Hatari za Hali ya Hewa Zinazoikabiri Tanzania
Orodha ya Yaliyomo
Muhtasari wa Nchi
Tanzania ni moja wapo ya nchi kubwa Afrika Mashariki na ina idadi ya watu na uchumi unaokuwa kwa kasi. Ukuaji wa uchumi umechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza umasikini katika miaka ya hivi karibuni; Walakini, asilimia 28 ya watanzania wameendelea kuwa chini ya kiwango cha umaskini cha kitaifa. Kupanda kwa joto, ukavu wa muda mrefu, mvua nzito na kuongezeka kwa kiwango cha bahari kunaifanya Tanzania kuwa nchi ya 26 katika orodha ya mataifa yaliyo karibu zaidi na hatari za hali ya hewa. Idadi ya sasa ya watu ya milioni 56 inatarajiwa kuongezeka hadi 130 milioni ifikapo mwaka 2050. Asilimia thelathini na mbili ya watu hawa wanaishi ndani maeneo ya mijini, na asilimia 75 ya watu hao wanaishi katika makazi yasiyokuwa rasmi ambayo yanazidi kuwa hatarini kutokana na uhaba wa maji, mafuriko na joto kali. Katika maeneo ya vijijini, kuna utegemezi wa hali ya juu wa kilimo cha kutumia mvua na ufikiaji mdogo wa huduma za afya, elimu na umeme. Mavuno ya mazao muhimu, ambayo ni pamoja na mahindi, maharagwe, mtama na mchele, yanakadiriwa kupungua katika
miongo ijayo, hali ambayo itahatarisha maisha na usalama wa uwepo wa chakula. Maisha na usambazaji wa chakula pia hutegemea uvuvi uliopo katika pwani na miundo mingine ya maji (kama maziwa na mabwawa), ambao unazidi kutishiwa na joto la bahari na joto la maji safi, na kujaa kwa mchanga baada ya mvua nzito. Hatari za hali ya hewa ikiwamo kuongezeka kwa Kiwango cha bahari kunaweka miundombinu ya pwani, idadi ya watu wa pwani (karibu asilimia 25 ya jumla ya watu wa nchi nzima), na mazingira ya pwani kwa ujumla kuwa hatarini kufurika, kujaa chumvi na kupigwa na madhoruba zaidi.
Â
Muhtasari wa Hali ya Hewa
Utofauti wa topografia (muundo wa ardhi) wa Tanzania unaigawanya nchi katika maeneo manne tofauti ya hali ya hewa: 1) ukanda wa pwani wa joto na unyevu (hii ni pamoja na kisiwa cha Zanzibari): una joto la joto, wastani wa 27-30 ° C, na upata milimita 750-1,250 za mvua kwa mwaka, ambapo Zanzibar inapata 1,400-2,000 mm; 2) Bonde la joto la kati na lenye ukame: hili upata mm 500 tu ya mvua; 3) eneo lenye maziwa baridi ya kiwango kirefu kaskazini na magharibi (nyumbani kwa maziwa na mabonde ya ufa wa Afrika Mashariki) upata milimita 750-1,250 ya mvua kila mwaka; na 4) Nyanda za juu za kaskazini mashariki (kama Kilimanjaro) na kusini magharibi: ni sehemu ya maeneo baridi zaidi ya nchi na joto wastani wa 20-25 C. Nyanda za juu kusini magharibi na bonde la Ziwa Tanganyika magharibi upata mvua nyingi, zaidi ya 2000 mm kila mwaka. Hii imechangiwa kuwepo katika eneo la kitropiki la kati linaloungana, mvua ni za misimu. Kaskazini na mashariki kuna misimu miwili ya mvua, msimu wa kwanza ni Machi hadi Mei na msimu wa pili kutoka Oktoba hadi Desemba. Kanda za kusini, magharibi na kati zina msimu mmoja tu wa mvua kutoka Oktoba hadi Mei.
Historia ya Hali ya Hewa
Hali ya kihistoria ya hali ya hewa inajumuisha yafuatayo:
• Kuongezeka kwa joto wastani wa 1 ° C (kati ya miaka 1960-2006).
• Mabadiliko madogo katika muundo wa mvua (precipitation) kiujumla; ambao umepungua kidogo kutoka 1961 hadi 2013, haswa kuanzia Machi hadi Juni (sambamba na msimu mkuu wa mvua).
