Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Tanzania

Taasisi Katika Sekta ya Viwanja vya Ndege Tanzania na Masuala Muhimu

Orodha ya Yaliyomo

Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA)

Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania TAA ilianzishwa chini ya sheria ya wakala wa serikali No 30 ya mwaka 1997 ambayo ilizinduliwa rasmi Novemba 1999. Ni wakala unaojietegemea chini ya wizara ya uchukuzi (MOT) na hutoa ripoti kwa waziri. Pia una uongozi wa bodi ya ushauri ambayo ina wakurugenzi 10 ambao jukumu lao ni kutoa ushauri wa kishirika kwa wizara na katibu mkuu. Bodi haina mamlaka kamili kama shirika linalo jitegemea na mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA) huripoti kwa katibu mkuu.

Nembo ya TAA
Nembo ya TAA

Majukumu kwa ujumla yanabaki kwa waziri wa uchukuzi.

Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania(TAA) inafanya kazi Pamoja na wizara ya uchukuzi(MOT) kuwa mamlaka inayojiendesha ambapo hii itairuhusu kuwa kampuni ya kibiashara yenye majukumu kamili na maswala yote ya usimamizi wa uwanja wa ndege na utendaji kazi. Hii itasaidia usimamizi wa viwanja vya ndege kulingana na kanuni za kibiashara na itapunguza ushawishi wa kisiasa ambao kwa sasa unadhoofisha mchakato wa kufanya maamuzi. Pia itawezesha utendaji kazi wa viwanja vya ndege vidogo ambavyo havimudu gharama ya uendeshaji ili kuendelea na jukumu la kutoa huduma kwa umma. Kwa sasa ziada ya mapato inatumika kulipia shughuli zenye mapungufu ambapo huondoa rasilimali kutoka kwenye sekta ndogo na hairuhusu viwanja vikuu vya ndege kuongeza uwezo wao kibiashara.

Majukumu ya msingi ya Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanazania(TAA) ni:

> kuendesha, kusimamia, kuboresha na kuendeleza viwanja vya ndege Tanzania bara kwa ufanisi na kwa gharama nafuu.

> Kutoa huduma bora na salama katika kuwahudumia abiria na mizigo kwenye viwanja vya ndege ili kujenga taswira nzuri ya nchi kwa mataifa mengine duniani.

> Kutoa ushauri wa kitaalam kwa serikali katika maswala yanayohusu uendelezaji wa viwanja vya ndege.

> Kuhakikisha kwamba sera za serikali za viwanja vya ndege, kanuni na taratibu zinazohusiana na maswala ya viwanja vya ndege yanatekelezwa kwa viwango vya kimataifa.

> kuishauri serikali katika masuala ya kitaifa na kimataifa yanayohusu usimamiaji wa viwanja vya ndege.

> Kuunga mkono maendeleo ya kitaifa na kiuchumi kwa kutoa miundombinu muhimu uwanja wa ndege,vifaa na huduma mbalimbali.

Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA) ni mamlaka inayozalisha mapato. Ingawa inazalisha mapato yanayokidhi mahitaji yake ya kila siku ya matengenezo lakini haizalishi mapato ya kutosheleza matengenezo ya mara kwa mara au gharama za mtaji zinazohitajika kuendeleza sekta ndogo ndogo. Matokeo yake hali ya miundombinu muhimu ya viwanja vingi vya ndege bado ni mbaya. Ingawa viwanja vingi vya ndege vina matumizi ya chini, kuna haja ya kuboresha barabara za lami za ndege na kuhakikisha vifaa vya urambazaji vinatosha kuhakikisha usalama wa kiwango cha juu unapatikana. Isipokua viwanja viwili vya ndege vya kimataifa na viwanja vya ndege vikuu nane vya mkoa ambavyo vina barabara za lami,vingine vipo katika hali mbaya vina barabara za changarawe na nyasi. Matokeo yake usalama na

Ndege ya kampuni ya Auric ikituwa katika kiwanja cha ndege Dodoma
Ndege ya kampuni ya Auric ikituwa katika kiwanja cha ndege Dodoma

huduma nzuri katika viwanja hivi vya ndege hupatikana wakati wa kiangazi. Kwa kuongezea,ni viwanja vya ndege vinne tu vyenye mifumo ya taa ambazo zinaruhusu shughuli za uwanja wa ndege kuendelea kwa masaa 24. Hivyo viwanja vya ndege ni JNIA,KIA, Mwanza na Dodoma.

