Sera ya Faragha

SERA YA FARAGHA

Utangulizi

Orodha ya Yaliyomo

Ifahamutanzania.com inamilikiwa na kuendeshwa na Yourbackupemployee, Inc. shirika la Ontario.

Ifahamutanzania.com (“Kampuni” au “Sisi” au “Huduma”) inaheshimu faragha yako na tumeazimia kuilinda kupitia taratibu zetu za sera hii.  

Sera hii inafafanua baadhi ya aina ya taarifa binafsi tunazoweza kukusanya kutoka kwako au unazoweza kuzitoa unapotembelea tovuti ya https://Ifahamutanzania.com (the “Tovuti”) na utendaji wetu katika kuzikusanya, kuzitumia, kuzihifadhi, kuzilinda na kuzitoa taarifa hizo.

Kanuni za Msingi

Kwenye sera hii ya faragha, maneno haya yana maana ifuatayo:

“Mwanachama” maana yake ni mtu yeyote au chombo kilichojisajiri nasi ili kutumia Huduma. 

“Mtembeleaji” maana yake ni mtu yeyote anayetembelea sehemu yoyote ya Tovuti yetu.

“Wewe” na “Yako” maana yake, kutegemeana na muktadha husika, ni ama Mwanachama au Mtembeleaji.  

Sera hii hutumika kwa taarifa tunazokusanya:

Kwenye Tovuti hii.

  • Kwenye barua pepe, maandishi, na ujumbe mwingine wa kielektroniki kati yako na Tovuti hii.
  • Kupitia programu za simu na za kompyuta unazopakua kutoka kwenye Tovuti hii, ambazo zinatoa mwingiliano usiotumia kivinjari kati yako na Tovuti.
  • Unapokutana na matangazo yetu na programu zilizopo kwenye tovuti zinazomilikiwa na wengine pamoja na huduma, ikiwa programu au matangazo hayo ni pamoja na viungo vinavyoungia kwenye sera hii.

Haitumiki kwa taarifa zinazokusanywa na:

  • sisi nje ya mkondo wa intaneti au kupitia njia nyinginezo, ambazo ni pamoja na tovuti nyingine zozote zile zinazoendeshwa na Kampuni au upande wa tatu; au
  • upande wowote wa tatu, ikiwa ni pamoja na kupitia programu yoyote au maudhui (pamoja na matangazo) yanayoweza kuunganishwa hadi au kupatikana kutoka au kwenye Tovuti.

Tafadhali soma sera hii kwa uangalifu ili upate kuelewa sera na utendaji wetu kuhusiana na taarifa zako na jinsi tutakavyozitumia. Endapo hukubaliani na sera na utendaji wetu, chaguo lako ni kutotumia Tovuti yetu. Kwa kuifikia au kuitumia Tovuti hii, ni kwamba unakubaliana na sera hii ya faragha. Sera hii inaweza kubadilika kila wakati – bila kutoa taarifa.Kuendelea kwako kuitumia Tovuti hii baada ya kuwa tumefanya mabadiliko inachukuliwa kukubaliana kwako na mabadiliko hayo, kwahiyo tafadhali pitia sera kila wakati kwa ajili ya sasisho.

Watoto Chini ya Umri wa Miaka 13

Tovuti yetu haijawalenga watoto walio na umri wa miaka chini ya 13. Hakuna yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 13 anaweza kutoa taarifa yoyote kwa au kwenye Tovuti. Katika hali ya ufahamu wetu hatukusanyi taarifa binafsi kutoka kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 13. Kama umri wako ni chini ya miaka 13, usitumie au kutoa taarifa yoyote kwenye Tovuti hii au kwenye au kupitia kwenye huduma zake zozote zile au kujisajiri kwenye Tovuti, kutumia huduma yoyote ya maingiliano au maoni ya umma ya Tovuti hii au kutoa taarifa yoyote kwetu inayokuhusu wewe, ikiwa ni pamoja na jina lako, anwani, namba ya simu, anwani ya barua pepe au jina lolote la bandia au jina la mtumiaji unaloweza kutumia. Tukifahamu kwamba tumekusanya au kupokea taarifa binafsi kutoka kwa mtoto aliye na umri wa chini ya miaka 13 bila ya uhakiki wa idhini ya mzazi, tutafuta taarifa hizo. Ikiwa unaamini inaweza ikawa tuna taarifa yoyote kutoka kwa au kuhusu mtoto aliye na umri wa chini ya miaka 13, tafadhali wasiliana nasi kwa maswali@Ifahamutanzania.com.

