Lini na nini maana ya Siku ya Karume nchini Tanzania-2

Lini na nini maana ya Siku ya Karume nchini Tanzania?

Orodha ya Yaliyomo

Siku ya Karume ni siku ya mapumziko ya Umma nchini Tanzania, inayoadhimishwa kila tarehe 7 ya mwezi Aprili.

Pia inajulikana kama siku ya Sheikh Abeid Amani Karume, siku hii ni kumbukumbu ya kuuwawa kwa rais mzanzibari Abeidi Karume mwaka 1972.

Ukweli kuhusu Abeid Amani Karume

Sheikh Abeid Amani Karume (1905-1972), kiongozi wa kisiasa wa Tanzania, alikua makamu wa rais Mzanzibari wa jamhuri ya Tanzania. Alikuwa mmoja wa viongozi wasiojulikana sana Afrika.

Maisha ya awali

Sheikh Abeid Karume inaonekana alikuwa mtoto wa mwanamke mtumwa kutoka Ruanda-Urundi ambaye aliingia Zanzibar wakati mvulana huyo akiwa mdogo. Karume, alikuwa na elimu rasmi kidogo, mwaka 1920 akawa baharia anayefanya kazi katika boti za mizigo nje ya kisiwa hicho. Mwishowe alipanda cheo kuwa Serehangi. Akawa mwanachama wa Jumuiya ya mabaharia wa Uingereza, baada ya mwaka 1938 aliongoza kikundi cha boti za injini zilizobeba abiria kwenda na kutoka bandarini.

Maisha ya Siasa

Karume kwa mara ya kwanza aliingia kwenye siasa mwaka 1954 wakati alipochaguliwa kuwa Meya wa manispaa ya mji. Baadaye alikuwa rais wa taasisi ya kijamii ya wahamiaji wafanyakazi weusi iliyojulikana kama Zanzibar African Association. Mwaka 1957 kundi hili liliungana na Shirazi Association kuunda pro-British AfroShirazi Party (ASP) wakiwa na Karume kama Rais. Mwezi julai mwaka 1957, kwa kujikita moja kwa moja kwa jamii ya Kiafrika iliyounda nne ya tano ya watu, chama cha ASP kilishinda  siti nne kati ya tano katika baraza la kutunga sheria la kikoloni .

Katika miaka kabla ya mapinduzi ya mwaka 1964, Karume aliongoza ASP kupinga muungano wa utawala wa Kiarabu ambao ulionekana kuwa na nia ya kudumisha utawala wa kisiasa na kiuchumi wa jamii ya Kiarabu. Zanzibar Pemba, eneo lenye ukubwa sawa na Kisiwa cha Rhode, ilijitegemea mnamo Desemba 10, mwaka 1963. Mnamo Januari 12, mwaka 1964, wafuasi vijana wa ASP walimwangusha Sultan na kuanzisha utawala wa Kiafrika.

Wanajeshi na Viongozi wengine wakiomba dua kwenye kaburi la Abeid Karume
Wanajeshi na Viongozi wengine wakiomba dua kwenye kaburi la Abeid Karume

Karume alikuwa kiongozi wa Baraza la Mapinduzi na baadaye alikuwa rais wa Jamhuri mpya ya Watu wa Zanzibar. Alielezewa kama mtu mkubwa, mtaratibu, pia mpole, ambaye alikuwa mwaminifu, mwenye kutegemewa, na mwenye msimamo mkali hadi kufikia ukaidi. Msemaji fasaha wa lugha ya Kiswahili, Karume aliongea Kiingereza cha kusitasita. Alikuwa Muislamu mwaminifu na baba wa watoto wawili wa kiume. Jukumu lake katika mapinduzi halikuwekwa wazi; kuna madai kwamba alikuwa kiongozi asiyekuwa na maamuzi, hata mfungwa wa uongozi dhabiti ambao ulisemekana ulikuwa kwa Abdulrahma Babu, Kassim Hanga, na Hassan Moyo.

Lengo la kimapinduzi lilikuwa kuanzisha jamii yenye usawa kabisa, kwa hiyo, Rais Karume alitangaza ilani ya Zanzibar mnamo Machi 8. Hii ilitaifisha na kugawanya ardhi, asilimia 80 ilishikiliwa na Waarabu, ambao walikuwa asilimia 13 ya idadi ya watu.

Aprili mwaka 1964 Karume alifanya majadiliano kuhusu muuangano na Tanganyika ambapo Zanzibar ilibakia na mamlaka ya mambo ya ndani. Alikuwa makamu wa kwanza wa rais wa jamuhuri ya muungano, iliyopewa jina la Tanzania mwezi oktoba. Uvumi ulikuwa umesambaa kwamba Zanzibar iliokolewa kutoka kuwa serikali ya Kikomunisti au Tanganyika ingeenda kuwa ya Kikomunisti pamoja na kisiwa hicho.

Baada ya umoja huo, licha ya misaada mingi kutoka nchi za Mashariki, uchumi wa Zanzibar ulidumaa kwa kuwa kila mshirika alienda njia yake katika maswala ya ndani. Karume na Nyerere wote walisifu muungano huo kama mfano kwa nchi zingine za Kiafrika na wakatoa pingamizi juu ya ujumuishaji wowote wa ziada.

Kifo cha Karume

Mnamo Aprili 7, 1972, Karume aliuawa na watu wanne wenye silaha huko Dar es Salaam. Wajumbe wawili wa Baraza la Mapinduzi walijeruhiwa katika shambulio hilo.

Kwa nakala zaidi zinazohusu sikukuu bofya hapa!