Usafiri wa Anga – Muhtasari Mfupi wa Ndege za Abiria na Mizigo
Orodha ya Yaliyomo
Viwanja vya ndege Tanzania vina mchango mkubwa katika miundombinu ya usafirishaji nchini. Pamoja na kuwa mlango wa kimataifa, viwanja vya ndege vina historia ya kutumika kwa ajiri ya usafiri wa ndani na kuongoza kwenye utoaji fursa za kimaendeleo vijijini. Kwa ujumla, nchi ina viwanja vya ndege 368, na viwanja 58 miongoni mwa viwanja hivyo vya ndege viko chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) upande wa bara. Viwanja vingi vya ndege ni viwanja binafsi vya kutua ndege vinavyomilikiwa na kampuni za uchimbaji madini na waendeshaji wa shughuli za utalii.
Licha ya historia ya muda mrefu ya sekta ya usafiri katika kuleta maendeleo ya nchi, uwepo wa makampuni machache ya ndege za kimataifa, na za kitaifa – Air Tanzania, unadumaza maendeleo ya usafiri wa anga. Wakati ambao njia nyingi za safari zina umbali mwingi, na huhitaji kusafiri kwa masaa mengi kwa njia ya barabara, lakini bado uhitaji wa usafiri wa anga umeendelea kuwa chini, na haukuwi kwa
haraka ukilinganisha na nchi nyingine. Hali hii inachangiwa na kasi ya maendeleo na ukweli kwamba watu wengi hawawezi kusafiri hasa kwa kutumia usafiri wa anga kutokana na kuwa na uchumi wa chini. Uhitaji mdogo, gharama kubwa za uendeshaji, na ushindani mdogo umepelekea bei za tiketi za ndege kuwa kubwa ukilinganisha na sehemu nyingine duniani na hali hii imeathiri ukuaji wa sekta hii ya usafiri wa anga.
Umbo la 6 linaonesha maeneo yenye viwanja vya ndege ndani ya Tanzania. Viwanja vya ndege vimetapakaa sehemu mbalimbali za nchi hasa katika miji mikubwa ambayo ni maeneo tegemezi ya watu  na biashara.
Maelezo ya Usafiri wa Anga
Abiria
Kwa sasa, kuna abiria zaidi ya milioni tatu, na takribani 48% ni abiria wa kimataifa, na 58% ni abiria wa ndani. Abiria wa kimataifa wanapatikana sana katika viwanja vya ndege vinne (4): Dar es Salaam, Kilimanjaro, Zanzibar na Arusha, na abiria wengi wa ndani pia hutumia viwanja hivi vya ndege ikiwa pamoja na kiwanja cha ndege cha Mwanza. Viwanja vya ndege vingine vingi hutumiwa na abiria wachache. Kati ya viwanja vya ndege 56 vilivyowekwa kwenye orodha ya TAA, ni 15 tu vilivyokuwa na abiria angalau 2500 kwa mwaka mzima wa 2011. Hali hii inawiana na abiria 50 kwa wiki, abiria mmoja kwa ndege mbili kwa wiki, na kwa makadirio namba ya waliofika na wanaoondoka inafanana. Hivyo basi, kwa ujumla inaonesha kuwa kuna viwanja vya ndege vingi vyenye abiria wachache, na kuna viwanja vya ndege vichache vyenye abiria wengi. Mchoro wa 29 chini aya mbili kwneda chini unaonesha idadi ya wasafiri kwa kipindi chote cha mwaka kwa viwanja vya ndege vikubwa kumi na viwili nchini.
Kwa sekta hii kwa ujumla wake, makadirio yanaonesha kuwa abiria wanatarajiwa kuongezeka kwa 10.9% kwa mwaka mpaka mwaka 2016
kwa kuangalia mwaka 2011 kama msingi. Kiwango hiki cha ukuaji ni sawa na kiwango cha ukuaji kilichotabiriwa na waliofanya utafiti wa awali kuhusu mradi huu. Wakati abiria wengi wanatumia uwanja wa ndege wa JNIA wa Dar es Salaam, ukuaji kidunia unaonesha uwepo wa kiwango kidogo cha abiria karibia katika viwanja vyote vya ndege. Kuna matarajio ya ukuaji wa JNIA kwa 12% kwa mwaka kwa kuongezeka kiwango cha abiria kutoka milioni 1.8 ya mwaka 2011 mpaka milioni 3.2 kwa mwaka 2016. Makadirio haya yanaendana makadirio ya ukuaji kihistoria kutoka mwaka 2001 mpaka mwaka 2010, hali ambayo ni sawa na ukuaji wa wastani wa 13% kwa mwaka kiutendaji halisi.
