Sherehe Ya Tohara / Sherehe Ya Jando
Orodha ya Yaliyomo
Katika jamii ya wamaasai- tohara ni moja ya sherehe muhimu zaidi ambayo wanaume na wanawake lazima wapitie. Leo sherehe hii inazingatiwa kuwa na umuhimu zaidi kwa wavulana kuliko wasichana. Wamaasai wengi hawatahiri (kufanya tohara) tena wasichana wao lakini wanaendelea na zoezi hili kwa wavulana.
Masharti
Sherehe ya tohara kwa wavulana hufanyika zaidi kati ya umri wa miaka 16 au 17. Miaka ishirini iliyopita, wavulana hawakutahiriwa hadi walipozingatiwa kuwa wamekomaa (watu wazima). Mzee wa kimaasai wakati mmoja alituambia kwamba, hadi mvulana atakapokuwa na
umri wa kutosha kuweza kubeba ndama mchanga hadi nyumbani kwake, hatoweza kutahiriwa (kufanyiwa tohara). Wazee husubiri hadi kuwe na wavulana wengi wa kutosha kuzingatiwa kama wanaume madhubuti, imara na wenye uwezo wa kulinda jamii. Wakati mwingine wavulana hulazimika kungojea hadi wanapofika kati ya umri wa maka 20 na kuendelea, wakati kaka zao wadogo wanakaribia katika rika lao. Ni katika hatua hii ndio uamuzi unachukuliwa wa kutahiri wavulana, na wavulana hao hupewa ruhusa ya kuanzisha kambi zao wenyewe na pia kufanya mila kadhaa za kitamaduni. Wavulana wengine ambao kesi zao zinaonekana kuwa maalum wanaweza kutahiriwa kabla ya hatua hii kufikiwa. Sababu zake ni za ki-asili. Kwa mfano, mvulana Anaweza kutahiriwa ili kuchukua mali ya baba yake aliyefariki (aliyekufa). Mvulana anaweza pia kutahiriwa kwa sababu dada zake wadogo wamekua na kufikia umri wa kuolewa na hawawezi kutahiriwa kabla yake. Wavulana katika kitengo hiki wanajulikana kama Ilng’eeliani na kawaida husemekana kuwa wanatengeneza / wanaunda rika Jipya.
Olaiguenani na Olopolosi-Olkiteng
Wazee wa Kimaasai hukutana na kuamua kwamba wavulana wao wako tayari kutahiriwa. Nyumba inajengwa ambayo wavulana wataenda kucheza na kufanya mila kadhaa. Wanacheza kwa siku nne, siku mbili zikijulikana kama siku “nyeupe” na zingine mbili kama siku “nyekundu”. Baada ya hili ng’ombe uchinjwa. Wakati uchezaji huu unaendelea, Msemaji Mkuu, anayejulikana kama Olaiguenani, uchaguliwa kati ya wavulana. Anapewa kirungu, Orikna, ambacho kimekuwa cheusi kwa kupakwa tope (matope), kama fimbo za ofisi. Anabarikiwa na maneno fulani na kupewa uongozi wa kikundi chake (rika lake). Yeye ndiye anayekunywa kwanza damu ya moto ya ng’ombe aliyechinjwa. Anatakiwa kuwa mtu mzima kiakili kuliko wengine, anaye-heshimiwa sana na baraza lake linachukuliwa kwa uzito na wote. Kikundi kinatawanyika na kusubiri mwaka mwingine au miwili, na baada ya hili wazee ukutana tena ili kuamua tarehe ambayo ibada kubwa ijayo itafanyika. Hii ndio ibada wakati wavulana wanakamata, wanamshikilia na kumwangusha ng’ombe mwenye nguvu kwa pembe zake, bila kutumia chochote zaidi ya mikono yao. Ni katika sherehe hii pia kwamba mvulana ambaye ng’ombe wake mchanga atachinjwa kwa niaba ya kikundi uchaguliwa, na anajulikana kama Olopolosi-Olkiteng. Anakuwa kiongozi wa sherehe ya ibada hii.
Enkangoo Ntaritik
Baada ya sherehe hii kumalizika wavulana wanatahiriwa katika nyumba zao, na wanabaki kuwa waanzilishi kwa kipindi cha muda hadi watakapokuwa tayari kuanza mafunzo yao kama mashujaa. Wakati wamepona na wamelishwa vizuri, ujenga nyumba inayojulikana kama Enkangoo Ntaritik — Nyumba ya ndege na ni hapa ndipo wanaponyolewa kwa mara ya kwanza tangu mwanzo wa tukio hili.
Katika miaka ya hivi karibuni nyumba hizi hazijajengwa, wavulana wengi wananyolewa katika nyumba zao. Katika hatua hii vijana hawa mashujaa -Jlmurran-wanajulikana kama Ilkiliyani.
Kwa nakala zaidi zinazohusu kabila la kimaasai bofya hapa!