDHAA FULANI HUSIKA, TARATIBU, TIBA, MADAWA, MTAZAMO, AU TAARIFA NYINGINE AMBAYO INAWEZA KUWA IMETAJWA, KUJADILIWA, AU KUFAFANULIWA KATIKA TOVUTI YA IFAHAMU TANZANIA. AU KATIKA VITU VYA IFAHAMU TANZANIA. AU KUPITIA HUDUMA ZETU AU HUDUMA ZA MWANACHAMA WA TATU. UTABIRI HAUFANYIKI NDANI YA BIASHARA YA KUTOA USHAURI WA KIFEDHA AU UWEKEZAJI NA WAFANYAKAZI WAKE AU WALIOPEWA MIKATABA SIO WASHAURI WALIOSAJILIWA. UTEGEMEZI WAKO JUU YA TAARIFA ZINAZOTOLEWA NA IFAHAMU TANZANIA., NA MFANYAKAZI WA IFAHAMU TANZANIA. AU MTU ALIYEPEWA MKATABA, NA MSIMAMIAJI WA MWANACHAMA WA TATU, NA MDHAMINI WA IFAHAMU TANZANIA. AU NA MTUMIAJI YOYOTE WA TOVUTI YA IFAHAMU TANZANIA. NI KWA UCHAGUZI NA HIARI YAKO. MAAMUZI YOYOTE NA YOTE UTAKAYOYACHUKUA AMBAYO YANATEGEMEA KWA UJUMLA AU SEHEMU YA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA IFAHAMU TANZANIA. AU WADHAMINI WAKE AU VINGINEVYO IKO KATIKA TOVUTI UTAKUWA NI WAJIBU WAKO BINAFSI.

ZAIDI YA HAPO, TAARIFA KATIKA IFAHAMU TANZANIA. ZINAZOHUSU SIFA ZA KIMETAFIZIKIA ZA, IKIWEMO LAKINI SIO TU, AURAS, CHAKRAS, NEMBO NA MAANA YOYOTE NA ZOTE, BIDHAA NA TAARIFA ZA KIMIUNGU, TAFSIRI ZA NDOTO, ELEMENTI, RIPOTI NA TAARIFA ZA KIANGA NA KIZODIAC, FUWELE (CRYSTALS), JIWE, MADINI, MAWE, HARUFU ZA MAUA, ELIXRS YA VITO, TIBA YA HARUFU, MAWE YA VITO, UAGUZI (TAROTI, KUSOMA VIGANJA, MAJANI YA CHAI, UTABIRI NA NYENZO ZA USOMAJI WA UTABIRI), NGUVU NA UPONYAJI WA KIROHO, NA NYENZO ZA KUHAMASISHA ZIMETENGENEZWA KWA KUBUNIWA NA HAZIJATHIBITISHWA KISAYANSI. UNASHAURIWA KUTAZAMA TAARIFA HII NA TAARIFA YA WANACHAMA WA TATU KAMA MAKISIO NA KAMA BURUDANI TU.

  • VITENGO VYA IFAHAMU TANZANIA.VINATOA ILANI JUU YA UTHIBITISHO WOTE, IWE NI UMEELEZWA AU KUASHIRIWA, IKIWEMO UTHIBITISHO JUU YA BIDHAA AU HUDUMA ZINAZOTOLWA NA BIASHARA ZILIZOORODHESHWA KATIKA Tovuti, NA UTHIBITISHO WA KUASHIRIWA WA UWEZO WA WAUZAJI BIDHAA, UIMARA DHIDI YA LENGO FULANI, NA KUTOKUINGILIA. HAKUNA TAARIFA YA MDOMO AU YA MAANDISHI UTAKAYOPEWA NA MWAKILISHI MMOJA WAPO WA VITENGO VYA IFAHAMU TANZANIA. ITATENGENEZA UWAKILISHWAJI AU UHAKIKISHO.

ILANI JUU YA MADHARA YATAKAYOSABABISHWA KATIKA KOMPYUTA YAKO AU PROGRAMU KWA MUINGILIANO WAKO NA TOVUTI AU MAUDHUI YAKE. WAGENI WANABEBA HATARI ZOTE ZA VIRUSI, MINYOO NA MAMBO MENGINE.

IFAHAMU TANZANIA. haibebi wajibu wowote juu ya uharibifu wa kompyuta yako au programu yako au mtu yoyote utakayewasiliana nae kutoka katika kompyuta iliyodhurika na hivyo kuhamisha msimbo au data zilizodhurika. Kwa mara nyingine, unatazama na kutumia tovuti, au mabango au ujumbe wa kujitokeza au matangazo yanayoonekana hapo, kwa hatari yako mwenyewe.

  • ILANI JUU YA MADHARA YATAKAYOSABABISHWA NA KUPAKUA

Unapakua taarifa kutoka katika tovuti kwa hatari yako mwenyewe. IFAHAMU TANZANIA. haitoi uhakikisho wowote kwamba unachopakua hakina msimbo wa kuharibu kompyuta yako, ikiwemo, lakini sio tu, virusi na minyoo.