Taarifa Tunazokusanya Kuhusu Wewe na Jinsi Tunavyozikusanya

Tunakusanya taarifa za aina mbalimbali kutoka na zinazohusu watumiaji wa Tovuti yetu, pamoja na taarifa:

  • ambazo zinaweza kukutambulisha binafsi, kama vile jina, anwani ya posta, anwani ya barua pepe, na namba ya simu (“taarifa binafsi”);
  • kuhusu maoni yako au mabandiko mengine; na/au
  • kuhusu muunganisho wa intanteti yako, vifaa unavyotumia kuifikia Tovuti yetu na maelezo ya utumiaji.

Tunakusanya taarifa hizi:

  • Moja kwa moja kutoka kwako unapotoa taaifa hizo kwetu
  • moja kwa moja kwa mifumo ya kompyuta unavyopita kwenye tovuti. Taarifa zilizokusanywa kwa mifumo ya kompyuta zinaweza kuwa ni pamoja na maelezo ya matumizi, anwani za kompyuta zilizotumika kutembelea tovuti, yaani “IP addresses”, na taarifa zilizokusanywa kupitia vidakuzi, kioleza cha wavuti, na teknolojia zingine zinazotumika kufuatilia matumizi ya tovuti.

Taarifa Unazotoa Kwetu. Taarifa tunazokusanya kwenye au kupitia Tovuti yetu ni pamoja na:

  • Taarifa unazotoa kwa kujaza fomu kwenye Tovuti yetu. Hii ni pamoja na taarifa zilizotolewa wakati wa kujisajiri ili kutumia Tovuti yetu, kujiunga kwenye huduma zetu au kwa vifaa vya matangazo kupitia barua au barua pepe, mabandiko au maoni, kununua bidhaa, au kuomba huduma zaidi. Aidha, tunaweza kukuomba taarifa zako unaposhiriki mashindano au matangazo yaliyodhaminiwa nasi, na wakati unaporipoti tatizo la Tovuti yetu.
  • Kumbukumbu na nakala za mawasiliano yako (pamoja na anwani za barua pepe), endapo unawasiliana nasi.
  • Majibu yako kwenye tafiti na maswali ambayo tunaweza kukutaka uyajibu kwa lengo la kutafiti.
  • Taarifa zinazotokana kwa kutumia program zetu za kwenye vifaa vya mkononi kama vile simu (endapo tunakuwa nazo): Wakati unatumia programu zetu za kwenye simu, tunaweza kukusanya taarifa fulani fulani za kifaa unachotumia na taarifa zinazohusiana na matumizi, hiyo ikiwa ni pamoja na taarifa zingine zilizotajwa sehemu mbalimbali ndani ya sera hii ya faragha.Taarifa za Kifaa: Tunaweza kukusanya taarifa kuhusu aina ya kifaa unachotumia na mfumo wa uendeshaj kifaa husika. Wakati wowote unapopakua programu au mafaili mbalimbali au unapotumia programu zetu za vifaa vya mkononi au huduma; hapo hatutahitaji mifumo yetu iifikie mifumo ya kifaa chako, au kufuatilia taarifa yoyote inayohusiana na eneo kutoka kwenye kifaa chako cha mkononi. Data za matumizi ya bidhaa: Tunaweza kutumia programu za uchambuzi za kwenye vifaa vya mkononi kama vile simu ili kupata ufahamu wa kutosha wa namna gani watu wanatumia programu zetu. Tunaweza kukusanya taarifa kuhusu ni mara ngapi huwa unatumia programu husika na data zingine kuhusu utendaji wake.

Vile vile unaweza kutoa taarifa ili zichapishwe au kuoneshwa (kwenye sera hii, “kubandikwa”) kwenye maeneo ya wazi ya Tovuti, au kusambaza kwa watumiaji wengine wa Tovuti au watu wa upande wa tatu (kwa pamoja, “Michango ya Mtumiaji”). Michango Yako ya Mtumiaji hubandikwa kwenye tovuti na kusambazwa kwa wengine kwa utashi wako mwenyewe kwa kuzingatia vihatarishi. Hatuwezi kudhibiti matendo ya watumiaji wengine wa Tovuti ambao unaweza kuwa umechagua kuwashirikisha kwenye Michango ya Mtumiaji unayotoa. Hivyo basi, hatuwezi na hatukuhakikishii kwamba Michango ya Mtumiaji unayotoa haitaonekana kwa watu usiowakusudia.   

