Misukosuko Ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Katika Karne ya 21
Orodha ya Yaliyomo
Kuanzia katikati ya miaka ya 1990 na kuendelea hadi miaka ya 2000, uchumi wa Tanzania ulikuwa tayari una changamoto ya kuzorota na usambazaji wa chakula umeathirika kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi waliongia kutoka nchi jirani za Rwanda, Burundi, na Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo); kutokana na hali hii nchi ilihamuwa kuomba misaada ya kimataifa kusaidia katika utunzaji wa wakimbizi. Wakati
huo huo, Tanzania ilikuwa ni eneo la vitendo vya kigaidi mnamo mwaka 1998 wakati ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam ulipolipuliwa; Watu 11 waliuawa, na wengine wengi walijeruhiwa.
Uchaguzi Mwaka 2000
Mkapa alikuwa amechaguliwa tena mwishoni mwa 2000 huku kukiwa na changamoto ya madai ya udanganyifu wa uchaguzi huko Zanzibar. Maandamano kadhaa ya vurugu yalifuatia, ikiwamo yale ya mnamo tarehe Januari 2001 ambapo nguvu za jeshi la polisi zilisababisha zaidi ya watu 40 kufa na watu 100 kujeruhiwa. Zanzibar pia ilizidi kupata matatizo na waislamu wa siasa kali. Maandamano kadhaa, shambulio la vurugu, na mabomu katika miaka ya 2000 yalitokea kwa sababu ya vikundi kadhaa vya siasa kali vilivyoandamana kupinga na kuilazimisha serikali kufuata maoni na sera zao. Pia mwishoni mwa mwaka 2004, watu 10 walifariki jijini Dar es salaam na mafuriko ya tsunami ya Bahari la Hindi; serikali ilikosolewa kwa kutofanya mikakati ya kutosha kuonya umma juu ya tishio la mafuriko kabla halijatokea.
Baada ya zaidi ya muongo mmoja wa kujiandaa, Tanzania, Uganda, na Kenya ilizindua Jumuiya ya Uhamiaji ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mnamo mwaka 2005 ili kujaribu kuhamasisha shughuli za kiuchumi katika eneo hilo. Mnamo mwaka 2009 Tanzania ilitia saini makubaliano ya kuruhusu watu na bidhaa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kupita huru kwenye mipaka, ambayo kwa wakati huu pia inajumuisha Burundi na Rwanda.
Uchaguzi Mwaka 2005
Wakati huo huo, uchaguzi wa pamoja wa rais na wabunge wa Tanzania ulifanyika mnamo Desemba 14, 2005. Waziri wa zamani wa mambo ya nje Jakaya Mrisho Kikwete, kama mgombea wa CCM, alichaguliwa; CCM yenyewe kiujumla ilishinda kwa nguvu katika Bunge la Kitaifa. Katika uchaguzi wa mwaka wa urais na wa kisheria, uliofanyika Oktoba 31, Kikwete alishinda muhula wa pili kama rais, kwa asilimia 61 ya kura. CCM, ingawa ilipoteza viti kadhaa kwa upinzani, bado ilikuwa na idadi kubwa ya wabunge. Uchaguzi huo ulifuatiwa na madai kutoka kwa vikundi kadhaa vya upinzani vilivyodai kwamba kura zilibadilishwa, na pia waangalizi wengine wa ndani na kimataifa walibaini masuala ya kutokuwepo kwa uwazi wakati wa mchakato wa upigaji kura.Chapisho hili limefadhiliwa na washirika wetu Wigs
Mapema mwaka huo, Zanzibar ilikuwa ilifanya kura ya maoni ya kuamua kama iunde serikali ya umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi wa Oktoba; asilimia 66 ya wapiga kura walipendelea kwenda na mwelekeo huo. Katika miaka iliyofuata, hata hivyo, kulikuwa na madai ya uhuru zaidi na vile vile wito wa kujitoa kutoka kwenye muungano na Tanzania bara.
Changamoto ya Rushwa
Rushwa, changamoto ya muda refu nchini Tanzania, ilibaki kuwa shida ya kutatiza chini ya utawala wa Kikwete, licha ya ahadi zake na juhudi za kupunguza athari zilizokuwa tayari zimetokea. Changomoto kubwa ilikuwa Edward Lowassa, mwanachama maarufu wa CCM na mshirika wa
Kikwete, ambaye alikuwa waziri mkuu lakini alijiuzulu mnamo mwaka 2008 baada ya kuingizwa katika kesi inayohusiana na rushwa; Lowassa alikana madai hayo. Mawaziri wengine wawili pia walijiuzulu kwa kashfa hiyo hiyo mwaka huo, na muda mfupi baadaye Kikwete alitengua baraza lake la mawaziri. Ufutaji mwingine wa baraza la mawaziri uliohusiana na matatizo ya ufisadi ulikuja mnamo 2012 wakati Kikwete alipofukuza mawaziri sita kwa madai ya utumiaji mbaya wa pesa za serikali. Ijapokuwa maafisa wengine wa serikali walikuwa wameshtumiwa kwa madai ya ufisadi, kukamatwa kabisa ilikuwa ni wachache sana. Lakini tofauti ilitokea mnamo Julai 2015 wakati mawaziri wa zamani Basil Mramba na Daniel Yona kila mmoja alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani kwa tuhuma zinazohusiana na rushwa.
