Dawa za Asili Tanzania

Utafiti wa Kuboresha Tiba za Jadi na Mtafiti Rebecca Marsland

Orodha ya Yaliyomo

Mazungumzo na Waganga

Rebecca Marsland kutoka chuo cha Edinburgh, Uingereza ameeleza kwamba waganga ambao aliozungumza nao kwenye utafiti wake wengi walipendezwa sana na fursa ya kujifunza jinsi ya kuboresha dawa zao. Walisema kuwa wangetamani kuwa na teknolojia ya kuandaa dawa zao kwa njia ya vidonge. Hii ingewasaidia kuhifadhi dawa zao kwa muda mrefu. Kwa hali ilivyo, utayarishaji wa dawa za asili ni biashara ndefu. Huko Kyela, mahali pa karibu zaidi kupata dawa ni juu katika Milima ya Livingstone ambayo inapakana na pwani ya kaskazini ya Ziwa Nyasa. Hii ni safari na inachukua siku kadhaa kwa miguu. Mganga Mzee Richard aliniambia hii ndio sababu ambayo hakutaka mtoto wake

Mganga wa Kienyeji Tanzania
Mganga wa Kienyeji Tanzania

amfuate na kuwa mganga. Alimtaka awe na maisha bora kuliko haya, alielezea zaidi kuwa safari hizi za kwenda milimani zilikuwa ngumu. Safari hii ya kuchosha sio tatizo la mwisho kwani ukirudi nyumbani, wakati huo huo unabidi kukabiliana na foleni ndefu za wagonjwa wanaosubiri dawa. Alisema kuwa kutoka asabuhi anavyoamka hakuna hata muda wa kuoga hadi jioni ambapo mgonjwa wa mwisho ndio anapoeenda nyumbani.

Mganga mmoja ambaye hufanya dawa za Kiislamu na pia hutumia miti shamba alielezea hitaji la teknolojia mpya kama ifuatavyo:

Lengo letu katika matibabu yetu ya kutumia tiba za jadi ni kujua jinsi ya kupunguza magonjwa mbalimbali ambayo hupunguza umri wa kuishi wa wanadamu – hii ina maana na kuashiria kwamba tunachohitaji ni msaada mkubwa – kwa mfano, iwapo mgonjwa analala nyumbani kwetu, lazima alale bila chandarua, mara nyingi bila ngao [jina la dawa ya wadudu inayotumika ‘kutibu’ vyandarua], na kwa hivyo hii inamaanisha kuwa tunaondoa ugonjwa mmoja, ambao unarithiwa na mwingine. Kwahiyo basi, kuna vitu vingi ambavyo waganga wanahitaji msaada, kwa mfano wanahitaji mashine ya kuwasaidia kusaga dawa zao kuwa poda, na kuzigeuza kuwa vidonge. Katika umbo hili tunaweza kutumia ‘njia fupi’, kwa sababu kwa mfano, unaweza kuitwa kutibu mgonjwa huko Mwanza, lakini mmea ambao unahitaji kutibia haupatikani Mwanza, na kila ukisafiri unahitaji kuwa na madawa, mizizi na vifurushi vingi vya mimea … huwa tunachimba vya kututosha kwa siku tatu – hali hii tata mara nyingi uishia kwa dawa kuisha au kuoza – kwa sababu zinalowa sana, kwa hivyo tunahitaji utaalamu wa serikali au mtu atusaidie kutengeneza vidonge, na mashine za kusaga poda, na kukandamiza. Kwa njia hizo dawa zetu zitakuwa haziharibiki – hiyo itatusaidia sana.

Tofauti ya Dawa za Kisasa na za Jadi ni Ndogo

Kwa hivyo, kwa mtazamo huu, hakuna tofauti kubwa kati ya kuchimba mizizi na matibabu kwa kutumia njia ya kugawa vidonge – ni kitu kimoja, lakini moja ni kazi kubwa zaidi kuliko nyingine. Baada ya kazi hii yote, dawa zingine zinaweza kuoza (ingawa zingine huweza kubaki na nguvu zake kwa miaka kama zimeandaliwa na kuhifadhiwa kwa usahihi). Waganga pia waliniambia kwamba wangependa kuwa na utaalam wa kujua jinsi ya kupima (kupima) dawa zao, ili waweze kupata kipimo kizuri zaidi kwa watu. Kwa sasa hawana chaguo ila kwenda na uzoefu wao wenyewe.

