Mtoto wa Tabibu na Mfalme wa Nyoka

Mtoto wa Tabibu na Mfalme wa Nyoka

Orodha ya Yaliyomo

Sehemu ya kwanza

Kulikuwa na tabibu msomi, alikufa na kumwacha mke wake na mtoto wa kiume, alipokuwa mkubwa mkewe alimwita yule mtoto jina kulingana na mapenzi ya baba yake, Hassee′boo Kareem′ Ed Deen′.

Mtoto alipokwenda shule, na kujifunza kusoma, mama yake alimpeleka kwa fundi mshona nguo ajifunze hio biashara lakini hakufanikiwa kujifunza. Basi baada ya hapo, akapelekwa kwa mhunzi, akashindwa kujifunza biashara hii pia. Baada ya hapo akajaribu biashara zingine nyingi lakini hakuweza kujifunza biashara yoyote. Hatimae mama yake akasema, “Basi kaa nyumbani kwa muda” hili likaonekana kumfaa.

Siku moja alimuuliza mama yake, baba yake alifanya biashara gani, akamwambia alikuwa tabibu mkubwa Sana.

“Vikowapi vitabu vyake?” akauliza.

“Ni muda mrefu tangu nimeviona” akajibu mama yake, “lakini nadhani viko hapo nyuma. Angalia uone”

Kwa hio akavitafutatafuta kidogo mwishowe akavipata, ila vilikuwa vimeharibiwa vibaya na wadudu, akaambulia kidogo kutoka kwenye vitabu hivyo.

Majirani wanne wakamfata mama yake na kumwambia, “Mwache mwanao aje na sisi twende msituni tukakate kuni.” Ilikuwa ni biashara yao kukata kuni, kupakia kwenye punda, na kuuza mjini kwa ajili ya kukoka moto.

“Sawa” akasema, “kesho, ntamnunulia punda, halafu mtaenda naye.”

Kwa hiyo kesho yake, Hasee’boo, na punda wake,aliondoka na wale watu wanne, wakafanya kazi kwa bidii, na kupata pesa nyingi sana siku hio. Hili likaendelea kwa siku sita, lakini siku ya saba,mvua kubwa ilinyesha,ikabidi wakae chini ya miamba ili wasiloe.

Hassee′boo akawa amekaa peke yake kwa pembeni, na, kwa kuwa hakuwa na chochote cha kufanya, akachukua jiwe na kuanza kugongagonga chini. Akashangazwa kusikia sauti ya utupu inatoka ardhini na kuwaita wenzake akisema, “Inaelekea kuna shimo hapa chini.”

Watu wakichimba shimo
Walihamuwa kuchimba shimo

Walipomsikia alipogongagonga tena, wakaamua wachimbe ili wajue ni nini kinasababisha sauti hio ya utupu; hawakuchimba mbali sana kabla ya kukutana na shimo kubwa, kama kisima, ambalo lilikuwa limejaa asali mpaka juu.

Baada ya hapo hawakukata kuni tena, nguvu zao wakazielekeza kuvuna asali na kuiuza.

Kwa nia ya kuvuna asali haraka iwezekanavyo, walimwambia Hassee’boo aingie kwenye shimo ili akavune asali, wao wakiiweka kwenye vyombo na kupeleka mjini kuiuza. Walifanya kazi kwa siku tatu wakitengeneza pesa nyingi sana.

Mwishowe kukawa na asali ndogo imebakia kwenye shimo, wakamwambia aikwangue wao wanaenda kuchukua kamba ya kumvutia nje.

Lakini badala ya kuleta kamba, wakaamua kumuacha kwenye shimo, ili wajigawie pesa wao wenyewe. Alipokuwa ameshakusanya pamoja asali yote iliobaki, alipoita ili apewe kamba, hakupata jibu, alipokaa peke yake kwa siku tatu kwenye shimo akajua pasi na shaka kuwa wenzie wamemuacha.

Wale watu wanne walienda kwa mama yake wakamwambia walitengana msituni, wakamsikia simba anaguruma, na hawakumuona tena mwanawe wala punda wake.