Taarifa Tunazokusanya Kupitia Teknolojia za Ukusanyaji Data Zinayojiendesha Zenyewe: Kadri unavyoperuzi na kushiriki kwenye Tovuti yetu, tunaweza kutumia teknolojia za ukusanyaji data zinayojiendesha zenyewe ili kukusanya baadhi ya taarifa kuhusu kifaa chako, vitendo vya kuperuzi, na mipangilio, pamoja na:

  • Demografia. Maelezo ya upitiaji wako kwenye kurasa mbalimbali za Tovuti yetu, ikiwa ni pamoja na data za mwenendo, data za mahali ulipo, kumbukumbu za utembeleaji kwenye Tovuti, na data zingine za mawasiliano na zana unazozifikia na kuzitumia kwenye Tovuti.
  • Taarifa kuhusu kompyuta yako na uungaji wa intaneti, ikiwa ni pamoja na anwani yako ya kompyuta unayotumia kutembelea tovuti, yaani “IP address”, mfumo wa uendeshaji wa kompyuta, na aina ya kivinjari.
  • Uzoefu wako wa nyuma kwenye Ifahamutanzania.com pamoja na bidhaa na huduma zake.

Taarifa tunazokusanya kwa kutumia mifumo inayojiendesha yenyewe ni data za kitakwimu na zinaweza kuwa pamoja na taarifa binafsi, lakini tunaweza kuzihifadhi au kuzihusisha au kuziunganisha na taarifa tunazokusanya kwa njia zingine au tunazopokea kutoka vyanzo vya upande wa tatu. Vile vile tunaweza kukusanya taarifa zinazokuhusu kutoka kwenye vyanzo vya umma vilivyopo kama vile taarifa kutoka kwenye magazeti, blogu mbalimbali, na tovuti za kibiashara au data zinazokusanywa na upande wa tatu. Tunaweza kutumia taarifa hizo kuwa nyongeza ya taarifa zako binafsi zilizohifadhiwa nasi. Vile vile tunaweza kukusanya taarifa zinazokutambulisha binafsi ambazo umezitoa kwa hiari yako kwenye tovuti, bila ya sisi kutoa ombi lolote kwako la kufanya hivyo. Inatusaidia kuboresha Tovuti yetu na kutoa huduma bora na za kibinafsi kwa watumiaji wa tovuti, ikiwa ni pamoja na kutuwezesha: 

  • Kukisia ukubwa wa hadhira yetu na mwelekeo wao wa kutumia Tovuti.
  • Kuhifadhi taarifa kuhusu mambo unayopendelea, kutusaidia kuboresha Tovuti yetu iweze kukidhi upendacho wewe binafsi.
  • Kuongeza kasi yako ya kutafuta unachohitaji kwenye Tovuti yetu.
  • Kukutambua unaporudi tena kwenye Tovuti yetu.

Teknolojia tunayotumia kwa ukusanyaj huu wa data kwa mfumo unaojiendesha ni pamoja na: 

