Vitu vya Kweli 10 vya Kuvutia Kuhusu Kabila la Maasai

Vitu vya Kweli 10 vya Kuvutia Kuhusu Kabila la Masai!

Orodha ya Yaliyomo

Kabila la Masai ni la watu wanaopatikana Afrika ya mashariki. Ni maarufu ulimwenguni kwa tamaduni yao ya kipekee na “kivutio maarufu cha kitalii” kwa watu wanaotembelea eneo hilo. Mimi binafsi, naliona ni la kuvutia! Kwahiyo leo ninakushirikisha kujuwa vitu vya kweli kumi kuhusu kabila la Masai!

#1 Kabila la Masai linaishi zaidi ya nchi moja.

Maasai wakiimba na kucheza - Ngorongoro Tanzania
Maasai wakiimba na kucheza – Ngorongoro Tanzania

Mara nyingi, makabila ni maalum katika eneo moja. Hata hivyo, kabila la Masai linaishi mashariki, kati na kusini mwa Kenya vile vile kaskazini mwa Tanzania! Kwa mujibu wa ripoti kuna zaidi ya wamasaai 840,000 waishio Kenya, na wasiopungua 800,000 Tanzania. Pamoja na idadi yote hii , haishangazi kwamba kuna vitu vya kweli vingi vya kusisimua kuhusu kabila ya wamasai.

Ingawaje, hizi ripoti haziwezi kuaminika moja kwa moja. Inaonekana, wamasai wengi Kenya wanaona sensa ya taifa kama ni ‘kuingiliwa na serikali na kufanywa kwa makosa ya kuhesabiwa kwa makusudi. Zaidi ya  hili, Tanzania hawafanyi sensa ya kwa mujibu wa makundi ya kikabila – hivyo ni vigumu kukadiria ni wamasai wangapi wanaishi Tanzania.

#2 Kabila la wamasai linaundwa na sehemu kumi na sita.

Neno sehemu kwa kimasai ni ‘Iloshon’- hivyo kuna Iloshoni kumi na sita katika jamii ya kimasai.

Ambazo ni:

  • Ildamat
  • Ilpurko
  • Ilkeekonyokie
  • Iloitai
  • Ilkaputiei
  • Ilkankere
  • Isiria
  • Ilmoitanik
  • Iloodokilani
  • Iloitokitoki
  • Ilarusa
  • Ilmatatapo
  • Ilwuasinkishu
  • Kore
  • Parakuyu
  • Ilkisonko (pia wakati mwingine hufahamika kama Isikirari)

#3 Damu ni sehemu ya mlo wa kimasai.

Maasai wakichoma ng'ombe mshale kutowa damu ya kunywa
Maasai wakichoma ng’ombe mshale kutowa damu ya kunywa

Kwa sehemu kubwa, wamasai wanaishi kwa kutegemea maziwa na nyama ya mifugo yao. Hivi ndivyo wanavyopata virutubisho vya protini na karoli.Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya wamasai wameongeza aina nyingine za vyakula katika mlo wao: chakula cha mahindi, viazi, mchele na kabichi. Ingawaje Kulingana na jadi, jambo hili halikubaliwi. Hii ni kwa sababu wamasai wanaona kutumia ardhi kwa ajili ya kilimo cha mazao ni kama uhalifu n ani kinyume na uoto wa asili kwa vile inafanya ardhi isifae kwa malisho ya mifugo.

Na hapo kuna damu! Wamaasai hunywa damu katika matukio mbalimbali: wanapokuwa wagonjwa, punde tu wanapotahiriwa au punde tu wanapojifungua. Baada ya Ilamerak (neno la kimasai linalohusu wazee ) pia hunywa damu kuzuia uchovu baada ya kunywa kilevi. Sio tu kwamba damu ina protini nyingi, ni nzuri pia kwenye mfumo wa kinga. Hata hivyo idadi ya mifugo inapopungua, hamu ya damu inakuwa ndogo. Hii ni hakika moja wapo ya ukweli wa kabila ya Kimaasai.

#4 Wamasai wameitwa kutokana na lugha yao wenyewe.

