Mabadiliko ya hali ya hewa Tanzania
Mabadiliko ya hali ya hewa Tanzania

Tanzania Inavyokabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa

Orodha ya Yaliyomo

Matukio ya hali ya hewa, kama ukame, mafuriko, na dhoruba, kihistoria yamegharimu Tanzania kwa kiasi kikubwa sana. Athari zilizokadiriwa za mabadiliko ya hali ya hewa zinaweza kuongeza gharama hii, na kuzorotesha maeneo muhimu ya maendeleo ambayo yanaweza kuzuia nchi kwenda mbele zaidi. Kwa kutambua ukweli huu, Serikali ya Tanzania na jamii ya wafadhili tayari wameanzisha harakati za kuangalia changamoto zinazohusu hali ya hewa uliopo na kuweka vipaumbele vya kuboresha sehemu zote zilizo dhaifu. Walakini, mahitaji kadhaa ya kukabiliana na hii hali yanabaki, pamoja na kuingiza mabadiliko ya hali ya hewa katika mikakati muhimu ya nchi, kuamua vipaumbele kwa sekta muhimu kama kilimo na usalama wa chakula, na kuendeleza Mkakati wa Kitaifa wa Mabadiliko ya hali ya hewa ambao umeunganishwa na malengo ya kisekta. Kukamilisha vipaumbele hivi kutahitaji kuvuka vizuizi vikuu vilivyopo kuhusu upatikanaji wa data, na uwezo mdogo wa kutabiri mabadiliko ya hali ya hewa ya baadaye na tathmini ya athari katika sekta.

Athari za Hali ya Hewa na Udhaifu Wake

Hali ya Hewa ya Muda Mrefu na Muda Mfupi

  • Joto limeongezeka kwa karibu joto la 1.0 ° C tangu 1960, wastani wa 0.23 ° C kwa muongo mmoja.
  • Mvua ya kila mwaka imepungua kwa kiwango cha wastani cha asilimia 3.3 kwa muongo mmoja.
  • Mifumo ya uangazi imekuwa migumu zaidi kutabirika, na kuongezeka kwa kiwango cha mvua kupunguwa katika hafla fupi.
  • Joto la bahari ya Bahari ya Hindi limeongezeka 1 ° C tangu 1950.

Hali ya Hewa Inayotarajiwa

Misimu ya mvua Tanzania
Misimu ya mvua Tanzania

Aina za Hali ya Hewa Tanzania

  • Kuongezeka kwa wastani kwa 1.0-2.7 ° C katika joto la kila mwaka ifikapo miaka ya 2060, na kwa 1.5-4.5 ° C ifikapo miaka ya 2090.
  • Mabadiliko ya makadirio ya mvua ya mwaka ifikapo miaka ya 2060 itapungua kati kwa asilimia 1 hadi ongezeko la asilimia 18 kutoka wastani wa 1970-99.
  • Asilimia kubwa ya mvua inatarajiwa kuwa katika misimu mikubwa ya mvua.
  • Kuongezeka kwa kima cha bahari cha 0.75-1.90 m ifikapo 2100

