Mganga wa Tiba Asilia

Waganga wa Tiba Asili (WTA) na Wanasayansi: Kuondoa Pengo Katika Utafiti wa Kisasa wa Afya

Orodha ya Yaliyomo

Dawa za asili (DZA) nchini Tanzania

Kutambuliwa kwa Waganga wa Tiba Asili (WTA) kama watoa huduma za afya nchini Tanzania kulianza wakati wa wakoloni wa Ujerumani. Wakoloni hao, wakati wote waliwashuku WTA kama kama tishio kwa mfumo wao wa utawala na waliwahusisha na uchawi na kutostaarabika. Hata hivyo, baadhi ya wamisionari wakristo walikubali tiba asili kutoka kwa WTA katika huduma zao za kitabibu na walionyesha nia ya

Waganga na Wajerumani
Waganga na Wajerumani

kuzisoma. Kwa Kutambua umuhimu wa tiba asili, mwaka 1895, madaktari wa jeshi la Ujerumani walishauriwa rasmi kukusanya vielelezo vya mimea na kuzipeleka kwa uchunguzi wa kisayansi Ujerumani. Hadi kufikia 1907, dawa za asili ziliingizwa katika mfumo wa utunzaji wa afya wa wakati huo “Ujerumani Afrika Mashariki”. WTA katika Tanganyika walipewa vyeti vinavyoonyesha maeneo yao ya kufanyia kazi na magonjwa waliyotibu.

Licha ya kuanzishwa kwa Sheria ya uchawi na wakoloni wa Kiingereza mwaka 1929, WTA bado waliruhusiwa kufanya kazi katika jamii ambazo wazee wa jadi waliwaruhusu kufanya hivyo. Matumizi ya DZA hayakutambuliwa na Serikali ya Tanzania tangu uhuru hadi hapo Wizara ya Afya ilipotoa Sheria mpya ya Madaktari wa Tiba na Madaktari wa Meno ya mwaka 1968. Hadi sasa, inakadiriwa kuwa kuna zaidi ya WTA 75,000 kwa Tanzania Bara. Hivi sasa, inakadiriwa kuwa, angalau 60% ya Watanzania wakazi wa mijini na 80% ya wakazi wa vijijini wanategemea WTA kwa mahitaji yao ya msingi ya huduma za afya. Serikali imeonyesha kujitoa kwake kisiasa kukuza DZA na kwa sasa Sera ya Afya ya Tanzania inatambua DZA pamoja na mifumo mingine ya Tiba Mbadala (TM) ya afya. Utashi wa kisiasa wa serikali umeimarishwa zaidi na sheria iliyopitishwa na Bunge mwaka 2002 kuanzisha Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala.

Pengo lililopo kati ya waganga wa tiba asili na waganga wa tiba za kisayansi (WTS)  wakati wa kufanyia kazi mifumo ya DZA na ya Kawaida ya Huduma za Afya, ni sababu kuu inayosababisha kukosekana kwa maelewano labda ni kutokana na ukosefu wa lugha ya kawaida juu ya mtazamo wa vyanzo na usimamizi wa matatizo ya kiafya. Dawa za asili hazichukulii mtu kama mwili tu, lakini pia zinazingatia mazingira ya kijamii  yaliyo hai au yaliyokufa (mababu) na nguvu zisizoshikika za ulimwengu (roho na miungu). DZA huona ugonjwa / maradhi kama sio tu matokeo ya kutofanya kazi kwa kwa viungo kwa sababu zinazoonekana kama inavyoonekana na mwanasayansi / WTS, lakini pia inaweza kuwa ni kwa sababu ya “nguvu isiyoonekana”. Kwa hiyo, matibabu katika DZA hayatumii tu vitu vinavyoonekana bali pia rasilimali kutoka ‘’ulimwengu” au dunia isiyoonekana.

