Mganga akiwa kazini kwake

Ubaguzi Dhidi ya Waganga wa Jadi Kutoka kwa Madakitari na Watabibu wa Kimishionari

Orodha ya Yaliyomo

Katika majira ya joto 2002, nilifanya mazungumzo ya kina na wanachama wa CHAWATIATA (Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia) Kyela. Lengo langu lilikuwa ni kupata picha kuhusu wasiwasi wao kama watabibu lakini pia kuchunguza zaidi nini matumaini yao na matarajio yao katika kazi wanazozifanya. Majibu yao kuhusu maswali niliyouliza yalianza kutufahamisha jambo kuhusu “tiba za kisasa”. Waganga wanafahamu kwamba madakitari wa kisasa, wakristo, na watu wengine wajionao “wakisasa” wanawaona wao ni “duni” na kwamba jambo hili linachangia wao kutengwa katika sera za serikali zihusuzo afya. Hisia hizi zilionyeshwa bayana kwangu baada ya tafakuri ya kina

Kanisa la Kilutherani la Azania Front Dar es salaam
Kanisa la Kilutherani la Azania Front Dar es salaam

kuhusu jinsi matabibu wa kimishionari na madakitari wa kisasa wanavyowaona waganga wa jadi. Kuna mgawanyiko wa kazi, kati ya aina hizi mbili za tiba, na hili linapingwa na waganga wa jadi ambao wangependelea madakitari wa kisasa kuwapatia wagonjwa wawafundishe kutumia baadhi ya mbinu zao, kama vile dripu na sindano. Hata hivyo, waganga wa jadi wanakubali kwamba, kwa upande mmoja, utaalamu wao kuhusu magonjwa yanayohusiana na uchawi upo sahihi. Hatahivyo, wanataka kutengwa kwao katika mgawanyo wa uasili-ukisasa uishe na  wanakemea mambo yote yakitamaduni ambayo yanahusishwa na kuongezeka kwa ushirikina Kyela. Mwishowe, wanategemea kuchukuwa maarifa na mbinu za tiba za kisasa, kama vile chandarua zilizotiwa dawa yakuzuia mbu na vidonge kwa faida zao wenyewe.

Mgawanyo wa Kazi na Kuzingatia mipaka

Waganga wa jadi niliowafanyia mahojiano walionyesha kuguswa sana na hisia hasi zilizowekwa juu yao na madakitari wa kisasa pamoja na watabibu wa kimishionari. Jambo hili ilikuwa ndiyo sababu ya kufadhaika na hasira. Waganga wa jadi wanaona jambo hili ni dhihaka katika ushindani au biashara; hawakujali kwamba madakitari wa kisasa wanadhani wao ni wajinga, kiasi kwamba wanawakatisha tamaa wagonjwa wasiende kuwaona. Walisisitiza kwamba japokuwa wao walikuwa tayari kushirikiana, kwa mfano, kuwashauri wagonjwa kwenda hospitali ya serikali, lakini kitendo hiki hakifanywi na upande wa pili. 20 Wangependa madakitari wa kisasa kuwashauri wagonjwa, ambao wameshindwa kuwatibu vizuri, au ambao wamelogwa waende kuwaona. Inajulikana vizuri hakuna tumaini la kumtibu mtu aliyelogwa hospitali.  Mazungumzo yanayofuata yayaonyesha jinsi waganga wa jadi wawili wanavyoonyesha ukosefu wa wagonjwa kutoka hospitali kwenda kwa mganga wa jadi kwamba jambo hili lina ushawishi wa kihistoria toka katika tiba za kimishionari. Nilianza kwa kuuliza kwanini watu wanaosema hawawezi kutumia miti shamba kwasababu wao ni wakristo, wanafanya kwa kificho. Mganga akajibu:

Wanasema vitu hivi kwasababu ya waliyojifunza toka kwa wamishionari. Wamishionari walituweka kando moja kwa moja na walikuwa na matatizo na sisi, walikuwa wakipinga sana tiba za jadi. Ni wamishionari. Dini. Waliwatafuta wagonjwa ‘kamwe usiende kwa waganga, na kutibiwa kule, haina maana. Ni mazoea tu’. Lakini kilichomaanishwa ni kwamba kila mmoja angeanza kwenda kwa kificho. ‘Umempeleka wapi?’ (dakitari wa kimishionari angeuliza = mgojwa angejibu) Nimempeleka kwa mganga’ (akaanza kucheka), ‘ndiyo bwana, nenda pale, hatuwezi kukutibu. Ha! Umempeleka kule – hatuwezi kukupokea; umeshaenda kule (kwa mganga).’ Ndiyo hivyo, watu wakaanza kwenda hospitali.

