Mabasi ya Mwendokasi Jijini Dar es Salaam

Vitu Muhimu Kuhusu Mabasi ya Mwendo Kasi Jijini Dar es Salaam

Orodha ya Yaliyomo

Mfumo wa usafri wa mabasi ya mwendo kasi Dar es Salaam, ni mfumo ulioanza kazi Dar es Salaam Tanzania, tarehe 10 Mei 2016. Mfumo huu wa usafiri unajumuisha awamu  6 na awamu ya kwanza ilianza kujengwa April  2012 na kampuni  ya ujenzi  ya  Austria ya ‘Strabag International GmbH’.   Ujenzi wa awamu ya kwanza ulikamilishwa Desemba 2015 kwa jumla ya gharama ya Euro (fedha ya umoja za nchi za ulaya) milioni 134  zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania.Awamu hii ya kwanza ya mradi ni ya urefu wa kilomita 21.1 ambayo ina barabara mahsusi katika njia kuu tatu yenye stesheni 29 za basi.Mfumo wote huu wa usafiri uko chini

Msongamano wa Magari Dar es salaam
Msongamano wa Magari Dar es salaam

ya uangalizi wa Usafiri Salama Dar es Salaam, Rapid Transport (UDART)chini ya uangalizi wa Shirika la Uangalizi wa Usafiri Nchi Kavu na Baharini (SUMATRA).Kwa sasa, barabara zinahudumiwa na mabasi  140 yaliotengenezwa Uchina, aina ya Golden Dragon zikitoa huduma ya express na  huduma za kawaida kwa masaa 18 kila siku kuanzia saa 11 asubuhi mapaka saa 5 usiku.

Historia

Kutokana na ongezeko la kasi la watu katika jiji, Serikali ilianza kuchora  mpango wa mfumo wa usafiri wa mwendo kasi mwaka 2003.Serikali ilitabiri ongezeko la watu kukua zaidi ya milioni 5 ifikapo mwaka 2015 hali iliyoleta umuhimu wa kukaribisha Taasisi ya ushirikiano wa Kimataifa wa Japan (JICA) kuweka mpango mama wa  usafiri katika mji huu Juni 2008. Ikapendekezwa mifumo ya usafiri wa mabasi ya mwendokasi na usafiri wa mfumo wa ‘metro’ ila usafiri wa ‘metro’ haukupitishwa maana ulikuwa na gharama kubwa za ujenzi na uendeshaji.Mradi ukawekwa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu chini ya kitengo Cha Usafiri wa Mwendokasi na Dar (DART) ikajengwa chini ya notisi ya Serikali tarehe 25 Mei 2007.Kilomita 130 za mwendo kasi zikapangwa zihudumie 90% ya idadi ya watu katika jiji na mradi ukagawanywa katika awamu sita, kulingana na gharama kubwa ya uwekezaji iliyohitajika.Gharama za awali za mradi ziligharimiwa na Benki ya Dunia, iliyotoa $ milioni 180 kujenga awamu ya kwanza ya mradi.

 

Awamu za Mradi 

Awamu ya kwanza

Awamu ya kwanza ya BRT ni ya kilomita 21 inayotoka Kimara mpaka Ubungo na kuishia Kivukoni/Morocco.Ujenzi wa awamu ya kwanza ulianza Aprili 2012 na kukamilika Desemba 2015 na kampuni ya ‘Strabag International GmbH’. Njia hii imejengwa kubeba wasafiri 300,000 kwa siku katika stesheni 29 za basi.Njia hii ina kilomita 21 za barabara kuu na  na kilomita 57.9 ya barabara lishi (barabara zinaingia na kuungana na barabara kuu), vituo vikubwa 5 na stesheni  29.Njia hii iliwekwa kwenye matumizi ya muda mfupi mnamo Aprili 24 2015 na kuwekwa rasmi katika matumizi kamili 10 Mei 2016 baada ya makubaliano ya nauli.

Matumizi ya Muda Mfupi

Tarehe 24 April 2015, Shirika la Usafiri wa Mwendokasi Dar (UDART) ilisaini mkataba na UDAR-RT wa kutoa huduma ya Usafri wa Mwendokasi Dar es Salaam. UDA-RT ni taasisi maalum iliyoundwa na UDA na mashirika mawili ya Daladala, Shirika la Waendeshaji na Wenye Mabasi Dar es Salaam (DARCOBOA) na UWADAR, kutoa hizi huduma za usafiri kwa muda. Huduma hizi za muda zilikusudiwa kutoa mafunzo kwa waendeshaji wa baadae na kuwajengea  wazawa uwezo wa kuendesha mradi. Katika kipindi hiki cha muda, Daladala zilikuwa zikendelea na usafirishaji katika barabara hizi.

