Treni ya Tazara na Abiria

Uchambuzi wa Kina Kuhusu Usafiri wa Reli Nchini Tanzania

Orodha ya Yaliyomo

Mwaka 2008 Tanzania ilikuwa na kilomita 3,689 (2,292 maili) za barabara ya reli, ikiwa ya 46 duniani kwa urefu. Inajumuisha kilomita 2,720 (maili 1,690) za milimita 1,000 (futi 3 na inchi 3 3/8) na kilomita 969 (maili 602) za milimita 1,067 (futi 3 na inchi 6). Tarehe 31 mwezi wa tatu 2015, serikali ya Tanzania ilitangaza itatumia bilioni 14.2 za kimarekani za mikopo ya biashara kuunda miundombinu ya reli nchini kote kabla ya 2021 na kuifanya nchi kuwa kitovu cha usafirishaji katika afrika mashariki.

Barabara za reli Tanzania

Mapendekezo yameshafanywa kwajili ya usafiri wa reli kuunganisha Mtwara kwenda kwenye machimbo ya makaa ya mawe sehemu za magharibi, au hata kuiunganisha na Mbeya.

Kituo cha Treni Kigoma
Kituo cha Treni Kigoma

Reli ya kati, kati ya Kigoma na Dar es Salaam inabeba mizigo ya kimataifa na abiria kutoka Burundi, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda kwenda bahari ya Hindi, na kipande kutoka Tabora hadi Mwanza inabeba mizigo na abiria kati ya Uganda na bahari ya Hindi.

Bandari kavu ya Isaka ni mji mdogo na ipo katika reli ya Mwanza katika makutano yake na barabara kuu ya lami ielekeayo Kigali. Imepata kuendelezwa katika kinachotambulika kama “bandari kavu” kwaajili ya kupokea mizigo inayosafirishwa kwa njia ya barabara na kutoka Burundi na Rwanda na kuisafirisha kwa njia ya reli za mizigo kuelekea bandari ya Dar es salaam. Yapo mapendekezo ya kujenga barabara ya reli kutoka Isaka hadi Rwanda/Burundi.

Reli ya TAZARA

Mamlaka ya barabara ya reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA), zamani ikiitwa TanZam inahudumu kilometa 1,860 (maili 1,156) ya milimita 1,067 (futi 3 na inchi 6) ikiwa ni barabara nyembamba (ni sawa na barabara za reli zilizopo Zambia na kusini mwa Afrika) kati ya Dr es Salaam na Kapiri Mposhi Zambia, kati ya kilomita hizi, kilomita 969 au maili 602 zipo Tanzania na kilomita 891 au maili 554 zipo Zambia. Reli hii si sehemu ya shirika la reli Tanzania, na kwasababu ya utofauti wa geji basi hakuna uingiliano na barabara nyingine za reli. Lipo eneo la kupokea na kusafirisha mizigo katika kontena kati ya TAZARA na shirika la reli Tanzania katika Kidatu karibu na Morogoro. Hii inaruhusu kontena kusafirishwa kutoka maeneo ya mbali hadi kutoka Uganda na Kenya kupitia kivuko katika ziwa Victoria na kutoka eneo la Kidatu kuelekea reli ya kusini mwa Afrika kuptia Zambia.

Safari ya Treni kutoka Dar es salaam mpaka Mbeya
Safari ya Treni kutoka Dar es salaam mpaka Mbeya
  • Bandari ya Dar es Salaam – kilomita 8 kutoka TRC
  • Kidatu – inakatisha muunganiko na shirika la reli Tanzania, ikiwa na sehemu ya kupokea na kusafirisha kontena.
  • Mbeya
  • Mpaka wa Tunduma – Zambia

Usafiri wa Reli maeneo ya mjini – Reli ya abiria Dar es Salaam

Historia

Kabla ya uzinduzi, Dala dala ilikuwa ndiyo njia pekee ya usafiri wa umma ndani ya mji.

Uzinduzi

Safari ya uzinduzi ilianza tarehe 29 mwezi wa kumi 2012. Watu hupendelea zaidi kuiita Treni ya Mwakyembe kwa heshima ya  Harrison Mwakyembe, waziri wa Uchukuzi na Usafirishaji wakati huo.

