Mtandao wa Barabara Tanzania

Mtandao wa Barabara Tanzania – Barabara Kuu, Lishi na za Kimataifa

Orodha ya Yaliyomo

Mtandao wa barabara wa Tanzania ni kilomita 86,472  (mi 53,731) kwa  urefu ambapo kilomita 12,789 (mi 7,945 ) imeainishwa kama barabara kuu na kilomita  21,105 (mi 13,114 ) kama barabara za kikanda.

Barabara

Wakala wa barabara Tanzania(TANROADS)- Wakala mkuu wa barabara chini ya wizara ya kazi, usafiri na mawasiliano- ilianza kufanya kazi Julai 2000 na ni  wakala anayehusika na maboresho na maendeleo ya barabara kuu na mtandao wa barabara wa kikanda Tanzania Bara. Jumla ya mtandao wa barabara zilizoainishwa Tanzania Bara ni Kilomita 86,472 sawa na (maili 53,731) kulingana na sheria ya barabara ya mwaka 2007. Wizara ya kazi kupitia wakala wa barabara (TANROADS) inasimamia mtandao wa barabara wa  taifa ambao ni takribani kilomita 33,891 (maili 21,059 ), inajumuisha kilomita 12786 (maili6,945) za barabara kuu na kilomita 21,105 (maili 13,114 ) barabara za kanda. Mtandao uliobaki ni takribani kilomita 53,460 (maili33,220 ) za ukanda wa mjini. Barabara za wilaya na za vumbi  ziko chini ya uangalizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Mnamo mwaka 2007, kulikuwapo barabara za kilomita 91,049 (maili 56,575 ) ikiwa pamoja  na kilomita  6,578 (maili 4,087 ) za barabara za lami. Mtandao huu wa barabara unashika nafasi ya 51 kwa urefu ulimwenguni .

Barabara Kuu

  •     Dar es salaam na Dodoma (kilomita 451 (maili 280) zote lami): Barabara A-7 inazounganisha Dar es salaam na Morogoro halafu barabara ya B – 129 inaunganisha Morogoro na Dodoma
  •     Dar es salaam na Iringa (kilomita 492 (maili 306) zote lami): Barabara A-7 inaunganisha miji hiyo
  •     Dar es salaam na Tanga (kilomita 354(maili 220) zote lami). Barabara A-7 inaunganisha Dar es salaam na Chalinze halafu barabara ya A-14 inaunganisha Chalinze na Tanga
  •     Dar es salaam na Mtwara (kilomita 556(maili 345) zote lami) .Barabara B-2 inaunganisha miji hiyo

Kipande cha barabara kilichobaki cha Dar es salaam kina lami. Daraja refu la Mkapa lipo kwenye kipande hiki kilichopanuliwa hadi mto Rufiji

  • Tanga na Arusha (kilomita 435 (maili 270) zote lami): Barabara ya A-14 inaunganisha Tanga na Segera, kuanzia hapo barabara ya B-2 inaunganisha mwisho wa barabara na makutano ya Himo. Barabara ya A-23 baada inafuatia na kuelekea magharibi ya Moshi na Arusha
  • Dodoma na Mwanza kwenye ziwa Viktoria (kilomita 701(maili 436) zote lami). Barabara ya B-129 inaelekea magharibi mwa Manyoni
    Mfano wa Barabara Kuu Tanzania
    Mfano wa Barabara Kuu Tanzania

    ikifuatiwa na barabara ya B-141 kaskazini mwa Singida, kuanzia hapo barabara ya B-141 kaskazini mwa Singida, inayofuatiwa na barabara ya B-3 inayoelekea zaidi magharibi mwa Nzega. Kipande cha mwisho kipo kwenye barabara ya B-6 kupitia Shinyanga kuelekea Mwanza

  • Dar es salaam na mpaka wa Rwanda kwenye maporomoko ya Rusomo (kilomita 1,281(maili 796) zote lami): Kuanzia Nzega kwenye mkoa wa Tabora barabara ya B-3 inakwenda hadi kwenye mpaka na Rwanda (km 380(mi 240)
  • Kigoma na mpaka wa Burundi katika Manyovu: barabara yote ni lami
  • Mwanza na Musoma (kilomita 218 (maili 135) zote lami): Barabara B inaunganisha miji yote hiyo kisha inaendelea magharibi hadi kwenye mpaka na Kenya
  • Arusha na Namanga kwenye mpaka wa Kenya (kilomita 106 (maili 66): Barabara ya A -104 yote ina lami
  • Iringa na Mbeya (kilomita 330 (maili 210) zote lami): Barabara ya A-104 inaunganisha miji hiyo, ambapo mwisho wake ni Tunduma kwenye mpaka na Zambia.

Barabara kuu Tanzania zinatambulishwa na namba zinazofuata mfumo wa namba za ngazi mbili ikitanguliwa na A- na B-, kama inavyofanyika kote  Afrika Mashariki. Zifuatazo ni orodha za Barabara kuu za Tanzania. Kwa sasa Tanzania imeanzisha mfumo wa namba kwa barabara kuu ambazo zinaanziwa na “T” lakini hadi kufika sasa uteuzi wa “A” unaonekana kote.