  • Vidakuzi (au vidakuzi vya kivinjari). Kidakuzi ni faili dogo linalowekwa kwenye kitunza data cha kompyuta yako. Unaweza kutoruhusu vidakuzi vya kivinjari kwa kuuhisha mpangilio husika kwenye kivinjari chako. Walakini, endapo utachagua mpangilio wa aina hiyo, yaani wa kutoruhusu vidakuzi vya kivinjari, unaweza shindwa kuzifikia baadhi ya sehemu za Tovuti yetu. Ni endapo tu umerekebisha mpangilio wa kivinjari chako ili kisiruhusu vidakuzi, vinginevyo mfumo wetu utatoa vidakuzi pale unapokielekeza kivinjari chako kwenye Tovuti yetu.
  • Vidakuzi Vitumiavyo Programu ya Adobe Flash. Vipengele fulani vya Tovuti yetu vinaweza kutumia vitu vilivyohifadhiwa ndani ya kifaa chako (au vidakuzi vinavyotumia programu ya Adobe Flash) ili kukusanya na kutunza taarifa zinazohusu mambo unayopendelea na urambazaji hadi, kutoka na kwenye Tovuti yetu.Vidakuzi vinavyotumia programu ya Adobe Flash havisimamiwi na mpangilio ule ule unaotumika kwenye vidakuzi vya kivinjari. Kwa taarifa kuhusu kusimamia faragha yako na mpangilio wa usalama kwa vidakuzi vinavyotumia programu ya Adobe Flash, angalia.
  • Violeza vya Wavuti. Kurasa za Tovuti yetu au za barua pepe zetu zinaweza kuwa na mafaili madogo ya kielektroniki yanayofahamika kama violeza vya wavuti, yaani “web beacons”, (ambavyo pia vinatambulika kama “gifs” “pixel tags”, na “single-piexl gifs) ambazo zinaruhusu Ifahamutanzania, kwa mfano, kuhesabu watumiaji waliotembelea hizo kurasa au waliofungua barua pepe na kwa ajili ya takwimu zingine zinazohusiana na tovuti (kwa mfano, kurekodi umaarufu wa maudhui fulani ya tovuti na kuthibitisha mfumo na utimilifu au uaminifu wa mtambo wa mtandao unaohifahdi kumbukumbu zote, yaani seva.
  • Kidakuzi cha DoubleClick DART: Google, akiwa kama mfanya biashara kutoka upande wa tatu, wanatumia vidakuzi kutoa matangazo ya SEJ. Utumiaji wa Google wa kidakuzi cha DART inawezesha kutoa matangazo kwa watumiaji kwa kuzingatia utembeleaji wao kwenye tovuti ya SEJ na tovuti zingine kwenye intaneti. Watumiaji wanaweza kutochagua kutumia kidakuzi cha DART kwa kutembelea Google ad and content network privacy policy.Baadhi ya wabia wa matangazo yetu wanaweza kutumia vidakuzi na violeza vya wavuti kwenye tovuti yetu.

Hatukusanyi taarifa binafsi kwa kutumia mifumo inayojiendesha yenyewe, lakini tunaweza kuambatanisha taarifa hii kwenye taarifa binafsi kuhusu wewe tunazokusanya kutoka kwenye vyanzo vingine au unazotupatia.

Utumiaji Vidakuzi wa Upande wa Tatu na Teknolojia Zingine za Ufuatiliaji.

Baadhi ya maudhui au programu, ikiwa ni pamoja na matangazo kwenye Tovuti vinatolewa na upande wa tatu, ikiwa ni pamoja na watangazaji wa bidhaa au huduma, mitandao ya matangazo na seva, watoaji wa maudhui, na watoaji wa programu. Hawa wahusika wa upande wa tatu wanaweza ama kutumia vidakuzi peke yake au vidakuzi pamoja na violeza vya wavuti au teknolojia zingine za ufuatiliaji kwa ajili ya kukusanya taarifa kuhusu wewe pale unapotumia tovuti yetu. Taarifa wanazokusanya zinaweza kuhusiana na taarifa zako binafsi au wanaweza kukusanya taarifa ambazo ni pamoja na taarifa binafsi, taarifa kuhusu mambo unayofanya mtandaoni kwa muda fulani na unayofanya kwenye tovuti mbalimbali na kwenye huduma zingine za mtandaoni. Wanaweza kutumia taarifa hizi ili kukuonesha matangazo kwa kuangalia mapendeleo yako au maudhui mengine yaliyolengwa.

Hatudhibiti teknolojia hizi za ufuatiliaji kutoka upande wa tatu au jinsi zinavyoweza kutumika. Kama una maswali yoyote kuhusu tangazo au maudhui mengine yaliyolengwa, itabidi uwaulize wahusika wa matangazo au maudhui hayo moja kwa moja. Kwa taarifa kuhusu jinsi unavyoweza kutochagua kupokea matangazo yanayolenga mtumiaji kutoka kwa watoaji wengi, angali  NAI Consumer Opt Out.

