Mganga wa Kienyeji

Maamuzi ya Unguja Kusajili Waganga wa Kienyeji

Orodha ya Yaliyomo

Mji wa Unguja, Zanzibar – Waganga wa kienyeji wa Unguja na mikoba yao ya madawa, maandiko matakatifu na matibabu ya kusuguwa mwili (massage) wanasajiliwa na mamlaka kwa nia ya kuratibu watendaji wanaotibu kila kitu kuanzia msongo wa mawazo mpaka ngiri.

Wameshasajiliwa takriban waganga 340 kwani Unguja, ambayo ni sehemu ya nchi za Afrika Mashariki Tanzania, ilipitisha Sheria ya Dawa Mbadala za Kienyeji mwaka 2009.

Inakadiriwa, kuna watabibu zaidi ya 2000 au waganga wa kienyeji, wanaotumaini kujisajili, alisema Hassan Combo Msajili wa Serikali katika baraza linalowarekodi.

Maoni ya mganga wa kienyeji Mwanahija

Mganga Mwanahija Mzee akimsuguwa mwili mtoto wa miezi mitatu
Mganga Mwanahija Mzee akimsuguwa mwili mtoto wa miezi mitatu

Mganga wa Kienyeji Bi Mwanahija Mzee ameshajisajili. Anawahudumia wagonjwa katika kliniki yake yenye wagonjwa wengi, ambapo wakina mama hupanga foleni mapema jua la asubuhi linapotoka wakiwa wamewakumbatia watoto wao wagonjwa.

Familia moja inatafuta ahueni kwa mtoto wao anaesumbuliwa na ngiri ya kitovu, wanaogopa kuwa wakimpeleka mtoto hospitalini akapasuliwe, atakufa. Mwanamke mjamzito ambaye mimba zimekuwa zikitoka mara kwa mara kaenda kupata uhakikisho, kuwa mitishamba na maombi yatamuokoa mtoto wake.

“Watu wanakuja hapa kwa sababu kweli ninawasaidia. Nimekutana na wagonjwa wengi ambao kwanza walienda mahospitalini na hawakupata msaada au walipewa madawa ila hayakufanya kazi” alisema Mwanahija Said 56.

“Hii ni kazi yangu ya siku sita kwa wiki kwa zaidi ya miaka ishirini hivyo naifanya vizuri sana, najua zaidi yao. Wagonjwa wanaokuja kwangu hawafi”

Wazazi wa Mwanahija Mzee nao walikuwa waganga wa kienyeji Unguja, kisiwa katika Bahari ya Hindi.

Masharti ya Usajili

Ili Kusajiliwa, mganga angalau anatakiwa awe na miaka 18, uzoefu wa miaka mitatu na barua ya mapendekezo kutoka kwa mganga wa kienyeji aliefundishwa. Baraza la wajumbe 11 linalojumuisha wahudumu katika uzazi, matabibu walioheshimika, wazee wa kijiji na wanasheria wanayaidhinisha maombi kila mwezi.

Wakati Serikali haijaribu kuwalazimisha waganga njia za kazi, inajaribu kufanya kazi nao katika kudhibiti ubora,alisema msajili wa Serikali Combo, kwa mfano kuhakikisha mimea inayotumiwa kwa dawa ni ya kiwango sawa.

Kundi linalowezeshwa na ofisi ya msajili linawawaunganisha madaktari na waganga wa kienyeji kuwapa elimu ya utabibu kwa magonjwa maalum kama shinikizo la juu la damu, kisukari na uja uzito. Waganga wanawashirikisha madaktari kwa kuwapa taarifa za takwimu na mahitaji ya wagonjwa, alisema.

Nguvu za mizimu

Baadhi ya waganga wanatumia mimea.Wengine wanatumia maandiko matakatifu ya Kiislamu, Kurani. Wengi wanatumia zote mbili. Imani

Sheikh akijaribu kumwamsha mwanamke kwa kumwagia maji kwenye shingo - Zanzibar
Sheikh akijaribu kumwamsha mwanamke kwa kumwagia maji kwenye shingo – Zanzibar

katika mizimu kama majini inatumika sana.

Baadhi ya waganga, kama Haji Mrisho, wanatoa baraka hasa kwa wakina mama wajawazito kuwakinga vichanga vyao ambavyo havijazaliwa visikumbwe na majini. Wengine kama mashekhe katika kliniki ya Mitishamba ya Shifaa wanasoma Kurani kuyatoa majini yanayolaumiwa kwa magonjwa mbalimbali.

Mwanahija Mzee anatumia michanganyiko ya kusuguwa mwili (massage kwa kiingereza), madawa kutoka kwa mizizi, mimea na matawi na aya za Kurani, ambayo yanaweza kuandikwa katika sahani kwa kutumia rangi nyekundu ya chakula. Kisha sahani inasuuzwa na maji kunywewa kama sehemu ya dawa.

Maoni ya Wagonjwa

Wagonjwa kama Fatma Hamad wanasema wanawaamini waganga wa kienyeji kuliko huduma za afya kama hospitali za serikali zilizozidiwa na watu, zinazofadhiliwa chini ya mahitaji, ambapo wengi wanahisi maradhi yao hayatibiwi vizuri.

Fatawi Haji Hafidh, meneja katika Hospitali ya Makunduchi, hospitali ya pili kwa ukubwa inayoendeshwa na serikali katika kisiwa kikuu cha  Unguja, anasema madaktari na wauguzi wanaweza wasipate muda wa kuwaona wagonjwa au vifaa vya kiuchunguzi.

Mjamzito akihudumiwa na daktari hospitali
Mjamzito akihudumiwa na daktari hospitalini

Wagonjwa nao wanaweza kushindwa kumudu bei za madawa yalioagizwa, au wanaweza kuacha kuzitumia kabla hawajamaliza kipindi chake,  hali inayopelekea kujirudia na kuongezeka kwa tuhuma kwa hospitali zinazoendeshwa na Serikali, alisema.

Wengi wanaamini majini ndio tatizo tu.

Fatma Hamad alimpeleka binti wake wa miaka miwili hospitali baada ya mguu mmojawapo wa kichanga huyo kupooza kwa homa kali. Waliposhindwa kupata tatizo kupitia miyonzi ya X, hospitali wakapendekeza atafute mganga wa kienyeji.

Mwanahija Mzee akamkanda huyo mtoto na baada ya kumwona mara kadhaa, uwezo wake kutembeza mguu ukaimarika taratibu. Mama yake ameichukua hii kama uthibitisho kwamba ugonjwa ulisababishwa na kukumbwa na majini, “lazima ni jini kama alivosema Bi Mwanahija” alisema Hamad.

Kwa nakala zaidi zinazohusu tiba za asili bofya hapa!