Demografia ya Tanzania

Demografia ya Watu wa Tanzania

Orodha ya Yaliyomo

Makala hii inahusu taarifa za demografia za wananchi wa Tanzania, ikiwemo uwiano wa idadi ya watu, Makabila, kiwango cha elimu, afya ya watu, hali ya kiuchumi, uhusiano wa kidini, na mambo mengine yanayowahusu wananchi.

Mgawanyo wa idadi ya watu nchini Tanzania hauna usawa kabisa. Watu wengi wanaishi kwenye mpaka wa kaskazini au pwani ya mashariki, huku sehemu kubwa ya nchi ikibaki na watu wachache. Uwiano hutofautiana kutoka kwa kila kilomita ya mraba 12 (31 / sq mi) Mkoani Katavi hadi 3,133 kwa kila kilomita ya mraba (8,110 / sq mi) jijini Dar es Salaam. Takriban asilimia 70 ya idadi ya watu wanaishi vijijini, ingawa asilimia hii imekuwa ikipungua kuanzia miaka ya 1967. Japokuwa Dar es Salaam ndio jiji kubwa zaidi lakini Kisheria mkoa wa Dodoma, uliyopo katikati mwa Tanzania, ndio mji mkuu, ingawa hatua ya kuhamisha majengo ya serikali kwenda Dodoma imedorora.

Idadi hii ya watu ina karibu makabila 125. Wakiwemo Wasukuma, Wanyamwezi, Wachaga, na Wahaya ambao wana zaidi ya watu milioni 1 kwa kila kabila.

Tanzania ina zaidi ya lugha 100 tofauti zinazozungumzwa, hali inayoifanya kuwa nchi yenye lugha nyingi zaidi Afrika Mashariki. Lugha zinazozungumzwa nchini Tanzania zinatoka kwenye familia zote nne za lugha za Kiafrika: Kibantu, Kikushi, Nilotiki, na Khoisan. Kiswahili na Kiingereza ni lugha rasmi za Tanzania. Kiswahili kinatokana na tawi la Kibantu la familia ya Niger-Kongo. Watu wa Sandawe uzungumza lugha ambayo inaweza kuwa inahusiana na lugha za Khoe za Botswana na Namibia, wakati lugha ya watu wa Hadzabe, ingawa ina konsonanti zinazofanana, ila ni lugha isiyohusishwa nazo. Lugha ya watu wa Iraqw ni Kikushi. Lugha nyingine ni lugha za Kihindi na Kireno (zinazozungumzwa na Wagoa na Wamsumbiji).

Ingawa idadi kubwa ya wakazi wa Zanzibar walitoka bara, lipo kundi moja linalojulikana kama Shirazis linarudisha asili ya wazanzibari kwa walowezi wa mwanzo (kutoka uajemi) wa Kisiwa hicho. Wasio Waafrika wanaoishi bara na Zanzibar ni asilimia 1 ya idadi ya watu wote. Jumuiya ya watu wa Asia, ikiwa ni pamoja na Wahindu, Sikhs, Shi’a na Waislamu wa Sunni,

Msikiti wa Gaddafi Dodoma Tanzania
Msikiti wa Gaddafi Dodoma Tanzania

Parsis, na Goa, imepungua kwa asilimia 50 katika miaka ya 2000 na mwanzoni mwa miaka ya 2010 hadi 50,000 upande wa Tanzania Bara na 4,000 kwa Zanzibar. Inakadiriwa kuwa Waarabu 70,000 na Wazungu 20,000 (ambao ni asilimia 90 wanatoka Uingereza) wanaishi nchini Tanzania. Zaidi ya watu 100,000 wanaoishi Tanzania ni wa asili ya Asia au Ulaya.

Kwa kuzingatia takwimu za mwaka 1999–2003, zaidi ya watu 74,000 waliozaliwa Tanzania walikuwa wakiishi katika nchi za Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo, ambapo 32,630 wakiishi nchini Uingereza; 19,960 nchini Canada; 12,225 nchini Marekani; 1,714 nchini Australia; 1,180 nchini Uholanzi; na 1,012 katika Uswidi.