Mtaalamu wa mimea akiuza dawa za asili mkoani Shinyanga
Mtaalamu wa mimea akiuza dawa za asili mkoani Shinyanga

DZA zilikosa dhamira ya kisiasa na msaada, kwani kwa wakoloni zilionekana kuwa tishio. Kwa kuwa, DZA zinachukuliwa kuwa sehemu ya utamaduni wa Kiafrika, njia iliyotumiwa na wageni kupotosha mfumo huu wa huduma ya afya, ilileta kutokuaminiana au mzozo wa kimtazamo kati ya WTA na matabibu wa kimagharibi au wa kawaida. Zaidi ya hayo, dawa za asili zilikosa msimamo wa serikali na hivyo zilikosa mfumo wa sera na sheria. Mapungufu hayo hapo juu hayakuepukika kwa sababu, kidogo sana au wakati mwingine hakuna kilichojulikana kuhusu DZA na hakukuwa na mipango mahususi ya muda mrefu iliyosaidia ukuaji wake. Lakini, kwa sasa, watu wengi wanaelewa vizuri umuhimu wa DZA na idadi kubwa ya watu duniani hutumia DZA na bidhaa zitokanazo na mimea ya tiba zaidi ya hapo awali. Ni kupitia tu ushirikiano rasmi kati ya WTA na wanasayansi / WTS, kwamba mapungufu yaliyopo yanaweza kurekebishwa na kwa hiyo kutoa matumizi endelevu ya DZA kwa afya bora za watu wetu.

Kuziba mapengo/kuondoa tofauti

Jaribio lililofanywa na Wizara ya Afya (WYA) kutoa sheria mpya ya Madaktari wa Tiba na Madaktari wa Meno ya 1968 ilikuwa kwa wakati unaofaa kwa kubadilisha mawazo ya Watendaji wa Kawaida wa Afya kuelekea kwenye dawa za asili. Sheria lilithibitisha uwepo wa WTA na haki yao ya kufanya kazi Tanzania. Msimamo wa kisiasa wa serikali kukuza TZA umeelezewa wazi katika Sera ya Afya ya Tanzania ambayo iliundwa mwaka 1996 na Sera ya Tiba Asili na Tiba Mbadala na sheria za mwaka 2000, na 2002 kwa pamoja,  ambazo zote zinatambua jukumu la WTA na DZA katika mfumo wa huduma za afya nchini. Hatua kwa hatua, serikali iliruhusu utafiti wa kisayansi uliolenga kuunganisha DZA na mifumo ya afya ya Kawaida, kupitia kuanzishwa kwa Kitengo cha Utafiti wa Tiba Asili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1974. Kitengo hiki kilipandishwa hadhi kuwa Taasisi ya Tiba Asili (TTA) mwaka 1991. Idara za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) za mimea, Kemia, Sayansi ya Bahari na Microbiolojia zote zinahusika katika kufundisha lakini pia zinafanya utafiti wa bidhaa za asili. Ndani ya Wizara ya Afya, kitengo cha DZA kimekuwepo tangu mwaka 1989. Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu pia ilijiunga katika harakati hizo na kuanzisha idara ya utafiti wa dawa za asili mwaka 2002 ili kuimarisha mahitaji yaliyopo katika utafiti na maendeleo katika DZA. Kwa kutambua thamani ya maarifa ya asili, Taasisi na Wizara ya Afya, wamefanya kazi pamoja na mwishowe kuja na sera ya DZA tangu mwaka 2000.

