Sikukuu za Umma nchini Tanzania - Sherehe za Mapinduzi Zanzibar

Sikukuu za Umma nchini Tanzania

Orodha ya Yaliyomo

Sikukuu za Umma nchini Tanzania ni kwa mujibu wa Sheria ya sikukuu za Umma (ilivyorekebishwa) mwaka, 1966 na huzingatiwa nchini kote.

 

Historia

Sheria ya Sikukuu za Umma (Iliyorekebishwa) ya mwaka, 1966 imeorodhesha sikukuu kumi na mbili za umma katika ratiba yake. Kwa sasa, Tanzania ina jumla ya sikukuu za umma kumi na saba: sikukuu nane za kidini, sikukuu tatu za kitaifa, mbili kumbukumbu za vifo vya viongozi waasisi wa majimbo yake na nne zilizobaki kwa ajili ya umuhimu mwingine wa kitaifa.

Rais wa Tanzania anaweza kutangaza sikukuu za nyongeza kwa hiari yake, kwa mfano, wakati wa siku ya uchaguzi mkuu. Rais wa Zanzibar anaweza kufanya vivyo hivyo katika visiwa vinavyojitawala kwa kiasi vya Zanzibar. Mfano wa hivi karibuni wa hii ilikuwa tarehe 4 Novemba 2015 ambapo Rais Kikwete alitangaza sikukuu ya kitaifa kwa siku inayofuata kusherehekea Magufuli kushinda uchaguzi wa urais.

Orodha ya mwaka 2020

Tarehe Jina Maelezo
1 Januari Sikukuu ya Mwaka mpya
12 Januari Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar  Kuashiria mwisho wa Usultani wa Zanzibar
7 Aprili Siku ya Karume  Maadhimisho ya mauaji ya Rais wa Zanzibar  Abeid Karume
Ijumaa ya Wiki Takatifu

Machi au Aprili

Ijumaa Kuu  Maadhimisho ya kusulubiwa kwa Yesu
Jumatatu baada ya Pasaka

Machi au Aprili

Jumatatu ya Pasaka Siku inayofidia Jumapili, Maadhimisho ya kufufuka kwa Kristo
26 Aprili Sikukuu ya Muungano Muungano wa Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar mwaka 1964
1 mei Sikukuu ya Wafanyakazi
1 Shawwal (Mwezi wa 10 kwa kalenda ya Kiislamu) Eid al-Fitr (Sikukuu  baada ya mfungo wa Ramadhani) Kuashiria mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani

Mwisho wa kufunga

7 Julai Sikukuu ya Sabasaba Kilele cha Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ya kila mwaka
8 Agosti Sikukuu ya Nane Nane Sikukuu ya Wakulima
14 Octoba Siku ya Nyerere Kumbukumbu ya kifo cha Julius Nyerere, baba wa Taifa
12 Rabi’ al-awwal (Mwezi wa 3 kwa kalenda ya kiislamu) Sikukuu ya Maulidi Maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad
9 Disemba Sikukuu ya Uhuru Kusherekea  mwisho wa utawala wa Uingereza mwaka 1961.
25 Disemba Sikukuu ya Krismasi Kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu
26 Disemba Siku ya kufungua Zawadi
Jumla Siku 15
Bango lenye salamu za Maulid huko Kisutu, Dar es Salaam.
Bango lenye salamu za Maulid huko Kisutu, Dar es Salaam.

Orodha ya mwaka 2016

Tarehe Jina Maelezo
1 Januari Sikukuu ya Mwaka mpya
12 Januari Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar Kuashiria mwisho wa Usultani wa Zanzibar
25 Machi Ijumaa Kuu Maadhimisho ya kusulubiwa na kufa kwa Yesu
28 Machi Jumatatu ya Pasaka Maadhimisho ya kufufuka kwa Kristo
7 Aprili Siku ya Karume Maadhimisho ya mauaji ya Rais wa Zanzibar  Abeid Karume
26 Aprili Sikukuu ya Muungano  Muungano wa Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar mwaka 1964
1 Mei Sikukuu ya Wafanyakazi
7 Julai Sikukuu ya Saba saba  Kilele cha Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ya kila mwaka
7 Julai* Eid al-Fitr (Sikukuu baada ya mfungo wa Ramadhani) Kuashiria mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani (siku 2)
8 Agosti Sikukuu ya Nane Nane Sikukuu ya Wakulima
14 Septemba* Eid al-Adha (Sikukuu ya kuchinja)
14 Oktoba Siku ya Nyerere Kumbukumbu ya kifo cha Julius Nyerere, baba wa Taifa
9 Disemba Sikukuu ya Uhuru Kusherekea  mwisho wa utawala wa Uingereza mwaka 1961.
25 Disemba* Sikukuu ya Maulidi Maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad
25 Disemba Sikukuu ya Krismasi Kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu
26 Disemba Siku ya Kufungua Zawadi
Jumla Siku 16

* inaashiria, inategemea muandamo wa mwezi

Kwa nakala zaidi zinazohusu sikukuu bofya hapa!