Changamoto ya Katiba Mpya ya Serikali Tatu
Kikwete alipitia tukio la uandaaji wa katiba mpya wakati wa kipindi chake cha pili. Alipendekeza kwanza mapitio ya kikatiba mnamo 2011, na mwaka uliofuata tume ilianzishwa. Baada ya kukusanya maoni mengi kutoka kwa watanzania kote nchini na wataalam wa sheria ya katiba, tume hiyo ilipendekeza masuala kadhaa, kama kwenda kwenye mfumo wa serikali wenye tija tatu. Mkutano wa wabunge-wenye wajumbe wa Bunge la Kitaifa la Tanzania na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na zaidi ya wajumbe 200 kutoka mashirika ya asasi za kiraia- walikagua maagizo na walipewa majukumu ya kupitisha rasimu ambayo itawasilishwa kwa kura ya maoni ya kitaifa; theluthi mbili ya wapiga kura walihitajika kwa idhini kupita. Wabunge wengi wa CCM walioshiriki katika mkutano wa wabunge hawakuunga mkono pendekezo la kubadilika kwa serikali iliyokuwa na madaraka, wakihofia kwamba matokeo ya mabadiliko kama haya yatapendelea upinzani, wakati wapinzani wengi waliunga mkono pendekezo hilo; hii ilisababisha mgongano mkubwa. Jinsi majadiliano ya rasimu yalivyokuwa yanaendelea, wapinzani hawakuridhishwa hata kidogo. Na mnamo mwaka 2014 chama kikuu cha upinzani, Chadema, na vyama vingine vya upinzani vikahamua kuunda muungano, UKAWA, na kushinikiza bunge la katiba kusikiliza kesi ya malalamiko yao. Kitendo hicho, pamoja na kura za haraka na zilizokuwa na utata juu ya rasimu iliyopendekezwa na wabunge wengine, ilisababisha toleo la rasimu kupitishwa kwa kura ya maoni ambayo haikujumuisha muundo wa serikali tatu. Ingawa lengo lilikuwa la kura ya maoni ya Katiba kufanywa kabla ya uchaguzi wa rais na sheria wa Oktoba 2015, mwezi Aprili tume ya uchaguzi ilitangaza kwamba kura ya maoni itahitaji kucheleweshwa.
Uchaguzi Mwaka 2015
Na muda wa Kikwete wa kujiuzulu ulivyokuwa unakaribia baada ya mihula miwili kama rais, CCM ilianza mchakato wa kuchagua mgombea
wa uchaguzi wa urais wa 2015. Mnamo Julai 2015 ilimchagua waziri wa serikali John Magufuli, ambaye alikuwa na sifa ya kuwa na maadili na mkali juu ya ufisadi. Kiongozi wa muda mrefu wa CCM na waziri mkuu wa zamani Lowassa aliondoka katika chama hicho baada ya uteuzi wa Magufuli, alikasirika kwa kunyimwa nafasi hiyo; na muda si mrefu alijiunga na Chadema. Chadema, wakati huo, walikuwa wamefanya kazi kubwa kuongeza umaarufu wake na kupata wafuasi; na ilipofika mwaka 2014 ilizidi kupendwa na wapiga kura vijana. Chama hiki na washirika wake katika umoja wa Ukawa – uwepo wao ulikuwa ni muhimu kwani kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania wapinzani huwa wemegawanyika walikuwa na muungano – hali iliyofuatiwa na makubaliano ya kuchagua mgombeaji mmoja wa uchaguzi wa rais. Mara tu baada ya Lowassa kujiunga na Chadema, alipewa kiti cha mgombea wa urais wa umoja huo.
Uchaguzi wa rais na wabunge mnamo Oktoba 25, 2015, ndio uliokuwa ukigombewa sana nchini, kwa sababu ya hasira juu ya ufisadi na mwako mkubwa ulioleta na umoja wa upinzani. Matokeo ya uchaguzi yalipoanza kutangazwa, ilikuwa wazi kwamba wagombea kadhaa wa CCM wamepoteza viti vyao vya wabunge kwa wagombea wa Ukawa. Mnamo Oktoba 28 mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar alibatili uchaguzi huko, akidai kuwa sheria za uchaguzi zimekiukwa; waangalizi wa kimataifa walihofia uamuzi huo Pia siku hiyo, Lowassa alitaka kura za Urais zihesabiwe tena, akidai kuwa kulikuwa na makosa. Bila kujali, matokeo ya urais yalitolewa siku iliyofuata, na Magufuli alitangazwa mshindi kwa asilimia 58 za kura; Lowassa alichukua karibu asilimia 40. Licha ya changamoto ya kupoteza viti kadhaa, CCM ilifanikiwa kuendelea kuwa na idadi kubwa katika Bunge la Kitaifa.
Uchaguzi wa rais wa mitaa na wabunge wa Zanzibar ulirudiwa tena mnamo Machi 20, 2016. Chama kikuu cha upinzani, Civic United Front (CUF), kiliendelea kudai kwamba mgombea wake, Seif Sharif Hamad, alikuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Oktoba 2015, na kwa sababu hiyo alisusia marudio ya uchaguzi. Kilichofuatia, mgombea mwenza, Rais Ali Mohamed Shein wa CCM, alishinda kwa zaidi ya asilimia 90 ya kura. Wanadiplomasia kadhaa walielezea msimamo wao wa mwanzo kwamba uchaguzi wa Oktoba haukufaa kufutwa na kurudiwa.
Hizi ni baadhi tu ya changamoto mbalimbali ambazo nchi ilipitia ilipoanza karne ya 21. Kwa nakala zaidi zinazohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, gonga hapa!