Gazeti la Citizen lilitoa taarifa mwezi wa kwanza 2013 kwamba “Zambia ilipinga” mradi huu kutumia reli ya TAZARA kwa madai ya kwamba mradi haukuandaliwa vizuri. Maafisa wa Zambia walisisitiza suala hili kupelekwa katika bodi ya wakurugenzi kwaajli ya kuidhinishwa kwasababu serikali zote ni wanahisa wenye hisa sawa. Waziri Mwakyembe alikataa tuhuma hizi akisema kwamba taratibu zote zilifuatwa. Mjumbe katika bodi ya TAZARA asiyependa kutambulika aliongelea kuhusu jambo hili kwakusema walishindwa kukutana kwaajili ya mkutano wa robo ya mwaka kwa miezi sita iliyopita.

Taasisi ya Ugavi na Usafirishaji ilitoa tuzo kwa Mwakyembe mwezi wa kumi na mbili 2013 kwakuanzisha huduma hii.

Tanzania Railways Limited (TRL) ilizinduliwa tarehe 1 mwezi wa nane 2016, ikihudumu safari ya uwanja wa ndege mara 3 muda wa asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi na mara 3 muda wa jioni kuanzia saa 9:55 jioni.

Njia tofauti za usafiri wa reli

Njia ya TRL

Reli ya Tanzania (milimita 1,000 (futi 3 inchi 3/8)) inahudumu kutoka stesheni ya Pugu kwenda mjini kupitia Gongo la Mboto, FFU Mombasa, Banana, Karakata(Uwanja wa ndege), Vingunguti Mbuzi, SS Bakhresa, Kamata (stesheni ya Kariakoo BRT) na mwishowe kufika mjini.

Stesheni ya Treni ya TAZARA jijini Dar es salaam
Stesheni ya Treni ya TAZARA jijini Dar es salaam

Reli ya TAZARA

TAZARA (milimita 1,067 (futi 3 inchi 6)) inatoa njia mbili katika mtandao wa kilomita 20.5. Ya kwanza ni kutoka katika kituo cha Dar es Salaam hadi Mwakanga ambayo imepita katika viunga vya mji. Inaishia Kwa Fundi Umeme, Kwa Limboa, Lumo Kigilagila, Sigara, Kitunda road, Kipunguni B, Majohe na Magnus. Ya pili inatoka katika kituo chache cha Dar es Salaam hadi Kurasini kupitia Kwa Fundi Umeme, Yombo, Chimwaga, Maputo, Mtoni Relini na Kwa Aziz Ali Relini.

Uendeshwaji

Huduma inapatikana wakati wa asubuhi na jioni katika siku zote za wiki (ukitoa Jumapili pamoja na sikukuu za kitaifa)

Bei ya Tiketi

TRL na TAZARA ilipendekeza nauli nafuu ya shilingi 800 (US$0.50) na 700 kila moja kwa safari moja. Hatahivyo, mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra) ikaweka nauli ya watu wazima shilingi 600 (US$0.27) NA 500 wakati wanafunzi wakilipa shilingi 100 (US$0.07).

Fedha

Mwezi wa Tano 2013, reli ya TAZARA ilitoa ripoti kuongezeka kwa mapato kutoka shilingi milioni 40 hadi milioni 50.

Hadi kufikia mwezi wa kumi na moja 2013, TRL ilikuwa inajiendesha kwa hasara. Ina gharimu shilingi milioni 4 kila siku kuendesha sehemu hii wakati mapato ni shilingi milioni 2. Gharama kubwa za uendeshaji zimekuwa zikichangiwa na injini na magari moshi ambayo si gharama nafuu kwa safari fupi.

Upanuzi katika kipindi cha baadaye

RAHCO, kampuni inayoshikilia hisa za TRL, ilitoa zabuni mwezi wa tisa 2013 ikikaribisha zabuni kwaajili ya upembuzi yakinifu kuhusu muundo wa barabara mpya ya reli kutoka katika kituo kikuu kwenda vituo vinne: Lugurunu (Morogoro Road), Chamazi (Kilwa Road), Pugu (kupitia Julius Nyerere International Airport) na Kerenge.

Matukio

Tarehe 26 mwezi wa kwanza 2015, reli ya TAZARA ilienda mrama na kupita njia iliyokosewa.

Kwa nakala zaidi zinazohusu usafiri bofya hapa!