Mipango ya mabadiliko ya hali ya hewa na uchumi - mwaka 2050

Tanzania ya Mwaka 2050: Mabadiliko ya Uchumi na Hali ya Hewa

Orodha ya Yaliyomo

Muonekano wa Tanzania utakuwa na utofauti mkubwa kabisa katikati ya karne hii ya 21. Tanzania ina malengo ya kufikia hadhi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, pamoja na kujumuisha sekta ya kilimo cha kisasa kitakachowainua wakulima wadogo kutoka kwenye

Ukulima wa kisasa wa kutumia trekta na mashine zingine
Ukulima wa kisasa wa kutumia trekta na mashine zingine

umaskini, kuongezeka kwa ugawaji umeme, na Pato la Taifa kuimarika kupitia uzalishaji wa umeme unaotengenezwa kwa kutumia rasilimali za gesi asilia na makaa ya mawe. Idadi ya watu itakuwa karibu mara tatu kutoka milioni 45 mwaka 2010 hadi milioni 130 mwaka 2050 — na kwa mara ya kwanza, Watanzania wengi wataishi mijini kuliko vijijini.

Kufikia mwaka 2050, hali ya hewa ya Tanzania pia itabadilika. Joto tayari limeshaongezeka na mvua haziwezi kutabirika vizuri kwa sasa. Joto linaweza kuongezeka kwa angalau 1 ° C, labda 3 ° C katika maeneo kadhaa. Mategemeo ya kupungua kwa mvua ndani ya nchi yanaweza kusababisha uhaba wa maji, hali itakayosababisha Tanzania kuhitahitaji kulisha watu wengi wakati kukiwa na mvua kidogo katika maeneo muhimu ya kilimo. Kwenye pwani, sehemu muhimu katika sekta, idadi ya watu tayari imeshaongezeka haswa katika makazi yasiyokuwa rasmi kwenye maeneo ya mijini ambayo hayawezi kuendelea kuhifadhi wahamiaji wapya-mvua kubwa ina uwezekano wa kuathiri haya makazi, miundombinu, na mizunguko ya watu katika shughuli zao za kujikimu kimaisha. Sekta muhimu za kiuchumi tayari ziko hatarini pia kutokana na hali ya hewa; ifikapo mwaka 2050, gharama za kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa zinaweza kufikia takribani Dola za Kimarekani bilioni 1 kwa mwaka (GCAP 2011).

Kujenga uthabiti dhidi ya utofauti wa hali ya hewa na mabadiliko ya hali ya hewa ya muda mrefu ni suala la maendeleo la haraka kwa Tanzania, na miongo ijayo itakuwa muhimu sana kuwa ndani ya mipangilio ya uchumi wa nchi. Mandhari nzuri za aina mbalimbali na rasilimali asili za Tanzania tayari zinaathirika na mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na changamoto za sasa za maendeleo zinazotokana na ongezeko la kasi la idadi ya watu, utumiaji wa rasilimali uliopita kiasi, na uharibifu wa mazingira. Gharama za kiuchumi za hatari zinazohusiana na hali ya hewa zinaweza kudhoofisha uchumi mzima: kwa mfano, ukame wa mwaka 2005/06 uliathiri mamilioni ya watu na kugharimu takribani asilimia 1 na zaidi ya Pato la Taifa. Kufikia mwaka 2030 mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza

Mabaki ya vifaa vya umeme na uchafu mwingine Kariakoo
Mabaki ya vifaa vya umeme na uchafu mwingine Kariakoo

kuhesabiwa katika gharama halisi za uchumi zitazofikia asilimia 2-3 ya Pato la Taifa kwa mwaka (GCAP 2011), hali itakayotishia lengo la kufikia kima cha kipato cha kati. Gharama hizi zinazotarajiwa zinawakilisha changamoto ambazo zinazunguka vipaumbele vya Tanzania katika ukuaji wake wa msingi na upunguzaji wa umasikini, kuanzia katika sekta ya kilimo hadi nishati na kutoka vijijini hadi maendeleo ya miji.