• Kuongeza kasi ya upungufu wa theluji kwenye Mlima Kilimanjaro;
ambapo asilimia 85 imepunguwa kwenye kilele cha Kibo kuanzia mwaka 1912 hadi 2009.
• Kupanda kwa kiwango cha bahari cha cm 4-20 kwa muongo mmoja (1955-2003) kila mahali isipokuwa Zanzibar, ambayo kumbukumbu inaonyesha kupungua kwake kwa kiwango cha bahari kulikuwa kati ya miaka 1984-2004.
Hatari za Hali ya Hewa Zinazotarajiwa
Mabadiliko yanayotarajiwa hapo ifikapo 2050 ni pamoja na:
• Ongezeko la wastani wa joto la kila mwaka la 1.4 hadi 2.3 ° C; ongezeko kubwa la joto katika magharibi / kusini magharibi.
• Kuongezeka kwa kipindi cha mawimbi ya joto (kwa siku 722) na ukavu (hadi siku 7).
• Uwezo wa kuongezeka kwa wastani wa mvua ya kila mwaka (kati ya asilimia -3 hadi +9), haswa upande wa kaskazini mashariki; kushuka kwa mvua kati ya miezi Julai-Septemba.
• Kuongezeka kwa idadi ya mvua kubwa (asilimia 7-40) na kiwango (asilimia 2-11).
• Kupanda kwa kiwango cha bahari kwa cm 16 hadi 42 cm.
• Kutoweka kwa barafu katika mlima Kilimanjaro.
Athari Katika Sekta na Udhaifu
Kilimo
Kuongezeka kwa joto, ukame wa muda mrefu zaidi na mvua za mara kwa mara na kali huweka uzalishaji wa mazao na mifugo nchini Tanzania katika hatari. Sekta ya kilimo ni takribani asilimia 25 ya Pato la Taifa na inaajiri asilimia 75-80 ya watanzania. Karibu asilimia 80 ya uzalishaji wa kilimo hutokana na kilimo cha mvua, na za pembejeo ndogo zilizo katika mazingira magumu na rahisi kuathiriwa na hatari za hali ya hewa zinazojitokeza sasa. Theluthi moja ya ardhi ya mazao, hekta milioni 4, imetengwa kwa ajili ya mahindi, ambayo inawakilisha asilimia 40 ya ulaji wa nishati za mwili (calories) kitaifa. Wakati kuongezeka kwa joto kunaleta faidi kwa kilimo cha mahindi yaliyonyeshwa na mvua kwenye nyanda za juu, uzalishaji wa kitaifa unakadiriwa kupungua kwa kiwango cha 8-13 ifikapo 2050 kutokana na kuongezeka kwa joto, ukame, mmomomyoko na uharibifu utokanao na mafuriko. Makadirio ya mavuno ya maharagwe, mtama na mchele yanafuata mwenendo huo huo wa mahindi, ambapo yanatarajiwa kupungua kwa asilimia 5-9 ifikapo 2050. Kuongeza kwa ukali wa joto na usambaaji wa mende wa aina ya “Coffee berry borer beetle” kutasababisha kupungua kwa uzalishaji wa kahawa kutoka kilo 225 / ha sasa hadi chini ya kilo 100 / ha mnamo mwaka 2060. Pwani, mazao ya mihogo na mchele yanaathirika na kuongezeka kwa chumvi kwenye ardhi, kujaa kwa maji kwenye ardhi (utopeutope) na kuongezeka kwa kiwango cha bahari. Uzalishaji wa mifugo, unaofanywa na asilimia 60 ya kaya za vijijini na ambao pia ni asilimia 25 ya Pato la Taifa la kilimo, uko hatarini kutokana na kuongezeka kwa joto, mafuriko, uharibifu wa ardhi ya malisho na magonjwa, kama homa ya Bonde la Ufa.
Rasilimali za Maji
Tanzania ina rasilimali kubwa ya maji (kilomita 962 kwa mwaka inayoweza kufanywa upya); Walakini, sehemu kubwa ya ukame mkali na yenye ukame wa kati (ambayo ni hadi asilimia 50 ya nchi) na misimu ya mvua inayobadilika husababisha uhaba wa maji wa muda. Kuongezeka kwa joto, ukame wa muda mrefu na matukio makubwa ya mvua yanatishia mabonde kuu ya mito tisa na maziwa matatu kubwa katika bara la Afrika (Victoria, Tanganyika na Nyasa).
