Sherehe za wapiganaji wa kimaasai

Sherehe za Wapiganaji wa Kimaasai

Orodha ya Yaliyomo

Baada ya tohara na sherehe za ujio wa umri, vijana wa kimaasai wanakuwa wanaume kamili na kuingia katika hatua nyingine ya maisha yao ambayo ni kizazi kipya cha wapiganaji. Kizazi kipya cha wapiganaji wa kimaasai uandaliwa kwa kipindi cha takribani miaka 7, vijana hawa uendelea kuwa wapiganaji kuanzia miaka 15 hadi 30. Kizazi kipya cha wapiganaji uongozwa na kufundishwa na wapiganaji wabobezi/wakubwa katika kuiba mifugo, mbinu za kivita na mbinu za uwindaji, kizazi hiki kipya cha wapiganaji utambulika kwa jina la “ilkeliani”. Katika kipindi hiki chote kizazi kipya cha wapiganaji uishi na familia zao. Pindi wafikiapo balehe uondoka katika nyumba za familia na kuishi na wapiganaji wengine katika kijiji kilichojengwa kwa ajili ya wapiganaji, wapenzi wao na viongozi wao wakuu ambao uendelea kuwaelekeza wapiganaji. Mara nyingi kiijiji/kambi za wapiganaji “Manyata” ujengwa kando kando ya maji na malisho mazuri na ujumuisha

Kizazi kipya cha wapiganaji wa kimaasai
Kizazi kipya cha wapiganaji wa kimaasai

kaya 49 (namba ya bahati kwa Wamaasai). Nyumba hizi ujengwa na wazazi hasa wakina mama wa wapiganaji, ndani ya nyumba hizi kunakuwa na kitanda cha mwenzi wa mpiganaji na cha mama wa msichana pamoja na kitanda cha mpiganaji.

Ndoto za kijana wa kimaasai

“Ni ndoto ya kila kijana wa Kimaasai kuwa mpiganaji. Neno lenyewe linaonekana kuwa na nguvu isiyo ya kawaida. Mpiganaji anatakiwa kuwa na nguvu, akili ujasiri, mwenye kujiamini, jasiri, busara na hekima. Anatakiwa kuwinda na kuua simba kwa ajili ya vazi lake la kichwani, kulinda mifugo dhidi ya wanyama wakali, kurudisha mifugo iliyoibiwa au kupotea mara nyingi kutoka kwenye umbali mrefu na kulinda jamii yake. Wapiganaji wa kimaasai ufurahia umoja wao, ushirikiana katika mambo mbalimbali kwa pamoja. Katika huduma mbalimbali ambazo wapiganaji wanazozitoa katika jamii wanayoishi, wapiganaji uongeza kiwango cha furaha kisichopimika, kukabiliana na hatari mbalimbali na mahusiano. Bila nyimbo zao, mashairi yao, kujihusiana na wanawake kuonyesha uanaume/urijali wao, maisha ya Maasai yasingekuwa kama yalivyo hivi leo” -Tepilit Ole Saitoti.

Kadri wapiganaji wa kimaasai wanavyozidi kukua wanaweza kuishi katika maeneo ya mbali yaliyojitenga na mara nyingi uenda katika misitu ambapo kuna kambi za sherehe maalum zilizojengwa kwa ajili ya wapiganaji walio katika maeneo ya msituni. Wakiwa huko wapiganaji uendelea na elimu yao na kuomba kwa Mungu pekee ambaye umwita “Engai”. Baada ya miaka mingi ya kulinda mifugo yao dhidi ya vifaru, simba wanaowinda, kutongoza wasichana, kutunza na kupendezesha nywele zao ndefu kwa kutumia udongo mwekundu na kuendeleza ubunifu wao katika upiganaji, changamoto kutoka kwa wapiganaji wa kizazi kipya huwa kubwa sana na wapiganaji wakongwe ulazimika kuwaandaa wapiganaji wa kizazi kipya ili wawe watu wazima, hatua hii uitwa “Eunoto”.

Wapiganaji wa Kimaasai wakijifunza kupambana
Wapiganaji wa Kimaasai wakijifunza kupambana

Sherehe za ujio wa umri kabla ya kufikia hadhi ya upiganaji mwandamizi “Eunoto” ufanyika katika vijiji vilivyojengwa na wapiganaji maalumu kwa ajili ya sherehe hizo. Wapiganaji wa kimaasai wa kizazi kipya ufika katika sherehe wakiwa na mavazi maalumu ya sherehe pamoja na fimbo nyeupe badala ya mkuki. Mkuki ni mojawapo ya kifaa cha thamani ambacho mpiganaji anatakiwa kuwa nacho. Mara nyingi upambwa kuashiria amani na upande wake wa juu hauchomekwi ardhini. Kubeba fimbo nyeupe uonyesha kuwa wapiganaji wa kizazi kipya wako tayari kuingia katika hatua ya utu uzima.