Jinsi Tunavyotumia Taarifa Zako

Tunatumia taarifa kuhusu wewe ambazo tunakusanya au unazotupatia, ikiwa ni pamoja na taarifa zozote binafsi:

  • Kuwasilisha Tovuti yetu na maudhui yake kwako.
  • Kukupatia taarifa, bidhaa, au huduma unazoomba kutoka kwetu.
  • Kutimiza malengo mengine yoyote ambayo umeyatolea taarifa.
  • Kutimiza wajibu wetu na kutekeleza haki zetu zinazotokana na mikataba iliyoingiwa kati yetu na wewe, ikiwa ni pamoja na utoaji bili na ukusanyaji.
  • Kukuarifu kuhusu mabadiliko kwenye Tovuti yetu au kuhusu bidhaa zozote au huduma tunazotoa au kuzitoa kupitia Tovuti yetu.
  • Kukuruhusu kushiriki kwenye vipengele shirikishi kwenye Tovuti yetu. Hii ni pamoja na: ujumbe wa tahadhari, ujumbe wa kukuarifu unaopata kutoka kwenye programu wakati hutumii programu husika, ujumbe wa tahadhari ya mfumo, huduma kwa wateja, na zaidi. Katika wakati wowote, unaweza kuamua kutochagua huduma hizi. 
  • Kwa njia yoyote tunayoweza kueleza unavyotoa taarifa.
  • Kwa madhumuni mengine yoyote kwa idhini yako.

Vile vile tunaweza kutumia taarifa zako kuwasiliana na wewe kuhusu bidhaa na huduma zetu wenyewe ambazo zinaweza kuwa ni zenye maslahi kwako. Ikiwa hutaki tutumie taarifa zako kwa njia hii, tafadhali wasiliana nasi kupitia wasiliananasi@Ifahamutanzania.com.

Tunaweza kutumia taarifa tulizokusanya kutoka kwako ili kutuwezesha kuonesha matangazo kwa watoa matangazo wetu wanaotangaza kwa hadhira iliyolengwa. Na ingawaje hatuoneshi taarifa zako binafsi kwa madhumuni tajwa bila idhini yako, endapo unabofya au unajirikisha kwenye matangazo yanayotokea kwenye Tovuti, watoa matangazo husika wanaweza kuchukulia unakidhi vigezo vilivyolengwa.

Utoaji wa Taarifa Zako

Tunaweza kutoa taarifa za jumla zinazowahusu watumiaji wetu, na taarifa ambazo hazimtambulishi mtu yeyote, pasipo na vizuizi.

Tunaweza kutoa taarifa binafsi tunazokusanya au unazotupatia kama ilivyoelezwa kwenye sera hii ya faragha.

  • Kwa kampuni zetu tanzu na washirika
  • Kwa wakandarasi, watoa huduma, na wahusika wengine wowote kutoka upande wa tatu tunaowatumia kusaidia biashara yetu.
  • Kwa mnunuzi au mrithi mwingine inapotokea kuungana kwa kampuni, ununuliwaji wa kampuni, uuzaji wa kampuni tanzu, urekebishaji wa muundo wa kampuni, kufanya mabadiliko, ufilisi, au uuzaji wowote au uhamishaji wa baadhi ya mali zetu au mali zetu zote, iwe ni kwa ajili ya shaka shaka iliyopo au kama sehemu ya kuwa mufilisi, kuvunja kampuni, au jambo lolote sawa na hayo, ambapo taarifa binafsi zilizokuwa kwetu kuhusu watumiaji wa Tovuti yetu, taarifa hizo ni miongoni mwa mali zitakazohamishwa.
  • Kutimiza malengo au madhumuni yaliyokufanya utoe taarifa zako. Kwa mfano, ikiwa unatupatia anwani yako ya barua pepe ili kutumia kipengele cha Tovuti yetu cha “tuma barua pepe kwa rafiki”, tutatuma maudhui ya barua pepe hiyo na anwani yako ya barua pepe kwa wapokeaji; yaani waliotumiwa barua pepe husika.
  • Kwa madhumuni mengine yoyote tuliyoweka wazi wakati unatoa taarifa.
  • Kwa idhini yako.

Vile vile tunaweza kutoa taarifa zako binafsi:

  • Kutimiza takwa lolote la mahakama, sharia, au mchakato wa kisheria ikiwa ni pamoja na kujibu ombi lolote la serikali au la udhibiti.
  • Kutekeleza au kutumia mapatano yetu mengine ikiwa ni pamoja na kwa madhumuni ya utumaji bili na ukusanyaji.
  • Ikiwa tunaamini kuweka wazi taarifa hizo ni muhimu au ni jambo muafaka ili kulinda haki, mali, au usalama wetu, wateja wetu, au wengineo. Hii ni pamoja na kubalishana taarifa na kampuni na mashirika mengine kwa madhumuni ya kuzuia udanganyifu na kupunguza vihatarishi vya mikopo.