Mama yake, alilia sana, wale majirani wanne wakatia mfukoni sehemu ya mgao wa mtoto wake.

Tukirudi kwa Hassee’boo.

Alipoteza muda akitembeatembea mle shimoni, akiwaza mwisho wake utakuaje, alikula mabaki ya asali, kulala kidogo, kukaa na kufikiri.

Nge
Nge

Siku ya nne, akiwa katika mazingira haya, akamwona nge kadondoka chini, mkubwa, akamuua.

Ghafla akafikiria, “Huyu nge katokea wapi? Lazima kuna shimo mahala.Vyovyote vile nitalitafuta”

Kwa hio akatafuta mpaka alipoona mwanga katika ufa mdogo; akachukua kisu chake, akachimbuachimbua, mpaka alipotengenza shimo kubwa ambalo angeweza kupita; akatoka nje, akatokea sehemu ambayo hjawahi kupaona tena.

Akaona njia, akaifata mpaka alipofika kwenye nyumba kubwa sana, ambayo mlango wake ulikuwa haujafungwa.Akaingia ndani, akaona milango ya dhahabu, kufuli za dhahabu, funguo za lulu,viti vizuri vimepambwa kwa vito vya dhamani,na katika chumba cha mapokezi, akaona kiti cha kupumzikia kimefunikwa kwa utandazo mzuri,ambapo akakaa na kulala.

Akajikuta kanyanyuliwa kutoka kwenye kiti cha kupumzikia na kuwekwa kwenye kiti kingine. “Msimdhuru; mwamsheni polepole,” alipofungua macho yake, akajikuta kazungukwa na nyoka wengi, mmoja wao amevalia rangi nzuri za kifalme.

“Hujambo!” akasema kwa nguvu, “Wewe ni nani?”

“Mimi ni Sulta′nee Waa′ Neeo′ka, mfalme wa nyoka, na hii ni nyumba yangu. Wewe ni nani?”

 

Sehemu ya pili

“Mimi ni Hassee’boo Kareem Ed Deen.”

“Unatoka wapi?”

“Sijui ninatoka wapi wala nina kwenda wapi”

“Basi, usijisumbue kwa sasa, hebu tule; nadhani una njaa, mimi nna njaa”

Kisha mfalme akatoa amri na baadhi ya nyoka wakaleta matunda mazuri sana, wakala, wakanywa na kuongea.

Walipomaliza maongezi, mfalme akatamani kusikia kisa cha Hasseeboo; akamwambia yote yaliotokea, kisha akoamba kusikia kisa cha mwenyeji wake.

“Basi” akasema mfalme wa nyoka, “kisa changu ni kirefu, ila utakisikia. Miaka mingi iliopita, niliiacha hii sehemu na kwenda kuishi kwenye milima ya Al Kaaf’, ili kubadili upepo. Siku mmoja nikamuona mtu nisiemjua anakuja nikamwambia, ‘Unatoka wapi’ akasema, ‘ninatangatanga nyikani.’ ‘Wewe ni mtoto wa nani?’ nikauliza, ‘Jina langu ni Bolookee′a. Baba yangu alikuwa sultani; alipokufa nilifungua

Nabii
Nabii

kisanduku,ndani nikakiona kifuko, ambacho ndani kilikuwa na kisanduku kidogo cha shaba; nilipokifungua, ndani kulikuwa na maandiko yaliofungwa kwa kipande cha nguo ya sufi , na yote ilikuwa ni sifa ya nabii fulani. Alielezewa kama mtu mzuri na wa ajabu sana, nikawa na tamaa sana ya kumuona; lakini nilipofanya uchunguzi, nikaambiwa bado hajazaliwa. Basi nikaamua nitatangatanga mpaka ntakapomuona. Nikaondoka mjini kwetu, nikaacha mali zangu zote, nikawa natangatanga, lakini bado sijamuona huyo nabii.’