Wasiwasi huu wa kupima dawa za asili huko pia kwenye sayansi ya matibabu iitwayo biomedicine (tawi la dawa linalohusika na utumiaji wa

Dawa ya Jadi ya Ngetwa
Dawa ya Jadi ya Ngetwa

kanuni za biolojia na biokemia kwa utafiti wa kimatibabu au mazoezi) au taaluma ya tiba. Moja ya masilahi makubwa ya taaluma ya tiba za kisasa katika dawa za ‘jadi’ ni kutambua na kupima dawa za mitishamba, na inapowezekana, kutenganisha ‘kiungo hai’ (active ingredient) kitakachoweza kutengenezwa kwa kiwango kikubwa. Walakini, taaluma ya tiba sio peke yake iliyohusishwa katika kuchukua aina hii ya utafiti kwa lengo kuu la uzalishaji mkubwa. Tayari kuna mifano iliyofanikiwa sana ya tiba za jadi zilizotengenezwa nchini Tanzania. Dawa ‘ya jadi’ ngetwa ‘imetengenezwa katika kiwanda kaskazini mashariki mwa Tanzania na kuuzwa kwa wateja wa kimataifa. Bidhaa hiyo ilipitia miili kadhaa hadi ilipofikia umbo la unga uliosambazwa katika mifuko ya dozi moja baada ya kuidhinishwa. Ngetwa iliyokuwa katika umbo la maji ilikuwa inaharibika haraka sana. Ngetwa sasa hivi ni biashara kubwa, na inatangazwa kwenye mabango yanayoonekana sana jijini Dar es Salaam. Bila shaka mafanikio yake yatakuwa yamewapa mwamko wa kutimiza malengo zaidi waganga huko Kyela, ambapo ilipokuwa ikipatikana mnamo mwaka 2005.

Ngetwa ni kesi ya kugeuza ulimwengu kuwa kijiji . Kwani Inachukua teknolojia ya kisasa inayotumiwa kutengeneza dawa nyingi, lakini tofauti na maandalizi yanayotumika kwenye taaluma ya tiba, ngetwa sio kitu – inachukua jina lake kutoka kwa familia ya Ngetwa, na kila pakiti ina picha ya mganga ambaye alitengeneza kichocheo chake cha asili mbele. Licha ya teknolojia ya “kisasa” inayotumiwa kutengeneza, kusambaza na kuuza ngetwa, bado inaendelea kwa aina nyingine zinazoifanya itambulike kama dawa ya ‘jadi’, kwa mfano orodha ndefu na kamili ya magonjwa ambayo inaweza kutumika kutibu inawakilisha orodha ya matangazo ya dawa kwenye vibanda vya waganga katika masoko ya Dar es Salaam. Badala ya kuwa na dawa nyingi tofauti kutibu hali nyingi tofauti, ngetwa ni dawa moja tu inayotumika kutibu matatizo mengi.

Ubunifu Endelevu wa Tiba za Jadi

Ubunifu huu katika tiba za jadi sio muhimu tu kwa katika mtazamo wa uponyeshaji wake. Chanzo cha nguvu ya waganga ni mara kwa mara katika kile Rekdal anachofafanua kama ‘umbali wa kiutamaduni’ . Walakini, unaweza kuhoji pia kuwa utumiaji wa teknolojia ya ‘kisasa’ pia unaashiria morali ya kubadilisha hadhi ya hizi dawa inayopewa na taaluma ya tiba. Kama Appadurai anavyosema, ubunifu wa kiufundi ni wa kijamii na kisiasa, sio tu ya kiufundi:

Utengenezaji Dawa za Tiba za Kisasa
Utengenezaji Dawa za Tiba za Kisasa

matumizi ya vitu vya teknolojia ya hali ya juu … ni muhimu kwa mabadiliko katika muundo wa vitu. Kitu kitakachohitaji kuelezewa zaidi ni ni ubadilikaji wa thamani, hali ambayo inaashiria matumizi mapya ya udhibiti wa kisiasa wa bidhaa za ubunifu kama huo.