Uhasama

Uhasama wa tiba za kimishionari kwa kwa tiba za jadi unajulikana vizuri. Sababu za jambo hili ni tata. ‘Waganga wa kienyeji wanahusishwa na vitendo vya kishirikina, na kwa hakika uhusiano unaweza kuwa wenye utata kwa wote Wakristo na wasio wakristo. Kufahamu mengi kuhusu ushirikina ili kuweza kuutambua, hiyo maana yake unashiriki katika vitendo hivyo. Hali hii ya mashaka katika kipengele hiki katika kazi ya mganga haijawahi kumuacha muaguzi hata mmoja. Kama ambavyo mganga aliniambia ‘ni Mungu ndiye atanihukumu siku ikifika’. Kwa hakika, kwa mzee huyu, ni Mungu wa wakristo ndiye aliyemwomba ‘ruhusa’ dawa zake zifanye kazi. Kwahiyo, kwa baadhi ya wakristo, kitendo cha kutumia “tiba za jadi” moja kwa moja ni uovu, lakini kwa mganga, ufanisi wa tiba zake unategemea maamuzi ya Mungu juu ya nia yake. Tiba za kisasa na Ukristo zimekuwa zikifungamana  na dhana ya ukisasa katika Tanzania, na kama nilivyoonyesha mwanzo, maana ya maadili inayohusiana na ‘ustawi’ na ‘maendeleo’ inahusiana na hili. Uhusiano kati ya tiba za kisasa, Ukristo na ukisasa inaweza ikaonekana katika hatua za awali kuhusu tiba za kisasa Tanzania, katika misheni pamoja na ujenzi wa hospitali za awali. Mambo haya

Hospitali ya Mtakatifu Benedict Ndanda
Hospitali ya Mtakatifu Benedict Ndanda

yanaonyesha jinsi mpangilio wa sehemu na muda katika misheni na tiba za hospitali ziliundwa mahususi kuchochea ‘ukisasa’ kwa watumiaji, na kuwahimiza kuwaza kwa busara dhidi ya ushirikina. Tiba za kisasa zinaweza kutokuwa na ushawishi mkubwa kwa watumiaji Tanzania kama madakitari wa kisasa walivyotegemea, lakini kuna vipengelele kuhusu ‘ukisasa’ wake ambao unaipatia ushawishi mkubwa. Kwahiyo, katika dondoo inayofuata, tunamsikia mganga, aliyefunzwa katika Uisilamu na tiba za ‘asili’, akielezea jinsi uwezo wa haraka wa wakutoa matibabu ambao ‘hospitali za kisasa’ unafaidika kama matokeo ya teknolojia ya kisasa, mara nyingi unahusishwa na dini.

Maoni ya Waganga

Wote wanaosema ‘Mimi ni Mkristo’ au ‘Mimi ni Muisilamu’, siwezi kufanya vitu hivyo kwasababu ni dhambi wanafanya makosa makubwa…Tiba hizi zimeletwa na Mungu..hakuna sehemu katika Biblia au Korani inayosema hivyo. Hizo tiba za kiasili zipo ndani ya vidonge wanavyowapatia hospitali – wanaweza wakasema ‘Sitaki kutibiwa na miti shamba’ lakini wataenda hospitali. Lakini huko hospitali ni miti shamba ileile, lakini wametumia utaalamu wao, wanatengeneza vidonge ili waweze kukupatia huduma ya haraka, ni njia ya mkato. Tofauti ni kwamba sisi tunachimba mizizi, tunachemsha – inachukua muda mrefu.

Uchunguzi wake kwamba vidonge wapewavyo wagonjwa hospitali si lolote zaidi ni aina rahisi tu ya miti shamba ina ukweli kiasi. Aspirini

Mti waQing-Hao unaotumika kutengeneza dawa
Mti waQing-Hao unaotumika kutengeneza dawa

inatokana na magome ya mti wa willow, kwinini kutoka magome ya mti wa cinchona, na hivi karibuni dawa ya malaria isiyoleta usugu, artemisinin inatokana na mti wa dawa wa Kichina qinghao. Mganga huyu alionyesha kipengele cha ‘uasili’ wa tiba zake kwa jinsi anavyotumia mikono yake katika matibabu yake, ambayo alitofautisha na dawa zinazotengenezwa kwa wingi na kupatikana hospitali ambazo hazina mfanano wowote na chanzo chake cha ‘asili’. Katika hoja zake alikwepa mambo yote yanayohusu tiba za kwenye Korani, kama vile kuosha aya za Korani katika maji, au kutoa jini, mambo ambayo hayapatikani katika tiba za kisasa. Alikuwa anasisitiza tu vile vipengele katika tiba zake ambavyo vilikuwa na manufaa katika mazungumzo yetu. Kwa maneno mengine yeye kuchukua upande katika jambo hili inafunua zaidi kuhusu mabishano yanayoendelea kati ya ‘jadi na ukisasa’ kuliko hata inavyoelezea kuhusu kazi zake za kila siku kama mganga. Kama tutakavyoona zaidi, waganga wanatoa madai yakupendelea teknolojia ambayo awali ilihusishwa na tiba za kisasa, na kwa maana hii nao dai lao linaegemea ukisasa.

