Sikukuu za Umma nchini Tanzania
Orodha ya Yaliyomo
Sikukuu za Umma nchini Tanzania ni kwa mujibu wa Sheria ya sikukuu za Umma (ilivyorekebishwa) mwaka, 1966 na huzingatiwa nchini kote.
Â
Historia
Sheria ya Sikukuu za Umma (Iliyorekebishwa) ya mwaka, 1966 imeorodhesha sikukuu kumi na mbili za umma katika ratiba yake. Kwa sasa, Tanzania ina jumla ya sikukuu za umma kumi na saba: sikukuu nane za kidini, sikukuu tatu za kitaifa, mbili kumbukumbu za vifo vya viongozi waasisi wa majimbo yake na nne zilizobaki kwa ajili ya umuhimu mwingine wa kitaifa.
Rais wa Tanzania anaweza kutangaza sikukuu za nyongeza kwa hiari yake, kwa mfano, wakati wa siku ya uchaguzi mkuu. Rais wa Zanzibar anaweza kufanya vivyo hivyo katika visiwa vinavyojitawala kwa kiasi vya Zanzibar. Mfano wa hivi karibuni wa hii ilikuwa tarehe 4 Novemba 2015 ambapo Rais Kikwete alitangaza sikukuu ya kitaifa kwa siku inayofuata kusherehekea Magufuli kushinda uchaguzi wa urais.
Orodha ya mwaka 2020
Tarehe | Jina | Maelezo |
1 Januari | Sikukuu ya Mwaka mpya | |
12 Januari | Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar | Â Kuashiria mwisho wa Usultani wa Zanzibar |
7 Aprili | Siku ya Karume |  Maadhimisho ya mauaji ya Rais wa Zanzibar  Abeid Karume |
Ijumaa ya Wiki Takatifu
Machi au Aprili |
Ijumaa Kuu | Â Maadhimisho ya kusulubiwa kwa Yesu |
Jumatatu baada ya Pasaka
Machi au Aprili |
Jumatatu ya Pasaka | Siku inayofidia Jumapili, Maadhimisho ya kufufuka kwa Kristo |
26 Aprili | Sikukuu ya Muungano | Muungano wa Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar mwaka 1964 |
1 mei | Sikukuu ya Wafanyakazi | |
1 Shawwal (Mwezi wa 10 kwa kalenda ya Kiislamu) | Eid al-Fitr (Sikukuu  baada ya mfungo wa Ramadhani) | Kuashiria mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani
Mwisho wa kufunga |
7 Julai | Sikukuu ya Sabasaba | Kilele cha Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ya kila mwaka |
8 Agosti | Sikukuu ya Nane Nane | Sikukuu ya Wakulima |
14 Octoba | Siku ya Nyerere | Kumbukumbu ya kifo cha Julius Nyerere, baba wa Taifa |
12Â Rabi’ al-awwal (Mwezi wa 3 kwa kalenda ya kiislamu) | Sikukuu ya Maulidi | Maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad |
9 Disemba | Sikukuu ya Uhuru | Kusherekea mwisho wa utawala wa Uingereza mwaka 1961. |
25 Disemba | Sikukuu ya Krismasi | Kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu |
26 Disemba | Siku ya kufungua Zawadi | |
Jumla | Siku 15 |
Orodha ya mwaka 2016
Tarehe | Jina | Maelezo |
1 Januari | Sikukuu ya Mwaka mpya | |
12 Januari | Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar | Kuashiria mwisho wa Usultani wa Zanzibar |
25 Machi | Ijumaa Kuu | Maadhimisho ya kusulubiwa na kufa kwa Yesu |
28 Machi | Jumatatu ya Pasaka | Maadhimisho ya kufufuka kwa Kristo |
7 Aprili | Siku ya Karume | Maadhimisho ya mauaji ya Rais wa Zanzibar  Abeid Karume |
26 Aprili | Sikukuu ya Muungano | Â Muungano wa Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar mwaka 1964 |
1 Mei | Sikukuu ya Wafanyakazi | |
7 Julai | Sikukuu ya Saba saba | Â Kilele cha Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ya kila mwaka |
7 Julai* | Eid al-Fitr (Sikukuu baada ya mfungo wa Ramadhani) | Kuashiria mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani (siku 2) |
8 Agosti | Sikukuu ya Nane Nane | Sikukuu ya Wakulima |
14 Septemba* | Eid al-Adha (Sikukuu ya kuchinja) | |
14 Oktoba | Siku ya Nyerere | Kumbukumbu ya kifo cha Julius Nyerere, baba wa Taifa |
9 Disemba | Sikukuu ya Uhuru | Kusherekea mwisho wa utawala wa Uingereza mwaka 1961. |
25 Disemba* | Sikukuu ya Maulidi | Maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad |
25 Disemba | Sikukuu ya Krismasi | Kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu |
26 Disemba | Siku ya Kufungua Zawadi | |
Jumla | Siku 16 |
* inaashiria, inategemea muandamo wa mwezi
Kwa nakala zaidi zinazohusu sikukuu bofya hapa!