Changamoto za Miundombinu ya Usafiri wa Anga Tanzania
Orodha ya Yaliyomo
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere
JNIA ni mlango mkuu wa kutokea na kiunganishi kikuu cha uchukuzi ndani ya nchi. Inahudumia mji mkuu wa Dar es salaam na ukadiriwa kuwa na umbali wa kilometa 10 kutoka kati kati ya jiji. Kwa mwaka 2011 uwanja ulirekodi mapito ya abiria bilioni 1.8 wakiwakilisha aslimia 72 ya jumla kuu ya abiria wa viwanja vya ndege vya TAA na asilimia 60 ya jumla ya abiria wote wa angani. Uwanja huu wa ndege umekuwa kwenye marekebisho mazito kwa miaka mitano iliyopita, yakihusisha
> Maboresho ya njia kuu ya kurukia,
> Ukarabati wa eneo la kuegeshea ndege kwa kituo cha kimataifa,
> Utengenezaji wa sehemu ya pili kwa ajili ya usafiri wa anga kwa ujumla
> Na ujenzi wa sakafu ya urefu wote moja kwa moja kwenye njia ya kukimbilia, hivyo basi miundombinu ya uwanja ipo kwenye hali nzuri
kiasi cha kutosha kuhudumia kiwango kinachotarajiwa cha uchukuzi kwa miaka mingi ijayo. JNIA ina viwanja viwili kimoja kikiwa na mita 3000 chenye kufaa ndege aina zote na kingine cha mita 1000 kwa ajili ya usafiri mzima wa anga na vyombo vya anga.
Uwanja wa ndege huu una vituo viwili vya abiria: kituo cha zamani cha kwanza ambacho hutumika kwa ndege zisizo na ratiba na ndege ndogo zenye ratiba za ndani, wakati kituo cha pili ndio msingi wa kituo kinachoandaa ndege za kimataifa na ndege za ndani. Maelezo yanaonyesha karibia uchukuzi wote hufanyika kituo cha pili.
Uwezo wa kutowa huduma wa kituo cha pili ni abiria milioni 1.2 kwa mwaka na huu umeongezwa na ongezeko la kiwango cha sasa. Msongamano kwenye kituo unatarajiwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa kama makadirio ya uchukuzi yanavyoonyesha kwamba kulikuwa na ongezeko la idadi ya abiria kufikia milioni 3.2 katika mwaka 2016. Kutokana na muda uliowekwa kutengeneza mchoro na kujenga jengo la kituo, inaonekana kwamba jengo jipya halitakamilika na kuanza kazi kabla ya mwaka 2016. Jengo lililopo haliwezi kuhudumia kwa ubora wa hali ya juu na halifai kwa kutangaza na kuvutia watembeleaji na watalii kwenye nchi. Hivyo basi linahitaji maboresho na ukarabati haraka iwezekanavyo. Tofauti na hapo kituo kipya cha kisasa kinatakiwa kujengwa.
TAA imeandaa mpango madhubuti kwa maendeleo ya kituo cha tatu. Utafiti wa uandaaji wa mpango huu kwa idara ndogo ya viwanja vya ndege unagharamiwa na Benki ya dunia chini ya idara ya miradi ya usafirishaji. Kupitia mapendekezo ya utafiti huu, rasilimali zimewekwa kuhakiki mpango huu wa TAA kwa kutoa mapendekezo ya kituo kipya cha abiria. Vituo vipya vikubwa mara nyingi hufaa zaidi kwa maendeleo ya mikopo ya sekta binafsi. Inashauriwa aina hii ya kugharamia miundombinu ya usafiri wa anga mipya itumike. Pia mradi utatoa ushauri wa kutathmini aina ya nzuri ya njia za kugharamia.