Utafiti wa ushirikiano kati ya waganga wa tiba asili na madaktari (waganga wa tiba za kisayansi)

Kama washikadau wa huduma za afya, WTA kutoka nchi kadhaa, ukijumuisha na Tanzania, wameonyesha kujitoa kwao kupambana na VVU / UKIMWI. Jaribio shirikishi linaloendelea kati ya WTA na wanasayansi nchini Tanzania limeanzishwa kwa lengo la kutathmini usalama, ufanisi na sumu katika dawa za asili  zinazotumiwa na WTA katika matibabu kwa  wagonjwa wa VVU / UKIMWI. Uchambuzi makini wa maarifa ya WTA juu ya VVU / UKIMWI ulirekodiwa kupitia safu za semina na dodoso zilizopangwa uliwezesha Taasisi kuwatambua WTA wa kweli na wenye ujuzi wa juu wa VVU / UKIMWI.  Makubaliano rasmi yalifikiwa kupitia warsha za kielimu na kwa kuwashirikisha washirika wa kisheria kutoka pande zote mbili ambapo makubaliano yalifikiwa na mwaka 2005 angalau WTA saba wakishirikiana walitia saini Mkataba wa Makubaliano (MWM) na TTA. Maswala yanayohusu mwenendo wa maadili, usiri, usambazaji wa matokeo ya utafiti na Haki miliki (HM) yote yalizingatiwa ndani ya MWM zilizosainiwa. Njia hii ilisaidia TTA kutambua kwa urahisi waganga wa kweli wa ugonjwa kama VVU / UKIMWI na

Chuo kikuu cha mlimani - Dar es salaam
Chuo kikuu cha mlimani – Dar es salaam

imetoa mafunzo ya kuheshimiana na kuaminiana kwa watendaji kutoka katika mifumo yote ya huduma za afya. Hivyo,  idadi kubwa ya dawa kutoka kwenye mimea kadhaa ya dawa inayotumiwa na WTA katika tiba ya VVU / UKIMWI imerekodiwa. Uchambuzi wa matokeo ya utafiti ulifafanua zaidi kwamba dawa hizi ni salama, na zinafaa dhidi ya maambukizo mengi ya hatua ya pili yanayohusiana na VVU / UKIMWI, ukijumuisha kuhara, kikohozi cha mara kwa mara, homa, Vidonda/maambukizi mdomoni na shida za ngozi. Utafiti uliofanyika kupitia machapisho mbalimbali, umeonyesha uhusiano mzuri kati ya mimea ya tiba inayotumiwa na WTA wanaoshirikiana, ambayo inaonyesha uchochezi katika kinga ya mwili na kuzuia maambukizi ya virusi na kurekodiwa kwa taarifa za utafiti wa tiba asili za mimea ile ile ya dawa iliyoripotiwa kutoka sehemu zingine duniani. Mwelekeo huu unahimiza utafiti zaidi juu ya mimea ya tiba inchini Tanzania kwa uwezo wao katika tiba ya VVU / UKIMWI.

Mradi mwingine muhimu wa DZA na VVU / UKIMWI unaoendeshwa katika hali ya kuaminiana kati ya WTS ni Kikundi kazi cha UKIMWI Tanga (KKCUT). Ripoti za KKCUT zilionyesha kuwa WTA 120 walipatiwa mafunzo juu ya utoaji ushauri na utunzaji wa waathirika wa UKIMWI, kukuza matumizi ya kondomu na mabadiliko ya tabia katika jamii. Kazi mahususi za vitendo zikijumuisha utunzaji wa nyumbani, ilikuwa ni sehemu ya programu. Vikao vya kielimu kwa WTS na WTA viliandaliwa na zaidi ya yote, rufaa zote za wagonjwa zilishughulikiwa kwenda na kutoka pande zote mbili.