Namba ya Barabara Urefu Mtandao Inapitia Hali Yake Maoni Zaidi
A7 492 km Dar es Salaam – Iringa Chalinze – Morogoro – Mikumi Paved
A14 315 km Chalinze – Horohoro Segera – Tanga Paved Inaendelea ndani ya Kenya mpaka Mombasa
A19 620 km Masasi – Mbamba Bay Tunduru – Songea – Mbinga Paved/Unpaved Imewekwa lami: Masasi – Ngomano (56 km) na Namtumbo – Mbinga (168 km)
A23 117 km Arusha – Holili Moshi Paved Inaendelea ndani ya Kenya mpaka Voi
A104 1,218 km Tunduma- Namanga Mbeya – Iringa – Dodoma – Kondoa – Arusha Paved Sehemu nzima ya barabara kuu ya Cairo-Cape Town Highway, imewekwa lami hivi karibuni: Dodoma – Babati (257 km)
B1 263 km Segera – Himo Paved Inaunganisha A14 na A23
B2 561 km Dar es Salaam – Mtwara Kilwa – Lindi Paved Imewekwa lami kilometa 30 kwenda Kilwa Masoko kutokea Nangurukuru
B3 625 km Singida – Rusumo Falls Nzega – Isaka – Kahama Paved Inatumika kama B6 Nzega – Tinde (42 km), na kuendelea kama RN3 ndani ya Rwanda mpaka Kigali
B4 293 km Makambako – Songea Njombe Paved
B5 120 km Mingoyo – Masasi Paved Inaunganisha B2 kwenda A19
B6 1,071 km Makogolosi – Sirari Rungwa – Tabora – Shinyanga – Mwanza Paved/Unpaved Imewekwa lami: Nzega – Sirari (kilometa 524), Inatandaa na B3 Nzega – Tinde (42 km)
B8 1,128 km Kasesha – Mutukula Sumbawanga – Mpanda – Kasulu – Biharamulo – Bukoba Paved/Unpaved Imewekwa lami: Lusahunga (B3) – Mutukula (287 km)
B129 388 km Morogoro – Manyoni Dodoma Paved
B141 308 km Rungwa – SIngida Itigi – Manyoni Paved/Unpaved Imewekwa lami: Itigi – Singida (160 km)
B143 151 km Singida – Babati Paved
B144 390 km Makuyuni – Kukirango Karatu – Ngorongoro – Serengeti National Park Paved/Unpaved Imewekwa lami: Makuyuni – Ngorongoro (79 km), iliyobakia haiwezi kuwekwa lami kwa sababu ni hifadhi ya taifa
B163 230 km Usagara – Biharamulo Sengerema – Geita Paved/Unpaved Haijawekwa lami: Bwanga – Biharamulo (68 km), lami imeanza na kupitia Chato kwenda Bukoba
B182 171 km Nyakasanza – Kyaka Kimisi – Burigi Game Reserve – Omurushaka Paved/Unpaved Imewekwa lami: Omurushaka – Kyaka (57 km), inaunganisha B3 kwenda B8
B182 W 111 km Omurushaka – Murongo Unpaved Inagawanyika kutoka B182 na kuendelea mpaka mpaka wa Murongo kuvukia Uganda
173 km Bulahu – Lamadai Bariadi Paved/Unpaved Imewekwa lami: Bariadi – Lamadai (72 km), na inatambulika kama barabara kuu na TANROADS lakini haina namba.
59 km Nyakasanza – Kobero Ngara – Kabanga Paved Imegawanyika kutoka B3 mpaka kwenye mpaka wa Kobero kuvukia Burundi, na kuendelea kama RN6 huko mbele

Barabara za Mikoa

  • Mkoa wa mtwara: barabara za lami zinazounganisha Mtwara na Masasi na kuanzia hapo hadi kufikia karibu na Nangoma. Barabara zisizo na lami zinaelekea Mtambaswala na daraja la kisasa lililopo kwenye mpaka wa Msumbiji. Mwaka 2012 benki ya maendeleo ya Afrika
    Barabara isiyokuwa na lami
    Barabara isiyokuwa na lami

    iliidhinisha mkopo wa kukarabati barabara hii, ambao ulifuatiwa na mkopo wa ziada wa bilioni 7.659  Yen (dola milioni za kimarekani 77.9) pia kutoka Japan

  •  Mikoa ya magharibi ndio ina huduma mbovu zaidi ,ikiwa haina barabara kuu za lami isipokua Kigoma na Ujiji .Barabara ya vumbi moja tu inayoelekea chini ya magharibi mwa nchi, inayofuatia ni Kasulu na Sumbawanga ambayo inakumbwa sana na mafuriko kusini mwa Mpanda kati ya Tunduma ndani ya kusini magharibi mwa makutano ya Nyakanyazi karibu na Kibondo kaskazini-magharibi, umbali wa karibu kilomita 1000 hakuna barabara kuu katikati mwa nchi

Barabara Kuu za Kimataifa

Barabara kuu ya Cairo-Capetown, barabara kuu #4 iliyo katika mtandao wa barabara kuu ya Afrika inayopita kaskazini mwa mji wa Namanga kwenye mpaka wa Kenya na mpaka wa Zambia kwenye mji wa Tunduma kusini magharibi, kupitia Arusha, Dodoma, Iringa na Mbeya. Kipande cha kuingilia mbuga ya taifa ya Tarangire na Iringa ambayo kwa imemalizika kuwekwa lami kati ya Babati-Kondoa-Dodoma-Iringa. Kwa sasa hakuna haja tena ya kupitia njia ndefu ya mashariki kutokea Arusha kuelekea Iringa kupitia Moshi na Morogoro ina lami. Hii njia ni kilomita 921(maili 572) kulinganisha na kilomita 689(maili 428) kwa njia ya Arusha-Dodoma-Iringa.

Upande wa kusini magharibi kutokea Iringa kuelekea Tunduma, njia kuu ya Cairo-Capetown inafuata njia kuu ya Tanzania inayounganisha Zambia na Dar es salaam.

Kwa nakala zaidi zinazohusu miundombinu bofya hapa!