 

Idadi ya Watu

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, Tanzania ilikuwa na jumla ya wakazi 44,928,923 tofauti na wakazi 12,313,469 kwa mwaka 1967, hii inasababishwa na kiwango cha ukuaji wa asilimia 2.9 kila mwaka. Asilimia 44.1 ya watu inawakilisha kundi la umri wa chini ya miaka 15, huku asilimia 35.5 ikiwakilisha kundi la umri wa miaka 15-35, asilimia 52.2 ikiwa ni kundi la umri wa miaka 15-64, na asilimia 3.8 ikiwa ni kundi la wenye umri zaidi ya miaka 64.

Kwa mujibu wa marekebisho ya Matarajio ya Idadi ya Watu Duniani ya mwaka 2012, watoto walio chini ya umri wa miaka 15 walifanya asilimia 44.8 ya idadi ya watu wote, huku asilimia 52.0 ni wenye umri wa miaka 15–64 na asilimia 3.1 wenye umri wa miaka 65 au zaidi.

Jumla ya watu Idadi ya watu kwa umri 0–14 (%) Idadi ya watu kwa umri 15–64 (%) Idadi ya watu kwa umri 65+ (%)
1950 7,650,000 46.0 51.8 2.2
1955 8,741,000 45.7 52.0 2.3
1960 10,074,000 45.8 51.8 2.4
1965 11,683,000 45.8 51.7 2.4
1970 13,605,000 46.2 51.3 2.5
1975 15,978,000 46.4 51.1 2.6
1980 18,687,000 46.5 50.8 2.6
1985 21,850,000 46.4 51.0 2.7
1990 25,485,000 46.0 51.3 2.7
1995 29,944,000 45.3 51.9 2.8
2000 34,021,000 44.8 52.3 2.9
2005 38,824,000 44.6 52.4 3.0
2010 44,793,000 44.8 52.0 3.1

Muundo wa idadi ya watu

Muundo wa idadi ya watu (01.07.2013) (makadirio) :

Kundi la Umri Wanaume Wanawake Jumla %
Total 23 267 957 23 864 623 47 132 580 100
0-4 4 191 004 4 121 103 8 312 107 17,64
5-9 3 608 891 3 551 955 7 160 846 15,19
10-14 2 735 494 2 728 687 5 464 181 11,59
15-19 2 494 983 2 490 960 4 985 943 10,58
20-24 2 179 173 2 160 970 4 340 143 9,21
25-29 1 730 600 1 754 007 3 484 607 7,39
30-34 1 289 114 1 563 083 2 852 197 6,05
35-39 1 207 182 1 394 428 2 601 610 5,52
40-44 1 032 605 1 088 697 2 121 302 4,50
45-49 770 149 797 868 1 568 017 3,33
50-54 604 621 629 580 1 234 201 2,62
55-59 422 141 459 343 881 484 1,87
60-64 347 604 387 334 734 938 1,56
65-69 223 365 243 517 466 882 0,99
70-74 179 960 207 795 387 755 0,82
75-79 115 076 130 796 245 872 0,52
80+ 135 995 154 500 290 495 0,62
Kundi la Umri Wanaume Wanawake Jumla Asilimia
0-14 10 535 389 10 401 745 20 937 134 44,42
15-64 12 078 172 12 726 270 24 804 442 52,63
65+ 654 396 736 608 1 391 004 2,95

Takwimu muhimu

Utafiti wa demografia wa hali ya Huduma za Afya Tanzania wa mwaka 2010 (TDHS) unakadiria kuwa kiwango cha vifo vya watoto wachanga kwa mwaka 2005-10 kilikuwa 51. Usajili wa matukio mengine muhimu nchini Tanzania haujakamilika. Idara ya Idadi ya Watu kutoka Umoja wa Mataifa iliandaa makadirio yafuatayo.