“Nikamwambia, ‘Unategemea utampata wapi, kama bado hajazaliwa? Labda kama ungekuwa na maji ya joka, pengine unaweza kuendelea kuishi mpaka umpate. Lakini hamna faida kuliongelea hili; maji ya joka yako mbali sana.’

‘“Basi” akasema, ‘Kwa heri, lazima niendelee kutangatanga.’ Nikamuaga akaende zake.

“Sasa, mtu huyo alipotangatanga mpaka alipofika Misri, alikutana na mtu mwingine ambaye alimuuliza, ‘Wewe ni nani?’

‘“Mimi ni Boolokea, wewe ni nani?’

‘“Ninaitwa Al Faan. Unaenda wapi?’

‘“Nimeacha nyumba yangu, mali zangu namtafuta nabii.’

‘“H’m” akasema Al Faan; ‘Naweza kukuelekeza kazi bora kuliko kumtafuta mtu ambaye hajazaliwa bado. Twende tukamtafute mfalme wa nyoka atatupatia dawa. Kisha tutaenda kwa Mfalme Suleiman tukatafute pete zake, tutaweza kuwatumikisha majini na kuyaamrisha yatufanyie chochote tunachotaka.’

“Bolookeea akasema, ‘Nimemwona mfalme wa nyoka katika milima ya Al Kaaf.’

“Sawa” akasema Bolookeea, ‘twende zetu.’

Al Faan aliitaka pete ya Suleiman ili aweze kuwa mwana mazingaombwe mkubwa na kuyamiliki majini na ndege wa angani, wakati alichotaka Bolookeea ni kuweza kumuona nabii.

Walivokuwa wakienda, Al Faan akamwambia Bolookeea, ‘Tutengeneze kizimba ili tumvutie mfalme wa nyoka aje aingie; kisha tutaufunga mlango na kumbeba juu kwa juu.’

‘“Sawa’ akasema Bolookeea.

Wakatengeneza kizimba na mle ndani wakaweka kikombe cha maziwa na kikombe cha divai, wakatuletea Al Kaaf; na mimi, kama mjinga, nikaingia ndani, nikanywa divai yote nikalewa. Kisha wakaufunga na kuukaza mlango wakaondoka na mimi.

“Akili ziliponirudia nikajikuta kwenya kizimba, nimebebwa na Bolookea, nikasema, ‘Wana wa Adamu sio wazuri. Mnataka nini kutoka kwangu?’ Wakanijibu. ‘Tunataka dawa tuweke kwenye miguu yetu, ili tuweze kutembea kwenye maji katika safari yetu pale patakapohitajika.’ ‘Basi’ nikasema, ‘Nendeni tu.’

“Tulienda mpaka tulipofika sehemu ina miti minigi sana; na miti hio iliponiona ikasema, ‘Mimi ni dawa ya hiki,’ ‘Mimi ni dawa ya kile,’ ‘Mimi ni dawa ya kichwa,’ ‘Mimi ni dawa ya miguu,’ mti mmoja ukasema, ‘Yeyote atakaeweka dawa yangu kwenye miguu yake, atatembea kwenye ya maji.’

“Nilipowaambia wale watu wakasema, ‘Hicho ndicho tunachotaka’ wakaona ni kitu cha manufaa sana.

“Kisha wakanirudisha milimani na kuniacha huru, tukaachana.”

“Waiponiacha, waliendelea na njia zao mpaka walipofika baharini, wakaweka ile dawa na kutembea. Zikapita siku nyingi, mpaka walipokaribia kasri la Mfalme Suleiman, ambapo walisubiri mpaka Al Faan alipoziandaa dawa zake.

“Walipofika katika sehemu ya Mfalme Suleiman, alikuwa amelala, alikuwa anachungwa na jini, mkono wake kaulaza kifuani kwake, na ile pete iko kidoleni kwake.