Alaunoni

Kwa pamoja, wapiganaji wa kizazi kipya na wapiganaji wakongwe umchagua kiongozi wao aitwaye “alaunoni” ambaye utoka katika kundi la wapiganaji wa kizazi kipya lengo hasa ni kuwawakilisha wapiganaji wa kizazi kipya pindi wanapoelekea hatua ya utu uzima. Kiongozi huyu ni lazima awe anaheshimiwa, ambaye maisha yake ya nyuma hayahusiani na malalamiko ya aina yoyote. Anapaswa awe na afya njema, mwenye mifugo mingi, awe na asili ya kuzaliwa ya kimaasai, asiwe amewahi kuua mtu yoyote, asihusike na laana ya aina yoyote na wazazi wake wanatakiwa wawe hai na wenye kuheshimika. Kuchaguliwa kwa “alaunoni” kunatakiwa kuizinishwe na kiongozi wa kiroho wa kimaasai anayeogopeka na kuheshimiwa na wamaasai “laiboni”. Katika kipindi hiki wapiganaji wa kizazi kipya uuacha ujana na mambo yake na kuingia utu uzima. Mbali na yote hayo ni heshima kubwa pindi mpiganaji anapochaguliwa, kiongozi wa wapiganaji wa kimaasai wa kizazi kipya “alaunoni” anatakiwa kuchaguliwa bila kufahamu kinachoendelea. Ni heshima ambayo kila mpiganaji anaitamani. Baada ya kuchaguliwa kwa kushtukizwa “alaunoni” upewa kito cha shaba kilichokunjwa “insuritia” ambacho uning’ing’ia katika shingo yake pindi kinapovaliwa pamoja na ngozi ya kondoo. Wapiganaji wengine wawili; mmoja kati yao ni “olabaroenkeene” ambaye ng’ombe wake utolewa kafara na “olaigwanani” aliyechaguliwa miaka kadhaa iliyopita pindi sherehe ya tohara ilipofanyika, kwa pamoja watamsaidia kiongozi wa kizazi kipya “alaunoni” kufanikisha zoezi zima la ibada za Eunoto katika siku nne zijazo za sherehe.

Wamaasai uishi katika nyumba zilizojengwa kwa kutumia kinyesi cha ng’ombe na kuezekwa kwa paa la tambalale. Kwa ajili ya sherehe ya kufikia hadhi ya upiganaji, nyumba zenye paa lenye umbo la pia ujengwa mahususi kwa ajili ya sherehe hizo hii uitwa “o-singira”. Chakula kinachoandaliwa katika sherehe hizo ujumuisha nyama na maziwa, chakula hiki uliwa na watu wote isipokuwa bia zilizotengenezwa kwa asali unywewa na viongozi na kutunzwa hapo. Baada ya “o-singira” kujengwa, wapiganaji pamoja na wazee wao uenda mtoni na kupaka chaki nyeupe katika nyuso zao kitendo hiki kinaitwa enturoto. Baada ya zoezi zima kukamilika wapiganaji urudi katika vijiji vyao huku wakiimba, katika hatua hii wapiganaji wa kimaasai wa kizazi kipya wanakuwa wapinganaji wakongwe au wabobezi.

Wamaasai wakiwa katika sherehe ya Enuoto
Wamaasai wakiwa katika sherehe ya Enuoto

Enuoto

Kipengele cha sherehe ya kufikia hadhi ya upiganaji “Eunoto” chenye hisia kali zaidi ufanyika siku inayofuata. Wapiganaji wa kizazi kipya unyolewa nywele zao na mama zao. Kwa takribani kipindi cha miaka ishirini wapiganaji wa kimaasai uacha nywele zao zikue, uzipamba nywele zao na kuziwekea rangi kwa kutumia udongo mwekundu. Nywele hizi unyolewa kuonesha ishara ya ukomo wa upiganaji wao, kutokana na kitendo hiki wapiganaji wengi huwa na jazba, utetemeka mwili kwa jazba na kulia. Ujana wao hauko nao tena, kwani sasa ushirika wa upiganaji linakuwa jambo la zamani lililowatupa mkono.

Hatimaye, wapiganaji wa kizazi kipya wako tayari kuingia katika hatua ya utu uzima, kuoa na kulea familia. Ili kufanikisha hili mwanamke uchaguliwa kutoka katika familia inayoheshimika na kuozeshwa kwa kiongozi wa wapiganaji wa kizazi kipya “alaunoni”. Wasichana wa Kimaasai uchumbiwa pindi wawapo wachanga, sababu wazazi wa pande zote mbili utamani watoto wao kuwa na mwenza ambaye watajenga nae familia. Wazazi wa mvulana upeleka zawadi kwa wazazi wa mtoto wa kike aliyezaliwa, wazazi hawa uendelea kupeleka zawadi mpaka pale msichana atakapofikia umri wa kuolewa. Hata hivyo hakuna uchumba usiokuwa na mipaka. Endapo mwanamke amechaguliwa kuolewa na kiongozi wa wapiganaji wa kizazi kipya “alaunoni”, mipango yote ya ndoa ya zamani uvunjwa. Jambo hili ufanywa kwa ajili ya kulinda jamii ya Maasai.

Wapiganaji wa kizazi kipya ni watu wazima sasa, wanaweza kuoa. Vijiji “Manyata” maalumu vilivyojengwa kwa ajili ya sherehe uachwa bila kukaliwa na watu. Jua linapozama wapiganaji wa kimaasai walioingia katika hatua nyingine ya utu uzima urudi nyumbani na kukabiliana na majukumu ya utu uzima ambayo ujumuisha kuoa na kulea familia.

Kwa nakala zaidi zinazohusu kabila la kimaasai bofya hapa!