Mapungufu katika Sekta Muhimu

Upatikanaji wa Chakula

Mabadiliko ya hali ya hewa yana uwezo wa kubadilisha kiwango cha chakula moja kwa moja na kwa njia zingine, na pia kuwa athari kwa uwepo na upatikanaji wa chakula. Mifumo ya kilimo inayotegemea mvua na ile ya nyanda za juu katika maeneo ya maziwa makuu na sehemu zingine za Afrika Mashariki inatarajiwa kuathiriwa sana na mabadiliko ya hali ya hewa, kwa kuongezeka kwa mabadiliko ya joto na ukali wake, hali itakayoweza kusababisha kupungua kwa mavuno ya mazao kwa maeneo haya. Utafiti wa hivi karibuni unakadiria kuwa ongezeko la joto la 5 ° C katika Afrika Mashariki linaweza kusababisha kupungua kwa uzalishaji wa chakula kwa karibu asilimia 20 ifikapo miaka ya 2090 na kitu. Hali zingine za hali ya hewa (mfano kujaa kwa maji na chumvi kutokana na kuongezeka kwa kima cha bahari, uharibifu wa mazao kwa sababu ya dhoruba) na hali zingine zisizo za ki hali ya hewa (kama mmomonyoko, masuala ya utawala wa rasilimali) zinaweza kuzidisha uwepo wa kiwango cha chakula cha kutosha kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Hatua za kubadilika zinaweza kusaidia kupunguza athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa kwenye kilimo na usalama wa chakula. Programu inayohusika na mabadiliko ya hali ya hewa “Tanzania’s National Adaptation Programme of Action (NAPA)” imeweka ajenda inayohimiza watu kufanya vituatavyo kama kipaumbele:

  • Tumia vyema data za hali ya hewa, utabiri wa hali ya hewa, na zana zingine za usimamizi, na kupanua mtandao wa ukusanyaji wa data ya hali ya hewa
  • Unda ufahamu juu ya athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa
  • Ongeza utumiaji wa mbolea.
  • Boresha usimamizi bora wa uzalishaji wa mifugo
  • Tumia umwagiliaji wa matone kwa mikoa maalum
  • Dhibiti wadudu, magugu na magonjwa
  • Kuongeza udhibiti wa kibaolojia wa nzige
  • Kukuza maarifa asilia

Rasilimali za Maji

Nchini Tanzania, kiwango kikubwa cha utofauti tayari kimeshaonekana katika upatikanaji wa maji nchini kote, kulingana na muundo wa ardhi, mwelekeo wa mvua, na hali ya hewa. Katika vyanzo vya maji vya ardhini, kama maziwa ya Tanganyika, Victoria, na Turkana,

Ziwa Tanganyika Tanzania
Ziwa Tanganyika Tanzania

uhusiano uliogundulika kati ya kubadilika kwa kiwango cha maziwa na misimu ya mvua unaonyesha uwezekano wa kupunguwa kwa maji miaka ijayo kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa. NAPA ya Tanzania, ambayo inapata ushauri kutoka kwa wadau, imeorodhesha rasilimali za maji kati ya sekta tatu za juu zinazohitaji kuchungwa kwa ukaribu zaidi. Sekta ya maji pia inaathiriwa zaidi na idadi ya masuala yasiyokuwa ya ki hali ya hewa kama usimamizi duni, miundombinu isiyofaa, na uchafuzi wa mazingira, yote haya yanachangia zaidi katika kupunguza uhakika wa usambazaji wa maji na ubora. Kwa upande wa athari zinazohusiana na hali ya hewa, orodha inaweza kuzidi hizi. NAPA inataja mabadiliko ya mitiririko ya maji kwenye mabonde ya mito, kuingiliwa kwa mifumo ya mazingira, na kujaa kwa maji kwenye ardhi kutokana na kuongezeka kwa mtiririko wa maji kama athari ziwezekanazo kutokea. Kupitia athari hizi, mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kuathiri wingi wa maji na ubora, hali itakayosababisha upatikanaji wa rasilimali za maji kwa matumizi ya binadamu na kwa kilimo, viwandani, na matumizi ya nishati kulegalega.

Afya

Tofauti ya hali ya hewa pia inaathiri afya nchini Tanzania, na mabadiliko ya hali ya hewa yanawezekana kusababisha matatizo mapya, na kusababisha athari kadhaa za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja (zilizofupishwa hapa chini):

 