“Bolookeea alipomkaribia jini moja likamwambia, ‘Unaenda wapi?’ Naye akajibu, ‘Niko hapa na Al Faan; ataichukua hio pete.’ ‘Toka hapa’ jini likasema; ‘toka kabisa. Huyo mtu atakufa’

Sehemu ya tatu

Al Faan alipomaliza maandalizi yake, alimwambia Bolookeea, ‘Nisubiri hapa.’ Kisha akenda kuichukua ile pete, ambapo mlio mkubwa ulitokea, akatupwa kwa nguvu zisizoonekana umbali wa kutosha.

“Akajinyanyua huku akiziamini nguvu za madawa yake, akaifata ile pete tena, pumzi yenye nguvu ilimpuliza na akateketea na kuwa majivu muda ule ule.

“Bolookea alipokuwa anaangalia haya yote sauti ikasema ‘Nenda zako; huyu kiumbe asiofaa kashakufa.’ Akarudi; alipofika kwenye ziwa tena, akaweka dawa miguuni mwake, na kupita, akaendelea kutangatangaa kwa miaka mingi.

“Siku moja asubuhi alimwona mtu kakaa chini akamwambia, ‘Habari za asubuhi,’ yule mtu akamjibu.

Kisha Bolookeea akamuuliza, ‘Wewe ni nani?’ nae akamjibu ‘Jina langu ni Jan Shah. Wewe ni nani?’ Kwa hio Bolookeea akamwambia yeye ni nani na kumwomba amweleze historia yake. Huyo mtu, alikuwa akilia na kutabasamu mara kwa mara, akasisitiza kukisikia kisa cha Bolookeea kwanza. Baada ya kukisikia akasema;

“Sawa ukae chini, na nitakueleza kisa changu chote mwanzo mpaka mwisho. Jina langu ni Jan Shah. Baba yangu ni Tooeegha′mus sultani maarufu. Kila siku alikuwa akienda msituni kuwinda wanyama; siku moja nikamwambia, “Baba naomba niende na wewe msituni leo,” lakini akamwambia, “Ubaki nyumbani” “Panakufaa hapa.” Nikalia sana kwa uchungu, kwa kuwa nilikuwa mwanae wa pekee, kipenzi chake, hakuweza kuyavumilia machozi yangu, akasema, “Sawa basi, tutaenda. Usilie”

‘“Ndipo tukaenda msituni, tulienda na wahudumu wengi; tulipofika pahala, tulikula na kunywa, halafu kila mmoja akaenda kuwinda.

‘“Mimi na watumwa wangu saba tulienda mpaka tulipomuoana swala mmoja mzuri, tukamkimbiza mpaka baharini lakini hatukumkamata. Swala alipoingia kwenye maji, mimi na watumwa wangu wanne tukachukua mashua, wale wengine watatu wakarudi kwa baba yangu, tukamfukuzia swala huyo mpaka ufukwe wa bahari ukawa hauonekani, tukamkamata na kumuua. Ghafla upepo mkali ukaanza kuvuma tukapoteza njia yetu.

‘“Wale watumwa watatu walipofika kwa baba yangu, akawauliza, “Yuko wapi bwana wenu? Wakamueleza kuhusu yule swala na mashua. Akalia, “Mwanangu kapotea! Mwanangu kapotea!” akarudi mjini na kunililia kama nimekufa.

‘“Baada ya muda tukatokea kwenye kisiwa kimoja kilichokuwa na ndege wengi. Tukapata matunda na maji, tukala tukanywa, na usiku tukapanda kwenye miti tukalala mpaka asubuhi.

‘“Kisha tukaenda na mashua mpaka kisiwa cha pili, na, tulivoona hamna mtu hapo, tukakusanya matunda, tukala, tukanywa na kupanda kwenye miti kama awali. Kipindi cha usiku, tulisikia wanyama wakilia na kupiga kelele karibu yetu.

‘“Asubuhi, tukaondoka mapema iwezekanavyo, tukaja katika kisiwa cha tatu. Tukiwa tunatafuta chakula, tukauona mti una mtunda mengi mmekundu yanafanana na matufaha yenye michirizi, tulivokuwa tunataka kuanza kuyachuma, tukasikia sauti inasema, “Msiuguse huo mti: mti huo ni wa mfalme.” Usiku ulivokaribia baadhi ya nyani wakaja, ambao ilielekea walikuwa wameridhia kutuona, wakatuletea matunda yote tuliokula.