Wakati mtiririko wa mito wa baadaye utakuwa unasukumwa sana na mambo yasiyokuwa ya kihali ya hewa kama mabadiliko katika matumizi ya ardhi, makadirio ya hali ya hewa yanaonyesha kuongezeka kwa mtiririko wa mito Pangani na Rufiji, ambayo itaongeza hatari ya mafuriko na kuzama, na kupungua kwa mtiririko wa maji wa Wami / Ruvu, hali ambayo itaongeza uhaba wa maji katika miji ya Dar es Salaam, Morogoro, Kibaha na Dodoma (na idadi ya watu zaidi ya milioni 6). Upatikanaji wa maji pia utategemea muondelezo wa mito ambayo inatokea nchi jirani, kwani asilimia 13 ya rasilimali za maji zilizopo Tanzania zinavuka mipaka ya nchi. Sehemu za mijini Bara hutegemea kimsingi vyanzo vya maji vilivyopo kwenye uso ardhi ambavyo vinazidi kuchafuliwa na kutishiwa zaidi na matukio ya mvua nzito zinazoosha madini, uchafuzi wa kibiashara na kutoka majumbani katika mito, maziwa na maeneo ya mvua. Kiwango cha maji kilichopunguzwa wingi wake na ubora, vitasababisha miji ya pwani kuzidi kutegemea maji ya chini ya ardhi, ambayo tayari yako katika hatari ya kujaa chumvi.
Afya ya Binadamu
Magonjwa ya kuhara na malaria, magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo nchini Tanzania, yanaweza kuongezeka kwa sababu ya kuongezeka kwa joto na matukio makubwa ya mvua. Wakati viashiria vya afya vimeboreka kiujumla, urefu wa maisha wa Tanzania ni miaka 65 tu. Inakadiriwa mafuriko yanatishia kulipuka zaidi kwa magonjwa yanayotokana na maji kama kipindupindu na typhoid, kwani ni asilimia 61 tu ya watu wanapata maji ya kunywa kutoka katika vyanzo bora na ni asilimia 19 tu wana makazi yaliyoboreshwa na mfumo wa maji taka/machafu. Programu thabiti za kiafya zimepunguza kuongezeka kwa ugonjwa wa Malaria na vifo katika miaka ya hivi karibuni, lakini bado asilimia 93 ya watu wanabaki hatarini kwa ugonjwa wa malaria, na kesi mpya zinaibuka katika maeneo ya kihistoria ambayo hayana ugonjwa wa Malaria kama Tanga, Kilimanjaro na nyanda za juu za Arusha. Pia kasi ya uhamiaji ambao haukupangwa mijini kwa kiasi kikubwa unahatarisha watu wengi kutokana na mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha. Huko Dar es salaam, mafuriko mnamo Desemba 2011 na Januari 2012 yalisababisha vifo vya watu 40 na kuhamisha watu zaidi ya 10,000.
Nishati
Karibu asilimia 40 ya uzalishaji nishati nchini Tanzania ambayo tayari haitoshelezi hutoka katika nguvu ya mabwawa (hydro) yaliyopo katika mazingira magumu kutokana na kuongezeka kwa uvukizi wa maji, kujaa kwa matope na ukame wa muda mrefu. Ukame uliokuwa wa muda mrefu kupita kiasi mnamo Oktoba 2015 nusura husababisha kusitisha kwa uzalishaji wa umeme kwa nchi nzima. Wakati mtiririko wa mito kwa siku zijazo unaweza kuongezeka katika mabonde ya Pangani na Rufiji,
yote muhimu kwa uzalishaji wa umeme, kuongezeka kwa uvukizi na maji kujaa matope vitaipa Tanzania shinikizo kubwa kwenye kuzalisha umeme, ambao kwa sasa unafikia asilimia 16 hadi 18 tu ya idadi ya watu. Hii ni mifano michache tu ya hatari za hali ya hewa ambazo tayari Tanzania imeshapitia katika sekta ya nishati.