Njia ya AthariAthariMatokeo ya Athari
Moja kwa moja– Miili kushindwa kujikinga dhidi ya viwango vya joto la hali ya juu, haswa mawimbi ya joto (heat waves).
– Kubadilika kwa masafa na / au kiwango cha hali zingine za hali ya hewa kali (ukame, mafuriko, dhoruba, nk).
– Kubadilika kwa viwango vya magonjwa yanayosababishwa na joto na baridi, haswa magonjwa ya moyo na mishipa.
– Vifo, majeraha, na uharibifu wa miundombinu ya afya ya umma
Zisizo Moja kwa moja (kwa sababu ya hitilafu za mifumo ya ikolojia)– Athari kwenye viwango na shughuli za vekta na vimelea.
– Kubadilika kwa ikolojia ya wadudu wa kwenye maji na chakula wanaoweza kuambukiza magonjwa.
– Kubadilika kwa uzalishaji wa chakula (haswa mazao) kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa, na wadudu na magonjwa yanayohusiana.
– Mabadiliko ya ubora, kiwango, na usambazaji wa maji safi.
– Kiwango cha bahari kuongezeka hali itakayosababisha kuhamahama kwa watu na uharibifu wa miundombinu.
– Kuongezeka kwa viwango na athari za kibaolojia za uchafuzi wa hewa, pamoja na poleni za mbegu na fangasi (spores).
– Kubadilika kwa jamii, uchumi na idadi ya watu kwa sababu ya mabadiliko mabaya ya hali ya hewa. Hali itakayoleta athari kwenye uchumi, miundombinu, na usambazaji wa rasilimali.
– Mabadiliko katika viwango vya kijiografia na matukio ya magonjwa yanayotokana na vekta.
– Mabadiliko ya hali ya kuhara na magonjwa ya kuambukiza kama vile kipindupindu.
– Janga la utapiamlo na njaa inayoathiri ukuaji wa watoto na maendeleo, haswa katika jamii zilizo hatarini.
– Majeraha, kuongezeka kwa magonjwa ya kuambukiza (kutokana na watu wanaohama kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kujazana kwa watu, uchafuzi wa maji ya kunywa).
– Pumu na shida za mzio, shida zingine za kupumua za muda mrefu na vifo.
– Kiwango kikubwa cha athari zinazoathiri afya ya umma (kama afya ya akili, shida ya lishe, magonjwa ya kuambukiza, vita vya kikabila).

Kwa sasa Malaria ndiyo inayoongoza kwa vifo nchini Tanzania, na inakadiriwa kuwa asilimia 16 ya vifo vinavyoripotiwa. Mabadiliko ya hali ya

Mapambano dhidi ya Malaria Tanzania
Mapambano dhidi ya Malaria Tanzania

hewa yanaweza kukuza kiwango cha milipuko ya ugonjwa wa malaria kwa kutoa mazingira mazuri ya uzalishaji wa vekta (mbu wa aina ya Anopheles). Kwa kuongezea, malaria inaweza kuongezeka kwa kiwango cha juu katika maeneo ya nyanda za juu za nchi, ambapo maambukizi ya ugonjwa huo hapo awali yalikuwa chini. Jamii katika maeneo haya zina uwezekano wa kuwa na ukosefu mkubwa wa kinga asilia dhidi ya ugonjwa wa malaria, kwa sababu ya kutokuwa na mazoea na ugonjwa huo. Uwezo wao wa kukabiliana na ugonjwa wa Malaria pia unaweza kuwa dhaifu, kwa sababu ya umaskini na mifumo ya kiafya isiyo na vifaa vya kutosha kukabiliana na ugonjwa huo. Sehemu muhimu ya kutatuwa changamoto hizi itakuwa katika kuangalia athari zisizo za kihali ya hewa zinazohusika na uwezo wa kukabiliana na umaskini na ubora na upatikanaji wa mfumo wa afya nchini Tanzania.