  • HAKI YAKO WEWE BINAFSI NA TIBA YAKO IKITOKEA HAUJARIDHISHWA NA Tovuti, HUDUMA HUSIKA, AU MADHARA MENGINE YOYOTE ITAKUWA NI KUMALIZA NA KUTOENDELEA KUTEMBELEA, AU KUTUMIA Tovuti.
  • KIWANGO CHA MWISHO CHA UWAJIBIKAJI WA VITENGO VYA IFAHAMU TANZANIA.KWAKO KWA HASARA AU MADHARA UNAYOWEZA KUWA UMEYAPATA KWA UHUSIANO NA Tovuti AU MASHARTI HAYA HAKITAZIDI (i) KIWANGO ULICHOLIPA, KAMA ULILIPA CHOCHOTE, KWA VITENGO VYA IFAHAMU TANZANIA. KWA UHUSIANO NA Tovuti NDANI YA MIEZI 12 KABLA YA TUKIO LILILOSABABISHA UWAJIBIKAJI KUTOKEA, AU (ii) $100.
  • VITENGO VYA IFAHAMU TANZANIA.VINATOA ILANI JUU YA MADHARA YOYOTE (i) YASIYO YA MOJA KWA MOJA, MAALUMU, YA AJALI, ADHABU, KIPEKEE(EXEMPLARY), UTEGEMEZI AU KAMA MATOKEO YAKE, (ii) UPOTEVU WA FAIDA, (iii) PINGAMIZI KATIKA BIASHARA (iv) MADHARA YA SIFA, AU (v) UPOTEVU WA TAARIFA AU DATA.
  1. UCHAGUZI WA SHERIA NA MAHALI

Sheria ya Florida itaongoza Masharti haya, pamoja na madai, sababu zitakazozua matendo au mtafaruku utakaozuka kati yako na IFAHAMU TANZANIA. (“Madai”), bila kujali mgongano wa sheria. KWA MADAI YOYOTE YATAKAYOLETWA NA MDAI YOYOTE, UNAKUBALI KUTUMA NA KUKUBALIANA NA HUKUMU BINAFSI NDANI, NA MAHALI PEKEE NI, MAHAKAMA YA SERIKALI YA JIMBO INAYOPATIKANA Jimbo la Pinellas, Florida.

13. USITISHWAJI

  • Unaweza kusitisha Masharti haya muda wowote kwa kufunga akaunti yako, kuacha kuendelea kutumia Tovuti, na kutaarifu IFAHAMU TANZANIA. taarifa ya kusitisha matumizi hapa. Tafadhali pitia Sera ya Faragha kwa taarifa zaidi juu ya nini tunakifanya na akaunti yako inapositishwa.
  • Tunaweza kufunga akaunti yako, kuisimamisha uwezo wako wa kutumia sehemu fulani ya Tovuti, na/au kukupiga marufuku kwa pamoja kutoka katika Tovuti kwa sababu yoyote au bila sababu, na bila kutoa taarifa au kuwajibika kwa namna yoyote. Kitengo chochote kama hichi kinaweza kukuzuia kuitembelea akaunti yako, Tovuti, Maudhui Yako, Maudhui ya Tovuti, au taarifa yoyote inayohusiana.
  • Ikitokea kuna usitisho wa Masharti haya, ambapo wewe au sisi, Vipengele 1,5,6,10 – 14 vitaendelea kufanya kazi na kutumika, ikiwemo haki yetu ya kutumia Maudhui Yako kama ilivyoelezewa katika Kipengele cha 5.
  1. MASHARTI YA JUMLA

  • Tunahifadhi haki ya kurekebisha, kusahihisha, au kusitisha kuendeleza Tovuti kwa hiari yetu, muda wowote, kwa sababu yoyote au bila sababu, na bila kutoa taarifa au kuwajibika.
  • Tunaweza kukupa taarifa, ikiwemo zile zinazohusiana na mabadiliko katika Masharti kwa barua pepe, barua pepe za kawaida au mawasiliano kupitia Tovuti.
  • Labda ielezwe tofauti na Kipengele cha 10 juu, la sivyo hakuna kitu humu kinalenga, wala kitakuwa, kinapingana na haki au tiba za mwanachama wa tatu yoyote.
  • Masharti haya yanabeba makubaliano kamili kati yako wewe na sisi kuhusiana na matumizi ya Tovuti, na yako juu ya makubaliano mengine yoyote kati yako wewe na sisi juu ya suala hili. Washirika wanakubali kwamba hakuna imani inayowekwa juu ya chochote kilichowasilishwa lakini hakijaelezewa ndani ya Masharti haya.
  • IFAHAMU TANZANIA. ikishindwa kwa namna yoyote kufuata haki yoyote au kipengele cha Masharti haimaanishi inavua haki yake ya kushtaki kisheria juu ya haki au kanuni husika. Kushindwa kwa mshirika yoyote kutekeleza sehemu yoyote ya haki zilizotolewa humu haitamaanisha wanavua uwezo wao wa kushtaki kisheria haki zao zingine hapa na kuendelea.
  • Kama sehemu yoyote ya Masharti haya imegundulika haiwezekani kutekelezwa au ni batili, basi sehemu hiyo itarekebishwa ili kuendana na malengo ya washirika au kuondoa kiwango cha chini cha uhitaji ili Masharti yaweze kutumika kwa nguvu yote.
  • Masharti, na haki yoyote au wajibu wowote hapa na kuendelea, hayawezi kukabidhiwa, kuhamishwa au kutolewa leseni ndogo na wewe bali tu mpaka ukiwa na ridhaa kabla ya IFAHAMU TANZANIA. katika maandishi, lakini yanaweza kukabidhiwa au kuhamishwa na sisi bila kipingamizi chochote. Ukabidhi wa aina yoyote kutoka kwako itakuwa ni kukiuka Masharti haya na ni batili.
  • Vichwa vya vipengele katika Masharti ni kwa kurahisisha tu na havina madhara yoyote kisheria na haziathiri mkataba.