Katika mwaka wa fedha wa 2011, jumla ya mapato yaliyopatikana yalifika Tshs bilioni 32.9 ambayo yalikua chini kidogo kuliko makadirio ya bajeti na 2% + chini ya jumla ya mwaka uliopita. Mapato yanatokana na vyanzo vya anga na biashara. Mapato mengi hutokana na anga, kimsingi yanapatikana kutoka kwa malipo ya huduma za abiria na malipo ya kutua na maegesho ambayo kwa pamoja yanachangia takriban 73% ya mapato yote. Mapato kutoka kwa vyanzo vya kibiashara kama ada ya kukodisha na idhini,matangazo na maegesho ya magari uwanja wa ndege ni sawa na 27% ya mapato yote. Kwa kuongezea mapato mengi (86%) hutoka kwenye shughuli za JNIA wakati viwanja vingine vya ndege vinachangia 8% tu ya mapato na ofisi kuu 6% iliyobaki. Kwa ujumla ni viwanja vya ndege vya JNIA na Mwanza tu ndio vinazilisha mapato.Viwanja vingine  vyote vya ndege hufanya kazi kwa hasara.

Gharama za uendeshaji wa mamlaka ya anga Tanzania TAA zinafikia Tsh bilioni 30.1, ambapo ofisi kuu inafikia 38%, JNIA 36% na viwanja vingine vya ndege 26% ya gharama. Walakini matumizi haya yanawakilisha 20% tu ya jumla ya matumizi kwa mwaka na 80% iliyobaki ya matumizi ya mtaji utegemea msaada wa serikali pamoja na msaada kutoka kwa mashirika ya kimaendeleo. Inatagemewa kwamba msaada wa serikali utaendelea kuwa wa muhimu mpaka wakati ambapo sekta ndogo zitakua zimefikia ukubwa wa kujiendesha zenyewe na pale viwanja vikubwa vya ndege vya ndani vitafikia hatua ambapo vitazalisha mapato. Inatazamiwa kwamba JNIA itaendelea kuwa mzalishaji mkuu wa mapato katika sekta ya viwanja vya ndege na juhudi zaidi zinatakiwa kuelekezwa kwenye kituo kipya kwa kutumia ipasavyo mkakati wa ushirikiano wa umma na kibinafsi kwa maendeleo yake.

Kwa ujumla  sekta hii ya viwanja vya ndege inategemea sana katika uwekezaji wa mtaji kutoka kwa serikali kufanya maboresho ya viwanja vya ndege. Michango kama hiyo siyo sehemu ya mizania (balance sheet) ya TAA na deni linapopatikana la maboresho ya viwanja vya ndege linashughulikiwa na serikali.

Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)

Mamlaka ya usafiri wa anga tanzania (TCAA) ilianzishwa mnamo novemba 2003 kama shirika kulingana na sheria ya mamlaka ya usafiri wa anga. Sheria inaelekeza mamlaka kudhibiti usalama na uangalizi wa kiuchumi wa sekta ndogo ya anga. Kuna aina tatu za huduma zinazodhibitiwa: usafiri wa anga, huduma za anga na urambazaji angani. Kwa sasa TCAA inaendelea kutoa huduma za urambazaji angani

Ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Anga

lakini shirika la kimataifa la uchukuzi wa anga (ICAO) lilipendekeza kwamba huduma hizo zinapaswa kutolewa na shirika tofauti na mamlaka ya udhibiti. Utafiti mkuu wa upembuzi yakinifu pia umependekeza kwamba pendekezo hili linapaswa kuzingatiwa.

Kwa ujumla Tanzania inaunga mkono uamuzi wa Yamoussoukro wa novemba 1999 ili kukomboa usafiri wa anga barani Afrika. Hii inatekelezwa kikanda chini ya  udhamini wa jumuiya ya Afrika mashariki. Mpaka pale makubaliano yatakapofikia tamati, Tanzania inaendelea kudumisha usalama wa usafiri wa anga kwa pande mbili. Kwa upande wa utoaji wa haki, serikali tayari imekubali kuweka huru masoko na kwa sasa inajadili uwezekano wa kutoa haki ya tano ya uhuru kwa wachukuzi wote wa Afrika bila masharti. Serikali imelegeza vizuizi vya masafa ikiwa ni Pamoja na aina za ndege zinazopaswa kutumiwa na idadi kubwa ya msongamano kwa kuzingatia ukubwa wa soko linalotumiwa, sera huria zimeundwa kuongeza biashara na kuongeza idadi ya abiria ili kuchochea ukuaji.

Mambo Muhimu

Kulingana na ukaguzi wa sekta ya uchukuzi wa anga, kuna baadhi ya mambo muhimu ambayo yanahitaji kushughulikiwa ili kuboresha uendeshaji wa sekta hii haswa kuhusiana na mahitaji ya miundombinu.

1. Uwepo wa mipango ya sekta

Kikwazo kikubwa katika pengo la maarifa ya kusonga mbele ni ukosefu wa mipango ya kutambua mahitaji muhimu ya sekta. Wakati mahitaji mbalimbali yamegunduliwa na TAA, yanahitaji kuwekwa ndani ya mpango wa jumla ambao utatoa mfumo wa maendeleo ya baadae kwa sekta. Kwa sasa wanaotunga sera au wawekezaji hawana imani kuwa maendeleo ya sekta hii yanafanywa au kupangwa kwa usawa. Kwa hivyo, kuna uhitaji wa haraka wa kuandaa mpango mkuu wa usafiri wa anga ambao rasilimali zitakuwa zimeshawekwa. Inapendekezwa kuwa timu ya mpango mkuu inapaswa kuajiriwa haraka iwezekanavyo.