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) upo katika mguu wa Mlima Kilimanjaro na ukadiriwa kuwa na umbali wa kilometa 450 kutoka Dar es Salaam. Uwanja huu upo katikati ya Arusha na Moshi unakadiriwa kuwa na umbali wa kilomita 50 kutoka kila mji. Na ni uwanja wa pili
wa kutokea wa kimataifa kwa ukubwa. Kimkakati umekaa karibu na vivutio vikubwa vya watalii vya Mlima Kilimanjaro na Mbuga za wanyama za Tanzania za Serengeti, Bonde la Ngorongoro na Ziwa Manyara. Watalii wengi huingia nchini kupitia (KIA) ambapo ndio njia fupi kutokea Nairobi pia ambapo ni kitovu cha usafiri wa anga wa kanda.
Uwanja wa ndege huu una mita 3,607 na unaweza kuhudumia ndege na vifaa vyake kwa kufanya kazi masaa 24 kwa siku, na siku 7 za juma. Jengo la kituo ni dogo na mara nyingi huwa na msongamano.
Uwanja huu wa ndege ni ulikuwa wa kwanza kama mradi wa kiushirikiano baina ya taasisi binafsi na umma kwenye sekta ya usafiri anga ya afrika ilipofunguliwa kwa kikundi cha wawekezaji mwaka 1998 kwa miaka 25. Kundi hili la wawekezaji lilifanya shughuli mpaka mwaka 2009 ambapo serikali ilinunua hisa za mwekezaji mkubwa, Mott Mcdonald, na sasa kampuni ya uendeshaji inayofahamika kama (Kilimanjaro Development Company) inaendelea kufanya kazi. Vifaa vipo kwenye hali nzuri na vimekuwa vikifanyiwa marekebisho na ukarabati kwa mwaka 2000 lakini pia udumishaji wa mara kwa mara utahitajika kwa kipindi cha karibuni. Makadirio yanaonyesha hadhi miundombinu ya usafiri wa anga inayotakiwa kufikiwa itagharimu Dola Milioni 15.6. TAA inakadiria vifaa vya uwanja vilifikia uwezo wake wa kumudu mwaka 2006 na kituo kikubwa kilihitajika haraka sana. Inawezekana uwanja wa pili ungeweza kuwa kivutio kwa sekta binafsi na njia hii ilitakiwa kuchukuliwa kama chanzo cha mapato.
Viwanja vya ndege vingine vya ndani
Kiwanja cha ndege cha Mwanza
Kwa viwanja vilivyobakia, Mwanza ndio kikubwa zaidi na kina abiria wengi wa ndani na kipo kama ifuatavyo. Kipo ukanda wa ziwa, uwanja
wa Mwanza unahudumia ukanda ambao ni tajiri kwa maliasili hasa zaidi kwenye uvuvi kutoka Ziwa Viktoria na madini kutoka mji na vijiji vinavyozunguka
Uwanja huu umepokea fedha kutoka Benki ya Waarabu ya maendeleo ya kiuchumi kwa  Afrika na fedha za OPEC kwa maendeleo ya kimataifa kwa kwa ajili ya kuendeleza na kurekebisha miundombinu ya usafiri wa anga ikiwamo njia za kutembelea ndege. Upande mwingine wa vifaa unahusisha  eneo la kuegeshea ndege za mizigo, kituo kipya cha abiria na utanuzi wa eneo la maegesho ya ndege vyote ni vipengele vya mipango ya TAA ya maendeleo.
Kiwanja cha ndege cha Arusha
Uwanja wa ndege wa Arusha upo karibu na mjini na una wasafiri wengi wanaopita, hata hivyo unahudumiwa na ndege ndogo zikitoa jumla ya huduma zote za usafiri wa anga na huduma za mkataba. Ndege kubwa kama Precision Air zimesimama kutoa huduma kupitia uwanja huu kutokana na ubora mbaya wa njia za kutembelea ndege na kuhamishia huduma zake KIA. Ukarabati wa njia za ndege na eneo la maegesho umekuwa ukiahirishwa kutokana ukaribu wake na KIA ambao una kila aina ya vifaa na huduma. Kwa matokeo hayo uwanja huu umekuwa haupewi kipaumbele cha maboresho ingawa ni wa tatu kwa idadi ya abiria wa ndani katika orodha ya viwanja vinavyoendeshwa na TAA ambapo mwaka 2011 zaidi ya abiria 112,000 wametumia uwanja huu.