Muda Vizazi hai kwa mwaka Wafu kwa mwaka Mabadiliko ya asili kwa mwaka CBR* CDR* NC* TFR* IMR*
1950-1955 402,000 184,000 218,000 49.0 22.4 26.6 6.74 153
1955-1960 464,000 198,000 267,000 49.3 21.0 28.3 6.80 143
1960-1965 535,000 218,000 322,000 49.1 20.1 29.0 6.80 136
1965-1970 616,000 239,000 384,000 48.7 18.9 29.8 6.79 128
1970-1975 709,000 258,000 475,000 48.0 17.5 30.5 6.75 119
1975-1980 821,000 275,000 542,000 47.4 15.9 31.5 6.73 109
1980-1985 932,000 307,000 633,000 46.0 15.2 30.8 6.55 104
1985-1990 1,061,000 348,000 727,000 44.8 14.7 30.1 6.36 102
1990-1995 1,197,000 423,000 892,000 43.2 15.3 27.9 6.05 102
1995-2000 1,336,000 480,000 815,000 41.8 15.0 26.8 5.75 92
2000-2005 1,522,000 492,000 961,000 41.8 13.5 28.3 5.66 77
2005-2010 1,744,000 454,000 1,230,000 41.6 10.8 30.2 5.58 61
2010-2015 1,865000
2015-2020 2,052,000
* CBR = Kiwango cha makisio ya uzao (kwa 1000); CDR = Kiwango cha Makisio ya vifo (kwa 1000); NC = Mabadiliko ya Asili (kwa 1000); TFR = Kiwango cha jumla ya uzazi (idadi ya Watoto kwa mwanamke); IMR = Kiwango cha vifo vya watoto wachanga kwa kila vizazi 1000

 

Uzazi na vifo

Mwaka Idadi ya watu Vizazi hai Vifo Ongezeko la Asili Makisio ya Uzao Makisio ya Vifo Kiwango cha ongezeko la asili TFR
2009 1 667 889 577 393 1 090 496
2010 1 678 325 573 213 1 105 122
2011 1 687 203 565 099 1 122 104
2012 44 928 923 1 694 943 555 975 1 138 968 5.2

Matarajio ya Umri (Urefu wa Maisha)

Muda Matarajio ya Umri (Urefu wa Maisha) kwa Mwaka
1950–1955 41.25
1955–1960  43.03
1960–1965  44.31
1965–1970  45.83
1970–1975  47.70
1975–1980  49.90
1980–1985  50.64
1985–1990  50.86
1990–1995  49.61
1995–2000  50.06
2000–2005  53.65
2005–2010  58.82
2010–2015  62.78

Idadi ya Watu

Eneo 1967 (Idadi ya watu / Kiwango cha makisio ya Uzao / Kiwango cha jumla ya uzazi) 1978 (Idadi ya watu / Kiwango cha makisio ya Uzao / Kiwango cha jumla ya uzazi) 1988 (Idadi ya watu / Kiwango cha makisio ya Uzao / Kiwango cha jumla ya uzazi) 2002 (Idadi ya watu / Kiwango cha makisio ya Uzao / Kiwango cha jumla ya uzazi) 2012 (Idadi ya watu / Kiwango cha makisio ya Uzao / Kiwango cha jumla ya uzazi)
Tanzania, ikiwemo Zanzibar 12,313,469 / 47 / 7.3 17,036,499 / 49 / 6.3 22,455,207 / 47 / 5.4 33,461,849 / 43 / 4.2 44,928,923 / /
Zanzibar 354,815 / 48 / 7.3 476,111 / 48 / 7.1 640,675 / 49 / 6.4 981,754 / 43 / 4.5 1,303,569 / /

Uzazi na Uzao (Demografia na Utafiti wa Afya)

Kiwango cha Jumla ya Uzazi (TFR) (Kiwango cha Uzazi kinachotakiwa) na Kiwango cha Makisio ya Uzao (CBR):