Makadirio ya abiria katika viwanja vingi vidogo vya ndege ambavyo hutumiwa sana na wasafiri wa ndani yanatarajiwa kukua kwa kiasi ukilinganisha na wasafiri wa kimataifa, ambapo wanatazamiwa kuongezeka +e kwa kiwango cha 4% mpaka 8% kutegemeana na uwanja wa ndege na mchango wake katika uchumi wake wa ndani. Mwanza, ni uwanja wa ndege wenye watumiaji wengi mbali ya viwanja vya ndege vitatu vya kimataifa, unatarajia kukua kwa 8.6%, ukiwa na ongezeko la abiria kutoka abiria 320,000 kwa mwaka mpaka abiria 480,000 kwa mwaka 2016. Uwanja mwingine wa ndege ulio chini ya TAA wenye abiria wanaozidi 100,000 kwa mwaka ni Arusha ambako kiwango cha uhitaji kwa mwaka kwa sasa ni abiria 112,000 na inatarajiwa kufikia kuwa na abiria 158,000 kwa mwaka 2016. Katika viwanja vya ndege vingine vyenye watumiaji wengi kama vile Kigoma, Bukoba, na Mtwara kiwango cha abiria kwa mwaka kinatarajiwa kubakia chini ya abiria 30,000 mpaka abiria 40,000 (mchoro wa 29). Kiambatanisho namba 6 makadirio ya wasafiri wa anga kwa viwanja vya ndege vilivyoko chini ya TAA inadhihirisha kuwa viwanja vingi vya ndege vitaendelea kuwa na kiwango kidogo cha wasafiri wa anga kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Mchoro wa 29: Kiwango cha Abiria Katika Viwanja vya Ndege (’000)
S/N | Uwanja wa Ndege | Kimataifa | Nyumbani | ||||||||
2006 | 2007 | 2008 | 2009 | 2010 | 2006 | 2007 | 2008 | 2009 | 2010 | ||
1. | Dar es Salaam | 659 | 754 | 823 | 788 | 870 | 486 | 581 | 604 | 578 | 697 |
2. | Kilimanjaro | 208 | 243 | 251 | 243 | 283 | 161 | 200 | 185 | 133 | 141 |
3. | Wanzi+ar | 197 | 221 | 207 | 222 | 216 | 289 | 300 | 292 | 281 | 325 |
4. | Arusha | / | / | 128 | 84 | 86 | 76 | 61 | 125 | 107 | 139 |
5. | Bukoba | – | – | – | – | – | 22 | 24 | 24 | 22 | 18 |
6. | Dodoma | – | – | 146 | 84 | 1 | 7 | 6 | 5 | 5 | 6 |
7. | Kigoma | 2 | – | 1 | 1 | – | 18 | 22 | 25 | 22 | 24 |
8. | Moshi | – | – | – | – | – | 1 | 1 | 1 | 1 | 1 |
9. | Mtwara | 3 | / | 1 | 31 | 1 | 24 | 28 | 22 | 22 | 25 |
10 | Mwanza | 10 | 6 | 1 | 8 | 13 | 184 | 217 | 410 | 203 | 200 |
11. | Shinyanga | – | – | – | – | – | 14 | 12 | 10 | 8 | 6 |
12. | Tabora | – | – | – | – | – | 11 | 12 | 13 | 13 | 11 |
13. | Others | 64 | 9 | 1 | 9 | 12 | 98 | 177 | 51 | 9 | 21 |
Jumla | 1,143 | 1,233 | 1,559 | 1,470 | 1,482 | 1,391 | 1,641 | 1,767 | 1,404 | 1,614 |
Chanzo: TCAA
Ndege za Mizigo
Ndege za mizigo zinapatikana katika viwanja vichache vya ndege nchini Tanzania, na nyingi ziko uwanja wa JNIA. Ndani ya mwaka 2011, JNIA ilihusika na usafirishaji wa mizigo kwa 89% dhidi ya viwanja vya ndege vyote vilivyopo chini ya TAA. Kuanzia mwaka 2005 mpaka 2011, usafirishaji wa mizigo katika JNIA uliongezeka +y kwa wastani wa 8.7% kwa mwaka kutoka tani 14,000 mpaka tani 23,000 kwa mwaka.