Mtandao wa mimea ya tiba na dawa za Asili

Mtandao ulizinduliwa Arusha, Tanzania Novemba 2003. Washirika wanaoshirikiana ni pamoja na Maabara ya Utafiti wa Tiba asili ya Magonjwa (Uganda), Taasisi ya Tiba Asili ya Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya ya Muhimbili (Tanzania) na Makumbusho ya Kitaifa ya Kenya. Mradi huu una lengo la kuanzisha jukwaa shirikishi la mpango ambalo linatoa fursa kwa wadau wote kushirikiana taarifa na uzoefu juu ya shughuli zao, kuoanisha njia zao na mbinu, na kufanya kazi pamoja kukuza miradi ambayo inakuza uhifadhi na uendelevu wake, usalama, na matumizi mazuri ya mimea ya tiba na bidhaa za mitishamba, na pia ujumuishaji wa TZA katika huduma za afya ya umma.  kufikia mwisho, mradi unazingatia: 1) tathmini ya shughuli za utafiti na mifumo ya sera ili kujua mapungufu na vipaumbele katika ngazi za kitaifa na zilizo chini ya mikoa; 2) kuimarisha uwezo wa utafiti na kuoanisha njia na mbinu za watafiti; 3) kukuza maendeleo ya miradi ya ushirika ya kikanda ili iweze kufikia idadi sahihi ya watu kwenye miradi ya utafiti yenye changamoto / “mkakati”,  na kupunguza kurudia rudia kwa

Dawa za asili zikiwa kwenye maonyesho
Dawa za asili zikiwa kwenye maonyesho

nguvu kazi au jitihada zinazofanywa; 4) kuimarisha uwezo wa vyama vya waganga wa jadi na ushirikiano wao na wadau wengine (wafanyikazi wa afya, watafiti, watunga sera); 5) kuchangia katika ukuzaji / urekebishaji wa sera  na mifumo inayofaa; na 6) kuanzisha michakato ya kuziba pengo kati ya watafiti, jamii na watunga sera, na kusambaza matokeo ya utafiti kwenye TZA na mimea ya tiba kwa Afrika Mashariki.

Maono na mfumo wa mkakati wa uhifadhi, usimamizi na matumizi ya bioanuwai katika Afrika Mashariki umeshatengenezwa. Ukuzaji wa mapendekezo ya Mradi ya Kikanda katika maeneo ya afya ya binadamu, mabadiliko ya ikolojia na afya, utengenezaji wa utajiri na ujengaji uwezo uko katika hatua ya juu ya maandalizi. Katika miaka 3 iliyopita, Mtandao ulifanya shughuli kadhaa za kuimarisha uwezo wa WTA na Vyama vya  WTA na ushirikiano wao na wadau wengine. Mtandao uliandaa semina kwa ajili ya kuandaa kanuni juu ya somo la utengenezaji wa madawa (materia medica) kwa utekelezaji wa Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala ya 2002. WTA na vyama vya WTA, ambao ni walinzi / wamiliki wa maarifa asilia ya matibabu ya mimea ya dawa, walihusika kikamilifu katika mchakato wa kutengeneza kanuni ambazo zitasimamia utendaji wao. Kupitia Mtandao huu, Baraza la  Asili na Tiba Mbadala Tanzania lilifanya warsha kadhaa za utangulizi juu ya utekelezaji wa Sheria ya mwaka 2002 Tanzania Bara ili kuhakikisha kwamba  WTA na vyama vyao wanaelewa Sheria hiyo.

Vivyo hivyo, zana za kufundishia / mwongozo wa WTS zinatengenezwa na Shirika la Afya duniani (WHO / AFRO) kuwaelekeza WTA juu ya utendaji kazi wa tiba asili. Inahitajika kutoa mwelekeo kwa WTA ili waweze kupata uelewa kama watendaji katika mfumo wa kawaida wa huduma ya afya. Lengo la programu ya mafunzo ya WTS ni kuongeza ufahamu wao juu ya jukumu muhimu linalochukuliwa kwa ufanisi na WTA katika kukuza na kutoa huduma ya msingi ya afya kwa asilimia 80 ya watu Afrika ambao hutembelea WTA mara kwa mara kwa mahitaji yao ya huduma za afya, na kuhamasisha WTS kushiriki katika shughuli za utafiti wa dawa za asili. 