Mwaka CBR (Jumla) TFR (Jumla) CBR (Mjini) TFR (Mjini) CBR (Vijijini) TFR (Vijijini) CBR (Zanzibar) TFR (Zanzibar)
1991-1992 42.8 6.25 (5.57) 42.1 5.14 43.0 6.59 (5.91)
1996 40.8 5.82 (5.1) 36.3 4.11 (3.5) 41.9 6.34 (5.5)
1999 41.4 5.55 (4.8) 34.4 3.16 (2.9) 43.5 6.48 (5.5)
2004-2005 42.4 5.7 (4.9) 34.6 3.6 (3.1) 44.8 6.5 (5.6) 38.0 5.3 (4.6)
2010 38.1 5.4 (4.7) 35.0 3.7 (3.3) 39.0 6.1 (5.3) 35,9 5.1 (4.8)
2015-16 37.2 5.2 (4.5) 35.1 3.8 (3.4) 38.1 6.0 (5.1) 36.3 5.1 (4.6)
2017 35.5 4.9 31.0 3.5 37.3 5.7 33.7 4.5

Kiwango cha Jumla ya Uzazi Tanzania

Kiwango cha Uzazi kinakadiriwa na Tafiti (TDHS) pamoja na Sensa ya Watu kwa nyakati tofauti. Tafiti za TDHS zilikadiria viwango hivi vya uzazi : :6.3 (1991–92), 5.8 (1996), 5.7 (2004–05), 5.4 (2010) na 2002 Sensa ya Watu ilikadiria 6.3

Mkoa 1967 1978 1988 2006-09 2017
Tanzania (Jumla kwa nchi) 7.3 6.3 5.4 5.4 4.9
Dodoma (Mji mkuu) 7.6 6.2 5.9 6.0
Arusha 7.5 7.0 6.0 3.2
Kilimanjaro 8.9 7.5 5.8 3.4
Tanga 7.7 6.2 5.1 4.6
Morogoro 6.2 6.5 4.3 3.7
Pwani 5.8 6.1 5.4 3.8
Dar es Salaam 5.0 5.4 3.4 2.8
Lindi 5.4 4.6 3.9
Mtwara 5.7 4.9 4.5 3.3
Ruvuma 7.1 6.1 5.0 3.7
Iringa 7.8 6.3 4.9 4.5
Mbeya 8.1 6.3 4.7 4.7
Singida 6.3 5.9 5.7 7.4
Tabora 6.7 6.0 5.4 6.9
Rukwa 6.1 6.2 5.7
Kigoma 6.6 7.2 6.5 5.7
Shinyanga 8.7 6.9 6.3 5.5
Kagera 7.5 7.3 6.9 4.7
Mwanza 8.1 7.1 6.1 6.0
Mara 8.0 6.9 5.9 6.4
Manyara 6.0
Njombe 4.2
Simiyu 7.6
Geita 6.9
Katavi 6.7
Songwe 5.4
Tanzania Bara 7.3 6.3 5.4 5.4 4.9
 Kaskazini Unguja 7.1 7.0 4.5
Kusini Unguja 6.2 6.5 3.2
Mjini Magharibi 6.1 5.2 3.6
Kaskazini Pemba 8.3 6.9 6.3
Kusini Pemba 8.2 7.6 5.5
Tanzania Zanzibar 7.3 7.1 6.4 5.1 4.5

Takwimu nyingine za demografia

Zifuatazo ni Takwimu za demografia za Tanzania kwa mwaka 2019 zinazotokana na Mapitio ya Idadi ya Watu Duniani.

Wakazi wakijaribu kuokoa manusura katika eneo la ajali iliyoua watoto wa shule, walimu na dereva wa basi ndogo katika kijiji cha Rhota kando ya barabara kuu ya Arusha-Karatu katika mkoa wa kaskazini mwa Tanzania wa Arusha, Mei 6, 2017
Wakazi wakijaribu kuokoa manusura katika eneo la ajali iliyoua watoto wa shule, walimu na dereva wa basi ndogo katika kijiji cha Rhota kando ya barabara kuu ya Arusha-Karatu katika mkoa wa kaskazini mwa Tanzania wa Arusha, Mei 6, 2017

Mtu mmoja huzaliwa kila baada ya sekunde 14

Mtu mmoja hufa kila baada ya dakika 1

Mtu mmoja huhama au huhamia nchini kila baada ya dakika 13

Mtu mmoja hupata faida katika kibiashara  kila baada ya sekunde 17

Zifuatazo ni takwimu za demografia zinazotokana na Kitabu cha CIA kilichokusanya Taarifa za Kweli Duniani, isipokuwa tu kama imeonekana tofauti.