‘“Kwa sasa, nikamsikia mmoja akisema, “Tumfanye huyu awe Sultani wetu.” Mwingine akasema, “Wa kazi gani? Wote watatukimbia asubuhi.” Lakini wa tatu akasema, “Sio kama tukiivunja mashua yao.” Kweli kabisa, tulivoanza kuondoka asubuhi, mashua yetu ilikuwa limevunjwa vipandevipande. kwahiyo hakukuwa na lingine ila kukaa hapo na kuburudishwa na nyani hao, ambao iliekea walitupenda sana.

‘“Siku moja nilipokuwa natembeatembea, nilifika katika nyumba kubwa ya mawe iliokuwa imeandikwa pembeni hivi, “Mtu yeyote atakayekuja katika kisiwa hiki, atapata tabu sana kuondoka, sababu nyani wanataka wampate mtu awe mfalme wao. Akitafuta njia ya kutoroka, atafikiri hakuna njia; lakiani kuna njia moja ya kutokea, ambayo iko kaskazini. Ukienda usawa huo, utakutana na nyika kubwa, amabamo kuna simba, chui na nyoka.Lazima upigane nao wote; ukiwashinda ndipo utakapoweza kwenda mbele.Utakuja tena kwenye nyika kubwa, ambayo ina siafu wakubwa usawa wa mbwa; meno yao ni kama ya mbwa, na ni wakali sana. Ni lazima kupigana na hawa nao, ukiwashinda, hakuna kizuizi chochote kingine njiani.”

‘“Nikawashirikisha wasaidizi wangu kuhusu hii taarifa, na tukufikia uamuzi ya kwamba, kwa kuwa tunaweza kufa, vyovyote vile, ni vyema tuyahatarishe maisha yetu ili kuutafuta uhuru wetu.

‘“Kwa kuwa wote tulikuwa na silaha, tuliondoka; tukaja katika nyika ya kwanza, tukapigana, na wasaidizi wangu wawili wakauwawa. Tukaenda kwenye nyika ya pili, tukapigana tena; wale wasaidizi wangu wengine wawili wakauwawa nikatoroka peke yangu.

‘“Baada ya hapo nikatangatanga kwa siku nyingi, nikiishi kwa chochote nlichopata, mpaka hatimae nikatokea katika mji, nilipokaa kwa muda kidogo, nikitafuta kazi lakini sikupata.

‘“Siku moja, alinifata mtu akasema,”Unatafuta kazi?” “Natafuta ndio” nikasema, “Twende zetu basi” akasema huyo mtu; tukaenda nyumbani

Nilimtisha na kumfukuza
Nilimtisha na kumfukuza

kwake.

“Tulipofika nyumbani kwake akatoa ngozi ya ngamia na kusema, “nitakuweka ndani mwa ngozi hii, na ndege mkubwa atakubeba mpaka kwenye kilele cha mlima kule. Akikufikisha hapo, ataichana hii ngozi kutoka kwako, kisha itakubidi umfukuze halafu uzisukume chini vito vya thamani utakazozipata huko. Ukishazisukuma zote chini, nitakushusha kutoka mlimani.”

‘“Kwahiyo akanitia kwenye ngozi; ndege akanibeba mpaka kileleni mwa mlima, na akawa anataka kuanza kunila, ndipo nikaruka, nikamtishia akaondoka, nikasukuma chini vito vingi sana. Kisha nikamwita yule mtu aniteremshe mlimani, ila hakunijibu, akaondoka.

‘“Nikakata tamaa na nafsi yangu kama mfu, lakini nilipokua nahangaika,hatimae,baada ya siku nyingi kuwa zimepita katika msitu mkubwa, nikaja katika nyumba iliokuwa peke yake, kikongwe aliekuwa anaishi humo akanipatia chakula na kinywaji nikazinduka.