Hata hivyo,kuna la zaidi kuhusu chuki za Wakristo na Waisilamu zinazoelekezwa kwa ‘tiba za jadi’ kuliko mashaka yaliyopo kuhusu wema na uovu, na kuhangaika na suala la ‘ukisasa’. Kama mganga mwingine alivyoelezea uelewa wake, ‘tumeingilia (wamishionari) biashara zao.’ Wamishionari wa mwanzoni waliamini kuwa huduma za afya ilikuwa ni nyenzo muhimu katika juhudi zao kuwabadilisha Waafrika kwenda kwenye Ukristo, na katika kipindi cha karibuni, serikali ya Tanzania imetegemea sana misheni kwenye utoaji huduma za kitabibu hususani wakati ambapo rasilimali za serikali zimekuwa zikipata msaada mdogo wa kifedha na kutumika zaidi ya uwezo wake. Kwahiyo, uhusiano kati ya Ukristo, tiba za kimishionari, na tiba za ‘asili’ inahitaji kueleweka si tu katika mazungumzo yahusuyo wema na uovu, lakini pia katika namna ya ushindani katika eneo la tiba. Miradi ya tiba za kisasa inapata fedha kidogo toka serikalini, kwahiyo kwa kiasi inategemea kushirikiana na Ukristo kwaajili ya kuaminika, lakini pia kuweza kujiendesha. (Japokuwa Watanzania wengi wanaweza kutofautisha miradi ya kitabibu inayofadhiliwa na misheni na ile ya serikali kama vitu viwili tofauti.) Ushindani huu unaonwa hasa unapotokea kwa wahudumu wa tiba za kisasa wa hadhi ya chini na wanaolipwa kidogo:

Mganga: Hakuna uhusiano mzuri. Tunapigia kelele sana kuhusu hili. Madakitari wenye kuheshimika, kama vile (anamtaja dakitari maarufu katika hospitali) wanafahamu kuhusu dawa za mitishamba. Ni wale tu wenye umuhimu mdogo, wa viwango vya chini – ndiyo wenye tatizo. Wana wivu, wanapendelea kama mgonjwa ataenda kwao na iwapo mgojwa ataamua kuja kutuona, sasa..

Beckie: Wote wa ngazi za chini, inawezekana hawana uwezo au kipato kama cha walio ngazi ya juu, labda ndiyo sababu wanaona wivu.

Wote: mmmmm

Mganga: Kwa mfano mara nyingi sana hao manesi, kama nikimpeleka mgonjwa wangu, nitasema ‘lala hapa chini’ na baada ya muda nitaleta dawa zangu – watasema ‘hapana – tutawataarifu polisi, kwanini umeleta dawa za miti shamba hapa!’ Ninawaambia ‘nipelekeni – watanifunga kwa nini? Polisi ni kwaajili yetu pia.

Hitimisho

Waganga wanafadhaishwa na mpaka unaowekwa na tiba za kisasa. Wauguzi wa tiba za kisasa wamekataa kuwashauri wagonjwa kwenda kwao, na wanawanyanyasa wale wanaowaona waganga. Waganga wenyewe, wanahisi wanaweza kuona katika hili – kama mmoja wao alivyosema – ‘tumeingilia biashara zao’. Wazo hili linaimarishwa pale wanapoona ni wauguzi wa ngazi za chini, na wanaolipwa kidogo (ambao hali yao ni rahisi kushindwa katika ushindani) ndiyo kizuizi kikuu. Kuna kipengele kimoja kuhusu kusita kuwashauri wagonjwa ambacho waganga wanakubaliana nacho hata hivyo; wanafahamu kuhusu uwezekano wakutokuendana kati ya dawa zilizotolewa na dakitari wa tiba za kisasa na za kwao. Kama mgojwa hafahamu ni dawa gani ametumia katika siku zilizopita, basi mganga anaweza kusubiri dawa ‘iishe’ mwilini, mpaka atakapoanza kumpatia tiba. Suluhisho la jambo hili katika macho yao ni kuweka sawa utofauti wa mawasiliano kati ya hospitali na mganga. Hii ingesaidia pia kuimarisha upande mmoja wa mmgawanyo wa kazi ambao wanaukubali – kwamba wao ni wataalamu wa magonjwa yanayosababishwa na uchawi.

Kwa nakala zaidi zinazohusu tiba za asili bofya hapa!