Kwa kutumia teknolojia na mbinu za taaluma ya tiba, waganga wanajitahidi kurudisha hadhi yao kwa msimamo mkubwa. Kwa sababu wametengwa na sera za serikali na kuachwa kwenye mijadala wa kitaifa juu ya maswala ya dharura kama VVU / UKIMWI na malaria, wanatumia (au wanatarajia kutumia) teknolojia ya biomedical kuhakikisha kuwa nafasi yao katika kituo hicho inatambuliwa. Mifano ya dawa za mitishamba inayozalishwa kwa wingi inaonyesha kwamba waganga wanatafuta njia za kujifunza kutoka kwenye teknolojia ya taaluma ya tiba kwa mtazamo wao wenyewe. Wapo makini kupima dawa zao wenyewe, lakini wanatafuta njia zingine tofauti na zile zinazotolewa na wanasayansi wa serikali ambao wamekuwa na mafanikia nao madogo mpaka sasa. Ubunifu mwingine ambao wangependa kufanya ni wa utata zaidi. Waganga wana nia ya kujifunza mbinu za taaluma ya tiba katika utoaji wa dawa, haswa kuchoma sindano au dozi za matone. Walinielezea kwamba hii itawawezesha kutoa ‘huduma ya kwanza’ kwa wagonjwa wanaofika na hali mbaya kama vile malaria kali, au ambao wamepungukiwa na maji mwilini kwa sababu ya magonjwa ya kuhara. Taaluma ya tiba, hata hivyo, inapinga haya kwa nguvu, kwani wanaogopa kwamba waganga hawana ujuzi au uwezo wa kujifunza hivi vitu, na kwamba taaluma hii ikitumiwa vibaya inaweza kuhatarisha maisha. Lakini matone na sindano pia yana thamani kubwa ya uwakilishi. Vitu hivi vinachukuliwa kuwa mbinu zenye nguvu zaidi za taaluma ya madawa ya kibaolojia ambapo mikononi mwa waganga vitachukua maana mpya, na kuziondowa zile za zamani. Matokeo ya huu “muingiliano wa kisasa” ni kitu ambacho taaluma ya tiba haiko tayari kuhatarisha.

Waganga walinialika nije kuzungumza nao kuhusu VVU / UKIMWI. Katika mkutano huo walitoa ombi la ufadhili, ambalo lilikuwa limeandikwa kwa msaada wa daktari kutoka hospitali, ili waweze kupata mafunzo ya kuwasaidia kujifunza zaidi juu ya VVU / UKIMWI, maambukizi na udhibiti wake. Pamoja na kujifunza ukweli wa kimsingi, walitaka kuhakikisha kuwa watu wote wa jamii yao huko Kyela watapata fursa ya kujifunza jinsi ya kujilinda na wagonjwa wao dhidi ya maambukizi ya bahati mbaya. Walikuwa tayari wakifundisha wanachama wao kwenye

Elimu Juu ya Ukimwi Ikitolewa kwa Wanavijiji Tanzania
Elimu Juu ya Ukimwi Ikitolewa kwa Wanavijiji Tanzania

mikutano kutorudia kutumia wembe wakati wanapotowa dawa kwa kuchanja ngozi. Walakini, pia walitaka kupatiwa glavu za plastiki zinazoweza kutupwa baada ya matumizi (disposable), haswa wakunga ambao shughuli zao zinawaweka karibu na damu nyingi mara kwa mara.Waliomba nisome pendekezo hilo, nitoe maoni, na, bila shaka, niwapatie maoni ya ufadhili. Ingawa daktari kutoka Hospitali ya Wilaya alikuwa amewasaidia kuandika pendekezo, hakukuwa na maoni kwamba ufadhili wowote ungeweza kutoka kwenye “mfuko wa wafadhili”.

Mipango kama hiyo ya ‘kushirikiana’ kati ya taaluma ya tiba za kisasa na tiba za jadi imesababisha wasiwasi juu ya ‘utawala wa kitamaduni’. Walakini, Kwa sababu hii ulikuwa ni mpango wa waganga wenyewe, inahitaji ufafanuzi wa kina zaidi. Labda hawa waganga walikuwa tayari wamesikia juu ya miradi kama hiyo na walitaka kujumuishwa. Semina za mafunzo ni jambo lililoenea sana nchini Tanzania, ni kitu ambacho hakiwezi kuonekana kama kimelazimishwa kutoka ‘nje’. Semina za mafunzo (zilizo na malipo ya kila siku) ni nyongeza kwenye kazi yoyote, kwa mshiriki yeyote katika miradi ya maendeleo. Ingawa walipendekeza mafunzo kama hayo waganga hawakuwa wakitafuta maarifa yao kubadilishwa na maarifa kutoka mahali pengine. Tayari walikuwa wamejua utaalam wao uko wapi, lakini bado walitamani kujifunza ustadi mpya. Waganga wanaonekana kuwa na mtazamo wazi wa maarifa, wanapenda ubunifu, na hawajali sana juu ya kulinda “uasili wa utamaduni” wao. Ujuzi wa tiba wa kitamaduni sio kwamba utabadilishwa na maarifa ya taaluma ya tiba ya kisasa kwa kutumia semina za mafunzo, badala yake utachagua kile kinachohitajika na kuiingiza katika maarifa yaliyopo tayari. Hili sio jambo jipya, uvumbuzi umekuwa sehemu ya ‘dawa za jadi’ angalau kwa muda mrefu tangu kuwasili kwa ‘dawa za kisasa’ katika Afrika Mashariki.

Kwa nakala zaidi zinazohusu tiba za asili bofya hapa!

Â