Maasai kipindi cha utotoni

Mtoto wa Maasai Kipindi cha Utotoni

Orodha ya Yaliyomo

Ujauzito katika utamaduni wa  kimaasai

Mwanamke mjamzito katika jamii ya wamaasai  uhudumiwa kama malkia. Uandaliwa chakula chake katika namna ya kuhakikisha wote yeye na mtoto watabaki na afya. Ujazo na pia ubora wa chakula ambacho mwanamke ula wakati ni mjamzito uangaliwa kwa umakini ili  kuhakikisha yeye na mtoto watakuwa na afya. Mwanamke mjamzito haruhusiwi kunywa maziwa yanayotoka kwa ng’ombe moja kwa moja;

Mwanamke Mmaasai Mjamzito
Mwanamke Mmaasai Mjamzito

ni kwa wakati fulani tu anaweza kunywa maziwa yaliyoondolewa mafuta au yaliyogandishwa. Mjamzito pia ufurahia lishe maalumu iliyotengenezwa kutoka kwenye mchanganyiko wa jadi wa mitishamba kwa ajili ya kutunza damu na kusafisha tumbo. Ujauzito uangaliwa kwa umakini na wakunga mpaka mama atakapo jifungua, ambapo baadaye mtoto wa maasai huyu ulelewa na jamii nzima.

Kujifungua mtoto kwa kimaasai

Pale mtoto wa maasai anapozaliwa , mtu muhimu wa kumuangalia ni mkunga. Mkunga katika utamaduni wa kimaasai anakazi kuu mbili. Kazi ya kwanza ni kumpokea mtoto na kumkaribisha katika dunia mpya .Ya pili, mkunga uhudumia kitovu hivyo umtenganisha mtoto kutoka kwa mama yake. Anapokata kitovu, utamka maneno yafuatayo “Sasa unajukumu la maisha yako kama nilivyo na jukumu la ya kwangu.” Maneno haya yanamuonya mtoto wa maasai anayeingia katika dunia mpya ya kwamba ametoka katika faraja na ulinzi wa tumbo la mama na sasa amekuwa kiumbe kilichojitenga na chenye maisha yaliyojitenga ya kwake mwenyewe na sasa  lazima  kuwajibika na maisha yake  ili asonge.

Baada ya sherehe za mwanzo ambazo uishia na maziko ya baada ya kujifungua, mama mwanzo kabisa ulishwa asali iliyochukuliwa kutoka kwenye mzinga wa nyuki wa eneo hilo. Kwa kuongeza, baba wa mtoto wa maasai au mwakilishi wake  uenda kutoa damu kutoka kwa ng’ombe. Namna ya kutoa damu kutoka kwa ng’ombe utegemea na njinsia ya mtoto. Kama mtoto ni wa kiume, baba anachukua kamba, bakuli na

Mama wa kimaasai akimbariki mtoto wake mpya kwa kumtemea mate
Mama wa kimaasai akimbariki mtoto wake mpya kwa kumtemea mate

mshale butu na anafanya jaribio la dhihaka la kumtatanisha ndama kabla ya kupata damu kutoka kwenye mshipa wa shingo wa ng’ombe. Kama mtoto ni wa  kike, taratibu ugeuzwa kinyume.

Baada ya baba au mwakalishi wake kutoa damu kutoka kwa ngo’ombe, huwa kuna baraka  ambazo zinazotolewa kwenye nyumba ambayo mtoto amezaliwa. Njia mojawapo ya kubariki nyumba na ambayo mara nyingi utumika, ujumuisha kuchinja kondoo au kutumia cheu (chakula alichokula ng’ombe / matapishi) ambayo imetafunwa na aidha kondoo wa kahawia au kondoo mweusi kwasababu rangi ya kahawia au nyeusi uchukuliwa kama takatifu katika utamaduni wa kimaasai.

Kukua kama mtoto wa kimaasai

Mtoto wa kiume wa maasai anapofikisha umri wa miaka minne au mitano, meno yake ya chini ya mbele hung’olewa. Katika umri huu kazi kubwa muhimu ya mtoto ni kuziangalia ndama na kondoo za familia. Katika umri wa miaka saba, upande wa juu wa sikio la kulia la mtoto utobolewa. Pia wakati huu mtoto anaanza kuwaangalia ndama wakubwa, na anaweza kuungana na mshiriki mkubwa wa familia katika kuchunga ng’ombe. katika umri huu pia mtoto wa maasai uweza kushiriki katika michezo ya watoto kama mapigano ya kinyesi cha ng’ombe na kuruka juu. Pia ufundishwa kutoka kwenye hadithi na mithali.

Katika umri wa miaka kumi na sita au kumi na saba, upande wa chini wa masikio ya watoto wa kiume hutobolewa. Katika wakati huu, wavulana wanaanza kuchukua majukumu mengi zaidi kama vile kupeleka kondoo na ng’ombe katika ardhi mpya ya malisho. Wasichana kwa upande mwingine wanaanza kukabiliana na majukumu yaliyohifadhiwa kwa ajili ya wanawake kama vile kuchota maji, kukata kuni na kupaka nyumba. Kabla ya wavulana kutahiriwa ( umri ambao wavulana utahiriwa utegemeana na ukomavu wa  mvulana uweza kuwa kati ya umri wa miaka kumi na saba hadi ishirini na zaidi) haruhusiwi kuweka mapambo katika masikio yake yaliyotobolewa na anaweza asibebe mkuki wa chuma cheupe. Hata hivyo, anaweza kujipamba mwenyewe kwa matawi  ya mzeituni na kubeba podo (begi la mikuki na mishale). Wasichana wadogo wa kimaasai pia ufata muundo kama wa wavulana. Wasichana ambao hawajaolewa, uvishwa majoho meusi na mnyororo uliopambwa na maganda madogo ,urembo wa ngozi unawekwa kwenye sikio lilotobolewa. Kwa ufupi kabla hawajaolewa, wasichana hunyoa vichwa vyao safi.

Kwa nakala zaidi zinazohusu kabila la kimaasai bofya hapa!