Sherehe ya Harusi ya Kimaasai
Orodha ya Yaliyomo
Katika jamii ya Wamaasai, ndoa uchukuliwa kwa umuhimu sana. Pale watu wawili wanapowekwa pamoja kuwa mume na mke, maharusi hawa wanatarajiwa kuishi pamoja milele; talaka sio chaguo labda kama mahari haikulipwa kwa utimilifu. Hata hivyo, kwa Wamaasai kushiriki ndoa na makabila na jamii zingine, talaka huanza kuingizwa taratibu, lakini ni kwa wenzi ambao wote wawili si Wamaasai.
Kuonyesha Nia
Sherehe za harusi ya kimaasai ni moja ya sherehe ndefu kwa kabila la Wamaasai. Uanza kwa mwanaume kuonesha kumhitaji mwanamke
na kumpatia mkufu ambao huitwa olpisisai. Neno hili uzunguka na familia pia na jamii usubiri mwanaume kujulisha nia yake. Yeye ufanya hivi kwa kutafuta wanawake umri wake mwenyewe ambao watapeleka zawadi ya pombe kwa mama wa msichana. Hatua hii ya kwanza uitwa Esirit Enkoshoke, na uonesha kwamba msichana amekwishachumbiwa sasa. Baada ya muda kidogo, mwanaume upanga kufanya nia yake iwe dhahiri kabisa. Ufanya hivyo kwa kuwasilisha zawadi ya pombe kwa baba wa msichana, ambayo itapelekwa na wasichana walewale
waliopeleka zawadi nyingine ya pombe kwa wanawake mapema. Pombe hii huitwa Enkiroret. Baba wa bi harusi mtarajiwa unywa pombe pamoja na ndugu zake, na marafiki kisha umwita kijana na kumtaka atamke nia yake na kuonesha msichana anayetaka kumwoa. (Hii huweza kuwa hatua muhimu sana kwani wazee wanaweza kujifanya hawamfahamu msichana anayetafutwa.) Mara baada ya familia kukubali ombi la mwanaume, pande zote mbili utengeneza mahusiano rasmi, ambayo kwa hakika upelekea kwa harusi kufanyika.
Wakati wa Kuchumbia
Mwanaume anaruhusiwa sasa kupeleka zawadi kwa familia ya mwanamke. Uanza kwa kuwapa zawadi kwa kadri anavyojisikia sawa, hadi kufikia hatua ambayo itakuwa dhahiri kwamba ameridhishwa na hali ya usalama wa ya familia ya msichana. Zawadi hizi zitatengeneza mahari ya bibi harusi, ambapo kusudi lake si kutengeneza utajijri kwa familia ya bibi harusi bali kuhalalisha ndoa. Kwa njia hii, mwanaume
uweka alama katika ile familia, na ikiwa mwingine yeyote akitaka kuisogelea familia hiyo na kutoa mahari, huwa inawekwa wazi kwamba msichana huyo tayari alikwishatolewa kwa familia nyingine.
Harusi ya kimaasai uanza na bwana harusi kuleta mahari, ambayo ujumuisha ng’ombe watatu,ambapo wawili ni jike na mmoja ni dume na wote huwa weusi, na kondoo wawili mmoja jike na mwingine dume. Kondoo dume uchinjwa siku ya harusi kuondoa mafuta yake, ambayo yatapakwa kwenye mavazi ya harusi. Mafuta yanayobakia uwekwa katika chombo kwa ajili ya bibi harusi kubeba na kwenda nayo nyumbani kwake, katika zizi la mumewe.
Baada ya Harusi
Kondoo jike upewa mama mkwe mtarajiwa na mume mkusudiwa. Tangu siku hiyo na kuendelea watachukuliana kama “Paker,” ikimaanisha yule aliyenipa kondoo. Pia kuna ndama ambaye mwanaume umpatia baba mkwe mtarajiwa. Na kuanzia hapo na kuendelea wataitana Pakiteng au Entawuo. Zawadi zote uhifadhiwa katika nyumba ya ndama ambayo hujulikana kama Olale.
Asubuhi hiyo, kichwa cha bi harusi unyolewa na upakwa mafuta ya kondoo. Bi harusi upambwa kwa Imasaa, ambazo ni mapambo mazuri ya shanga, na uwekwa katika vazi lake la harusi. Vazi hilo utengenezwa na ndugu zake, si mama tu. Kwa namna hii vazi la harusi ya kimaasai ni kiashiria cha umoja, wala si ubinafsi. Bi harusi ubarikiwa na wazee kwa kutumia pombe na maziwa, na uongozwa kutoka katika zizi la familia yake kwenda katika nyumba yake mpya, katika zizi la mumewe. Hapo, uingia katika nyumba ya mama wa mumewe, ambapo atakaa kwa siku mbili zinazofuata, ambazo bwana harusi hatalala naye wala kula chakula katika nyumba alimokaa. Hatimaye, baada ya hizo siku mbili, kichwa cha mke unyolewa na mama wa mwanaume, na sherehe imekwisha. Mwanaume na mwanamke ni watu wazima sasa waliooana.
“Uzee uashiria kipindi cha uwajibikaji kwa mwanaume na mwanmke, kuanzia ndoa, kujenga familia, na utafutaji wa utajiri na usalama kwa namna ya watoto na ng’ombe. Lakini hafla kadhaa za kijamii, sherehe, na mila pia uyajaza maisha yao. Mwanamke mwenye uwezo na uchaguliwa pekee kwa sifa, kama ambavyo mwanaume mwenye hekima na mpenda haki anavyojipatia heshima kwa wenzake. Katika sherehe za vikundi, wanawake na wanaume ufika kando, mara nyingi katika utaratibu na msafara wa kufurahisha, na kusalimiana kwa adabu na unyenyekevu wa kawaida. Utamaniwa na kuwa mfano wa kuigwa na vijana wote, mtu mzima wa kimaasai uangalia na kutumainia kipindi cha uzee sio wa kujitenga na kuhofu kuendelea bali wa kujihusisha katika maisha ya watu.’
-Tepilit Ole Saitoti
Kwa nakala zaidi zinazohusu kabila la kimaasai bofya hapa!