Machaguo Kuhusu Jinsi Tunavyotumia na Kutoa Taarifa Zako

Tunajitahidi kukupatia machaguo kuhusiana na taarifa binafsi unazotoa kwetu. Tumetengeneza mfumo ili kukupatia udhibiti wa mambo yafuatayo juu ya taarifa zako.

  • Teknolojia za Ufuatiliaji na Utangazaji. Unaweza kukifanya kivinjari chako kutokubali vidakuzi vyote vya kivinjari au baadhi ya vidakuzi hivyo, au kukufahamisha wakati vidakuzi vinatumwa. Kujifunza jinsi unavyoweza kusimamia mpangilio wa vidakuzi vinavyotumia programu ya Adobe Flash, tembelea ukurasa wa mipangilio ya programu ya Flash Player kwenye tovuti ya Adobe. IKiwa unalemaza au kukana vidakuzi, tafadhali fahamu kwamba baadhi ya sehemu za Tovuti hii zinaweza zisipatikane au zinaweza zisifanye kazi vizuri.
  • Ofa za Promosheni kutoka kwa Ifahamutanzania. Endapo hutaki anwani yako ya barua pepe pamoja na taarifa zingine za mawasilianokutumiwa na Ifahamutanzania kutangaza bidhaa au huduma zetu wenyewe, au za wahusika wa upande wa tatu, unaweza kutochagua kwa kutoa tiki kwenye visanduku husika vilivyooneshwa kwenye fomu tunayotumia kukusanya data zako au unaweza kufanya hivyo wakati wowote kwa kututumia barua pepe na kuelezea ombi lako kwa maswali@Ifahamutanzania.com. Kama tumekutumia barua pepe ya promosheni, unaweza kutuandikia tena barua pepe ukitaka kuondolewa kwenye usambazaji barua pepe kwa siku zijazo. Kutochagua huku hakuhusishi taarifa zilizotolewa kwa Ifahamutanzania kutokana na kufanya manunuzi ya huduma au miamala mingine.
  • Utangazaji Uliolenga. Endapo hutaki tutumie taarifa ambazo tumekusanya au unazotoa kwetu kwa ajili ya matangazo kutokana na matakwa ya watoa matangazo wetu kufikia hadhira lengwa, unaweza kutochagua kwa kututumia barua pepe kwenda wasiliananasi@Ifahamutanzania.com. Ili kutochagua huku kufanye kazi, unalazimika kukifanya kivinjari chako kikubali vidakuzi vya kivinjari.

Hatudhibiti ukusanyaji wa upande wa tatu au kutumia taarifa zako kukidhi maslahi yanayotokana na utangazaji. Hata hivyo, hawa wa upande wa tatu wanaweza kukupa njia za kuchagua taarifa zako kutokusanywa au kutumika kwa njia hii. Unaweza kuchagua kutopokea matangazo yanayolenga hadhira maalumu kutoka kwa wanachama wa Network Advertising Initiative (“NAI”) kwenye tovuti ya NAI.

Kuzifikia na Kurekebisha Taarifa Zako

Vile vile unaweza kututumia barua pepe kupitia wasiliananasi@Ifahamutanzania.com ili kuomba kuzifikia, kurekebisha au kufuta taarifa zako zozote binafsi ambazo umetupatia. Tunaweza tusifanyie kazi ombi la kubadili taarifa zako endapo tunaamini kubadili huko kunaweza kukiuka sheria au mahitaji ya kisheria au kusababisha taarifa kutokuwa sahihi.

Ikiwa unafuta Michango ya Mtumiaji kutoka kwenye Tovuti, nakala zako za Michango ya Mtumiaji zinaweza kubaki kuwa zinaonekana kwenye hifadhi au kurasa zilizohifadhiwa, au zinaweza kuwa zimetolewa nakala au kutunzwa na watumiaji wengine wa Tovuti.

Tafadhali fahamu kwamba, ombi lolote la kuboresha taarifa zako linaweza kuchukua hadi siku 30 kufanyiwa kazi na kwamba unaweza kuendelea kupokea mawasiliano kutoka Ifahamutanzania.com kwa kutumia taarifa zilizotolewa awali hadi pale ombi lako litakapokuwa limefanyiwa kazi.