Mifumo ya Mazingira
Kuanzia miamba ya matumbawe, hadi Serengeti, hadi kilele cha juu zaidi barani Afrika kwenye Mlima Kilimanjaro, Tanzania ina mazingira muhimu na viumbe hai vya kila aina vipatikanavyo ulimwenguni. Nchi inajumuisha maeneo manne yenye maji yaliyotuhama (wetlands) yanayotambuliwa kimataifa (maeneo ya Ramsar) na sehemu ya kusini ya Misitu ya pwani ya Afrika Mashariki ambayo ni kuu kwa viumbe mbalimbali. Utalii, ambao unachukua zaidi ya asilimia 20 ya mapato ya fedha za kigeni, unatokana na mazingira na wingi wa viumbe hai tofauti vilivyopo Tanzania, ambavyo sasa viko hatarini kutokana na hali ya hewa pamoja na hali zisizo za kihali ya hewa kama ubadilishaji wa ardhi za kulimia kwa matumizi mengine, ukataji miti, na uvuvi haramu na usio mwendelezi. Kuongezeka kwa joto la bahari, kuongezeka kwa kiwango cha bahari na uongezekaji wa chumvi unatishia misitu ya mikoko na miamba ya matumbawe muhimu kwa uvuvi, wanyama wa porini na kuhatarisha kizuizi kilichopo dhidi ya dhoruba. Joto la maziwa ya maji safi ya Tanzania limesababisha kupungua kwa virutubisho kuzunguka na kupunguza uzalishaji wa samaki. Kuongezeka kwa mchanga kwenye sakafu ya bahari kunakosababishwa na mvua nzito, kunatishia uvuvi, ambao hutoa ajira zaidi ya milioni 4 na chanzo muhimu cha protini katika mikoa ya pwani na mashambani. Kuongezeka kwa joto pia huongeza hatari ya moto wa mwituni, pamoja maeneo muhimu yanayokusanya maji, kama mteremko wa mlima Kilimanjaro, ambapo uchomaji moto umesababisha maji kupotea kwa na kupunguza kiasi cha maji ya muda mrefu. Kuongezeka kwa joto na mvua nzito pia hubadilisha kiwango cha aina za mimea na wanyama wa porini na athari mbaya zaidi ni kuhama kwa nyumbu, samaki wa maji safi na mbwa mwitu wa Afrika ambao wako hatarini kuisha kabisa.
Miundombinu
Tanzania ndio nchi iliyoathiriwa zaidi na mafuriko katika Afrika Mashariki. Kuongezeka kwa mvua kubwa kunaweza kuongeza athari za mafuriko kwa miundombinu na huduma za nishati, maji na usafirishaji. Kila mwaka kuanzia 2014 hadi 2017, mafuriko yaligusa miundombinu muhimu kutoka pwani hadi maeneo ya juu, kuharibu barabara, madaraja na majengo ya umma na ya kibinafsi. Ukuaji wa kiwango cha bahari unatarajiwa kugharimu karibu dola milioni 200 kwa mwaka ifikapo 2050 kutokana na ardhi itakayopotea na uharibifu wa mafuriko. Jijini Dar es salaam, thamani ya miundombinu ni tabkribani $ 5.3 bilioni ambayo inazidi kuwa hatarini dhidi ya mafuriko na kupanda kwa kiwango cha bahari.
Muktadha wa Sera
Mfumo wa Kitaasisi
Ofisi ya Makamu wa Rais, Idara ya Mazingira, ndio msingi wa kitaifa wa mabadiliko ya hali ya hewa chini ya Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa (United Nations Framework Convention on Climate Change – UNFCCC) na pia ofisi hii inaratibu Mkakati wa Kitaifa wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa (2012). Kamati ya Uendeshaji ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa ya Kitaifa (The National Climate Change Steering Committee – NCCSC) na Kamati ya Kitaifa ya Ufundi wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa (National Climate Change Technical Committee – NCCTC) ni mashirika ya serikali yanayohusika na shughuli za mabadiliko ya hali ya hewa. NCCSC ina majukumu ya uchambuzi, mwongozo wa sera na kuratibu shughuli za mabadiliko ya hali ya hewa kwa sekta zote, wakati NCCTC inapeana ushauri wa kiufundi kwa hatua kuu za kitaifa ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Kwa nakala zaidi zinazohusu hali ya hewa bofya hapa!