Kutokana na hatari zinazoonekana sasa, kupuuzia mabadiliko ya hali ya hewa katika maamuzi ya leo ya maendeleo kutakuwa na gharama kubwa siku za usoni. Ujumbe huu unapendekeza Tanzania ichukuwe hatua za kujumuisha kwa ufanisi zaidi mabadiliko ya hali ya hewa katika mipango ya maendeleo na fedha. Kwa kujifunza kutoka kwenye kesi za kimataifa za nchi ambazo zimeshaanza mchakato huu, mahojiano na wadau muhimu kutoka serikalini, washirika wa maendeleo na sekta binafsi, mikutano ya mashauriano yameweka malengo mawili makuu:

1. Kutathmini mipango ya mabadiliko ya hali ya hewa ya sasa na fedha nchini Tanzania
2. Kupendekeza hatua ambazo Tanzania inaweza kuchukua kutekeleza mipango iliyopo ya mabadiliko ya hali ya hewa na kutumia misaada ya kiufundi na kifedha kimkakati zaidi ili kuweza kufanikisha malengo yaliyowekwa katika hali ya hewa

UCHAMBUZI WA UWEKEZAJI KATIKA HALI YA HEWA SASA

Gharama za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa zinaongezeka, kwahiyo hatua za mapema ni muhimu kupunguza gharama za baadaye. Kukabiliana na hatari za sasa za hali ya hewa inakadiriwa kuwa takriban Dola za Kimarekani milioni 500 kwa mwaka, na nyongeza ya Dola za Marekani milioni 100-150 kila mwaka zinahitajika ili kujenga uthabiti zadi kwa mabadiliko yajayo. Wakati hali ya hewa inabadilika, rasilimali zinazohitajika kwa marekebisho zitaongezeka haraka pia, na uwezekano wa kufikia Dola za Kimarekani bilioni 1 kwa mwaka ifikapo mwaka 2030 iwapo hatua hazitachukuliwa dhidi ya athari za hali ya hewa zilizopo (GCAP 2011). Baada ya Kutambua hitaji hili la kujiandaa sasa kwa kuzingatia gharama za baadaye iwapo hatua hazitachukuliwa, mnamo mwaka 2013, Tanzania ilipitisha Mkakati wa Kitaifa wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa (NCCS) na Mkakati wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa wa Zanzibar (ZCCS) kuongoza mwitikio wa kukabiliana na hatari za hali ya hewa na kuhamasisha rasilimali zingine zinazohitajika kuchukua hatua . Mikakati ya kitaifa ya

Philip Mpango - Waziri wa Fedha na Mipango wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Philip Mpango – Waziri wa Fedha na Mipango wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

ukuaji wa uchumi inatambua pia hatari za hali ya hewa (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania [URT] Tume ya Mipango ya Ofisi ya Rais 2011). Hatua hizi za awali katika mkakati huu wa hali ya hewa zinaambatana na matokeo yaliyopatikana hivi karibuni yanayoonyesha kwamba ukuaji wa uchumi unaendana na shughuli za kukabiliana hatari za hali ya hewa, bila kujali kiwango cha mapato ya nchi, na kwamba maamuzi ya leo ni muhimu sana kuwezesha nchi kwenda kwenye uchumi bora na wenye uthabiti zaidi dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. (Tume ya Kimataifa ya Hali ya Hewa na Uchumi 2014).

Tanzania imehamasisha ukusanyaji wa fedha kwa ajili ya hali ya hewa, lakini matokeo yamekuwa machache. Kati ya 2003 na 2014, Tanzania ilipata zaidi ya Dola za Marekani milioni 200 katika makubaliano ya kimataifa yanayohusu hali ya hewa, na nyongeza ya Dola za Marekani milioni 400 ambazo zinategemewa kupatikana. Ingawa fedha ni kubwa, kuna upungufu mkubwa kutokana na rasilimali zinazohitajika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Zaidi ya asilimia 80 ya rasilimali / nguvu kazi zilizopo ni kutoka kwa washirika wa maendeleo wa ndani ya nchi, ambao wana ushirikiano mdogo sana na Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa (United Nations Framework Convention on Climate Change – UNFCCC). Licha ya kupitishwa kwa NCCS na ZCCS, ushirikiano wa asilimia 100 kwa 100 wa kifedha bado haujafayika kutoka vyanzo vya ndani au vya kimataifa kuidhinisha uungaji mkono utekelezaji wa taasisi hizi. Njia ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa imekuwa ya mradi, imegawanyika, na inaendeshwa na wafadhili na matokeo yamekuwa magumu kupimika.