Jina Masai kifasihi humaanisha “mtu anayeongea lugha ya Maa”. Lugha yenyewe ni sehemu ya tawi la watu wa Naili (Neolithic) mashariki ya familia ya lugha ya Nilo- Sahara. Ni lugha inayozungumzwa zaidi, kadri jinsi kabila linavyoweka umuhimu katika matamshi. Na kuendelea, kuna kamusi ya kimasai, pia Biblia imetafsiriwa kwa kimasai.

Kuna takriban lugha 36 za Nilo-Sahara, Kimasai ni moja apo. Watu wa kimasai hujifunza kiswahili na kingeraza shuleni. Hizi ni lugha za Kenya na Tanzania hususani.

#5 Wamasai wana mavazi yao ya kitamaduni.

Kawaida watu wa kimasai uvaa mashuka mekundu. Haya huitwa “shuka”. Yanafungwa kuzunguka mwili. Na uvaa shanga nyingi. Kutokana

Msichana wa Kimasai mwenye mavazi ya rangi za kitamaduni na shanga
Msichana wa Kimasai mwenye mavazi ya rangi za kitamaduni na shanga

na matukio, mashuka haya huweza kuwa na rangi tofauti tofauti. – japo katika sehemu kubwa ni mekundu. Pia, wanaume na wanawake uvaa karibia sawa.

Kabla ya uanzilishi wa “shuka”, watu wa kimasai walivaa ngozi za wanyama ambapo ni kawaida ya makabila ya maeneo haya ya hii dunia.

Pia ni kawaida kwa watu wa kimasai kuwa na matobo makubwa masikioni. Hii ni kawaida ya makabila mengi kama unavyoweza kuona katika picha za makabila mengine. Walakini, wamasai ufanya tofauti kidogo. Wakati makabila mengi uziba na mbao walipotoboa, wamasai ujaza matobo yao makubwa na shanga pamoja na hereni moja ya kuambatanisha kimtindo.

#6 Wamasai ujivunia ng’ombe zao.

Kabila la Kimasai uishi maisha ya kuhamahama. Hivyo, uhama sehemu hadi sehemu kwa mzunguko wa msimu. Wanafanya hivi ili wawe siku zote na malisho ya kijani kibichi na ardhi yenye rutuba kwa mifungo: ng’ombe, mbuzi, kondoo na punda.

Licha ya kuwa na wanyama wengine, ng’ombe hasa ndio maalum kwa watu wa kimasai. Katika jamii yao, ipo imani kwamba ng’ombe wote duniani ni wakwao. Vijana wa kimasai utumia ujana wao mwingi kukusanya ng’ombe!

Kama mmasai, utajiri na hali katika jamii upimwa na idadi ya ng’ombe alionao.

Kutokana na uwezo wao wa kuzoea mazingira tofauti tofauti, kabila la kimasai utegemea zaidi ng’ombe. Maziwa, nyama, jibini (na damu) inayofanya mlo wa kimasai utokana na ng’ombe, na nguo na magodoro wanayo vaa/tumia mara nyingi utengenezwa na ngozi ya ngombe. Sio hivyo tu lakini wana “manyata” neno la Maa lililo na maana nyumbani, ambazo zina kuta na madirisha yanayotengenezwa na kinyesi cha ng’ombe!

#7 Kuna dini tofauti ndani ya kabila la masai.

Kitamaduni, kabila la kimasai wamekuwa na imani ya Mungu mmoja daima,  ambaye jina lake ni Enkai au Engai. Mungu huyu anaasili ya kile kinachojulikama kama asili mbili (duel nature), na zina majina tofauti kidogo:

Engai Narok, au mungu mweusi – yeye ni mwema.

Engai Nanyokie, au mungu mwekundu – yeye ni mwenye kulipiza kisasi.

Hata hivyo, katika miaka ya karibuni washiriki wengi wa kimasai wamekuwa wanafuata dini ya wakristo. Wachache japokuwa sio wengi, wamebadili kuwa na imani ya kiislam.

#8 Kabila la masai ni la ndoa zenye mke zaidi ya mmoja.