2. Uwekezaji

Kituo namba 3 Kiwanja cha Julius Nyerere - Awamu ya 1 na 2
Kituo namba 3 Kiwanja cha Julius Nyerere – Awamu ya 1 na 2

Ingawa idadi kubwa ya mashirika ya maendeleo yametoa msaada kwenye hii sekta, sekta ya viwanja vya ndege bado inakosa uwekezaji. Umbali kati ya mji na mji na maeneo ya watalii ni mkubwa na kwa masoko kadhaa unaweza kufikiwa na usafiri wa anga tu. Ingawa misongamano imepungua katika barabara nyingi, kuna mbinu mkakati ya kuweka viwanja vingi vya ndege kufanya kazi kulingana na mahitaji ya kiuchumi,kijamii na maendeleo mengine. Kwa viwanja hivi vya ndege kunahitajika kuwa na kiwango cha chini cha usalama na kuzingatia pia na uhitaji wa kuvifanya vishughulike kwa misimu yote ambayo inakazia kwenye barabara za lami  za ndege au vipande. Mpango mkuu unatakiwa kutambua viwanja hivi vya ndege na kuhalalisha uwekezaji uliopendekezwa.

Sekta ya viwanja vya ndege ina nafasi kubwa ya kushirikisha wawekezaji wa sekta binafsi katika kusaidia haswa kwa mahitaji ya ardhi. Mpango mkuu unapaswa kuangazia na kutambua maeneo ambayo ushiriki wa sekta binafsi utakuwa na manufaa makubwa Zaidi. Kwa kuongezea  mshauri mtaalam wa manunuzi anapaswa kuajiriwa kutoa ushauri juu ya vitu hivyo vya miundombinu na kuweka mikakati ya namna uwekezaji huo unaweza kuhamasishwa na kuonyesha manufaa makubwa yaliyopo ya kuvutia uwekezaji huo.

3. Usalama

Usalama ni muhimu katika sekta ya usafiri wa anga na umakini unahitajika kuwekwa katika kuimarisha usalama katika viwanja vyote vya ndege. Utalii ni jambo muhimu katika uchumi na ni moja wapo ya njia za kuendeleza ukuaji wa uchumi.Sekta hii iko hatarini zaidi katika maswala ya kiusalama hata kama shida zinafikirika tu, biashara inaweza kuzorota kwa haraka. Kwahivyo kuna umuhimu wa mipango ya maendeleo ya viwanja vya ndege kuweka umakini wa kutosha ili kuimarisha kiwango cha juu cha usalama.

4. Mabadiliko

Kwa miaka kadhaa TAA imekua ikijadili uwezekano wa kuwa shirika linalojitegemea kutoka kwenye hali yake ya sasa kama shirika ambalo halijitegemei kikamilifu. Mabadiliko yaliyopendekezwa yanatazamiwa kuboresha utendaji kazi wa TAA, kuifanya iwajibike kikamilifu kwenye utendaji kazi na maendeleo ya viwanja vya ndege. Inaweza kukuza utawala bora na usimamizi bora kama biashara, ambapo inaweza kuvutia wawekezaji wa sekta binafsi kwa muda mrefu. Kwakweli, sekta binafsi zinapendelea kushirikiana na shirika linalojitegemea na lenye mamlaka yake ya usimamizi kwa muda mrefu, mamlaka inayojitegemea inaweza kuzingatia utambulisho kamili wa ushirika sawa na mamlaka ya viwanja vya ndege sehemu zingine ulimwenguni.

5. Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere

Maendeleo muhimu zaidi katika sekta hii yanahusu kituo kipya cha abiria JNIA, lango kuu la Tanzania. Kituo hiki kinahitajika kwa haraka kwasababu kituo kilichopo tayari kinafanya kazi nje ya uwezo wake na huduma zake za zamani hazitoi ubora unaofaa kwa wageni nchini. Kituo kipya kitakua ni uwekezaji mkubwa unaohitajika katika sekta ndogo na unatakiwa  kuvutia wawekezaji wa sekta binafsi. Rasilimali tayari zimetengwa kufanya mapitio ya mpango mkuu wa JNIA na kusahihisha pale inapohitajika. Kwa kuongezea, rasilimali pia zimetengwa kwa mshauri wa manunuzi kuandaa mfumo mzuri wa kifedha kwa kituo cha uwanja wa ndege ambacho kitatumika kutangaza kituo kilichopendekezwa kwa wawekezaji wa sekta binafsi. Kwa kuzingatia muda unaotakiwa wa kuandaa na kujenga kituo kipya, inapendekezwa kwamba shughuli za kukamilisha mpango mkuu wa JNIA na kutafuta fursa za uwekezaji zikamilike kwa haraka kwasababu mchakato kwa jumla unaweza kuchukua miaka mi 3 hadi mi 4 kukamilika.

Kwa nakala zaidi zinazohusu usafiri bofya hapa!