Fedha za sasa za hali ya hewa (a) hazitoshi kwa kile kinachohitajika kubadilika, (b) hazijalengwa katika mazingira yaliyo hatarini, na (c) zinasaidia miradi midogo badala ya mabadiliko makubwa. Licha ya hitaji la dharura la kujenga uthabiti, upatikanaji wa fedha za kukabiliana na hali ya hewa umekuwa ni changamoto, na viwango vya sasa vya ufadhili havitoshelezi kwani makadirio ya chini kwa sasa yanaonyesha kuwa angalau dola milioni 600 za kimarekani zinahitajika kila mwaka kwa marekebisho pekee. Cha kustaajabisha ni kwamba, ingawa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ni kipaumbele kilichotajwa cha NCCS na ZCCS, zaidi ya asilimia 65 ya hali ya hewa inaelekezwa kwenye shughuli za kupunguza. Kwa kuzingatia ukweli kwamba fedha za kimataifa za kukabiliana na hali ya hewa ni chache na fedha za umma zilizopo kwa ajili ya shughuli hii haziwezekani kufikia viwango vinavyohitajika, ni muhimu kuhakikisha kuwa fedha za hali ya hewa zinatumika kimkakati iwezekanavyo. Walakini, mipango ya mabadiliko ya hali ya hewa iliyopo ya kimkakati haionyeshi vipaumbele vya kisekta au kijiografia kushughulikia suala la mazingira yaliyo hatarini, hali ambayo inafanya ufanisi wa kufikia malengo kuwa changamoto. Sambamba, msaada wa kukabiliana na hali ya hewa na upunguzaji umeelekezwa zaidi kwenye ngazi za miradi inayofanya kazi peke yake kuzuia, lakini kimkakati na kimfumo bado ufanisi unaotegemea haujafikiwa.

CHUKUA HATUA LEO ILI KUFANIKISHA UTHABITI WA BAADAYE

Kwa Tanzania kuongeza upatikanaji wa fedha za hali ya hewa, noti hii ya sera inapendekeza nguzo nne muhimu za kujenga mazingira muhimu ya mafanikio:

»Uongozi madhubuti wa kuendeleza malengo ya hali ya hewa, kutetea mageuzi muhimu kwenye sera na mfumo wa taasisi, na kufafanua watendaji na majukumu
»Kupanga mipango ya mabadiliko ya hali ya hewa ambayo ni ya muda mrefu, inayolenga matokeo, na inayoendana vipaumbele vinavyoeleweka
»Mfumo wa kimkakati wa kupata vyanzo mbalimbali vya fedha za hali ya hewa
»Utekelezaji ambao unaojumuisha ufuatiliaji ulio wazi katika utendaji kwenye sehemu zilizowekezwa na matumizi ya fedha

Kuongezea juu ya NCCS na ZCCS, ambazo zimeweka kipaumbele cha kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, Tanzania lazima iweke michakato na mifumo ya kifedha ambayo itamudu changamoto kubwa zilizopo za ufadhili na utekelezaji. Maamuzi ya kimkakati lazima yachukuliwe ili kujipanga na kutumia rasilimali zilizo chache kugeuza mipango kuwa hatua za mabadiliko, kujifunza kutoka kwenye changamoto za zamani ili kufanikisha uthabiti mkubwa zaidi ambao utalinda maisha, uchumi, na mazingira.

Mapendekezo ya Ujumbe Huu ni Yafuatayo:

1. Kuutumia mfuko wa kitaifa wa hali ya hewa (NCF) kwa matarajio yanayoweza kufikika. Ingawa Tanzania Bara na Zanzibar ziko katika mchakato wa kukusanya fedha za kudumu za mabadiliko ya hali ya hewa, matarajio yanapaswa kuwa yanayoweza kufikika, ukizingatia gharama za kuanzisha na kusimamia fedha hizo na vile vile uwezo wa vyanzo vya fedha vinavyotarajiwa. Uzoefu unaonyesha kuwa muda na rasilimali zinazohitajika kutimiza mchakato wa kukusanya pesa mpya ni wa kiwango kikubwa, na gharama za usimamizi wa utendaji zinaweza pia kuwa kubwa. Ikiwa Tanzania itachagua kuanzisha mfuko wa hali ya hewa (au fedha), malengo na matarajio yanapaswa kuwekwa kiuangalifu na uwazi zaidi. Ili kuvutia upatikanaji wa fedha za hali ya hewa kwa kiwango kikubwa zaidi, itategemeana na ubora wa programu zilizotengenezwa kusaidia mchakato huu wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

