Waganga wa Kienyeji wa Tanzania dhidi ya Mila!
Ni ukweli usio na utata kwa wote waganga na matabibu wa kisasa kwamba kitengo cha waganga wa kienyeji wa Tanzania kimetengwa na taasisi za tiba za kisasa. Matabibu wakisasa wamechukulia kwamba imani ilio bora zaidi kwa waganga wa kienyeji ni ushirikina ambao mara nyingi huwafanya watu waugue sababu ya ‘madhara ya kisaikolojia’, na kwa hali mbaya zaidi, waganga wameiendeleza hii imani maana ni
nzuri kwa biashara na hupelekea vifo vibaya pale ushirikina unapowalenga watu walioshtakiwa kwa uchawi na hatimae kuuwawa vibaya na ‘waliowahasi’ au na wanaowawinda wachawi. Ni dhahiri kwamba hizi fikra za matabibu wa kisasa zina ukweli fulani na ni muhimu kwa sababu vifo vibaya vinatokea, lakini haiwakilishi picha kamili ya uhusiano ambao upo kati ya waganga na wachawi, kiushirikina na katika kutibu magonjwa. Kwa kesi nnayoileta hapa, waganga kwa njia moja au nyingine kimtazamo wanashiriki katika mahusiano yaliopo kati yao na mila kama ambavyo matabibu wataalamu wanavyoamini, lakini, kwa sababu ya ujuzi wao na mgawanyiko wa kazi, wamejiandaa kufafanua mitizamo yao kwa undani zaidi.
Mazungumzo na Mganga
Kule Kyela (moja ya eneo la mkoa wa Mbeya, Tanzania), kama ilivyo kwa sehemu mbali mbali Tanzania, watu 25 wanasema kuna uwezekano wa uchawi kuwa nyuma ya magonjwa yaliofafanuliwa kitaaluma kama malaria (haya ni mazungumzo kati ya mtafiti Beckie na Mganga, yakionyesha maoni haya):
Beckie:Kwanini mtu anaweza kuwa na malaria akaenda hospitali,ambapo akapewa dawa ya malaria,lakini hapati nafuu? au, ana dalili za malaria, lakini damu yake ikichunguzwa, hawapati vimelea vyovyote?
Mganga: Hawawezi kuviona.
Beckie: Mmmm
Mganga: Kama nilivosema, hawawezi kuviona hivo vimelea kwa sababu ya mila, ambazo inazificha visionekane vikiwa mwilini. Mila zinauandaa mwili uwe hivyo. Kwa hio hizo dawa haziwezi kufanya kazi. Mganga anaweza akatumia dawa zake na mgonjwa akapata nafuu. Sio ujuzi wao hapo (hospitalini), lazima utumie utundu na ujanja………Hivyo magonjwa yanayosababishwa na mila hayawezi kuonekana. Hayawezi kuonekana, lakini kama unaujua uchawi, basi, unaweza kuyafanyia kazi. Hata hivyo, inawapa (mahospitalini) ugumu…..Yeye (mtabibu mtaalamu) asiuingilie-sio mlango wake. Tunajua kuhusu wachawi. Hawezi kuingia hapo.
Kule Kyela,wanyakyusa wameweka wazi uhusiano kati ya wachawi na mila. Mila katika majadiliano hapo juu imetumika kuonyesha ubaya wa uchawi. Hata hivyo,mila na uchawi zina mahusiano katika njia ngumu zaidi, kwa sababu zinatengeneza mazingira ambayo uchawi wa aina mahsusi unaidhinishwa. Kama mtu hatekelezi jukumu lililoelekezwa kwenye mila, kwa mfano kuleta chakula (amapijilo) msibani kwa wakwe zake, basi watahukumiwa kwa imbepo sya bandu – ambayo inaweza kueleweka vizuri kama maneno ya watu. Ni haya maneno ambayo yanatamkwa na wanajamii wote (sio mtu mmoja) kwa hasira dhidi ya mtu ambaye anaweza kumfamyia mtu,au ndugu zake waugue. Ni mkusanyiko huu wa maneno haya ya kutokuridhishwa ambayo yana nguvu za kimazingaombwe, na ambayo yanatofautisha chanzo cha magonjwa ya aina hii ya mazingaombwe na kazi ya mchawi mmoja mmoja. Imbepo sya bandu haiwezi kueleweka kama uchawi wa moja kwa moja; inavyoeleweka inategemea na maono ya mhusika mwenyewe binafsi. Kutoka kwa mlengo wa ukoo na majirani waliokosewa, imbepo sya bandu ni kitendo cha hukumu ya kimaadili. Ni njia ya kumuondoa mtu aliesababisha tafrani na mtu asie na mahusiano mazuri na wenzake ya kijamii. Wale wanaopuuza kutimiza majukumu yao ya kimila wanaugua, na wasipotambua na kuomba radhi kwa umma kwa makosa yao, wanakufa. Kwa maneno ya kikongwe anaeyajua haya mambo ‘mimi ni mtu wa kitambo sana,na najua kila kitu. Kama mtu kafanya kitu kibaya ndio hivyo. Ataenda.  Ataondoka. ‘ Hii ni tofauti na uchawi, ubulosi, inayomaanisha kitendo kiovu cha mtu mwenye tamaa ya nyama ya binadamu.