Kiwanja cha ndege cha Kigoma
Uwanja wa Kigoma unahudumia mkoa wa Kigoma, mji muhimu wa Ziwa Tanganyika na bandari kuu ya Ziwa. Uwanja huu kwa sasa unahudumia takribani abiria 20,000 kwa mwaka ambao wanakadiriwa kuongeza mpaka abiria 29,000 ifikapo mwaka 2016. Uwanja pia unahudumu kama lango kuu muhimu kwa ndege kubwa za mizigo za Umoja wa Mataifa kuingia DR Congo. Uwanja una mitambo mikubwa na njia mbili za ndege zisizo sakafiwa, ndefu zaidi ikiwa na mita 1,767 pia imetandazwa lami duni kwenye eneo la maegesho ya ndege katika kila mwisho wa njia. Sehemu hii ya changarawe na lami duni pia inaleta wasiwasi wa usalama kwa shughuli za usafiri ya anga. Kipande chenye changarawe cha njia ya kupitia ndege kimekuwa na hali mbaya  kipindi cha hali ya hewa ya unyevu na kusababisha mashimo ya maji, kumong’onyoka na kuharibika kwa njia. Hivi karibuni ndege ya Air Tanzania iligonga ilipokuwa inatua na hii imesababishwa na  hali duni ya njia. Njia kuu ipo mbioni kusakafiwa kwa kiwango cha lami chini ya gharama za Benki ya Dunia.
Kiwanja cha ndege cha Tabora
Uwanja wa Tabora hutumika kwa kazi nyepesi na abiria kwa mwaka wanaokaribia kufikia 9,000 ambapo wanatarajia kuongezeka na kufikia abiria 14,000 kwa mwaka ifikapo 2016. Uwanja pia una njia mbili zisizosakafiwa zinazoingiliana moja na nyingine. Moja ikiwa na urefu wa mita 1,786 na upana wa mita 45, na nyingine ikiwa na urefu wa mita 1,555 na upana wa mita 30. Kipindi kilichopita kipande kidogo tu cha njia kuu kilitandazwa sakafu ya zege hali ambayo inakuwa mgumu kwa ndege kutumia kiwanja hiko. Barabara za changarawe zipo kwenye hali mbaya na ni hatari kwa usalama kwa kipindi cha hali ya hewa ya unyevu. Kwa msaada wa Benki ya Dunia fedha zinatolewa kwa maboresho ya njia kuu kwa kiwango cha lami,kwani ni moja ya miundombinu ya safari ya anga katika uwanja huu inayohitaji kurekebishwa haraka sana.
Kiwanja cha ndege cha Bukoba
Uwanja wa ndege wa Bukoba upo magharibi ya pwani ya Ziwa Viktoria, ndio mji mkubwa wa kanda ya Kagera. Matumizi ya uwanja huu yamekuwa kwa haraka kwa miaka mingi iliyopita na kwa mwaka 2011 abiria waliokuwa wakipitiaa walifkia 29,000. Makadirio ya uchukuzi yanaonyesha idadi hii itaongezeka na kufkia abiria 37,000 kwa miaka mitano ijayo. Hata hivyo uwanja unaonekana siyo salama kwa muendeshaji mkuu wa ndani ambaye alikataza kutua kwa ndege yake LET 410. Una njia moja iliyojengwa kwa changarawe yenye urefu wa mita 1,280 na upana wake upo kati ya mita 18 mpaka 30. Ubunifu wa mjengo wa uwanja ni duni na una eneo dogo la maegesho ambapo lipo karibu na njia ya kupitia ndege hivyo basi uegeshaji wa ndege unafanya njia ya kupita ndege kutowezekana, jengo dogo la kituo lenye uwezo wa ndege za mapanga madogo , hakuna mnara wa kuongozea, hakuna uzio wa ulinzi. Kwa msaada wa Benki ya Dunia, njia ya kupitia ndege itaboreshwa kwa kiwango cha lami, pamoja na njia ya gari za kubebea abiria , eneo la maegesho, mnara wa uongozaji na uzio wa ulinzi wa ulinzi vitawekwa pia.
Kwa nakala zaidi zinazohusu miundombinu bofya hapa!