 

Udhahifu wa Mfumo wa Ikolojia (Ecosystem)

Miamba ya Matumbawe (Coral Reefs)

Mazingira ya miamba ya matumbawe na rasilimali inazohifadhi ni muhimu sana kwa sababu ni makazi ya viumbe hai, chanzo cha chakula, usaidia ikolojia, na ni kivutio kikubwa cha utalii. Pia husaidia kulinda ufukwe wa bahari kutokana na uharibifu unaoletwa na dhoruba. Miamba ya matumbawe tayari iko katika hali mbaya kutokana matatizo yasiyo ya kihali ya hewa na yale yanayosababishwa na hali ya hewa, na kupauka kwa matumbawe (coral bleaching) kumeshatokea katika maeneo mbali mbali. Kwa mfano, mnamo 1998, kati ya asilimia 50-90 ya miamba ilibomolewa nchini Tanzania na Kenya. Vitu husika vinavyochangia athari kwenye miamba ya matumbawe ni pamoja na:

  • Joto la juu la bahari, pamoja na uchafuzi wa mazingira na athari zingine, zinaweza kusababisha kupauka kwa matumbawe.
  • Kupanda kwa viwango vya baharini kunaweza kubadilisha vipindi na viwango vya mwanga, na hivyo kuathiri aina za viumbe wanaosaidia kukuwa kwa mimea (photosynthetic species).
  • Miamba ya Matumbawe Tanzania
    Miamba ya Matumbawe Tanzania


    Kwenda kwa tindikali ya bahari kwa sababu ya kuongezeka kwa viwango vya kaboni dioksidi inaweza kuathiri vibaya matumbawe na viumbe wengine wa baharini kama vile uduvi na kaa, na mwishowe inaweza kutoa shinikizo kubwa kwa muundo, usambazaji, na tija ya mazingira.
  • Athari zinazoendelea za wanadamu kama vile mazoea ya uvuvi haramu, uvuvi wa kupita kiasi, uharibifu wa miamba ya matumbawe unaosababishwa na maboti, na uchimbaji zinaweza kuzidisha msongo wa mabadiliko ya hali ya hewa.
  • Kuongezeka kwa dhoruba kunaweza kusababisha uharibifu zaidi kwenye miamba, kitu ambacho kinaweza kuchukua muda mrefu kurekebishika. Kupotea kwa miamba hii kunaweza kuzidisha uharibifu unaosababishwa na dhoruba kwenye fukwe, mikoko, na makazi ya pwani na miundombinu.

Mikoko (Mangroves)

Rasilimali asili na mazingira mazuri yanayotokana na na mikoko husaidia ustawi wa jamii ambazo zinaitegemea. Mifumo hii ya mazingira pia hutumika kama tegemezi muhimu kwa athari za mabadiliko ya hali ya hewa kama dhoruba. Misitu mikubwa nchini Tanzania, kama ile ya Delta ya Rufiji, ambayo hiko hatarini zaidi kupotea ulimwenguni, na hekta 73,500 za mikoko kwenye kingo za bahari kati ya Rufiji-Mafia-Kilwa na miamba ya matumbawe inayohusiana nayo inasaidia sana kimaisha katika maeneo husika haswa kwenye uvuvi na bidhaa za misitu (mbao na miti) kwa sehemu kubwa ya idadi ya watu wa delta. Sensa kati ya miaka ya 1991 na 2000 iliofanywa na Shirikisho la Wanyamapori Ulimwenguni kwenye delta inaonyesha kwamba misitu ya mikoko imepunguzwa na kubadilishwa kwa kiasi kikubwa na kilimo cha ardhi na eneo kufyekwa kubakia wazi. Athari zote mbili za hali ya hewa na zisizo za hali ya hewa zimechangia mabadiliko haya. Athari zisizosababishwa na hali ya hewa ni pamoja na mabadiliko ya matumizi ya ardhi, ujenzi wa mabwawa, kukatwa na kusafisha kwa mikoko ili kutengeneza maeneo ya mabwawa ya samaki, msukumo wa ardhi, na kuzama ghafla au kushuka pole pole kwa uso wa ardhi .

