Mpangalio wa Kisiasa na Kijamii wa Kimaasai

Mpangalio wa Kisiasa na Kijamii ya Kimaasai

Orodha ya Yaliyomo

 

Mpangilio wa kijamii

Sifa kubwa ya tofauti katika Jamii ya kimaasai ni mfumo wa miaka ambao uwatofautisha wanaume wakubwa katika mifumo ya kimiaka ambayo inapishana kwa takribani miaka kumi na tano. Kila mfumo wa miaka uliowekwa umegawanyika katika pande mbili “upande wa kulia” ukifuatwa na “upande wa kushoto”. Kitu chenye umuhimu mkubwa kwenye jamii ni idadi ndogo ya wapiganaji ambao wameanzishwa

Wapiganaji wa Kimaasai wakiwa kambini kwao
Wapiganaji wa Kimaasai wakiwa kambini kwao

kufanya majukumu yao katika kipindi cha karibuni. Kwenye kipindi ambacho ukuwaji wa vijana kimwili ndio unashamiri vijiji vya wapiganaji utengenezwa katika kipindi hicho mpaka kundi lingine la wapiganaji linapo kuwa tayari limefuzu. Kuanzishwa Kwa safu mahiri ya wapiganaji wa vijiji kila baada ya miaka saba ni kitu ambacho kinajenga hali ya kujitegemea na uhuru wa muda wa kila mpiganaji kutoka kwa baba zao. Uhuru huo unaendelea mpaka kwa mama wa morani ambao wanachukuwa nafasi ya pili katika vijiji vya watoto wao wapiganaji.

Kila Kijiji cha wapiganaji ni tamaduni ambayo inayowafanya wapiganaji wote kuwa ndugu wa karibu. Hawamiliki mali yeyote binafsi na wanawajibika kutumia pamoja wakati, chakula na hata wasichana ambao ni wapenzi wao. Masharti katika mipangilio ya chakula na mienendo yao yanawaweka pamoja na kuwafanya waimarike zaidi katika kutegemeana wenyewe kwenye makundi ya rika lao.

Kijiji cha moja ya kundi la wapiganaji uachwa kabla ya kuanzishwa kundi lingine la wapiganaji, na kustaafu kwa wazee kunapelekea kutawanyika kwenye maeneo madogo hususani vijiji vya mbali ili kutumia kwa ufanisi zaidi maeneo ya kulishia mifugo na maji ya kunyweshea mifugo. Kama watu wazima, lengo kubwa la wanaume ni kuanzisha familia zao pamoja na ufugaji. Mabadiliko kwenda kwenye utu uzima uhusisha mageuzi ya kijana ambae alikuwa akitegemea wenzake kwenda kwenye kuwa mtu mwenye kujitegemea mwenyewe na mzoefu. Uhuru wa kila mmiliki wa mali miongoni mwa watu wazima katika vijiji uonekana kama kigezo cha kuonyesha mtu anayejitegemea ambao ni tofauti na utegemezi uliosisitizwa katika vijiji vya wapiganaji, sawa sawa na taswira ya kiongozi mwanaume wa kabila ambayo ni tofauti kabisa na taswira ya mpiganaji asiye na ubinafsi.

Mpangilio wa kisiasa

Mamlaka katika mfumo wa kiumri yamejengwa kutoka kwenye muunganiko wa kubadilishana makundi kiumri (A-B-C-D-E-F) ambapo wakubwa wa kundi A uleta kundi jipya la umri C, kushiriki kwenye sherehe inayojumuisha kuwasha moto halafu wanakuwa walinzi wa vijiti vya moto kwa ajili ya kundi C, na jukumu lao ni kuwakuza hawa kama wapiganaji hatua kwa hatua mpaka wanapokuwa watu wazima. Vile vile C mwishoni wanakuwa walinzi wa kundi E na kutengeneza uhusiano wa makundi ya kiumri A-C-E ambao ni tofauti na usambamba wa muunganiko wa vijiti vya moto vinavyowahusiana kati ya makundi ya kiumri B-D-F. Mpangilio huu pacha wa uwajibikaji unajumuisha muunganiko wa ushindani wa makundi ya umri yanayokaribiana (haswa kusini) na uhasama kati ya wazee na vijana (haswa kaskazini)

Udhibiti wa kijamii ya Kimaasai

Chifu wa Kimaasai na mmoja wa wazee wa kimaasai
Chifu wa Kimaasai na mmoja wa wazee wa kimaasai

Udhibiti wa kijamii miongoni mwa wamasai umejengwa kiimani katika uwezo wa wazee wa kutoa baraka au kutoa laana ambao umeunganishwa katika uwezo wao mkubwa wa kimaadili katika nyanja zote . Uwezo wa walinzi wa kutumia vijiti vya moto dhidi ya wapiganaji, au baba kwa watoto zao na wakubwa wote umesimama kwenye nguzo ya uwezo wao wa kutowa laana.

Migogoro

Migogoro miongoni mwa wamasai huwa inalenga katika nyanja mbalimbali za upambanaji. Wapiganaji uonekana kama walinzi wa mifugo ya kimasai mpaka sasa, ingawa wizi wa mifugo hupo kwa kiasi kidogo ukilinganisha na ilivyokuwa zamani. Matatizo makubwa yanayosumbuwa sana ni yale ya mambo ya ndani ya wamaasai, yanayohusu utoaji wa malazi kwa wapiganaji. Kwa upande mwingine kuna uhusiano wa shida kati ya wapiganaji na viongozi dhidi ya wizi wa baadhi ya bidhaa na uzinzi unaotokea kipindi cha ujana wao na kwenye upungufu wa chakula ambavyo vyote vinatokea kutokana ukapela na uhaba wa chakula unaowakumba, ambavyo ni tofauti na maisha wanayoishi matajiri na wakubwa wenye wake wengi. Kwa upande mwingine kuna ushindani uliopo kati ya vikundi vya wapiganaji vinavyofuatana.Upendeleo unaodaiwa na kila kundi la wapiganaji katika nyakati za ubora wao, unazuia warithi mpaka wanafunzi wawe tayari kuonyesha uwezo wao kwa nguvu. Uhasama huu saa nyingine usababisha mapigano makali sana. Maendeleo ya vikundi vya kiumri na vitengo vyake yako mbali sana kufikia hali iliyo tulivu na rahisi, kwahiyo mpiganaji ataendelea kutawala hata baada ya karne nzima ya amani.

Kwa nakala zaidi zinazohusu kabila la kimaasai bofya hapa!