Hata hivyo waganga, walielekea kwenye maono, kama walivoyachukua matabibu wataalamu, kwamba imbepo sya bandu imeenda mbali sana, na kama aina hii ya uchawi unahitaji kusitishwa, basi na mila isitishwe ambayo ndipo ilipotabiriwa. Kiuhakika sheria ndogo ndogo za mitaani ambazo zilipitishwa dhidi ya `Mila potofu ‘ ililenga mila ambazo zilikuwa na mahusiano na imbepo sya bandu, na waganga waliziunga mkono kikamilifu hizi sheria mpya ndogo ndogo za mitaani. Kwa mfano,mganga mmoja, ambaye imetokea kuwa ni myakyusa alikazania kuwa mila hizi lazima zisitishwe:
Nikiongea waziwazi, nakubaliana na ambalo serikali inawaza kulihusu hili. Nimefurahi sana-lakini Wanyakyusa hawazifuati sheria ndogo ndogo za mitaani. Naamini hili ndilo linalochangia gonjwa ambalo inabidi nilitibu…maana mpaka sasa hivi hizi mila potofu ni kama aina fulani ya uchawi. Kwa mfano,kama wewe ni dada yangu,na umeolewa…basi,utakapojifungua mtoto, lazima nije kwako na zawadi-wote huja na kuleta pesa. Bwana, akishajifungua hapo, ndio hivyo-unatumwa na mila-hili ni deni. Mila hii inaingiza uchawi. Kama hawaendi na zawadi kusema ‘asante kwa mtoto’ na ‘pole kwa misukosuko ya uzazi’-wanakupatia ‘sindano’ yao. Unaenda hospitalini, unadhani hii ni malaria, lakini…Ugonjwa huo haujaja sababu ya malaria, ni mila. Maana yao ni kukuua.
Bila kubagua, kila mwanachama wa CHAWATIATA (Chama cha Waganga wa Tiba Asilia Tanzania) ambao niliongea nao walipinga mila ilioelekezwa kwenye sheria ndogo ndogo za mitaani, maana wanahaisi inachangia matukio ya uvamizi wa kishirikina, ingawa mawazo yao yalitofautiana kidogo na matabibu wakisasa, waliunga mkono uvumbuzi huu na nguvu hii inayoenda kinyume na hisia ya sehemu kubwa ya jamii. Kulikuwa na watu wengi Kyela (lakini sio wote kwa vyovyote vile) ambao walifikiria kuwa sheria ndogo ndogo za mitaani zingedhoofisha mshikamano katika koo, maana upande mwingine ina maanisha katika hizi mila kuna sifa nzuri iliyokuwa inaimarisha mshikamano wa kiundugu. Kabla ya mazungumzo haya, nilikosea kudhani kuwa waganga, kwa sababu wanajulikama kama ‘wa kimila’ na sababu wanafaidika na biashara hii,wangechukua mlengo huu wa mawazo, lakini badala yake walikuwa pia na wasiwasi na huzuni sana juu ya idadi kubwa ya vifo ambayo vilikuwa na mwelekeo wa hizi mila. Kwa kesi hii maoni ya waganga wa ‘kienyeji’ ilikuwa ni kusitisha ‘mila’.
Matokea haya yanapingana na kuthibitisha kazi ya hivi karibuni ya Maia Green (Profesa wa Anthropolojia ya Jamii, Chuo Kikuu cha Manchester) inayohusika na kutafuta jinsi ya kuuzuia uchawi Tanzania. Anaeleza kuwa matabibu wa kisasa watafaidika kutokana na `kutokomezwa’ kwa imani za kichawi- kutoka kwenye mauzo dawa zilizokuwa zinatumika kutowa kinga, na kwa kutakasa idadi kubwa ya watu walioshtakiwa kwa uchawi. Wajumbe wa CHAWATIATA huko Kyela, hawakuwa tayari kuvumilia idadi kubwa ya kuumwa kulikodhaniwa kunahusishwa na imbepo sya bandu- ingawa hii haikuwi takwa lao kama wajasiriamali. Sheria ndogo ndogo za mitaani ziko kwa manufaa ya waganga ambao kwa wastani ni watu wenye utajiri katika jamii, na ambao wanategemewa kuwa wachangiaji muhimu katika matukio yanayohusiana na uzazi na vifo wa ndugu na majirani katika wilaya. Kwa upande mwingine, katika kuyaunga mkono matokeo ya Green na Mesaki kwamba wataalaam wanaopinga uchawi wana uhusiano na mambo ya kisasa, kwa sababu ni ‘wapenda maendeleo’,tunaweza kuona kwamba waganga Kyela wanatamani kuwasaidia watu wa kawaida wajikusanyie utajiri wa mali bila kuogopa matokeo ya wivu wa jirani zao, na kufanya kazi zao ziwe za kisasa kwa kuendana na teknolojia.
Kwa nakala zaidi zinazohusu tiba za asili bofya hapa!