Kwa nyongeza, wakati wowote unaweza kuchagua kutotumika kwa taarifa zako binafsi zinazokutambulisha ambazo zimekusanywa mtandaoni kwa madhumuni ya kutuma matangazo ya kutafuta masoko au mawasiliano ya promosheni, na unaweza kufanya hivyo kwa kufuata maelekezo ya kujiondoa yaliyomo kwenye kila kijarida au mawasiliano ya promosheni unayopokea.   

Haki Zako za Faragha za Ontario.

Kanuni za Kiraia za Ontario Sehemu ya 1798.83 zinaruhusu watumiaji wa Tovuti yetu ambao ni wakazi wa Ontario kuomba taarifa fulani fulani kuhusiana na utoaji wetu wa taarifa binafsi kwa upande wa tatu kwa madhumuni ya moja kwa moja ya kutafuta masoko. Kutoa maombi ya aina hiyo, tafadhali tutumie barua pepe kwa wasiliananasi@Ifahamutanzania.com.

Haki Ya Kulinda Data Zako Chini ya Kanuni za Ulinzi wa Data Jumla (GDPR)

Seva na ofisi zetu zipo Canada, kwahiyo taarifa zako zinaweza kusafirishwa hadi, kuhifadhiwa, au kuchakatwa nchini Canada. Wakati ambapo ulinzi wa data, faragha, na sheria zingine za Canada inaweza zisiwe na uwanda mpana sawa na zile za nchini kwako, bado tunachukua hatua nyingi kulinda faragha yako. 

  • Kama ni mkazi wa Eneo la Kiuchumi la Ulaya (kwa kifupi EEA), unazo haki fulani fulani za ulinzi wa data. Ifahamutanzania.com ina nia ya kuchukua hatua muafaka ili kukuruhusu kufanya marekebisho, kusahihisha, kufuta, au kudhibiti utumiaji wa Data Binafsi za kwako.
  • Kama unatarajia kujulishwa ni Data Binafsi zipi zinazokuhusu ambazo tunazitunza, na kama unataka kuondolewa kutoka kwenye mifumo yetu, tafadhali wasiliana nasi.

Katika mazingira fulani fulani, una haki zifuatazo za ulinzi wa data:

  • Haki ya kuzifikia, kuboresha au kufuta taarifa zako tulizo nazo. Vyovyote iwezekanavyo, unaweza kuzifikia, kuboresha au kuomba kufutwa moja kwa moja Data Zako Binafsi kwenye sehemu ya mipangilio ya akaunti yako. Endapo huwezi kufanya kazi hii wewe mwenyewe, tafadhali wasiliana nasi ili tukusaidie.
  • Haki ya urekebishaji. Una haki ya kurekebisha au kusahihisha taarifa zako endapo taarifa hizo hazipo sahihi au hazijakimilika.
  • Haki ya kupinga. Una haki ya kupinga mchakato wetu kuhusu Data Zako Binafsi.
  • Haki ya Kizuizi. Unayo haki ya kuomba tuzuie uchakataji wa taarifa zako binafsi.
  • Haki ya ubebaji wa data. Una haki ya kupewa nakala ya taarifa zako tulizonazo katika umbo, mashine zinazosomeka na muundo ulio kawaida kutumika.
  • Haki ya kuondoa idhini. Vile vile una haki ya kuondoa idhini yako wakati wowote pale ambapo Ifahamutanzania.com ilitegemea idhini yako kuchakata taarifa zako binafasi.
  • Tafadhali fahamu kwamba, tunaweza kukutaka uthibitishe utambulisho wako kabla hatujajibu maombi ya aina hiyo.
  • Una haki ya kulalamika kwa Mamlaka ya Ulinzi wa Data kuhusu ukusanyaji wetu na utumiaji wa Data Binafsi zilizo zako. Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Mamlaka ya Ulinzi wa Data iliyo karibu yako kwenye Eneo la Kiuchumi la Ulaya (EEA).

Usalama wa Data

Tumetekeleza hatua zilizolenga kulinda taarifa zako binafsi dhidi ya upoteaji wa bahati mbaya, na dhidi ya kufikiwa na kutumiwa na wasiorusiwa, kubadilishwa na kuwekwa wazi kwa wengine.