2. Kujenga uthabiti katika mipango ya mabadiliko ya hali ya hewa katika kila sekta. Badala ya kutegemea utaratibu mmoja wa ufadhili, kuingiza mabadiliko ya hali ya hewa katika mipango ya sekta zilizopo inachukuliwa kuwa njia yenye uwezekano mkubwa wa kufikia malengo makubwa, endelevu. Sekta na mazingira muhimu mengi yaliyo hatarini tayari zimelengwa kwenye uwekezaji wa kiwango cha juu. Kutumia fursa kama hizo — kupitia mabadiliko ya hali ya hewa, kwa mfano, mifumo ya ukusanyaji fedha za maji na kilimo pamoja na baadhi ya shughuli mahsusi za miundombinu ya miji-inaweza kuboresha malengo ya uthabiti wa hali ya hewa kwa kiasi cha Dola za Kimarekani bilioni 2 katika uwekezaji kupitia benki peke yake. Fedha za hali ya hewa zinaweza kutumiwa kimkakati kuingiza shughuli za uthabiti katika

Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Stiegler's Gorge Tanzania
Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Stiegler’s Gorge Tanzania

uwekezaji wa miundombinu iliyopangwa (kwa mfano, kukuza miundombinu ya maji inayojengwa, kuiga mizunguko asili ya maji kwenye miji – green infrastructure) au kubuni mipango mipya inayolenga sehemu mahususi zilizozorota kwenye sekta zilizo hatarini au maeneo ya kijiografia.

3. Kuwezesha hatua kuchukuliwa katika ngazi za mtaa. Tanzania inaweza kuhakikisha misaada ya kiufundi na fedha inafikia serikali za mitaa kwa ufanisi zaidi. Serikali za mitaa hazina bajeti ya matumizi kwa hatari zinazohusiana na hali ya hewa na zinahitaji kuwezeshwa ili kupanga na kukabiliana na changamoto hii. Taasisi husika, kama mifuko ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa katika ngazi za wilaya, zinaonyesha matokeo ya kutia matumaini kwa sababu sasa serikali za mitaa zina uwezo wa kukabiliana haraka zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa na pia kwenye kuweka vipaumbele vya kugharamia michakato ya hali ya hewa inayoweza kutofautiana na mipango ya serikali kuu. Ingawa michakato huu umefanyika kwa kiwango kidogo hadi sasa sanasana kwenye wilaya za vijijini, inawezekana kuwa na fursa sawa kama hizi kwenye maeneo ya mijini.

4. Kuongeza vyanzo vya fedha tofauti na kuthibitisha matokeo. Ingawa wataalam wa kukabiliana na hali ya hewa wanaonekana kwamba wataendelea kusaidia vipaumbele vyao, Tanzania inaweza na inapaswa kutambua kwamba fedha hazitatosha kukabiliana kikamilifu na mabadiliko ya hali ya hewa na itahitajika kuongezeka kwa vyanzo vya ziada, hivi ni pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na sekta binafsi. Fedha kutoka katika makampuni ndani ya nchi zinazohusiana na majukumu ya kampuni kwa kijamii (Corporate social responsibility funding), kwa mfano, zinaweza kusaidia malengo ya hali ya hewa, na labda kuinuwa kwa kiwango kikubwa uwekezaji wa gesi asilia ili kuchangia vipaumbele vya hali ya hewa vya kitaifa, sekta, au ngazi za chini za jamii. Hiko wazi, kwamba uwezo wa Tanzania wa kuvutia na kukusanya fedha za mazingira ya hali ya hewa kwa kiwango kikubwa utategemea jinsi nchi itakavyoonesha matokeo ya kazi iliyofanyika. Kufikia lengo hilo, mfumo thabiti wa ufuatiliaji utakuwa muhimu kuhakikisha kuwa fedha ziliwekwezwa kwenye hali ya hewa na utendaji wake vimefikia matarajio. Mfumo huo wa ufuatiliaji utawezesha kupima matokeo ya mipango ya kimkakati na viwango vya kifedha na (kama ukifanikiwa) unaweza kufungua zaidi fursa za kifedha, yote hii itategemeana na uwezo utakaoneshwa na Tanzania katika kutekeleza vipaumbele vyake.

Kwa nakala zaidi zinazohusu hali ya hewa bofya hapa!