Ndoa ya kimaasai
Ndoa ya kimaasai

Katika tamaduni ya Kimasai, mwanamke akiolewa anaoa kikundi kizima cha watu wenye umri sawa na mumewe. Mara nyingi wazee wa kabila upanga ndoa hizi. Kitamaduni, wanaume huwa (au walikuwa, japo inapoteza umaarufu) wanategemewa kutoa vitanda vyao kwa mgeni mwanaume. Mwanamke wa nyumba hio anaweza kulala na huyo mgeni kitandani, iwapo atachagua.

Vitu vingine vya kuzingatia kuhusu ndoa za kimasai ni kwamba mwanamke huwa ni mdogo zaidi ya mumewe. Hii umaanisha kabila la kimasai lina wajane wengi. Hawategemei kuolewa tena, jukumu la mwanamke katika ndoa umasaini ni kuzaa na kuwa na watoto.

#9 Watoto wa kabila la masai hawapewi majina mpaka miezi mitatu ya mwaka.

Sababu ya vifo vingi kwa wachanga na watoto katika jamii ya kimasai, watoto hawapewi majina mpaka watakapofikisha miezi mitatu. Pia kuna sherehe maalum ya kuwapa majina watoto wa kimasai. Hii ufahamika kama Enkipukonoto Eaji ambayo inatafsirika kama ” kutoka katika kipindi cha kutengwa”. Kabla ya sherehe, mama na mtoto utengwa na kuruhusu nywele kuota kuwa ndefu. Unyolewa baada ya sherehe. Hii ni ishara ya mwanzo mpya kwa mtoto.

#10 Wamasai wana  kalenda yao wenyewe.

Tarehe za msimu wa kimasai.

Kalenda ya kimasai inaweza changanya kidogo kutokana na kwamba hamna sheria za kimataifa zinazohusu majina ya miezi 12 wala maelewano juu ya mwezi upi ufata upi,” japo kila mtu anajua kuna miezi 12 na siku thelathini za kila mwezi. Siku 15 za mwanga na siku 15 za giza na siku ya 8 ujulikana kama ” siku ya kubadilika”

Kwa sababu hio, mchanganyiko mwingine ujitokeza mwishoni mwa kila mwezi ambapo siku mbili za mwisho wa mwezi zina mabishano kutokana na kwamba mwezi ” umekwisha chukuliwa” au kama ” bado” haujachukuliwa. Kuna misimu mikuu 3: mvua za muda mrefu, msimu wa manyunyu, na mvua za muda mfupi.

Mvua ndefu – Nkokua.

  1. Oladalu – Mwezi wa joto na jua kavu.
  2. Arat – Mwezi wa uhaba ambao mvua chache zinaponyesha usababisha mabwawa kusambaa kwenye mabonde.

3.Oenioing’ok   – Ng’ombe dume huwa wakali na kufukuza mifugo nyumbani nyakati za mchana. Inabidi wafungwe na kuachwa nyumbani.

  1. Olodoyiorie – Pia hufahamika kama Nkokua, mwezi mnyevu sana. Usiku vikundi vidogo vya nyota zinazojulikana kama jembe (Nkokua) uonekana.

Baada ya hii msimu mwingine unaanza, kipindi cha manyunyu, msimu wa katikati ya mwaka.

Msimu wa manyunyu – Oloirurujuruj

  1. Oleilepunye – Bado kuna unyevu lakini mvua huwa zimepunguwa.
  2. Arat – Maeneo yote ya vijijini uwa yana kijani kizuri na eneo la malisho huwa na viwavi vyenye nywele.
  3. Morusasin – Kunaweza kuwepo na mvua ya mawe kama kukinyesha, lakini mawe yake ni madogo sana.
  4. Oloiborraine – Mabwawa ya maji huwa wazi.

Mvua za muda mfupi – Oltumuret.

  1. Kushin – Ndege weupe kidogo na weusi, ambao ula katikati ya ngombe, utokea.
  2. Olgisan – Mvua unyesha maeneo ya nyanda za juu.
  3. Pushuka – Mimea kadhaa uota, miti mingi udondosha majani yake na maua utokea.
  4. Ntung’us – Huu ni mwisho wa mwaka.

Kwa nakala zaidi zinazohusu kabila la kimaasai bofya hapa!