Nyika

Nyika inajumuisha takriban asilimia 40 ya jumla ya eneo la ardhi ya Tanzania, na ni muhimu kwa ukuzaji wa mifugo. Ulishaji wa wanyama katika nyika tayari umesababisha mabadiliko katika aina za majani. Mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kupungua zaidi ukuaji wa majani, kupunguza uwezo wa kubeba, na kupunguza mafuta ya protini kwenye mimea. Mabadiliko haya yanaweza kuwa na athari kwenye uzalishaji wa maziwa na nyama katika mifugo, na inaweza kusababisha mahitaji ya virutubisho vya protini kwa wanyama. Hii inaweza kuleta changamoto ya kuongezeka kwa gharama ya uzalishaji wa mifugo na kupungua kwa upatikanaji wa maziwa na bidhaa za nyama. Kwa kuongezea, mabadiliko ya joto na uwepo wa hewa inaweza kuzidisha athari hizi kwa kutengeneza hali ambayo inaongeza kushamiri kwa magonjwa na wadudu wanaoshambulia mifugo.

Misitu

Misitu, ambayo inajumuisha miombo, ndio aina ya misitu mikuu inayokua sana Tanzania, na inachukuwa asilimia 50 ya jumla eneo la ardhi

Misitu ya Miombo Tanzania
Misitu ya Miombo Tanzania

la nchi. Misitu ni muhimu kwa aina tofauti za uhai inayozalisha, maliasili, urutubishaji wake wa mazingira, vitu ambavyo vinasaidia afya na ustawi wa jamii ambazo zinaitegemea, na vile vile misitu inasaidia katika kukuza uchumi. Misitu tayari hiko katika hatari ya mashinikizo kadhaa yasiyo ya kihali ya hewa, ambayo ni pamoja na usafishaji wa ardhi kwa matumizi ya kilimo, uhamaji wa jamii na kufyeka na utengenezaji wa mkaa, na uvunaji wa kuni ulio katika kiwango cha kasi kuliko ukuwaji wa misitu. Athari zinazotarajiwa za mabadiliko ya hali ya hewa, ni pamoja na kupunguzwa maeneo yalifunikwa na misitu na kubadilika kwa aina za misitu, spishi, na usambaaji wake, kunaweza kuzidisha hali hizi zisizo za kihali ya hewa, kuzidi kutishia mazingira.

Mikakati ya Kitaifa, Mipango, na Taasisi Husika

Mikakati ya kitaifa na Mipango

  • Mawasiliano ya Kitaifa ya Awali (Initial National Communication – 2005): Inashughulikia kupunguza na kurekebisha, na inajihusisha na utowaji wa habari juu ya uzalishaji wa gesi chafu, chaguzi za kupunguza, tathmini za udhaifu wa sekta muhimu, hatua za kukabiliana na hali iliyopo, na sera na muktadha wa kitaasisi wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
  • NAPA (2007): Inakagua udhaifu unaohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa katika sekta mbali mbali ambazo ni muhimu kwa uchumi wa Tanzania.

Mfumo wa Taasisi

  • Kamati ya Kitaifa ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa (National Climate Change Committee – NCCC) inashauri Idara ya Mazingira juu ya maswala yanayohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa.
  • Kituo cha Nishati, Mazingira, Sayansi, na Teknolojia: Inashirikisha Sekretarieti ya NCCC na inatoa msaada wa kiufundi na kiutawala kwa NCCC na timu za masomo za mabadiliko ya hali ya hewa.
  • Wakala wa hali ya hewa wa Tanzania: Hutoa data za hali ya hewa na habari za hali ya hewa na utabiri wa kuwajulisha wanamipango wa nchi.

Vipaumbele vya Marekebisho ya Serikali

NAPA imetowa vipaumbele vya sekta zilizo hatarini na mabadiliko ya hali ya hewa na miradi sita yenye umuhimu wa juu, iliyoorodheshwa kwenye sanduku hapa chini:

Sekta Zenye Kipaumbele kwa NAPAMiradi ya Kipaumbele ya NAPA
Kilimo na usalama wa chakula (pamoja na mifugo) (1)
– Maji (2/3)
– Nishati (2/3)
– Misitu (4)
– Afya (5)
– Wanyamapori (6/7)
– Utalii (6/7)
– Viwanda (8)
– Rasilimali za pwani na baharini(9)
– Makazi ya wanadamu (10)
– Maeneo ya mvua (11)
1.) Kuboresha usalama wa chakula katika maeneo yanayokabiliwa na ukame kwa kukuza mazao yanayostahimili ukame
2.) Kuboresha upatikanaji wa maji kwa jamii zilizo na ukame katikati mwa nchi
3.) Kuhamisha visima vya maji visivyo na maji kutoka kwa maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko katika mikoa ya pwani ya Tanzania Bara na Zanzibar
4.) Kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa kupitia uboreshaji wa msitu katika Mlima Kilimanjaro
5.) Utengenezaji wa mabwawa madogo ya umeme kwa jamii ndongo ndogo kuongeza mseto wa uchumi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
6) Kupambana na milipuko ya ugonjwa wa Malaria katika maeneo yenye mbu wengi.

Kuna maendeleo kidogo juu ya utekelezaji wa miradi hii au katika kuunganisha mabadiliko ya hali ya hewa kuwa ya mikakati ya maendeleo na mikakati ya sekta za nchi. Kwa hivyo, vipaumbele vinavyoendelea kwa sasa nchini Tanzania ni pamoja na:

  • Kujumuisha mabadiliko ya hali ya hewa kuwa mkakati wa sasa na miaka ijayo.
  • Kuweka vipaumbele kwa sekta muhimu kama kilimo na usalama wa chakula.
  • Kuunda Mkakati wa Kitaifa wa Mabadiliko ya hali ya hewa ambao unahusishwa na malengo ya kisekta na unaojenga uhusiano baina ya kukabiliana na gesi chafu na fursa za uzalishaji wa gesi, haswa kutokana na ukataji miti na uharibifu wa misitu.

Wahusika Muhimu na Majukumu Yalichokuliwa

Harakati kadhaa za shughuli za kurekebisha zinafadhiliwa na kutekelezwa na serikali za kigheni (bilateral donors), mashirika ya kimataifa na benki za maendeleo nchini Tanzania. Harakati zinazofadhiliwa na wafadhili zinalenga zaidi katika kukusanya data juu ya udhaifu wa mazingira katika sekta maalum, kubaini na kutathmini hatua zinazoweza kufanyika za kurekebisha, na kuandaa mipango ya hatua. Lakini mpaka sasa kuna maendeleo kidogo sana juu ya utekelezaji wa marekebisho yanayopendekezwa. Kuna pia idadi ya harakati zinazoshughulikia athari zisizokuwa za kihali ya hewa katika sekta mbalimbali ambazo zinahitaji kufanyiwa marekebisha, ingawa faida ya marekebisho hayo haziko wazi au hazitathiminiwa kiuwazi sana.

Vikwazo vya Kushughulikia Hali ya Hewa

Tanzania inakabiliwa na mahitaji kadhaa:

Kuongeza uwezo wa kukuza, kubuni, na kutekeleza mapendekezo ya kufadhili na miradi inayokidhi mahitaji ya wafadhili.

Kuongeza upatikanaji wa data wa habari za kutosha, za kuaminika za hali ya hewa pamoja na ukusanyaji wa data za kisasa na mifumo ya kuchakatuwa hizo data, pamoja na vifaa vya usambazaji.

Kuziba mapungufu katika uchambuzi wa athari za hali ya hewa, changamoto zake kwa jamii, mifumo ya mazingira, na sekta za uchumi, na hatua zinazoweza kubadilishwa.

Kuongeza kwa upatikanaji wa data za kisayansi kwa watengeneza sera na waandaaji mipango.

Kutatuwa hivi vikwazo na mahitaji haya itakuwa muhimu katika kuwezesha Tanzania kusonga mbele zaidi ya tathmini, mikakati, na majaribio kwenda kwenye utekelezaji wa kukabiliana na changamoto za hali ya hewa kwa muda mrefu 

Kwa nakala zaidi zinazohusu hali ya hewa bofya hapa!