Mizigo inayoingizwa nchini ni 90% ya mizigo yote inayosafirishwa na ndege. Theluthi ya mizigo hiyo inajumuisha mashine na bidhaa za umeme, sehemu ya tano inajumuisha vioo, na vyombo vya mawe, na vilivyobaki ni mizigo isiyojulikana. Vitu vinavyosafirishwa nje ya nchi hujumuisha kiwango kikubwa cha wanyama na mazao ya wanyama, mashine na chuma.
Kiwango cha mizigo katika viwanja vingine vya ndege kimekuwa kidogo ambapo viwanja vya ndege vikubwa vinashughulikia wastani wa tani 100 mpaka tani 200 kwa mwaka, huku viwanja vya ndege vinavyosalia vikiwa na kiwango kidogo sana cha mizigo. Uwanja wa ndege wa Mwanza ulikuwa na kiwango kikubwa cha mizigo kutokana na kusafirisha samaki, na bidhaa za samaki kwenda Ulaya kwa kutumia ndege za moja kwa moja. Hata hivyo hali imebadilika kutokana na changamoto zinazotokana na miundombinu ya uwanja wake kuwa ya kiwango cha chini pamoja na wasafirishaji kuamuwa kubananisha mizigo zaidi kwa wakati mmoja. Kwa sasa, mizigo iliyokuwa inabweba kupitia uwanja huo hubebwa na malori mpaka Nairobi, ambako husafirishwa kwa ndege mpaka Ulaya. Matokeo yake usafirishaji wa mizigo katika uwanja wa ndege wa Mwanza umeporomoka kutoka tani nyingi zilizokuwa zikisafirishwa kabla ya mwaka 2005.
Kiwango cha mizigo kinatazamiwa kuendelea kuwa cha chini, isipokuwa JNIA ambayo kiwango kinategemea kuongezeka kwa 9.6% kwa mwaka na kufikia tani 36,000 ndani ya mwaka 2016. Viwanja vingine vya ndege, vinatazamiwa kuwa na ongezeko la mizigo pale ambapo sekta maaalum za kiuchumi zitapanuliwa. Hivyo basi, kutokana na ukuaji wa sekta ya mafuta na gesi Mtwara inatarajia kuwa na ongezeko la mizigo kwa zaidi ya 50% kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Pia, uwanja wa ndege wa Mafia ambao unaweka nguvu katika sekta ya utalii unakadiriwa kuwa na ongezeko la soko la usafirishaji. Hata hivyo, ijapokuwa kuna ukuaji unatarajiwa katika maeneo tajwa, biashara kwa ujumla itabakia chini kwa takribani tani 1 kwa siku. Kuna maeneo mengine yenye kiwango cha chini sana ambayo nayo yanatarajiwa kuwa na ongezeko katika usafirishaji ni pamoja na Bukoba, Shinyanga, na Musoma.
Ingawa KIA inashikilia nafasi ya pili kwa kuwa na kiwango kikubwa cha mizigo, bado kiwango cha mzigo ambacho ni tani 4,000 kwa mwaka ni kidogo. Kwa ujumla wake, karibia 60% ni mizigo inayosafirishwa nje ya nchi, na takribani nusu yake ni mboga mboga. Vitu vingine vinavyosafirishwa hujumuisha vyuma, mashine na bidhaa za umeme, na mazao ya wanyama. Mizigo inayoingizwa nchini inajumuisha kemikali na mazao ya viwanda yanayohusiana na kemikali, mashine, usafiri na mazao ya mbogamboga.
Kunatazamiwa kuwa na ukuaji wa kiwango cha mizigo mpaka kufikia tani 5,000 kwa mwaka 2016 kwenye sekta hii ya usafiri wa anga.
Kwa nakala zaidi zinazohusu usafiri bofya hapa!