Usalama na ulinzi wa taarifa zako vile vile unakutegemea wewe. Ambapo tumekupatia (au ambapo umechagua) neno la siri ili kufia sehemu fulani za Tovuti yetu, una wajibu wa kulifanya neno hili la siri kuwa siri yako binafsi. Tunakutaka kutotoa neno lako la siri kwa mtu yeyote. Maneno ya siri ya akaunti za Wanachama na Watembeleaji yanakatwa vipande vipande, ikiwa na maana hatuwezi kuyaona maneno ya siri. Vile vile hatuwezi kutuma tena maneno ya siri yaliyopotea. Tutakachofanay ni kukupa tu maelekezo ya namna gani unaweza kuunda upya neno linguine la siri.

Tunakutaka uwe makini unapotoa kwenye majukwaa ya wazi ya Tovuti kama vile kwenye mabango ya ujumbe. Taarifa unazoshirikisha wengine kwenye maeneo ya wazi zinaweza kuonekana na mtumiaji yeyote wa Tovuti.

Kwa bahati mbaya, usambazaji wa taarifa kwa njia ya intaneti haupo salama kwa asilimia zote. Ingawaje tunafanya kila tuwezalo kulinda taarifa zako binafsi, hatuwezi kukuhakikishia usalama wa taarifa zako binafsi zilizosambazwa kwenye Tovuti yetu.  Usambazaji wowote wa taarifa unaufanya kwa utashi wako kwa kuzingatia vihatarishi. Hatuwajibiki kukabiliana na mipangilio yoyote ya faragha au hatua za kiulinzi zilizopo kwenye Tovuti,   

Uzuiaji wa Data

Tunazuia Taarifa Binafsi pale ambapo bado tuna biashara halali au mahitaji ya kisheria ya kufanya hivyo. Kipindi cha uzuiaji kitatofautiana kutegemeana aina ya data husika, lakini, kwa ujumla, tutarejea kwenye vigezo vifuatavyo kufahamu muda wa uzuiaji:

  • Endapo tuna mahitaji ya kisheria au ya kimkataba kushikilia data.
  • Endapo data ni muhimu katika kutoa Huduma zetu.
  • Endapo Wanachama wetu na/au Watembeleaji wana uwezo wa kufikia na kufuta data kwenye akaunti zao za Ifahamutanzania.com
  • Endapo Wanachama wetu na/au Watembeleaji wangetarajia kwamba, tungezuia data hadi wanapoziondoa au hadi akaunti zao kwenye Ifahamutanzania.com zinafungwa au kusitishwa.

Wakati hatuna mahitaji ya biashara halali ya kuendelea kuchakata Taarifa Zako Binafsi, ama tutafuta au kuziondolea utambulisho wa mhusika au, endapo hili haliwezekani (kwa mfano, kwa sababu Taarifa Zako Binafsi zimehifadhiwa kwenye utunzaji nyaraka kwa dharula), basi tutahifadhi Taarifa Zako Binafsi kiusalama na kuzitenga dhidi ya uchakataji wowote hadi ufutaji utakapowezekana.

Mabadiliko kwa Sera Yetu ya Faragha

sera yetu kubandika kwenye ukarasa huu mabadiliko yoyote kwenye sera yetu ya faragha kwa kuarifu kwamba sera ya faragha imerekebishwa kwenye ukurasa wa mwanzo wa Tovuti. Endapo tunafanya mabadiliko ya jinsi ya tunavyofanyia kazi taarifa binafsi za watumiaji wetu, tutakutaarifu kwa barua pepe kwa kutumia anwani kuu ya barua pepe iliyooneshwa kwenye akaunti yako na/au kupitia taarifa itakayowekwa kwenye ukurasa wa mwanzo wa Tovuti. Tarehe ya mwisho ambayo sera ya faragha ilipitiwa inatambulishwa kwa kuwekwa juu ya ukurasa. Una wajibu wa kuhakikisha tuna anwani yako ya barua pepe ya sasa na iliyo hai, na iwezayo kupokea barua pepe. Na pia unawajibu wa kutembelea Tovuti yetu mara kwa mara na sera hii ya faragha ili kuangalia mabadiliko yoyote. Ifahamutanzania.com ina haki ya kupitia na kubadilisha sera hii wakati wowote.

Taarifa za Mawasiliano

Kuuliza maswali au kutoa maoni kuhusu sera hii ya faragha na matendo yetu ya faragha, wasiliana nasi kwa:
wasiliananasi@Ifahamutanzania.com.