‘“Nikabaki hapo kwa muda mrefu sana, na huyo kikongwe alinipenda sana kama vile nilikuwa mtoto wake.

Sehemu ya Nne

‘“Siku moja kikongwe huyo alienda zake, na aknipatia funguo, akaniambia naweza kufungua milango yote kasoro mmoja alienionyesha.

‘“Alipoondoka, bila shaka huo ndio ukawa mlango wa kwanza kwa mimi kuufungua. Nikaona bustani kubwa ambamo kulikuwa na mkondo unapita. Kisha vikashuka videge vitatu vikakaa kando kando ya huo mkondo. Hapo hapo wakabadilika wakawa wanawake watatu warembo sana. Walipomaliza kuoga, wakavaa nguo zao, na, nilipokuwa naendelea kuwaangalia, wakabadilika wakawa ndege na wakaondoka zao.

‘“Nikaufunga mlango na kwenda zangu ila hamu ya kula nikawa sina, na nikaranda randa huku na kule. Yule mzee aliporudi, aliona kuna kitu hakijakaa sawa kwangu, na akaniuliza kuna nini. Nikamwelezea nimewaona wale wana wali na nimetokea kumpenda sana mmoja wapo,na kama sitamuoa ni heri nife.

‘“Yule mzee akaniambia hitaji langu haliwezi kutimia. Akaniambia wale viumbe watatu ni mabinti wa sultani wa majini, na nyumbani kwao ni safari ya miaka mitatu kutoka pale tulipo.

‘“Nikamwambia potelea mbali. Ni lazima nimpate awe mke wangu, au nife. Hatimae akasema, “Basi usubiri mpaka wakija tena, utajificha halafu uiibe nguo ya huyo unayempenda sana.”

‘“Nikawasubiri na walivokuja tena, nikaiiba nguo ya aliekuwa mdogo kuliko wote, ambaye jina lake lilikuwa Sayadaa′tee Shems.

Wanawake warembo wakioga kwenye mto
Wanawake warembo wakioga kwenye mto

‘“Walipotoka kwenye maji, huyu hakuziona nguo zake. Nikajitokeza na kusema, “Ninazo” “Ahh” akaomba, “Naomba nipatie hizo nguo, ni zangu, nataka niondoke.” Lakini nikamwambia, ‘“Nakupenda sana, nataka nikuoe” “Nataka niende zangu kwa baba yangu” akanijibu. “Huwezi kwenda” nikasema.

‘“Kisha dada zake wakapaa na kuondoka, nikamleta kwenye nyumba, na yule mzee akatuoza. Akaniambia nisimpatie hizo nguo nilizochukua ila nizifiche; sababu akizipata atapaa na kurudi nyumbani kwao. Nikachimba shimo ardhini na kuzificha.

‘“Siku moja nilipokuwa mbali na nyumbani, alizichimbua na akazivaa; akamwambia mtumwa niliempa kama mhudumu wake, “Atakaporudi bwana wako, mwambie nimeenda nyumbani; kama kweli ananipenda, atanifata” akapaa na kuondoka.

‘“Nilporudi nyumbani wakaniambia hili, nikahangaika sana, nikimtafuta kwa miaka mingi sana. Hatimae nikafika katika mji ambapo mtu mmoja akaniuliza,”Wewe ni nani?”Nikamjibu, “Mimi ni Jan Shah.” “Jina la baba yako ni nani?” “Taaeeghamus.” “Wewe ndie uliemuoa binti yetu?” “Binti yenu ni nani?” “Sayadaatee Shems.” “Ndie mimi.” Nikasema kwa kufurahiya.

‘“Wakanipeleka kwa binti yao akanipeleka kwa baba yake na kumwambia mimi ni mume wake; na kila mtu akafurahia.