Hitimisho

Mapitio ya kimtazamo ya kimataifa, kikanda na nchi juu ya DZA yameonesha kutambuliwa na jukumu ambalo WTA wanatimiza katika mfumo wa afya wa tiba asili. Tiba hizi zimeonyesha  kukubalika kitamaduni kwa watu wengi na zina uwezo wa kutatua shida za afya za watu kutoka katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea hata katika enzi hii za maendeleo ya kiteknolojia katika mfumo wa kisasa wa huduma ya afya. Zaidi ya hayo, biashara ya mimea ya tiba na ya kunukia imekadiriwa kama njia endelevu ya kupunguza umaskini na bado ina thamani ya ziada katika masuala la bioanuwai na malengo ya uhifadhi. Utambuzi wa  DZA ulimwenguni umesaidia kupunguza mapungufu yaliyopo kati ya WTS na WTA. Vyombo vya udhibiti vilivyopo, pamoja na Shirika la Afya duniani  (WHO)  na Umoja wa Afrika) (AU) vinahimiza mifumo ya kisheria iliyopo kulinda, kukuza na kuhakikisha matumizi ya busara ya DZA kupitia utafiti wa pamoja na elimu kwa watendaji wote wa mifumo miwili ya matibabu. Kwa kuongezea, sera na mfumo wa kisheria ambazo zinapaswa kudhibiti ushirikiano kati ya WTS na WTA,  zinapaswa kuzingatia kugawana kwa usawa faida zinazopatikana kutokana na juhudi za ushirikiano na HM. Nchini Tanzania, serikali imeongoza kutambuliwa kwa WTA kupitia Wizara ya Afya na jukumu lao kama wadau katika Sera ya Afya ya Tanzania. Mfumo wa kisheria umewekwa kupitia Sera ya Tiba Asili na Tiba Mbadala na Sheria ya mwaka 2000, na 2002, kwa pamoja, na miundombinu kadhaa wa kadha ya utafiti katika dawa za asili imeanzishwa. WTA wanazidi kujipanga kwa vyama na miradi inayoendelea ya kushirikiana ambayo hadi sasa imepunguza pengo kati ya WTA na WTS.

Mapendekezo na nini kinafuata

Kwa kuzingatia kile kilichoelezwa hapo juu, kuhusu pengo kati ya WTA na watendaji wa tiba za kibaolojia / watafiti katika tiba za kisasa za afya nchini Tanzania, sifa zifuatayo zinapaswa kupendekezwa. Kwanza, kuna haja ya kuimarisha na kuongeza ushirikiano uliopo na mafunzo ili kuruhusu kubadilishana uzoefu kati ya WTA na watendaji wa tiba za kibaolojia / watafiti wanaotumia itifaki na miongozo iliyopo ya Shirika la Afya duniani (WHO / AFRO). Kulingana na mapendekezo ya  Shirika la Afya Duniani (WHO), shughuli kama hizi zinapaswa kuzingatia magonjwa ya kipaumbele kama VVU / UKIMWI, malaria, kifua kikuu, ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu, nk. Pili, kuna haja ya kuanzisha jukwaa la kitaifa au mfumo ambao utaleta uhusiano wa karibu wa kufanya kazi kati ya wanasayansi / WTS na WTA, vyama vya WTA, ikiwezekana chama cha kitaifa cha WTA. Chombo hiki kinatarajiwa kudhibiti, pamoja na mambo mengine, masuala ya kugawana faida na HM. Mwisho, lazima kuwe na juhudi za makusudi zinazoelekezwa katika kuongeza uelewa na utetezi kwa dawa za asili kwa umma, watunga sera, watafiti, WTA na watumiaji wa mwisho kupitia vyombo vya habari, vipindi mahususi vya redio / televisheni, vipeperushi na vifaa vingine vya elimu ili kuhakikisha huduma mbili za mifumo ya afya zinapata njia ya kusaidiana badala ya kushindana.

Kwa nakala zaidi zinazohusu tiba za asili bofya hapa!