Idadi ya Watu

55,451,343 (makadirio ya Julai 2018)

48,261,942 (makadirio ya Julai 2013)

Muundo wa umri

Miaka 0-14: 43.4% (me 12,159,482 /ke 11,908,654)

Miaka 15-24: 20.03% (me 5,561,922 /ke 5,543,788)

Miaka 25-54: 30.02% (me 8,361,460 /ke 8,284,229)

Miaka 55-64: 3.51% (me 872,601 /ke 1,074,480)

Miaka 65 na zaidi: 3.04% (me 706,633 /ke 978,094) (makadirio ya 2018)

Umri wa Kati

jumla: miaka 17.9. Mlinganyo wa nchi kidunia: 215th.

me: miaka 17.6

ke: miaka 18.2 (makadirio ya 2018)

jumla: miaka 17.3

me: miaka 17.0

ke: miaka 17.6 (Makadirio ya 2013)

Kiwango cha Uzao

Vizazi 35.3 /1,000 idadi ya watu (makadirio ya 2018) Mlingano wa nchi kidunia: ya 19

Kiwango cha Vifo

Vifo 7.5 /1,000 idadi ya watu (makadirio ya 2018) Mlinganyo wa nchi kidunia: ya 112

Kiwango cha Jumla ya Uzazi

Watoto wanaozaliwa 4.71 /mwanamke (Makadirio ya 2018) Mlinganyo wa nchi kidunia: 20th

Kiwango cha ukuaji wa idadi ya watu

2.74% (Makadirio ya 2018) Mlinganyo wa nchi kidunia: 14th

Umri wa mama kuanza kujifungua

Miaka 19.8 (Makadirio ya 2015/16.)

Kumbuka: Umri wa kati wa mwanamke kuanza kujifungua 25- 29

Kiwango cha matukio ya kuzuia ujauzito

38.4% (2015/16)

Kiwango cha kuhama ama kuhamia nchini

(wa)mhamiaji-0.5 /1,000 idadi ya watu (makadirio ya 2018) Mlinganyo wa nchi kidunia: 127th

Uwiano wa utegemezi

Jumla ya uwiano wa utegemezi: 93.4 (makadirio ya 2015.)

Uwiano wa utegemezi kwa vijana: 87.4 (makadirio ya 2015)

Uwiano wa Utegemezi kwa wazee: 6 (makadirio ya 2015)

uwiano wa msaada unaowezekana: 16.6 (makadirio ya 2015)

Uhamiaji mijini

Idadi ya watu mijini: ni 33.8% ya jumla ya watu (2018)

Kiwango cha kuhamia mijini: 5.22% Kiwango cha mabadiliko ya kila mwaka (makadirio ya 2015-20)

Makundi ya kikabila

99% barani Afrika (ambapo 95% ni Wabantu kuna makabila zaidi ya 130), wengine 1% (watu kutoka Asia, Ulaya, na Uarabuni); Zanzibar – Waarabu, Waafrika, mchanganyiko wa Waarabu na Waafrika. Takribani watu 100,000 wanaoishi Tanzania wanatoka Ulaya au Asia.