‘“Kisha tukadhani ni vizuri tukatembelee nyumba kwetu kwa zamani, nalo jini la baba yake likatubeba kwa siku tatu mpaka huko nyumbani. Tukakaa huko kwa mwaka mzima kisha tukarudi, lakini baada ya muda mfupi mke wangu akafa. Baba yake alijaribu kunifariji, na akanitaka nimuoe binti yake mwingine, nikakataa kufarijika, na mpaka hii leo bado namlilia. Hicho ndicho kisa changu.’

“Bolookeea akaenda zake na akahangaika mpaka alipokufa.”

Kisha Sultaanee Waa Neeoka akamwambia Hassee’boo, “Ukiondoka kwenda nyumbani, utaniumiza sana.”

Hassee′boo hakupendezewa na wazo hili akasema, “Sitaweza kushawishika kukudhuru. Naomba niache niende nyumbani”

“Nitakuacha uende nyumbani kwenu” akasema mfalme, “lakini nina uhakika utarudi na kuniuwa.”

“Kwa nini, siwezi kudiriki kutokua na shukrani kiasi hiki,” akashangaa Hassee’boo. “Ninakuapia sitawezi kukudhuru.”

“Basi” akasema mfalme wa nyoka, “ukae na hili akilini mwako, ukienda nyumbani usiende kuoga sehemu ambayo kuna watu wengi.”

Naye akasema, “Nitakumbuka.” Kwahiyo mfalme akamwacha aende zake nyumbani, na akaenda nyumbani kwa mama yake, akafurahi sana kujua kwamba kumbe alikuwa hajafa.

Sultani wa mji ule akawa ni mgonjwa sana; na ikaamuliwa kuwa kitu pekee kitakachoweza kumponya ni kumuua mfalme wa nyoka, kumchemsha, na supu yake apewe sultani.

Kwa sababu alizozijua yeye, vizir akawaweka wanaume waoge hadharani na kutoa haya maagizo: “Akija mtu kuoga hapa na ana alama tumboni kwake, mkamateni mumlete kwangu.”

Hassee’boo alipokaa nyumabni yapata siku tatu, akasahau yale maonyo ya Sultaanee Waa Neeoka, akaenda kuoga na watu wengine. Ghafla akashikwa na maaskari na kuletwa kwa vizir, akaesema, “Tupeleke kwenye nyumba ya mfalme wa nyoka.”

“Sijui iko wapi hio nyumba” akasema Hassee’boo.

“Mfungeni” vizir akawaamuru.

Kwa hio wakamfunga na kumpiga mpaka mgongo wake ukawa umetepeta, aliposhindwa kuvumilia maumivu akalia, “Niachieni ntawaonyesheni hio sehemu.”

Kwahiyo akawapeleka kwenye nyumba ya mfalme wa nyoka na alipomuona akamwambia, “Je sikukwambia kwamba utarudi kuniua?”

“Ningefanyaje” akalia Hassee′boo, “Uangalie mgongo wangu!”

“Nani kakupiga vibaya hivo?” akauliza mfalme.

“Ni vizir.”

“Basi sina tumaini tena. Lakini lazima unibebe wewe mwenyewe.”

Walipokuwa wanaenda, mfalme akamwambia Hasee’boo, “Tukifika mjini kwenu, nitauliwa na kupikwa. Mchuzi wa kwanza vizir atakupatia wewe, ila usiunywe; uuweke kwenye chupa na uihifadhi. Supu ya pili ni lazima uinywe, nawe utakuwa tabibu mkubwa sana. Supu ya tatu ndio dawa ambayo itamponya sultani wenu. Vizir akikuuliza kama ulikunywa supu ya kwanza mwambie, “Nilikunywa.”  Kisha itwae chupa yenye ya kwanza na useme, “Hii ni ya pili ni ya kwako.”Vizir atainywa, na akishainywa tu, atakufa, na sie wawili tutakuwa tumelipa kisasi chetu.

Kila kitu kikatokea kama mfalme alivosema. Vizir alikufa na sultani akapona, na Hassee’boo akapendwa na watu wote kama tabibu mashuhuri mkubwa.

Kwa nakala zaidi zinazohusu hadithi bofya hapa!