Imani za Kila Maasai na Tamaduni Zao

Imani za Kila Maasai na Tamaduni Zao

Orodha ya Yaliyomo

Imani za Kimaasai

Wamaasai huamini katika Mungu anaeitwa ‘Nkai’, Mungu aliyepo kila mahali, japokuwa hawana uwezo wa kujua umbo wala nia yake, anaweza akadhaniwa kuwa na sifa zinazofanana na za mwanaadamu mzee sana. Heshima, maarifa yanayotokana na kuishi miaka mingi na

Mungu wa Maasai - Ngai - Nkai
Mungu wa Maasai – Ngai – Nkai

uwezo wake wa kitamaduni katika kubariki na kulaani umuongeza heshima Mungu huyu mwenye nguvu na anayeyajua yote.

Uwepo wa Imani za kimaasai za kichawi unajidhihirisha hasa katika wakati wa majanga na kujitoa muhanga, baadhi ya wazee wanadhaniwa kuwa wachawi na wamekuwa wakiogopwa kwa tabia zao zenye hila za kuombea watu mabaya, kupenda ushindani  na kuchukia mafanikio ya wenzao.

 

Wafuasi wa imani za Kimasai

Wasiwasi mkubwa ulioenea kuhusu uchawi unahusisha ukoo wa kinabii wa Loonkidigi. Katika kila eneo kuna nabii ambaye huwa anawasaidia washiriki wake kukabiliana na uchawi wa kawaida kwa kuwapa dawa za kinga na ushauri kwa ajili ya sherehe zao za kitamaduni. Nabii anahofiwa na kuchukuliwa kama mungu-mtu wakiamini kwamba ana uwezo wa kuona kila kitu na hivyo nguvu yake ya kukabiliana na uchawi hudhaniwa inatokana na ufahamu wake wa uchawi kama

Waumini ya dini ya kimasai
Waumini ya dini ya kimasai

Loonkidongi, kuna mitazamo maarufu yakushangaza dhidi ya washiriki wengine wa koo hizi. Loonkidongi huwa wanaishi katika makoloni madogo kwenye mipaka katikati ya sehemu za makabila, ambapo wanashukiwa kutenga eneo la uzazi kwa ajili ya watu wasioridhika, ulogana wao kwa  wao  na hata kuuza kwa siri hirizi mbaya kwa wachawi wa Kimasai.

 

Sherehe

Kunakuwepo na sherehe kadhaa zinazofuatana pale mashujaa wanapoingia kwenye kundi la wazee. Sehemu ya kwanza ya sherehe hizi ni sherehe ya enoto, ambapo mashujaa wanapandishwa hadhi ya kuwa mashujaa waandamizi. Ili kuhudhuria hafla hii mashujaa hawa wanatoka katika vijiji vyao na kuunda kijiji kimoja. Wakiongozwa na kiongozi wa kitamaduni (olotuno), ambae katika imani za kimaasai wakati mwingine huwa anadhaniwa kubeba laana zao na hivyo inatabiriwa kuwa atakufa mapema au kuishi maisha ya kimasikini. Baada ya eunoto kila shujaa urudi kijijini kwa baba yake akiambatana na mama yake. Sehemu ya pili ya sherehe hizi za kufikia umri inaitwa olghesher, ambapo mashujaa hawa  wanaunganisha mikono ya kushoto na kulia na kupandishwa kwenda kwenye hadhi ya uzee. Kwa pamoja huku wakipewa uwezo wa kubariki na kulaani na kuwa waangalizi wa makundi ya kiumri ya kizazi kijacho.

Tamaduni hizi za imani za kimaasai zinazohusu ibada za umri pia utumika kuunganisha shirikisho hili la Wamaasai kama watu. Sehemu za Keekonyukie kaskazini na Kisonko kusini, kila moja ina jukumu kuu la kuunganisha Maasai kupitia huu mfumo wa umri. Kuelekea katika kipindi hiki cha kufikia umri Wamaasai wote uelekea kaskazini wakingojea ishara ya ibada kutoka kwa Keekonyukie, wavulana kutoka kaskazini hufanya mashindano ya kunyang’anyana pembe ya ng’ombe, mara baada ya tukio hili la kitamaduni kumalizika ndipo kundi hili la umri uapishwa na kuunganishwa na sehemu nyingine za kabila. Miaka ishirini na mitano baadaye Kisonko ndiye mwenye jukumu la kufanya olghesher kuwapandisha vyeo na kutoa jina maalumu kwa  kundi hili la umri litakalokubalika na kutumika na Wamaasai wote. Wakati huo huo, makundi mengine ndani ya kabila inabidi yasuburi zamu yao kabla na wao kufuata. Njia hizi mbili za kitamaduni zinafanywa kwa kupokezana kati ya kaskazini na kusini, na kati ya muungano wa fimbo za moto (makundi ya kiumri) ambayo urudiwa kila baada ya miaka kumi na mitano, na kutoa mwelekeo wakati na sehemu muafaka kwa Wamaasai, wakimaliza mafunzo yao ya maisha kama watu binafsi na kuendeleza umoja wao.

Sherehe za wanawake zinafanyika mahususi kutokana na wasiwasi walionao juu ya masuala ya uzazi, na katika nyakati hizi uchezaji wao wa ngoma ni sehemu muhimu sana ya sherehe. Hizi ngoma wakati mwingine uishia na maonyesho ya hasira na hata vurugu dhidi ya wazee, pia ngoma hizi utowa fursa ya kubadilisha manyanyaso yaliyopo dhidi ya wanawake. Hata wazee katika imani za kimaasai uamini kuwa ngoma hizi zitatatua matatizo ya uzazi na kurudisha maelewano katika jamii.

 

Sanaa

Bidhaa mbalimbali za sanaa za kimaasai
Vikapu vya kimaasai

Sanaa ya maonesho katika jamii ya Wamasai uzingatia sana mapambo ya mwili na shanga ambazo huvaliwa na mashujaa,  zinazoendana wasichana na wanawake vijana wanaovalia shanga hizo kwenye mavazi ya bibi harusi. Mapambo haya yanaonyeshwa sana katika muziki na ngoma zao za mashindano ambazo ni maarufu sana katika jamii yao. Wazee huwa hawashiriki kucheza katika ngoma hizi bali wao utowa sauti na ishara zinazo fafanua misemo yao huku zikiendana na midundo ya ngoma, wakiwavutia watazamaji kwa kuonyesha mitindo ya majivuno waliyojifunza kipindi cha ngoma za ujana wao wakiwa mashujaa.

 

Dawa

Pamoja na unabii, washiriki wadogo wa ukoo wa Loonkidongi utumika kama waganga na katika imani za kimaasai inaaminika kuwa wana uwezo wa kugundua magonjwa na sababu za mikosi, utowa dawa na tiba mbalimbali za kitamaduni. Siri zao zinalindwa ili zisijulikane na Wamasai wengine zinahusishwa na sumu mbalimbali ambazo zipo ndani ya nguvu zao za uchawi, endapo watakasirishwa.

 

Kifo na maisha baada yakifo

Wamasai hawana utamaduni wakufanya misiba na pia imani za kimaasai zinaonyesha kwamba hawaamini katika maisha baada ya kifo. Walakini, kwa mzazi kuacha warithi inashiria ameishi maisha ya kujitolea kutunza familia kwa umakini jambo linatoa tumaini kwa mwendelezo wa kizazi chake. Kwa upande mwingine kutokuacha mrithi yeyote kunapelekea kusahaulika na uonekana kama laana.

Kwa nakala zaidi zinazohusu kabila la kimaasai bofya hapa!