Dini

Wakristo 61.4%, Waislam 35.2%, dini za watu 1.8%, nyingine 0.2%, wasio na dini 1.4% (makadirio ya 2010)

kumbuka: Wananchi wa Zanzibar karibu wote ni Waislamu

Uwiano wa jinsi

Katika uzao at birth: 1.03 (m)wanaume/mwanamke

Miaka 0-14: 1.02 (m)wanaume/mwanamke

Miaka 15–54: 1.00 (m)wanaume/mwanamke

Miaka 55-64: 0.75 (m)wanaume/mwanamke

Miaka 65 na Zaidi: 0.76 (m)wanaume/mwanamke

jumla ya watu: 0.99 (m)wanaume/mwanamke (makadirio ya 2013 estimate)

Matarajio ya umri wa kuishi baada ya kuzaliwa

Bibi wa Kitanzania
Bibi wa Kitanzania

Jumla ya watu: miaka 63.1

wanaume: miaka 61.6

wanawake: miaka 64.6 (makadirio ya 2018)

jumla ya watu: miaka 60.76

wanaume: miaka 59.48

wanawake: miaka 62.09 (makadirio ya 2013)

VVU/UKIMWI

Umri 15-49 Kiwango cha maambukizi ya VVU:

Ni jumla ya asilimia 4.5, huku asilimia 6.2 ni wanawake na asilimia 3.8 ni wanaume wakiwa wameambukizwa.

Watu waishio na VVU/UKIMWI:

Milioni 1.5 (makadirio ya 2017)

Vifo:

32,000 (makadirio ya 2017)

 

Lugha

Makala kuu: Lugha za Tanzania

Kiswahili au Swahili au Kiunguja (kutoka Zanzibar) (rasmi)

Kiingereza (rasmi)

Kiarabu (kinazungumzwa kwa wingi Zanziba)

Kujua Kusoma na Kuandika

Fasili: umri wa miaka 15 na Zaidi wanaweza kusoma na kuandika Kiswahili, Kiingereza, au Kiarabu

jumla ya watu: 77.9%

wanaume: 83.2%

wanawake: 73.1% (makadirio ya 2015)

Jumla ya watu: 69.4%

wanaume: 77.5%

wanawake: 62.2% (makadirio ya 2003.)

Matarajio ya umri wa kusoma

Kuanzia shule ya msingi hadi elimu ya juu:

jumla:  miaka 8 years

wanaume: miaka 8 years

wanawake: miaka 8 years (2013)

Ukosefu wa Ajira, umri wa vijana 15- 24

jumla: 3.9%

wanaume: 3.1%

wanawake: 4.6% (makadirio ya 2014)

Dini

Watanzania wengi siku hizi ni Wakristo na Waislamu. Uhusiano wa idadi ya wafuasi kati ya dini hizo mbili unachukuliwa kwa unyeti sana kisiasa na maswali kuhusu ufuasi wa dini hayakuwahi kujumuishwa katika dodoso za sensa tangu mwaka 1967.

Kwa miaka mingi makadirio yamekuwa yakijirudia kwamba kila theluthi moja ya watu wanafuata Uislamu, Ukristo na dini za jadi. Kwa kuwa kuna uwezekano kwamba hakuna asilimia kubwa ya wanadini wa jadi, machapisho mbalimbali yamekuwa yakishindana kutoa makadirio kwa kuwapa upande mmoja au mwingine sehemu kubwa ya theluthi hiyo au kujaribu kuonyesha mgawanyo sawa.

Makadirio kutoka katika Ripoti ya Pew yalionyesha Uislamu 36% na Ukristo 60% (2010).

Waliosalia ni Wahindu, Wabuddha, dini ya mazingira, na wasio na dini. Wakristo wengi ni Wakatoliki, Walutheri au Waadventista wasabato, ingawa idadi ya makanisa mengine ya Pentekoste, Waanglikana, na Wakristo wa Orthodox ya Mashariki nao pia wanawakilishwa nchini. Waislamu wengi wa Tanzania ni Sunni, ingawa pia kuna idadi ya wafuasi wa Ibadi, Shia, Ahamadiya, Bohora, na Sufi. Waislamu wamejikita katika maeneo ya pwani na katika maeneo ya bara wapo kando kando ya njia za zamani za misafara ya wafanyabiashara.

Kwa nakala zaidi zinazohusu jamii za watu bofya hapa!