Awamu ya Pili

Fedha za awamu ya pili zilpatikana Oktoba 2015. Awamu ya pili itakuwa ya Km 19 kutoka Kilwa mpaka Kusini  Kawawa  kupitia Kinondoni na itagharimu $ milioni 160 . Benki ya Maendeleo ya Afrika imekubali kugharamia $ milioni 141 ya mradi huu, na fedha zinazosalia zitatolewa na Selikali. Ujenzi wa mradi utaanza Juni 2019 na utachukua takriban miezi 36 kukamilika. Ujenzi wa mradi huu utahusisha na ujenzi wa barabara za juu mbili. Ujenzi wa Km 20.3 wa DART utaanzia Gerezani na Kituo cha BRT, Halmashauri ya Jiji, Itahusisha Barabara ya Kilwa, Barabara ya Changombe, Barabara ya Kawawa , Mtaa wa Gerezani, Uwanda wa Sokoine, na Barabara ya Bandari. Itakuwa tayari Desemba 2020.

Awamu ya Tatu 

Fedha za awamu ya tatu zimetolewa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa (IDA).Ujenzi utakuwa kutoka Gongo la Mboto hadi mjini katikati kupitia barabara ya Uhuru kutoka Tazara mpaka Kariakoo Gerezani. Ujenzi umepangwa kuanza 2021.

Moja ya Vituo cha Mabasi ya Mwendokasi
Moja ya Vituo cha Mabasi ya Mwendokasi

Miundombinu

 

Stesheni

Kuna aina tatu za stesheni katika njia kulingana na stesheni  ilipo na njia inayotumika: 

  • Vituo: Vituo viko katika mwanzo na mwisho wa barabara kuu.Vituo vinaruhusu uhamisho kutoka

barabara lishi na pia kutowa huduma mbalimbali za usafiri kama mabasi ya kanda na usafiri binafsi. Vituo vina maegesho ya magari kuruhusu watu kuegesha magari nyakati za mchana.

  • Stesheni za barabara kuu: Hizi ni stesheni kuu katika barabara kuu. Zinafikika kwa njia za waenda kwa miguu na zimejengwa kwa juu ili kuhakikisha usalama wa abiria.Kuna aina nne za stesheni kwenye barabara kuu zikiwa na nafasi ya mita 500 kati ya stesheni na stesheni(A,B,C na D) kutegemea na uhitaji wa wasafiri.
  • Stesheni za barabara lishi: Hizi stesheni zinawarushusu abiria kuhama kutoka barabara lishi mpaka vituo kwenye barabara kuu.

Mabasi

Mfumo wa BRT unaendesha mabasi 140 aina ya Golden Dragon.Kuna aina mbili ya mabasi yanayoendeshwa katika barabara, moja ina urefu wa mita 18 na uwezo wa kubeba abiria 150 na nyingine mita 12 na uwezo wa kubeba abiria 80

Njia na Vituo

Kuna awamu sita zilizopangwa ambazo zitahudumia 90% ya idadi ya watu na kwa sasa awamu ya kwanza ndio inayofanya kazi. Awamu ya pili iko katika ujenzi.

  • Awamu ya Kwanza kutoka Kimara mpaka kaskazini Kawawa mpaka Mtaa wa Msimbazi kumalilizikia Kivukoni km 20.9.
  • Awamu ya Pili kutoka Kilwa mpaka Kivukoni jumuisha Kusini Kawawa mpaka Barabara ya Kilwa km 19.3.
  • Awamu ya Tatu Kutoka Uwanja wa ndege mpaka Mtaa wa Uhuru kupitia Barabra ya Nyerere km 23.6.
  • Awamu ya Nne kupita Barabara ya Bagamoyo na Barbara Sam Nujoma km 22.8.
  • Awamu ya Tano Kupita Barabara ya Mandela  km 22.8.
  • Awamu ya Sita Kupita Barabara ya Zamani ya Bagamoyo: km 27.6.

 

Tuzo 

2017: Taasisi ya Sera ya Usafiri na Maendeleo: Tuzo ya Usafiri Endelevu.

2018: Taasisi ya Sera ya Usafiri na Maendeleo: Tuzo ya Usafiri Endelevu Ulimwenguni.

Kwa nakala zaidi zinazohusu usafiri bofya hapa!